Trending Videos
Title: Nandy - Kivuruge (Official Video)

Dec 29
Nandy - Kivuruge (Official Video)
Oct 5
Aslay - Natamba ( Official Music Video )
Aug 25
Alikiba - Seduce Me (Official Music Video)
Jul 29
Richmavoko ft Fid Q - Sheri (Official Video)
Jul 29
Harmonize - Sina Official Video
Dec 10
Darassa ft Ben Pol - Muziki ( Official Music...
Dec 9
MwanaFA Featuring Vanessa Mdee - Dume Suruali...
Dec 9
Ommy Dimpoz X Alikiba - Kajiandae (Official...

(Yesterday)

Michuzi

UBALOZI WA KUWAIT NA TAASISI YA DORIS MOLLEL WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WATOTO NJITI, HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA, DODOMA

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika, sehemu ya vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti, vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma. Wengine pichani ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Hospitali hiyo, Neema Tawale (wa pili kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Huduma za Uuguzi, Salome Kasanga.

The Ambassador of Kuwait in Tanzania His Excellency Hon. Jaseem Al Najem (L) Handing Over Equipments to support Premature babies at Benjamin Mkapa Hospital to the Executive Director of the Hospital, Dr. Alphonce Chandika, A support from the Embassy of Kuwait in Collaboration with Doris Mollel Foundation end of this week in Dodoma. second from left is Ms. Doris Mollel Founder of Doris Mollel Foundation and Ambassador to Preterm babies in Tanzania , Neema Tawale(second from right) together with Acting Director of Nursing at Benjamin Mkapa Hospital Sr Salome Kasanga. Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akieleza jambo kwa waandishi wa habari juu ya vifaa hivyo vilivyogharimu dola za Marekani elfu ishirini (20,000 USD) huku Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika (kulia) wakimsikiliza, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem,  Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Januarius Hingi wakati akitoa maelezo ya namna vifaa hivyo vitakavyosaidia wakina mama wanaojifungua watoto wanaozaliwa kawaida na wale wanaozaliwa kabla ya wakati.  Sehemu ya vifaa hivyo.

(Yesterday)

BBCSwahili

Umoja na amani ya Tanzania viko hatarini;Maaskofu wa kilutheri waonya

Maaskofu wa KKKT waorodhesha mambo yanayohatarisha

(Yesterday)

Malunde

FISSOO : TANZANIA NI YA PILI BARANI AFRIKA KWA UZALISHAJI WA FILAMU


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo amewataka Watanzania kutumia vizuri fursa za masoko ya filamu kwa ajili ya kujiingizia kipato kwa sababu Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa filamu barani Afrika ikitanguliwa na Nigeria.

Akizungumza Machi 23,2018 wakati wa uzinduzi wa Filamu ya "Laana ya Mke" katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema  ni lazima waigizaji watumie fursa zinazotengenezwa na Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kwenye eneo la masoko ya filamu.
''Tunapozungumzia filamu Tanzania ni ya pili baada ya Nigeria, na ukizungumzia Tanzania pia Shinyanga ipo ndani yake kwa hiyo hii ni fursa kwenu ambapo bodi ya filamu na Wizara zinashirikiana kuhakikisha kazi za sanaa zinapata masoko'', alieleza Fissoo.
Aliweka wazi kuwa Bodi hiyo imekuwa ikifuatilia kila hatua ya wasanii hivyo kuwataka kuungana na kuepuka migogoro.
Filamu ya Laana ya Mke imeandaliwa na wasanii wa Bongo Movies Shinyanga ambao wamemshirikisha mwigizaji maarufu wa Filamu nchini Blandina Chagula 'Johari' ambaye kwao ni Shinyanga. SHUHUDIA <<HAPA>> UZINDUZI WA FILAMU YA 'LAANA YA MKE' - BONGO MOVIES SHINYANGA

(Yesterday)

Michuzi

KAMPUNI YA DATA VISION KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUPELEKA NCHI KWENYE UCHUMI WA KATI

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamiiKAMPUNI ya International Data Vision inayohusika na masuala ya Utafiti, imeahidi kushirikiana na Serikali ili kuifikisha nchi kwenye uchumi wa viwanda.
Ahadi hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Geofrey  Maclean wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Pia amesema licha ya kueleza mafanikio ya shirika hilo ameeleza mbinu mkakati za kiubunifu  za kutofanya biashara kimazoea na hiyo ni kwa kuhusisha matumizi ya teknolojia(ICT) na tafiti mbalimbali na kujua mahitaji ya soko la dunia.
Aidha ameomba ushirikiano wa wafanyakazi na watu wanaowafikia katika maeneo mbalimbali.
Kuhusu kushirikiana na Serikali katika kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati Mwaijonga ameeleza wanaunga mkono dhamira hiyo na wanashiriki kwa namna mbalimbali kama vile kulipa kodi stahiki kwa Serikali, kutengeneza ajira na kuleta ubunifu mpya katika biashara.
Pia Mwaijonga amesemaleza wana mpango mpya wa kusafirisha maarifa (skills)ili  zikatumike katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuiongezea nchi kipato kitakachosaidia kuifikisha kwenye uchumi wa kati. Mkurungenzi  Mtendaji wa Kampuni  ya Data Vision International, Geofrey  Maclean Mwaijonga aizungumza na wafanyaazi wa kampuni hoyo  katika maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Wafanyaazi wa kampuni  Data Vision International  wakimsikiliza Mkurungenzi  Mtendaji wa Kampuni hiyo, Geofrey  Maclean Mwaijonga wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

(Yesterday)

VOASwahili

Trump aepusha serikali kufungwa kwa kupitisha dola trilioni 1.3

Rais Donald Trump amepitisha muswada wa matumizi ya dola za Kimarekani trilioni 1.3 Ijumaa kwa shigo upande, masaa kadhaa baada ya kutishia kuzuia hatua hiyo kwa sababu ilikuwa haiwatetei wahamiaji waliokuja Marekani wakiwa watoto wadogo na wala kutenga fedha za ujenzi wa ukuta mpakani.

(Yesterday)

Michuzi

AMOS CHEREHANI ENDORSES LIBE KUWA RAIS WA JUMUIYA DMV

Bwana Amos Cherehani usiku wa Alhamis March 22 amethibitidha kumu endorses Liberatus Mwang’ombe, ambae anawania kiti cha urais wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washington

(Yesterday)

MwanaHALISI

Maaskofu wa KKKT watoa waraka mzito kwa serikali

MAASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wametoa waraka mzito waliouta ‘Ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka’ ambao utasomwa kesho katika makanisa yote nchini kwa waumini wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Ujumbe huo wa Pasaka ambao umegusia mambo makubwa matatu ambayo ni Jamii na Uchumi, Maisha ya Siasa na Masuala Mtambuka na kusainiwa ...

(Yesterday)

Malunde

HUU HAPA UJUMBE WA PASAKA KUTOKA KWA MAASKOFU WA KANISA LA KKKT...WALIA NA MATUKIO YANAYOENDELEA TANZANIA

Bwana wetu Yesu Kristo mfufuka, alipowatokea wanafunzi wake wakiwa wamejifungia ndani kwa hofu ya Wayahudi, aliwasalimu na kujifunua kwao kwa salaamu ya kuwatakia amani. 


Wapendwa watu wa Mungu, katika umoja wetu, sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tunawasalimuni nyote kwa kuwatakia amani. Bwana wetu Yesu Kristo Amefufuka kweli kweli -Haleluya!. Yeye ni amani yetu, na pia ni amani kwa watu wote wenye mapenzi mema. Kwa kufufuka kwake, upendo umeishinda chuki; unyenyekevu umeushinda ubabe; nuru imelishinda giza; haki imeshinda udhalimu; msamaha umeshinda visasi; ujasiri umeshinda hofu; na kwa hiyo uzima umeshinda kifo.
Mwaka 2017, Kanisa letu limeadhimisha miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa. Tukiwa wana Matengenezo tumekumbushwa tena kuwa mwanadamu anaokolewa kwa Neema ya Mungu tu: Wokovu Hauuzwi; Mwanadamu Hauzwi wala kununuliwa; na Uumbajihauuzwi. Kanisa zima na dunia kwa ujumla tunaitwa kusimama pamoja na kuueleza ukweli huu unaoziweka huru dhamiri zetu (Yohana 8:31-32).
Matengenezo (Reforms) ni dhana ya kibiblia. Tangu zama za Agano la Kale, Mungu kwa nyakati mbalimbali aliteua wajumbe wake kuwasilisha ujumbe wake kwa jamii na kwa watawala wa dunia. Kwa Umungu wake, aliwainua wanawake na wanaume kwa makusudi ya kutoa unabii yaani, ujumbe wa Mungu kwa jamii au watawala. Wakati mwingine aliinua manabii kuwasemea wasiokuwa na sauti. Unabii na Matengenezo ni njia ya Mungu katika kusimika utawala wa haki na unaostawisha uhuru na amani.
Kwa namna ya pekee, manabii kama Daniel, walionya juu ya uongozi unaojenga uhalali wake katika wingi wa watu wanaokubaliana na uongozi huo hata kama ni katika makosa. Haikuwa rahisi kibinadamu kuukosoa mfumo kama huo lakini Mungu alitumia manabii kuzungumza na mfumo wa namna hiyo. Unabii wa Daniel 3:7 unasema, “Kwa hiyowatu WOTE, mara waliposikia sauti za baragumu, filimbi, kinubi,zeze, santuri, zumari, na sauti za ala nyingine za muziki,walianguka kifudifudi na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayoMfalme Nebkadneza aliisimamisha”. Hapa tunaona kosa la kiongozi kutengeneza sanamu, linasababisha kosa la watu wanaokubali kuiabudu hiyo sanamu. Tumetafakari na kusadiki kuwa, kosa la kiongozi au mfumo, haliwaondolei hatia wanaomfuata kiongozi au kuufuata mfumo, hata kama watu hao walikula kiapo cha kutii maongozi ya kiongozi huyo na mfumo wake. Mbele ya Mungu hakuna ile kanuni ya kuwajibika kwa pamoja. Kila mtu kwa dhamiri yake anawajibika mbele za Mungu. Kwa upande mwingine, pamoja na uwajibikaji wa mtu binafsi, Nabii Ezekieli anatukumbusha na kutuonya kuwa tusipoonya na kusimama katika zamu yetu, hatia na damu ya wasio na hatia, itadaiwa mikononi mwetu (Ezekiel 33: 8-9).
Adhimisho la kufufuka kwa Yesu Kristo (Pasaka) na maadhimisho ya miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa, yanatusukuma kutafakari utume wa Kanisa katika jamii kwa nyakati zetu. Tunaalikwa kupeleka ujumbe wa amani kwa watu wote na kusimama kwa ujasiri katika kuwasemea wasio na sauti katika jamii ili kuenzi roho ya Pasaka na Matengenezo katika nyakati zetu. Kama Kanisa na kwa nafsi zetu mmoja mmoja, tunaitwa kwa upande mmoja, kufundisha, kushauri na kutia moyo. Kwa upande mwingine, tunaitwa kuonya, kukaripia, kukemea na kuelekeza kwa uvumilivu wote na upendo (2 Timotheo 4: 1-5).
Wajibu huu kwetu sisi maaskofu ni wito na utume usiokwepeka; na kwa watu wote wa imani, wajibu huu hauna mbadala. Tunaagizwa kuchochea ujenzi wa madaraja ya maridhiano katika upendo na amani, na kuwa kinyume na mifumo yote inayoendeleza chuki na marafakano. Kwa kufanya hivyo, imetupasa kusema wazi wazi ujumbe wa amani, upendo, heshima, utu, ustahimilivu na maelewano. Mfumo wowote unaojengwa katika utii wa sheria bila upendo; heshima bila uhuru; na amani bila haki, unajengwa katika msingi usio imara. Kupuuza wito huu kuna madhara kwa jamii yetu. Ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga (Mathayo 7: 26). Tunasihi kwa machozi mengi, tuwe wajenzi wenye akili wajengao nyumba zao juu ya mwamba (Mathayo 7:24). Mwamba tunaotakiwa kujenga taifa letu lenye dini mbalimbali, vyama mbalimbali, na makabila mbalimbali, umetajwa katika sala kuu ya taifa letu, yaani, "DUMISHA UHURU NA UMOJA". Bila Uhuru hakuna umoja uwezao kuleta maendeleo; na bila umoja wa kitaifa, uhuru wetu hauleti amani endelevu. Kwa sababu ya nguvu ya dhamiri safi iliyo dira ya taifa letu, tunalazimika kumtii Mungu kuliko mwanadamu (Matendo 5:29).
B. TAIFA LETU NA AMANI YETUTunapoadhimisha sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tunatambua kuwa utume wa Kanisa letu katika taifa letu, unafanyika katikati ya changamoto kadhaa. Kwa kuwa Kanisa ni sehemu ya jamii, linaguswa na changamoto hizo. Katika kukaa pamoja na kuliombea taifa letu, sisi maaskofu wa KKKT, tumetafakari na kubaini changamoto hizo. Kwa njia ya salaam za Pasaka, tunaleta kwenu changamoto tatu ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.
1. Jamii na UchumiKiini cha Utume wetu katika jamii kinatuingiza kwa nia njema katika maisha ya uchumi na mshikamano wa kijamii. Neno la Mungu linatufundisha kuwa "Mwanadamu hawezi kuishi kwa mkate peke yake" (Luka 4:4). Pia neno la Mungu linatuhakikishia kuwa Bwana wetu Yesu Kristo alikuja ili tuwe na uzima tele (Yohana 10:10). Tunawiwa katika umoja wetu wa ubaba, kuipongeza serikali yetu kwa jitihada inazofanya kuboresha maisha ya wananchi. Tumeshuhudia jitihada na nia njema kuhusu uvunaji na umilikaji wa raslimali za nchi kwa manufaa ya taifa zima. Aidha, tunapongeza jitihada za ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kugharamia huduma za jamii. Hata hivyo, bila kukatisha tamaa jitihada hizo, tunawiwa kushauri yafuatayo:
I. Sekta binafsi na mashirika ya dini ni wadau wa maendeleo, si washindani wa serikali katika kuchangia maendeleo ya taifa. Mazingira yasiyo rafiki kuhusu wadau hawa, ni kikwazo kisicholeta mshikamano kati ya serikali na sekta binafsi na mashirika ya dini katika kuleta maendeleo. Jitihada za makusudi na za mara kwa mara zifanyike kuondoa dhana ya ushindani kati ya serikali na wadau hawa ili kuimarisha mahusiano mema kati ya serikali na sekta binafsi.
II. Ili mfumo wa ukusanyaji wa kodi uwe endelevu; jitihada za kukusanya kodi ziendane na elimu kwa mlipa kodi. Msisitizo wa uzalendo wa kulipa kodi uende sambamba na ustawi wa walipa kodi katika shughuli zao za biashara. Mivutano isiyo na tija kati ya walipa kodi (wafanya biashara) na mamlaka ya ukusanyaji wa kodi, inastawisha uadui unaopunguza makusanyo ya kodi na kujenga ushawishi wa rushwa. Mfumo wa kodi unaowafilisi wafanya biashara, haulengi kujenga uchumi wa viwanda.
III. Kutokana na ongezeko kubwa la vijana wasio na ajira; jitihada za wazi na za makusudi zifanyike ili msukumo wa uchumi wa viwanda ufikie matumaini yanayoshikika miongoni mwa vijana wasio na ajira. Sekta binafsi, wawekezaji na wadau wengine, wahakikishiwe usalama wa mitaji yao kisheria. Hili likifanyika ni kichocheo kizuri cha ujenzi wa viwanda.
IV. Uchumi wa viwanda (vidogo na vikubwa) uendane na uwekezaji katika sekta ya kilimo maeneo ya vijijini. Kilimo na ufugaji ndizo sekta zenye wigo mpana wa viwanda vinavyogusa maisha ya watanzania walio wengi. Utozaji holela wa kodi na ushuru wa mazao unakatisha tamaa wadau wa kilimo. Migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa upande mmoja, na wakulima/wafugaji na wawekezaji kwa upande wa pili, si kivutio cha uwekezaji katika sekta ya kilimo.
2. Maisha ya SiasaKwa umoja wetu katika utume, tunatambua siasa safi na uongozi bora kuwa ni misingi iliyoongoza maisha ya siasa katika taifa letu. Ujio wa vyama vingi mnamo 1992, haukuondoa umuhimu wa misingi hii bali ulipanua matumizi ya demokrasia iliyojengwa katika uhuru wa mawazo. Taifa ni mkusanyiko wa taasisi na watu mbalimbali, wenye lengo moja lakini kwa njia mbalimbali. Kutokana na wingi huu, taifa letu daima ni juu ya vyama, taasisi na makundi.
Taifa huongozwa na katiba iliyo kiini cha sheria zote. Taifa haliongozwi na ilani za vyama. Serikali haiongozwi na ilani za vyama. Serikali huongozwa na katiba, sheria, kanuni na mapokeo mema (misingi na tunu za taifa). Serikali husimamiwa na bunge huru lililo sauti ya wananchi. Wananchi ndilo chimbuko la madaraka ya bunge. Bunge halisimamiwi na ilani, chama chochote wala mtu awaye yote. Kwa umoja wetu na kwa nyakati zetu, hivi sasa tunashuhudia matukio yaliyo kinyume na tunu na misingi iliyolilea taifa letu. Baadhi ya matukio hayo ni:
I. Hofu iliyojengwa katika matukio halisi yakiwamo utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.
II. Kupungua na hatimaye kutoweka kwa uhuru wa kujieleza, kukusanyika, na kupata habari. Kwa mwenendo huu, kuna hofu kuwa hata uhuru wa kuabudu uko mashakani.
III. Kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi. Hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.
IV. Kukosekana kwa mazingira ya haki na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi zote zimeghubikwa na ubabe, vurugu, hila, na vitisho.
V. Utekelezaji wa mipango ya maendeleo wenye mwelekeo wa kiitikadi. Hatua hii imeimarisha ubaguzi wa kiitikadi katika taifa letu na kukuza migawanyiko.
VI. Kushamiri kwa chuki mioyoni mwa watu ambalo ni chimbuko la visasi, kukata tamaa, na ushiriki mdogo wa wananchi katika chaguzi na maisha ya siasa.
VII. Udhalilishaji wa kauli njema isemayo "Maendeleo hayana chama". Udhalilishaji huu unafanyika kwa njia ya kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo zinazotokana na watu wanaobadili vyama ili kuleta maendeleo. Tunajiuliza, kama maendeleo hayana chama, kwa nini mtu anajiuzuru chama fulani, eti kwenda kuleta maendeleo katika chama kingine? Mchezo huu unagharimu fedha nyingi na maisha ya watu wanaokufa, kujeruhiwa na uharibifu wa mali.
Mambo haya ni tishio linalohatarisha umoja na amani ya nchi yetu.
3. Masuala MtambukaKanisa ni alama ya uwepo wa utume wa kuleta na kutunza matumaini katika jamii. Ukimya wa Kanisa katika masuala yanayoigusa jamii ni ukwepaji wa wajibu wake. Lakini pia sauti ya Kanisa isiyomilikiwa na mtu isipokuwa Mungu tu, ni chachu ya amani na matumaini. Kwa dhamiri safi inayotokana na utambuzi wa "Wakati wa Mungu"(Kairos) katika taifa letu, tunawiwa kutambua masuala mtambuka yanayogusa maisha ya watu kipekee na kwa njia nyingi na kuyatolea ushauri ufuatao:
I. Kuhitimisha mabadiliko ya mara kwa mara katika mfumo wa elimu nchini ili kuondoa mwanya wa kila mtendaji mkuu wa wizara kuja na sera yake. Elimu ni kitovu cha ustawi wa taifa, kisiwe kinachokonolewa chokonolewa kila wakati. Sekta zote nchini hujenga mafanikio yake katika mafanikio ya mfumo thabiti wa elimu.
II. Uwezeshaji wa vijana kupata mikopo ya elimu ya juu uwe shirikishi na usiokuwa na "ubaguzi" kati ya wanafunzi wa vyuo binafsi na wale wa serikali; sayansi na sanaa; wazazi maskini na wenye nafasi; waliosoma shule binafsi na wale wa shule za serikali, n.k. Kwa kuwa huu ni mkopo, jitihada ziwekwe zaidi katika urejeshaji wa mkopo huo kwa kuzingatia kuwa huu ni mkopo kwa mtoto siyo kwa mzazi.
III. Vyombo vya usimamizi wa sheria na utoaji haki vionekane vinatenda haki sawa kwa watu wote na makundi yote bila kuacha ishara za fadhila au kukomoana.
IV. Wajibu wa serikali kikatiba katika kulinda uhai wa raia wake, uonekane unatekelezwa bila kuacha mwanya wa kuituhumu serikali. Ukiachwa mwanya katika ulinzi wa uhai wa raia, waweza kutumiwa na mamluki kujichukulia sheria mkononi kwa niaba ya serikali. Damu isiyo na hatia
ina madhara kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Mpaka sasa tumeshuhudia umwagaji wa damu unaotusuta sisi sote na mamlaka zote. Mungu anatusuta watanzania kama alivyomsuta Kaini: "Sauti yadamu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi" (Mwanzo 4:10).
V. Uhai wa mtu una thamani isiyopimika. Ni wajibu usiokwepeka kuulinda na kuutunza uhai kwa vitendo halisi. Endapo uhai umepotea katika mazingira yoyote, uchunguzi huru na wa haki ufanyike na taarifa zitolewe kwa wakati muafaka ili kujenga jamii yenye imani kwa serikali na vyombo vyake. Matukio ya mauaji ya askari wetu, mauaji ya raia, majaribio ya kuwaua wanasiasa, utekaji, na uteswaji visipochunguzwa na kutolewa taarifa, ni shina la hofu na uchungu katika jamii. Jamii iliyojaa hofu na uchungu, haiwezi kuwa na maendeleo wala kuwa na roho ya uzalendo.
VI. Ili kulipatia taifa letu ufumbuzi wa mambo yote tuliyotaja na kushauri kwa wakati huu na ujao; tunaisihi serikali ya awamu ya tano, kurejea mchakato wa upatikanaji wa KATIBA MPYA ya wananchi, iliyopendekezwa na wananchi kupitia Tume ya Warioba. Watanzania wengi wanaona na kuamini kuwa KATIBA MPYA ina majibu ya kukidhi mahitaji ya taifa letu kwa sasa na baadaye. KATIBA MPYA ni zao la utashi wa Watanzania kupitia tume ya Warioba iliyokuwa na uwakilishi mpana wa taifa letu.
VII. Aidha, tunawashauri raia wema, kwa njia za kidemokrasia kupitia majukwaa ya kikatiba yaliyo katika maeneo yao, kudai upatikanaji wa KATIBA MPYA. Itapendeza ikiwa KATIBA MPYA itapatikana kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano yatadumu iwapo kuna KATIBA MPYA inayolinda mazuri. Kiongozi mzalendo si mbadala wa KATIBA MPYA. Tanzania yenye amani na maendeleo ni tunda la itikadi zote, dini zote, makabila yote na makundi yote chini ya KATIBA MPYA.
C. HITIMISHOKufufuka kwa Yesu Kristo ni kiini cha Matengenezo ya Kanisa. Kwamba, katikati ya jamii iliyokata tamaa na kutawaliwa na hofu, Kristo alifufuka na kuleta matumaini mapya. Kwamba, katikati ya wasiwasi wa Kanisa kupoteza nguvu ya utume wake, Roho Mtakatifu aliongoza Matengenezo ya Kanisa. Kwa hiyo Matengenezo ni endelevu katika jamii ya watu na taasisi zao. Muasisi wa Matengenezo Dr. Martin Luther yungali analiwajibisha Kanisa kuzingatia utume wake unaoleta matumaini mapya kila siku. Waliobatizwa wote ni wamisionari tunaotumwa na Bwana wetu Yesu Kristo (Yohana 20:21). Imetupasa kuwa nuru na chumvi ya jamii na kuwa mawakala wa uhuru, umoja na amani.
Taifa letu lilipata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu. Roho ile ile ya majadiliano na maridhiano iliyokuwamo ndani ya waasisi wa taifa letu, inatakiwa kila wakati. Uhuru ulioletwa kwa majadiliano, utunzwe na kulindwa bila ulazima wa kumwaga damu ya watanzania. Uhuru naUmoja ndizo ngao zetu zilizolitunza taifa kwa zaidi ya miaka 50.
Sisi tulio maaskofu kwa neema ya Mungu, tunaleta wito kwenu wenye imani katika dini mbalimbali, kuliombea taifa letu. Kuwaombea wote wenye madaraka ili wajaliwe hekima, busara na upendo kwa taifa na watu wake. Kupitia jumuia ndogo ndogo na sharika zote, waombee viongozi wetu ili Mungu awajalie na kuwatunuku kiu ya kutenda haki, kusikiliza kuliko kusema, kuelekeza kuliko kuamrisha, kuunganisha kuliko kutawanya, kupenda watu kuliko kutamani kupendwa na watu, kutamani kutumika kuliko kutumikiwa (Marko 10:45), kuheshimu kuliko kuheshimiwa.
Ujumbe wa Pasaka unatuhimiza kuthamini uhai. Bwana wetu Yesu Kristo alikubali kufa ili kuhifadhi uhai wetu. Kwa kufa kwake na kufufuka, amekomesha kifo na mawakala wake. Tunaitwa kuthamini uhai na kutoruhusu tena watu kuteswa na kuuawa. Kwa hekima yote na unyenyekevu, tunasihi tena, kwamba ikubalike kuwa hitaji la watanzania walio wengi kwa sasa ni KATIBA MPYA. Katiba Mpya ipatikane ili kukuza na kuimarisha mfumo wa utawala utakaolinda uhai wa watu, raslimali za nchi, tunu za taifa, uhuru wa mihimili ya dola, na uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.
Tunawatakia Pasaka njema ya mwaka 2018, na Mungu awabarikininyote. (Yesterday)

Malunde

SERIKALI YAKIRI KUJICHANGANYA KIGEZO CHA UMRI WA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA SITA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu amefunguka na kuweka wazi utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo inasambaa imekuwa na makosa.
Semakafu amesema kuwa yametokea makosa ya kiuandishi ila kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita ni miaka 25 na siyo miaka 20 kama ambavyo inasomekana katika taarifa aliyotolewa jana
"Kumetokea makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile karatasi" alisema Semakafu 

Kufuatia makosa hayo serikali imetoa waraka mpya kurekebisha ule wa mwanzo, na kipengele cha miaka 20 wameweka 25.

(Yesterday)

Michuzi

Katiba na Sheria yajivunia utekeleziji wa Ilani ya CCM

Na Maura Mwingira, Dodoma 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Palamagamba Kabudi ( Mb) amesema, Wizara yake pamoja na Taasisi ambazo zipo chini yake, imeendelea kutekeleza ahadi zote za Ilani ya Chama cha Mapinduzi zinazoambatana na na matarajio ya wananchi kutoka kwenye sekta ya sheria. 
Waziri Kabudi ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi zake mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mjini Dodoma. 
"Wizara yangu imekuwa ikiwajibika vilivyo katika kuhakikisha kuwa inatekeleza ahadi zote za Ilani zinazoambatana na matarajio ya wananchi kutoka kwenye sekta ya sheria" ameeleza Mhe. Waziri 
Akazitaja ahadi hizo kati ya nyingi, kuwa ni, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubathirifu wa mali ya umma, kukuza, kulinda haki za binadamu na utawala wa sheria katika ngazi zote za uongozi, kuimarisha mfumo wa utoaji wa haki na kukamilisha mchakato wa Katiba mpya. Akiwasilisha Mpango na Bajeti ya Wizara na Taasisi zake nane, Waziri aliiomba Kamati hiyo kupitisha zaidi ya Sh. 183.223.058,000bn/- zikiwa ni fedha za mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo kwa Wizara na Taasisi zake. Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Palamagamba Kabudi amesema Wizara yake   pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika sekta ya sheria, ambapo pamoja na mambo mengine, wananchi wanauelewa mkubwa wa namna ya kutafuta na kupata haki yao kisheria. Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo na Taasisi zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.Pamoja naye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

(Yesterday)

Zanzibar 24

Magazeti ya Tanzania Leo Jumamosi March 24 2018

Kama kawaida Zanzibar24 tayari imeshakusogezea stori kubwa zilizotengeneza headline katika kurasa za mbele na nyuma za Magazeti ya Tanzania Leo Jumamosi March 24 2018. Chukua time yako kwa kupitia Stori zote kali za udaku, siasa, michezo, burudani na mambo mengine mbali mbali.

 

 

The post Magazeti ya Tanzania Leo Jumamosi March 24 2018 appeared first on Zanzibar24.

1 day ago

BBCSwahili

Kesi zinazowaandama Wanasiasa wa Upinzani Tanzania

Wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania wameendelea kutumia muda wao mwingi kulalamika kile wanachokiita kuminywa katika kufanya shughuli zao za kisiasa

1 day ago

Nasdaq

Tanzania expands main airport to boost passenger capacity


Nasdaq
Tanzania expands main airport to boost passenger capacity
Nasdaq
DAR ES SALAAM, March 23 (Reuters) - A new terminal building at Dar es Salaam's main airport will open in June 2019 after funding delays were resolved, the Tanzanian prime minister's office said on Friday. The project, which will cost more than 250 ...

1 day ago

Michuzi

PANITA YAISHAURI SERIKALI KUHUSU MUHIMU WA LISHE BORA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamiiJUKWAA la Lishe Tanzania(Panita) limeishauri Serikali kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kuhusu lishe kwenye jamii ya Watazania ili kuwa na taifa lenye uwezo wa kujituma na kuleta maendeleo.
Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa Program wa Panita, Jane Msagati wakati anazungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini kuhusu lishe bora.
Amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha suala la lishe linapewa kipaumbele nchini kwa jamii kupata elimu itakayosaidia kutambua umuhimu wa lishe bora katika Taifa.
"Ukosefu wa lishe bora mwilini unasababisha udumavu na utapiamlo na matokeo yake husababisha magonjwa ambayo ni gharama kuyatibu na wakati mwingine husababisha ulemavu wa kudumu.
"Tatizo la lishe chini limesababisha kuongozeka kwa watoto wenye udumavu wa mwili na akili.Serikali inatumia fedha nyingi kugharamia matibabu, na hiyo ni hasara kubwa,"amesema Msagati.Akizungumza kuhusu lishe  amesema ni msingi wa maendeleo kwa wote na jamii ihakikishe watoto wote wanapata lishe sahihi hususani siku 1000 za kwanza.
Pia amesema wababa wahusike kwenye malezi ya watoto na jamii ihakikishe kaya zinauhakika wa chakula kwa kuzalisha vyakula vya kutosha na kutotumia vyakula vyote kutengeneza pombe.
Amezungumzia umuhimu wa jamii kutengeneza bustani ndogondogo kuzunguka nyumba, bustani makasha/viroba kwa ajili ya mboga za majani.Pia kufuga wanyama wadogo kama kuku na  sungura.
Amesema ukosefu wa virutubisho mwilini husababisha njaa iliyojificha ambayo huchangia kwa kiwango kikubwa katika kusababisha magonjwa na vifo hususani kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na akina mama walio katika umri wa kuzaa
Kuhusu mafunzo ya lishe kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini, Msagati amesema wanatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha umma.
Msagati amesema wahariri wa vyombo vya habari ndio wenye jukumu la kupitisha habari kwenye vyombo vyao na hivyo kukutana kati ya Panita na wahariri hao kutatoa fursa ya kuelezea umuhimu wa kuzipa kipaumbele habari za lishe bora.
Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Bakari Kimwanga na Mgariri wa Jarida la Afya na Ajira kutoka Gazeti la Mwananchi, Lilian Timbuka wamezungumzia umuhimu wa mafunzo yaliyotolewa na Panita kuhusu lishe bora na kwamba watatumia vyombo vyao kuwa mabalozi wa kuhamasisha jamii kuzingatia lishe bora.Meneja wa Program wa Jukwaa la Lishe Tanzania(Panita), Jane Msagati akitoa mada kwenye semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika leo Dar es Saalam leo Semina hiyo ilikuwa inangumzia umuhimu wa lishe bora kwa jamii.Mwandishi Mwandamizi wa Mlimani TV, Annuary Mkama akitoa somo kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.Wahariri na waandishi wa habari wakisikiliza mtoa mada katika semina la lishe bora kutoka kwa Meneja wa Programu wa Panita Jane Msagati(hayupo pichani).Mtaalam wa masuala ya lishe kutoka Jukwaa la Lishe Tanzania(Panita), Deborah Esam akitoa mada kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

1 day ago

Arabiya

VIDEO: Dubai Crown Prince spreads joyful African spirit during Tanzania visit - Al


Al-Arabiya
VIDEO: Dubai Crown Prince spreads joyful African spirit during Tanzania visit
Al-Arabiya
The Dubai crown prince can be seen encouraging a local woman dressed in her colorful traditional clothing to sing. (Screengrab). Staff writer, Al Arabiya English Friday, 23 March 2018. Text size A A A. The Crown Prince of Dubai, Sheikh Hamdan bin ...

1 day ago

Zanzibar 24

Trump atoa onyo kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa Obama

Rais wa Marekani, Donald Trump ameamua kuweka wazi kuwa amechoshwa na kauli za vitisho kutoka kwa aliyewahi kuwa makamu wa Rais nchini humo wakati wa utawala wa Barack Obama, Joe Biden.

Trump amesema amechoshwa na kauli za vitisho juu yake zinazotolewa na mwanasiasa huyo mkongwe nchini Marekani kutoka chama cha Democratic na kuweka wazi kuwa haogopi chochote kwani anamjua toka enzi ni mtu asiyekuwa na nguvu kimwili na kiakili.

“Mpuuzi Joe Biden anajifanya kama mtu mwenye nguvu. Ukweli ni kwamba ni mtu dhaifu kimwili na kiakili mbaya zaidi anatishia kunipiga kwa mara ya pili hii. Nadhani hanijui vizuri nitamsambaratisha mara moja na kurudi nyumbani akilia njia nzima. Usipende kutishia watu.“ameandika Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Jumanne Machi 20, 2018 Joe Biden akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Masuala ya siasa cha Miami akisema kuwa kama wangekuwa wanasoma naye sekondari angemchakaza kwa masumbwi Rais Donald Trump.

“Wananiuliza ninauwezo wa kufanya mdaharo na Trump, nawajibu hapana. Natamani kama tungekuwa sekondari ningempeleka kwenye eneo la kufanyia mazoezi nimchakaze kwa makonde mazito. Haiwezekani Rais wa nchi awachezee wanawake kwa kuwatomasa halafu aje aombe radhi hadharani heti alifanya makosa, hapa chama cha Republican kilichemsha,“amesema Joe Buddeni kwenye video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook wa chuo hicho.

Joe Biden anatajwa kuwa ndiye atakayekuwa mgombea wa urais mwaka 2020 kupitia tiketi ya chama cha Democratic na atashindana na Rais Trump kama atapita kwenye kura za maoni kwenye uchaguzi huo.

The post Trump atoa onyo kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa Obama appeared first on Zanzibar24.

1 day ago

MwanaHALISI

ACT-Wazalendo waikaba Polisi

MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam imekiruhusu chama cha ACT-Wazalendo kulishtaki Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuzuia ziara za chama hicho. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Kesi hiyo namba 8 ya mwaka 2018 imepangwa kuanza kusikilizwa Aprili 4, mwaka huu mbele ya Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Rehema Sameji, na Jaji Rose Teemba. Chama hicho kimefunga ...

1 day ago

Malunde

VYUO 163 TANZANIA HAVINA SIFA YA KUDAHILI WANAFUNZI KOZI MBALIMBALI


 Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (Nacte) limezuia vyuo 163 kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahada, baada ya kukutwa na upungufu ikiwako kutokuwa na walimu wenye sifa.

Akizungumza leo, Machi 23 na waandishi wa habari, Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Nacte, DK Annastella Sigwejo amesema walifanya uhakiki kwa vyuo 459, kati ya hivyo 296 ndivyo vimekidhi vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa. 

"Kutokana na hali hiyo hivyo ndivyo vinaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili wa Machi na Aprili mwaka huu.”

Amesema licha ya kwamba vyuo vilivyosajiliwa viko 580 waliamua kujiridhisha kwa kuvifanyia uhakiki ambapo walifanikiwa kuhakiki vyuo 459.

Nacte wanawashauri wanafunzi kuhakikisha wanajiridhisha kuwa wanaomba kujiunga kwenye vyuo vilivyokidhi vigezo.

Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Twaha Twaha amesema kuwa majina ya vyuo vilivyoruhusiwa kudahili yamewekwa kwenye tovuti ya Nacte.

"Hivyo Nacte inashauri waombaji wa udahili kujiridhisha kwa kuangalia hiyo orodha iwapo chuo anachokitaka kinaruhusiwa kudahili,"amesema Twaha.
Na Beatrice Moses, Mwananchi

2 days ago

BBCSwahili

Jose Mourinho: Mtu mwenye akili zake anaielewa hali ya Manchester United

Mourinho ameshutumiwa mara kwa mara kutokana na mtindo wake wa uchezaji ambao unadaiwa kutokuwa na ubunifu hata kidogo na pia kutoangazia uchezaji wa kushambulia.

2 days ago

Malunde

TAIFA STARS YATANDIKWA GOLI 4-1 NA ALGERIA


Mechi ya kirafiki iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kati ya Algeria dhidi ya Tanzania imemalizika kwa Algeria kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1.

Mechi hiyo imepigwa usiku huu katika Uwanja wa Mustapha Tchaker huko Blida nchini Algeria.

Mabao ya Algeria katika mchezo huo ambao waliutawala kwa asilimia kubwa, yalifungwa na Baghdad Bounedjah kwenye dakika za 13 na 80, Shomari Kapombe akijifunga kwa kichwa dakika ya 43 na bao la mwisho likifungwa na Carl Medjan (52').

Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva kufuatia kona safi ya Shiza Kichuya mnamo dakika ya 20.

Matokeo hayo yanaleta taswira mbovu kwa Tanzania haswa kuelekea kupanda kwa ubora wa viwango vya soka duniani.

Kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Stars itakuwa ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki, dhidi ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mechi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam, Machi 27 2018.

4 days ago

BBCSwahili

Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya Mwanasoka bora Ureno.

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka bora ya mwaka 2017 nchini Ureno

4 days ago

MwanaHALISI

Yanga sasa kuja kidigitali

KLABU Yanga imezindua kipindi cha televisheni kilichopewa jina la ‘Yanga TV Show’ sambamba na mfumo wa kuwapa habari wanachama wake utakaoitwa ‘Yanga Kidigitali’ vinavyotarajiwa kuanza Aprili Mosi Mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea). Kipindi cha Yanga TV Show kitakuwa kinarushwa kupitia kituo cha televisheni cha Azam TV wakati mfumo wa kutoa habari kwa wanachama ...

4 days ago

BBCSwahili

Jose Mourinho: Mkufunzi wa Manchester United anaonekana kupitwa na wakati - Chris Sutton

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anaonekana kupitwa na wakati na tabia zake zimebadilika , kulingana na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton.

5 days ago

Malunde

HOTUBA YA RAIS WA TFF ALIPOZUNGUMZA NA WAHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO JUMATATU MACHI 19-2018

Naomba nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana mahali hapa siku ya leo tukiwa wazima wa Afya,
Lakini pia nichukuwe nafasi hii kuishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.Joseph Pombe Magufuli kwa ushirikiano mkubwa ninaoupata katika uendeshaji wa mpira wa miguu, nimekuwa karibu sana na Serikali kuhakikisha juhudi zetu za kuendeleza mpira zinafanikiwa kwa kasi kubwa sana na mafanikio ya ujio wa Rais wa FIFA ni kielelezo cha karibuni kuonyesha ushirikiano mkubwa tunaoupata toka kwa Serikali hasa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh.Dr,Harrison Mwakyembe na timu yake.
Lakini niwashukuru kwa nafasi ya kipekee ndugu zangu Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa mnayoifanya kuhabarisha umma kuhusu habari za mpira wa miguu,Pia pongezi zenu kwa kazi nzuri mliyoifanya wakati wa ujio wa FIFA, mlifanya kazi kubwa sana kutangaza ziara ya Rais wa FIFA, mmetupa heshima kubwa sana.
Ndugu zangu, leo nitaongelea mambo makubwa mawili ili waTanzania wapate kufahamu kinachoendelea katika mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini.
Moja nitaongelea kuhusu mambo ambayo tumeyafanya kwa kipindi cha miezi saba nilichokuwepo madarakani lakini la pili ni mambo yanayoendelea sasa hivi kwenye Shirikisho.
MAMBO AMBAYO TUMEYAFANYA KWA MIEZI SABA TOKA TUINGIE MADARAKANI
HALI NA SHUGHULI ZA TAASISIKwa Mazingatio ya Utekelezaji Makini na wa Maendeleo wa Shughuli za Taasisi Tulitambulisha Muelekeo na Dira ya TFF ambapo Kazi iliyo Mbele yetu ni Kuzitoa na Kuimarisha Utambuzi na Utekelezaji wake. Sasa ni wakati Tunajiandaa Kutoa baadhi ya Mipango yetu na kutoa Dira za Utekelezaji wake. Pamoja na Mipango hiyo Bado TFF tumekuwa Tukitekeleza Shughuli za Mpira katika Mgawanyiko wake na labda kwa kifupi kugusia Miongoni mwake.
Mashindano.Tumeendesha mashindano mbalimbali kwa ufanisi mkubwa yakiwemo mashindano ya Azam Sports Federation Cup, Ligi ndogo ya Wanawake kwa ajili ya kupata timu za kupanda daraja,Ligi Kuu ya Wanawake hatua ya makundi na hatua ya nane bora inayoendelea,Mashindano ya soka la ufukweni kwa timu za vyuo vikuu,Mashindano ya  kimataifa ya soka la ufukweni yajulikanayo COPA DAR ES SALAAM.
Azam Sports Federation cup;Mashindano hayo kwa msimu huu 2017/18 tumeyaendesha kwa ufanisi na umakini mkubwa tofauti na huko nyuma kwa kuhakikisha upangaji wa ratiba umekuwa wa wazi usio na upendeleo wowote ule hivyo kupunguza malalamiko,jambo lingine tulihakikisha timu zote zinapata stahiki zao kwa wakati na kiwango kilichopangwa,kadiri tunavyoelekea hatua za mwisho wa mashindano tutahakikisha changamoto zote zilizojitokeza huko nyuma tunakabiliana nazo na kuzitatua ili kuhakikisha mashindano hayo yanaisha vizuri.
Ligi kuu ya Wanawake;Mwaka huu tulianza kucheza Ligi ndogo ya Wanawake kutafuta timu za kupanda Ligi Kuu ya Wanawake katika vituo vya Dar es salaam na Dodoma,ikafuatiwa na Ligi ya Wanawake katika kituo cha Arusha na Dar es Salaam ili kupata Timu 8 za kucheza hatua ya Nane bora ya Ligi hiyo.
Katika hatua ya makundi, TFF ilizigharamia timu zote kwa asilimia 100 kuanzia malazi, usafiri, chakula, gharama za maadalizi ya timu na nauli ya kwenda na kurudi,ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mpira wa miguu wa Wanawake kwa TFF kugharamia kwa kiwango hiki.
Katika hatua ya Nane bora ya  Serengeti Lite Women Premier League vilabu vyote vilishapewa fedha zao kwa ajili ya hatua ya kwanza ambayo imesimama kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) ambayo inajiandaa na mashindano ya kufuzu michuano ya Afrika kwa Wanawake ambapo tayari timu ya Taifa ipo kambini ikijiandaa na mchezo huo dhidi ya Zambia.
Taasisi iliendesha kwa mafanikio makubwa mashindano ya soka la ufukweni (Copa Dar es Salaam) kwa kuzialika timu za Uganda, Malawi, Zanzibar na wenyeji Tanzania bara ambazo tulizigharamia malazi, chakula na usafiri wa ndani.
PROGRAMU ZA TIMU ZA TAIFAToka tumeingia madarakani, tumekuwa tunafanyia kazi program mbalimbali za maendeleo ya Timu za Taifa.
Taifa StarsTumekuwa tukiendelea na program mbalimbali za Timu ya Taifa za kuhakikisha inafuzu Fainali za kombe la mataifa Afrika 2019.
Kuhakikisha hili Taifa Stars ilicheza na Benin, Malawi, Botswana na wiki hii tunacheza na Algeria pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika kalenda ya mechi za kimataifa ya FIFA.
Ili kuongeza hamasa ya wachezaji tumeongeza posho ya ndani kwa asilimia 100 na asilimia 50 kwa posho za nje.
Kilimanjaro StarsTimu yetu ya Tanzania bara ilishiriki mashindano ya CECAFA yaliyofanyika nchini Kenya mwezi Desemba 2017, mbali na kushiriki ili ichukuwe kombe sababu nyingine ilikuwa ni kuendelea kupata mechi nyingi za kimataifa.
Timu ilicheza dhidi ya Rwanda, Kenya, Zanzibar na Libya, Tunaamini kwa wachezaji vijana waliokuwa sehemu ya kikosi hicho imewajengea uwezo katika soka la kimataifa.
Timu za Taifa za VijanaKatika eneo hili  tumekuwa na mpango wa muda mrefu kuhakikisha vijana wa timu zetu za Taifa za miaka chini ya 23, 20, 17 na 13 zinakuwa na maandalizi bora na kwa kuanzia toka tuingie madarakani tumekuwa na kambi za timu za vijana kila mwezi kwa kuwakutanisha siku 14 za mazoezi na kuwatafutia mechi za kirafiki za kimataifa.
Timu ya U23Timu ya Taifa chini ya miaka 23 ambayo ni kikosi cha pili cha timu ya Taifa kimeshaitwa kambini mara kadhaa na tumethibitisha kushiriki mashindano ya Olimpiki ambayo fainali zake zitafanyika nchini  Japan, lengo ikiwa ni kuhakikisha tunawapatia vijana hawa mechi nyingi za kimataifa ili wawe tayari.
Timu ya Vijana U20Timu ya Vijana U20 ambapo jana ilicheza na Morocco na Jumatano itacheza na Msumbiji, ikiwa ni maandalizi ya mechi dhidi ya timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo(DRC) ikiwa ni mchezo wa kufuzu fainali za Vijana Afrika chini ya miaka 20.
Timu ya Vijana U16Timu hii nayo imekuwa ikiingia kambini kila mwezi na hata sasa hivi ninavyozungumza na nyinyi, timu hii ipo kambini ikijiandaa kwa mashindano ya CECAFA na tunafanya jitihada za kuhakikisha inapata mechi mbili za kirafiki za kimataifa kabla haijaenda Burundi.
Timu hii ndiyo ambayo itashiriki fainali za Afrika chini ya miaka 17 zitakazofanyika hapa nchini mwaka 2019.
Baada ya kutoka Burundi itakuwa na program maalum kwa ajili ya kujiandaa kwa mashindano mengine ya kufuzu AFCON U17, 2019 ambayo yatafanyika nchini mwezi Agosti ambayo lengo ni kupata mwakilishi wa CECAFA na vijana wetu watashiriki kama wenyeji. TFF imeamua kushirikisha Timu yenye Umri mdogo zaidi kwa u17 bila ya kujali Matokeo zaidi ya Ujenzi wa timu kwa kuandaa timu moja katika matukio yote haya ili kuiweka tayari kwa Mashindano ya u17 ya 2019 mwakani ambapo vijana hawa ndio watakuwa rasmi u17
Timu ya Vijana ya U13Timu ya Vijana ya U13 katika kutafuta namna ya Kuwaimarisha vijana  hawa baada ya Utambuzi na Uteuzi wa timu imepata nafasi ya  kushiriki mashindano ya kirafiki ya vijana chini ya miaka 13 yatakayofanyika nchini Ubelgiji mwezi Agosti 2018,Tayari orodha ya kwanza ya wachezaji 69  waliopatikana katika mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMITA) ipo TFF na idara ya ufundi inaandaa utaratibu wa kuwaita pamoja na kupata michezo ya kirafiki dhidi ya Zanzibar kwa ajili ya kupata kikosi cha pamoja cha Tanzania.
Timu ya Taifa ya Wanawake U20Tumeanza kuandaa kikosi cha Vijana cha timu ya taifa ya Wanawake U20 ili kuwa na kikosi bora cha Twiga Stars kilichoandaliwa kwa muda mrefu na tayari ilishacheza michuano ya kufuzu fainali za vijana za Afrika chini ya miaka 20 na kutolewa na Nigeria.
Baadhi ya wachezaji wa timu hii wamepandishwa kikosi cha wakubwa na sehemu kubwa wanacheza Ligi Kuu ya Wanawake kupitia vilabu mbalimbali.
Tutaendelea na utaratibu wa kuwaita kambini kila wakati kutakapokuwa na nafasi ili kuzidi kuimarisha kikosi.
Twiga StarsKikosi cha Twiga Stars kimeingia kambini kwaajili ya maandalizi ya mashindano ya kufuzu fainali za Africa kwa Wanawake zitakazofanyika nchini Ghana baadaye mwaka huu.
Twiga Stars inakabiliwa na mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Zambia utakaochezwa Aprili 4,2018 Uwanja wa Taifa na marudiano kuwa Aprili 8,2018 nchini Zambia.
MAPATO NA MATUMIZI
MAPATOKatika kipindi cha miezi Saba(7),Shirikisho limefanikiwa kukusanya kiasi cha Tzs 3,670,397,199.00 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali  ambavyo ni pamoja na mapato kutoka kwa wadhamini Tzs 2,295,472,151 sawa na 62.5%ya mapato yote, makusanyo ya viingilio uwanjani Tzs 378,139,866 sawa na10.3%. 27.2% ilitokana na Fedha kutoka CAF na FIFA.
MATUMIZIKatika kipindi hiki Shirikisho lilitumia kiasi cha Tzs 3,752,001,171.00. Sehemu kubwa ya matumizi yalielekezwa kwenye usimamizi wa ligi mbalimbali pamoja na kuandaa timu za taifa ambapo jumla ya Tzs 2,409,150,732 sawa na 64% ya matumizi yote zilitumika.
Asilimia 36 ya Fedha zilizobaki ilitumika kulipia madeni ya Taasisi, Kulipa mishahara ya wafanyakazi, kusaidia mikoa katika maeneo ya miundo mbinu, kuwajengea uwezo wafanyakazi pamoja na kuendesha mafunzo mbalimbali.
Kama Rais wa TFF sijapokea HOJA wala USHAURI wala MAPENDEKEZO yoyote kutoka kwa Wajumbe wangu katika Ngazi zote kuhusiana na Matumizi ya Taasisi, Nasikitika kama kuna anayedai amehoji sijui wapi kwa kuwa kama Rais sijapokea hoja yoyote wala kuwasilishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji iliyopita ambayo Taarifa ya Kamati ya Fedha iliwasilishwa nakupokelewa na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
MADENIKatika kipindi hiki,Shirikisho lilianza zoezi la kutathmini madeni iliyoyarithi kutoka kwenye Uongozi uliopita, ambapo deni hilo linafikia Tzs 2,172,000,000linalodaiwa na watoa huduma mbalimbali, wafanyakazi,wachezaji na makocha.
Asilimia kubwa ya deni hili lilitokana na malimbikizo ya deni la TRA, Workers Compensation Fund na NSSF ambalo lililimbikizwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Shirikisho lilifanikiwa kulipa deni lote la michango ya wafanyakazi NSSF jumla ya Tzs 88,000,000 zilizokuwa hazijalipwa kipindi cha miaka miwili, na lilifanya majadiliano na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu ulipaji deni la kodi linalofikia Tzs 1,077,000,000, ambapo jumla ya Tzs 315,000,000 zimelipwa nakiasi kilichobaki tumekubaliana kitalipwa kwa awamu kadhaa mpaka deni lote litakapomalizika.
Pia shirikisho limefanikiwa kupunguza mishahara kwa wafanyakazi kutoka Tzs  85,063,092.00 mpaka kufikia 50,000,000.00 baada ya kupunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 44 mpaka 21.
Baada ya kuingia madarakani tulifanya majadiliano na makocha wa timu za Taifa kuhusu uhalisia wa malipo yao na kufanikiwa kuokoa zaidi ya dola laki mbili(USD 200,000) kwenye mikataba yao na fedha zilizookolewa zitasaidia shughuli nyingine za mpira wa miguu.
UFUNDI1. Kliniki iliyoendeshwa na Kocha PiaSundhage kutoka Sweden
2. Kozi ya ngazi ya awali ya makocha wa mpira wa miguu
ilifanyika katika mikoa ya Kigoma,Songwe, Lindi, Morogoro na Pwani
3. Kozi ya ngazi ya kati ya makocha wa mpira wa miguu
  Ilifanyika katika mikoa ya Kigoma mara mbili, Manyara na Morogoro.
4.Grassroot & Live your goal project
Kozi hii ilifanyika katika mikoa ya Lindi ambapo washiriki walitoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
 Pia kozi nyingine ilifanyika katika mkoa wa Mbeya ambapo washiriki walikuwa ni kutoka katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Katavi, Songwe na Rukwa
Aidha hii kozi ilifanyika Kigoma na kushirikisha washiriki wa mikoa ya Kigoma na Tabora.
5.Mafunzo ya awali ya Utawala mikoani
 Kuna kozi ya utawala na masoko iliyofanyika Dar es Salaam ili kuwaongezea watu wa masoko uwezo wa kuwavutia wadhamini.
6.Mafunzo ya waamuzi
  Mafunzo ya waamuzi wa FIFA na Waamuzi wa ngazi ya juu yalifanyika mara tatu jijini Dar es Salaam.
7. Kozi ya kupandisha daraja kwa Waamuzi
Kozi hii ilifanyika mara mbili katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.
8. Ziara za Mafunzo na kubadilishana uzoefu
 Zilifanyika ziara mbalimbali za Waamuzi wetu za kubadilishana uzoefu katika nchi mbalimbali.
9. Mpango wa ugawaji wa vifaa vya vijana na mafunzo
Tulipoingia madarakani tulikuta uongozi uliopita wameshanunua mipira na imekaa stoo, katika kutekeleza azma ya maendeleo ya vijana ili tuwe na timu za Taifa imara Shirikisho limegawa mipira (100 kwa kila Mkoa) saizi 4 na 3 kwa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, Mikoa imepewa vifaa vya kufundishia (cones and markers) ili vijana wapate fursa ya kuonesha na kuendeleza vipaji vyao kwa maslahi ya Mpira hapa nchini.
Uzinduzi wa zoezi hili ambalo linategemewa kuwa endelevu lilifanyika Uwanja wa Taifa Agosti 3, 2017.
Rais wa TFF aliwakabidhi wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa niaba ya Mikoa yao kwenye Kanda husika, Kwa upande wa Zanzibar Katibu Mkuu wa ZFA alikabidhiwa mipira hiyo kwa ajili ya Mikoa ya Zanzibar.
MASOKO NA HABARITumeendelea kuongeza wadhamini katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha Taasisi inanufaika na bidhaa zake.Lakini pia tumeendelea kuimarisha idara ya habari kwa kuwanunulia nyezo za kufanyia kazi.
UTAWALA BORAKatika kipindi hiki cha Miezi saba nimesimamia eneo hili kwa uadilifu mkubwa, Kamati zimekuwa zinakutana kabla ya vikao vya Kamati ya Utendaji ili kuhakikisha kila mmoja anashirikishwa.
Mfano, Wakati nilipokuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha,kwa miaka 4 nilikaa kikao kimoja cha Kamati ya Fedha,Katika Utawala wangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ndani ya miezi saba ameitisha vikao visivyopungua vitano.
Nilimuagiza Kaimu Katibu Mkuu kuhakikisha kila Kamati ya Fedha inapohitaji kukutana ahakikishe inakutana na Mtendaji Mkuu amekuwa anatekeleza.
Na kwa sababu nafasi ya Makamu wa Raisi Kikatiba ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango, basi hata mazungumzo ya Mkataba wa Udhamini wa Ligi Kuu msimu 2018/2019 yeye ndiye aliyekuwa anasimamia.
Nimekuwa nafanya hivi ili Taasisi iendeshwe kwa uwazi na kushirikisha kila mmoja,Na nimeendelea kusisitiza kuwa mapato ya matumizi ya Taasisi yatatolewa kwenye vyombo vya Habari ili yawe wazi kwa umma.
SEKRETARIETI YA TFFToka tuanze kuunda sekretarieti tumeajiri Wakurugenzi Watatu na Meneja mmoja na wote hawa waliajiriwa na Kamati ya Utendaji, Ofisi ya Katibu Mkuu haijawahi kuajiri mfanyakazi hata mmoja kufikia sasa.
Nafasi ambayo haijajazwa ni nafasi ya Katibu Mkuu ambako Ndugu Kidao Wilfred bado anakaimu.
Kwanza nikiri kazi nzuri inayofanywa na mtendaji mkuu aliyekuwepo katika kuhakikisha Taasisi inapiga hatua kwa kasi kila ninapokutana na watendaji wakuu wa FIFA, CAF na CECAFA wamekuwa hawasiti kunimwagia sifa kwa kuwa na sekretarieti mahiri iliyobadilika katika kufanyia kazi changamoto za Taasisi.
Raisi wa FIFA alisema anaona mabadiliko makubwa ya hatua tunazochukuwa, Lakini Katibu Mkuu wa FIFA alisema nina Sekretarieti ya Vijana wenye hali, nguvu na maono ya kuipeleka Taasisi mbele huo ndio ujumbe wao.
Nimeyasema haya kuwahakikishia nikiwa msimamizi wa sekretarieti, mambo yote ambayo Kaimu Katibu Mkuu amekuwa akiyafanya ni maelekezo yangu au utekelezaji wa maamuzi halali ya kamati ya Utendaji, Kwahiyo nichukuwe fursa hii kupongeza kasi ya sekretarieti katika kusimamia mambo mbalimbali.
 AJIRAKatika kipindi changu cha uongozi (Kamati ya Utendaji) kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Mkuu tumeweza kupunguza wafanyakazi kutoka Wafanyakazi 44 tuliowakuta wakati naingia madarakani hadi kufikia 21,Ni hatua kubwa na tunafanya upembuzi makini kabla hatujaanza kuajiri watu tuwe na mahitaji stahiki.
KATIBU MKUUKumekuwa na maneno mengi juu ya nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirikisho, Ndugu zangu wakati naanza kazi niliona ni muhimu nafasi hii ikaimishwe kwa mtu anayelijua shirikisho vizuri na ambaye sina shaka na uwezo wake,Sifa zote hizi alikuwanazo KIDAO WILFRED na wajumbe wa Kamati ya utendaji chombo ambacho kinahusika nakupitisha kilibariki awe Kaimu Katibui MKuu.
Kutoka nje ya Ofisi na kukaimu hii siyo mara ya kwanza,wakati Ndugu Tenga anashinda Uraisi alimuomba Bi.Lina Kessy ambaye alikuwa mtumishi wa Serikali kuwa Mratibu wa Ofisi, nafasi iliyokuwa kama Mkuu wa sekretarieti wakati huo.
Hata wenzetu wa CAF, Rais ndiye anayepeleka jina bila kujali Mchakato utakavyokuwa kwa maana wanaweza wakatangaza au wasitangaze,na hata Katiba ya TFF inahitaji Rais wa TFF atoe mapendekezo ya Katibu Mkuu ili Kamati ya Utendaji ijadili, haya yanafanyika kwa sababu Rais kama msimamizi wa Sekretarieti anafanya kazi kwa karibu sana na Katibu Mkuu hivyo FIFA wanahitaji watu hawa  wawe wanaoweza kufanya kazi kwa karibu sana,ndipo Rais wa TFF anapopewa kipaumbele cha mtu wa kufanya naye kazi kwakuwa ndio nguzo ya Taasisi kwakuwa Rais ndio mkuu wa Taasisi na Katibu Mkuu ndio mkuu wa Sekretarieti.
Lakini pamoja na yote hayo bado nilikuwa napeleka ajenda ya Ajira kwenye Kamati ya Utendaji ili kushauriana njia bora ya kupata Katibu Mkuu kwa maslahi mapana ya Mpira wa Miguu na siyo mtu.
Niwahakikishie kikao kijacho cha kamati ya Utendaji kitaamua njia sahihi ya kupata Katibu Mkuu na tutahakikisha tunakuwa na Katibu Mkuu ndani ya muda mfupi ujao.  
Mipango MbalimbaliTumekuwa katika Ujenzi wa Mipango Mbalimbali kama nilivyoainisha kwenye Ilani yangu ambapo Katibu Mkuu amekuwa Kiungo muhimu katika kunisaidia kwenye Ujenzi wa Mipango yangu hiyo lakini kwa bahati Mbaya Kaimu Katibu Mkuu Kidao amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kuandamwa na Maneno na Vitendo vinavyolenga na kufanikisha kumkwamisha na kumkosesha mazingira bora na rahisi ya kufanyia kazi zake na hivyo imekuwa ni atahri kwa TFF kwa Baadhi ya Mipango yake kuwa inakwama kutoka Mpaka sasa na hiyo ni athari kwa Mpira wetu kwa Ujumla.
Ndugu zangu jambo la pili ambalo nimeona niligusie ni jinsi vyombo vya maamuzi vya TFF vinavyofanya kazi,
Ndugu waandishi, TFF inafanya kazi kwa mujibu wa Katiba yake ya mwaka 2013 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2015. Katiba hii inataja Kamati ya Utendaji itaundwa na Wajumbe wafuatao;
1. Rais
2. Makamu wa Rais
3. Wajumbe 13 kutoka kanda zilizotajwa ibara 32 ya katiba ambazo ni Kanda namba 1-Kagera na Geita
Kanda namba 2- Mara na Mwanza
Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu
Kanda namba 4- Arusha na Manyara
Kanda namba 5- Kigoma na Tabora
Kanda namba 6- Katavi na Rukwa
Kanda namba 7- Mbeya, Iringa na Songwe
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma
Kanda namba 9- Lindi na Mtwara
Kmada namba 10- Dodoma na Singida
Kanda namba 11- Pwani na Morogoro
Kanda namba 12- Kilimanjaro na Tanga
Kanda namba 13- Dar es Salaam
4. Wajumbe wawili wanowakilisha vilabu vya Ligi Kuu
5.Mwenyekiti wa Chama cha Soka ya Wanawake.
6. Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba
7. Wajumbe wawili wa kuteuliwa na Rais wa TFF.
Rais wa TFF amepewa nafasi za kuteua wajumbe wawili wa kamati ya Utendaji ili kumsaidia kufanya kazi na watu ambao wanajua muelekeo wake lakini ambao anaamini watamsaidia kwenye maeneo mbalimbali katika Taasisi.
Kamati ya Utendaji inafanya kazi na vyombo mbalimbali ambavyo ni Kamati ndogondogo, Bodi ya Ligi na Kamati za Kisheria pamoja na Kamati za Uchaguzi.
Kamati Ndogondogo;    Fedha na Mipango    Mashindano(Kamati ya Tuzo na Soka la Ufukweni)    Ufundi na Maendeleo    Vijana    Wanawake    Waamuzi    Katiba, Sheria, na Hadhi za wachezaji.    Tiba    Ukaguzi (ambayo yenyewe ni kama Kamati huru)    Kamati za Kisheria;   Nidhamu    Rufani ya Nidhamu    Maadili    Rufani ya MaadiliKamati za Uchaguzi;    Uchaguzi    Rufani ya UchaguziUfanyaji wa kazi wa Kamati hizi umeelezewa katika Katiba ya TFF kwa maana Kamti za Kisheria zinajitegemea huwa haziingiliwi kwenye maamuzi yake.Ingawa vikao vyake vyote huwa vinaratibiwa na ofisi ya Katibu Mkuu.
Kwahiyo maamuzi ya Kamati hizi huwa ni ya kujitegemea hivyo watu wote ambao wamekuwa wanahukumiwa na Kamati hizi ni vyema wakawa wanajua utaratibu wa Kamati zinavyofanya kazi.Na mimi binafsi nimeendelea kuheshimu Kamati zifanye kazi bila kuingiliwa na mtu yoyote vile.
Ndiyo maana wakati nachaguliwa niliahidi kusimamia Taasisi kwa uadilifu mkubwa bila kumuonea aibu mtu yeyote, wala kumuogopa mtu na hii ni katika kuunga mkono juhudi za Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kupambana na uchafu  wa aina zote katika serikali,Nami nimeamua kusafisha Taasisi kama nilivyoahidi wakati wa Kampeni za uchaguzi ulioniweka madarakani,niseme wazi hakuna mtu asiye muadilifu atabaki katika mpira,Na nimpongeze  Kaimu Katibu Mkuu wangu kwa kusimamia kwa ujasiri mkubwa usimamiaji wa maagizo yote halali ya Kamati mbalimbali,Amekuwa anasimamia bila uoga bila kujali anavyosakamwa kwangu linanipa faraja sana.
Tumekuwa tunachukuwa hatua katika kila eneo tumeshaanza kuchukuwa hatua kwa wizi wa Mapato ya milangoni, kuna viongozi wamefungiwa,hatukuishia hapo tayari viongozi walioghushi leseni za usajili wamefungiwa,Hiyo yote ikiwa ni kuonesha sina masihara hata kidogo kwenye kuhakikisha mpira unakuwa sehemu ya watu waadilifu.
FIFA walituma Timu ya Uchunguzi(Investigation Team) kuangalia yale yote yaliyofanyika toka mwaka 2013 mpaka mwaka 2017,Timu ilikaa nchini kwa takribani wiki mbili ikifanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Katibu Mkuu,Yaliyogundulika yameacha doa kubwa na walitoa Ripoti na Maelekezo ya mambo ya kuyafanyia kazi na ya kuchukulia hatua.
Masharti yote haya yaliambatana na kuzuiwa kwa fedha zetu za miradi nia na wenzetu wachache, Lakini tumekosa pesa zinazoitwa Operation Cost ikiwa ni shinikizo la Dola Milioni Tatu ambazo tulipaswa kulipwa toka mwaka 2015-2018.
Karibia nchi zote Duniani zimenufaika kwa kupata pesa hizi, isipokuwa Tanza kuhakikisha tunatekeleza masharti ya FIFA, Hivyo tulipopata ripoti tumeamua kutekeleza kwa asilimia mia moja maagizo yote ya FIFA. Haya yanayotokea ni Miongoni mwa Matokeo ya Utekelezaji wa Taarifa za Wakaguzi wa TFF na Wakaguzi na Timu ya Uchunguzi kutoka FIFA. Jambo hili limepitia Hatua stahiki kwa Mujibu wa Taratibu zinazohusiana na Taarifa za kiUkaguzi na wahusika wameshirikishwa ipasavyo na Utetezi wao walipeleka kwenye Kamati husika ya Ukaguzi miezi iliyopita baada ya kutakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu.
Niseme tu unaposafisha Taasisi kuna gharama zake TFF inahitaji Kuungwa Mkono zaidi kwa Hatua Madhubuti inazochukua za Kujisafisha na Kusonga Mbele.
Katika VITA hii ya Kupambana na Udhalimu kwenye Mpira wetu Hatutarudi Nyuma, Tutapambana bila hofu wala woga almuradi Hakuna dhulma wala Uonevu wala Upendeleo kwa yeyote. Na Nitoe wito kama kuna Kiongozi au Mdau yoyote anayejua ana Pesa za TFF kinyume cha Utaratibu Natoa WITO Ajisalimishe Mwenyewe.
Ahsanteni kwa kunisikiliza naamini mtaniunga mkono ili kuusogeza mbele Mpira wa Tanzania.
Mwisho niwakumbushe TFF inaendelea na maandaalizi ya Matayarisho wa AFCON U 17,2019 .Timu ya ukaguzi ya CAF itakuja mwezi wa Tano, tumekuwa tunalifanyia kazi kwa ukaribu  na serikali kuhakikisha changamoto za viwanja vitavyochezea mashindano pamoja na viwanja vya mazoezi vinakuwa tayari kwa wakati.Tutaendelea kulitolea ufafanuzi kila wakati.

5 days ago

Michuzi

HOTUBA YA RAIS WA TFF ALIPOZUNGUMZA NA WAHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO LEO JIJINI DAR

UTEKELEZAJI WA TFF KATIKA MAENEO MBALIMBALI
Ndugu Waandishi wa Habari,Sekretarieti ya TFF, Watanzania wote wanaotuangalia na kutusikiliza,mabibi na mabwana habari za asubuhi.
Naomba nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana mahali hapa siku ya leo tukiwa wazima wa Afya,Lakini pia nichukuwe nafasi hii kuishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dr.Joseph Pombe Magufuli kwa ushirikiano mkubwa ninaoupata katika uendeshaji wa mpira wa miguu, nimekuwa karibu sana na Serikali kuhakikisha juhudi zetu za kuendeleza mpira zinafanikiwa kwa kasi kubwa sana na mafanikio ya ujio wa Rais wa FIFA ni kielelezo cha karibuni kuonyesha ushirikiano mkubwa tunaoupata toka kwa Serikali hasa Waziri mwenye dhamana ya michezo Mh.Dr,Harrison Mwakyembe na timu yake.
Lakini niwashukuru kwa nafasi ya kipekee ndugu zangu Waandishi wa Habari kwa kazi kubwa mnayoifanya kuhabarisha umma kuhusu habari za mpira wa miguu,Pia pongezi zenu kwa kazi nzuri mliyoifanya wakati wa ujio wa FIFA, mlifanya kazi kubwa sana kutangaza ziara ya Rais wa FIFA, mmetupa heshima kubwa sana.
Ndugu zangu, leo nitaongelea mambo makubwa mawili ili waTanzania wapate kufahamu kinachoendelea katika mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini.Moja nitaongelea kuhusu mambo ambayo tumeyafanya kwa kipindi cha miezi saba nilichokuwepo madarakani lakini la pili ni mambo yanayoendelea sasa hivi kwenye Shirikisho.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

6 days ago

Michuzi

WAZIRI MKUU ASHUHUDIA MCHEZO WA KIRAFIKI VIJANA WA NGORONGORO HEROES NA MOROCCO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Morocco nchini, Abdelilah Benryane, walipokutana  kushuhudia mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Timu ya Taifa Vijana  walio chini ya Umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes )na Timu ya Morocco. Ambao umefanyika jana kwanye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam March 18, 2018.  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya mashabiki wa Tanzania na Morocco walio kuja kushudia mchezo wa kirafiki wa Kimataifa  wa Timu ya Taifa Vijana  walio chini ya Umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes )na Timu ya Morocco.Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Balaozi wa Morocco Nchini Tanzania ,Abdelilah Benryane . mchezo huo umefanyika jana kwanye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam March 18, 2018.

6 days ago

BBCSwahili

Cristiano Ronaldo afunga hat-trick yake ya 50

Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick yake ya 50 tangu aanze kucheza soka ya kulipwa huku Real Madrid ikiilaza Girona na hivyobasi kupanda hadi nafasi ya tatu katika ligi ya La Liga.

6 days ago

BBCSwahili

Chelsea yaifuata Manchester United Nusu fainali -FA CUP

Michuano ya FA Cup kuelekea hatua ya nusu fainali imepigwa hapo jana kwa michezo miwili

1 week ago

Zanzibar 24

Richard Wambura afunguka baada ya TFF kumpiga stop kwenye soka

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura ambaye jana amefungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka, amesema hukumu hiyo imetolewa bila yeye kuhusishwa wakati alionana na Rais kabla ya maamuzi hayo.

Taarifa ya TFF iliyotolewa jana ilieleza kuwa Wambura alibainika na makosa matatu ya kimaadili ikiwemo kugushi nyaraka za Shirikisho pamoja na kupokea fedha kinyume na taratibu vitendo ambavyo vimetafsiriwa kuwa ni kulishushia hadhi Shirikisho hilo.

Baada ya maamuzi hayo Wambura amejitokeza na kuweka wazi kuwa katika hukumu hiyo hajashirikishwa kwa lolote hata kuitwa kutoa utetezi wake licha ya kukutana na Rais Wallace Karia pamoja na Katibu mkuu siku chache kabla ya kikao cha Kamati ya nidhamu.

Aidha Wambura ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kweli amegushi nyaraka za TFF kwanini jeshi la polisi halijahusishwa kwenye uchunguzi wakati ndio chombo chenye mamlaka ya kuthibitisha hilo.

Wambura pia amefafanua kuwa suala hilo limekuja baada ya yeye kuhoji juu ya uhalali wa nafasi mbalimbali ndani ya shirikisho ikiwemo nafasi ya katibu mkuu ambaye anatakiwa kuajiriwa lakini kwasasa haiko hivyo.

The post Richard Wambura afunguka baada ya TFF kumpiga stop kwenye soka appeared first on Zanzibar24.

1 week ago

Malunde

BAADA YA KUFUNGIWA, WAMBURA AIBUA MAPYA TFF

Ukimwaga mboga, namwaga ugali ni miongoni mwa misemo maarufu ya lugha ya Kiswahili ambao unaweza kutimia baada ya Makamu wa Rais wa TFF kufungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka kufuatia kutiwa hatiani na kamati ya maadili ya TFF.

Baada ya hukumu kutangazwa, Michael Wambura alizungumza na vyombo vya habari akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo lakini amesema kufungiwa kwake ni kwa hila na njama iliyopangwa na watu wachache.

Wambura ameibua hoja kadhaa akiituhumu TFF kuajiri baadhi ya watu bila nafasi hizo kutangazwa kama taratibu na kanuni zinavyoelekea, lakini pia ameituhumu tff kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa muda mfupili lakini hakuna kinachoonekana kufanywa kulingana na kiasi hicho cha pesa.

“Ni kweli kulikuwa na kikao lakini bado nasisitiza kilikuwa cha hila kilikuwa ni kikao ambacho kimeandaliwa kwa ajili ya kutoa maamuzi bila kujali hoja ambazo zitakwenda kujadiliwa. Ninasema hivyo kwa sababu siku ya Jumatatu nilikuwa TFF niliongea na Rais wa TFF pamoja na Katibu, Jumanne niliongea na Rais wa TFF lakini wote hawakuniambia kama kuna jambo lipo TFF linanihusu mpaka Jumanne nasafiri hakuna chochote kutoka TFF kuja kwangu lakini jioni saa 12 wanakwenda nyumbani kwangu kupeleka mashtaka.

“Kwa hiyo tayari kuna hila ambazo nilikuwa nimeziona katika jambo hilo, katika mashtaka yao msingi mkuu umeegemea katika kufoji document hakuna anaebisha walikuwa hawadaiwi, wote wanakiri kudaiwa katika barua mbalimbali za TFF lakini wanasema kwamba document zimefojiwa.

“Kiutaratibu kuna njia mbili, njia moja ni kupeleka polisi wakaangalie kama document imefojiwa baada ya kupata majibu ya polisi mnaelekea katika mkondo washeria ndio msingi wa hizi kamati. Hizi kamati haziwezi kuingia mahali ambapo kosa ni la jinai, ufojaji ni kosa la jinai sio la kimaadili kwa hiyo ilipaswa iende katika mfumo wa sheria ya jinai sio mfumo wa kimaadili.

“Kampuni ambayo wanasema document yake imefojiwa ilipaswa iitwe kwa sababu kampuni inaishi na ina wakurugenzi, kwa hiyo wakurugenzi ndio walipaswa kuitwa ikishajulikana hivyo kinachofuata ni kupelekwa polisi na kushtakiwa kama mhalifu mwingine lakini kwa sababu wameona hawana kesi ya msingi wakaamua kukaa na kamati walizoziunda wenyewe ili wamtoe Wambura katika nafasi kitu ambacho hakikubaliki.

“Kwa hiyo ninachoona yote haya ni kutokana na matatizo yaliyopo ndani ya TFF, jambo la miaka 14 iliyopita unataka kulijadili kwa siku moja kwa kumpa mtu notice usiku asubuhi aje mbele ya kamati, viongozi walikuwepo wengi wamepita hapo katikati wote walitakiwa waje kutoa ushahidi lakini hawakuitwa? Kwa nini walilipa? Au aliyelipwa alivunja ofisi?

“Isije ikawa kuna mtu amejilipa ndani ya TFF kwa jina la ile kampuni na kitu ambacho kipo, kuna watu wamelipwa pesa kwa kutumia jina la hiyo kampuni wakati hizo pesa hazijalipwa kwa kampuni ndiyo maana wanashindwa kutoa hizo document ndiyo maana tunasema walete nyaraka za hayo malipo kama hawajaiba wao wenyewe wanashindwa.

“Kama wanasema nimefoji barua nipo tayari twende polisi na mahakamani ndio maana nasema hili jambo limetengenezwa kimkakati halina mashiko hata kidogo ya kisheria, halina ushahidi ni jambo la uongo na kizandiki limetengenezwa na kikundi cha watu ambao wanaamini nikitoka kama mwenyekiti wa fedha mambo yao yatakuwa mazuri.

“Mimi nimechaguliwa na mkutano mkuu kwa zaidi ya kura asilimia 80, siwezi kuondolewa na watu watatu ambao hawakuchaguliwa hawana dhamana ya mkutano mkuu, haiwezekani. Kama unadhani nina kosa kanishtaki kule.

“Ni kweli kwamba kila uongozi unapokuja unakuwa na taratibu zake , sisi taratibu zetu za kiutendaji ni kwamba, nafasi ya katibu mkuu wa TFF lazima itangazwe kama makatibu wakuu wengine walivyopita, nafasi inatangzwa watanzania wenye sifa wanaomba kupitia makampuni ambayo ni huru, wanafanya usaili wanaajiriwa.

“Sisi pale kwetu kuna shida kidogo kuna watu wengine bado wana kazi mbili, kuna mtu mwinngine ameajiriwa huku anakuja pale kama secondment wakati kuna watanzania wengi wanaweza kuomba na kuajiriwa, sasa mtu ana kazi mbili.

“Suala la katibu mkuu anapaswa kuajiriwa, tulipochaguliwa kaimu katibu mkuu alikuwa Salum Madadi kwa sababu madadi alikuwa majiriwa wa TFF kwa hiyo alikuwa anakaimu nafasi kwa sababu alikuwa mwajiriwa wa TFF baadaye tulipokuja kumpa nafasi Wilfred Kidao yalikuwa ni makosa kwa sababu sheria zinakataza mjumbe wa mkutano mkuu kuajiriwa TFF na kidao ni mwenyekiti wa TAFCA hawezi kuajiriwa akawa mjumbe wa mkutano mkuu wakati huohuo.

“Tuna matatizo mengi, TRA wanatudai lakini bado tunakusanya kodi na tunazitumia, tunamatatizo ya fedha za wafadhili tunazihamisha matokeo yake ligi ya wanawake inasimama, wakati mwingine hata ligi kuu inasimama kwa sababu hakuna pesa lakini Azam wamelipa kwa hiyo tuna shida.

“Tunaposema tunataka tuweke nyumba kwenye mstari masuala ya kodi yaeleweke kodi zinazopokelewa na bodi zikalipwe TRA badala ya kuletwa TFF ndio mgogoro unapotokea. Bodi ya ligi ina kusanya kodi toka Azam, na wadhamini mbalimbali lakini kodi zile zinakuja kwetu TFF zikishakuja na kutumika mwenyekiti wa kamati ya fedha akisema hapana sio sahihi inakuwa issue.

“Matatizo mengi tutakuja kuyaona siku chache zijazo, watanzania watanielewa kwamba ndani ya TFF kuna matatizo makubwa sana na sio madogo kama watu wanavyofikiria, siku chache zijazo tutakuja kuyazungumza.

“Tumeshatumia kiasi cha shilingi 3 bilioni ndani ya miezi nane, kuna nini tumefanya? Zinapita tu. Jambo moja linapoanza uzuri wake linafuata na jingine kwa hiyo tutakwenda mpaka mahali tutakuwa sawa na ninaamini watafuata ninachokisema, bado tunahitaji kusafisha TFF kwa sababu haiko sawa.”

1 week ago

BBCSwahili

Europa League: Arsene Wenger hataki Arsenal wapangwe kukutana na Atletico Madrid

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Danny Welbeck (mawili) na Granit Xhaka naye Hakan Calhanoglu akawafungia Milan bao la kufutia machozi Alhamisi.

1 week ago

BBCSwahili

Welbeck asaidia Arsenal kulaza AC Milan 3-1 Europa League

Danny Welbeck alifunga mabao mawili Alhamisi na kuwawezesha Arsenal kuwalaza miamba wa Italia AC Milan 3-1 na kufuzu kwa robofainali katika ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

1 week ago

Zanzibar 24

TFF yampiga marufuku Michael Wambura kujihusisha na soka maisha yake

Habari za ndani zinasema Kamati ya Maadili ya TFF imemfungia makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura kutojihusisha na soka maisha yake yote.

Sekretariati ya Shirikisho la soka Tanzania TFF ilimfikisha Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kwenye kamati ya maadili akikabiliwa na tuhuma tatu ikiwemo kupokea fedha za malipo TFF za malipo ambayo hayakuwa halali.

Jana mchana afisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Wambura amefanya makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na katiba ya TFF.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TFF, baada ya kamati ya maadili kupokea malalamiko yanayomhusu Wambura na kukutana jana (Machi 14, 0218) kwa ajili ya kujadili, imemfungia maisha Wambura kujihusisha na masuala ya soka.

Kwa mujibu wa afisa habari wa TFF Clifford Ndimbo, Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo, kutuma kwa maandishi au kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya uwakilishi. Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa ajili ya kumtetea.

Emmanuel Muga amesema hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake kwa sababu kamati ilikuwa na dhamira yake ya kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo (jana Machi 14, 2018).

 

“Ni kweli sikupewa nafasi ya kumtetea kwa sababu kamati ilikuja ikiwa na dhamira yake kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo. Kwa hiyo nilivyowasilisha masuala ya kisheria ambayo ni ya kikanuni, kamati ilikataa ikasema sisi tunaamua tunavyoona” Emanuel Muga, Wakili wa Wambura.

“Kwa hiyo wakalifunga suala kwamba yanaenda kufanywa maamuzi, lakini hayo maamuzi yatafanyika wakati Wambura hajasikilizwa na Wakili wake hajasikilizwa.”

The post TFF yampiga marufuku Michael Wambura kujihusisha na soka maisha yake appeared first on Zanzibar24.

1 week ago

Zanzibar 24

Kamati ya maadili ya TFF yampiga stop Michael Wambura.

Kamati ya maadili ya TFF, imemfungia kifungo cha maisha kutojihusisha na shughuli za soka Makamu Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Michael Wambura.

Wambura amekutana na adhabu hiyo nzito kutokana na kupokea fedha zisizo halali kiasi cha shilingi milioni 84 na makosa mengine matatu.

Makosa hayo mengine matatu aliyokutwa nayo Wambura, ni kugushi nyaraka za malipo ya fedha, na kula njama kulipwa fedha na waliokua viongozi wa TFF Malinzi na Mwesigwa.

Kamati hiyo ya maadili imefikia maamuzi hayo kwenye kikao chao walichokutana jana (Jumatano).

The post Kamati ya maadili ya TFF yampiga stop Michael Wambura. appeared first on Zanzibar24.

1 week ago

Michuzi

SEKRETARIETI YA TFF YAMPELEKA MICHAEL WAMBURA KAMATI YA MAADILI

KAMATI ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF inakutana leo Jumatano Machi 14,2018 pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala la Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura aliyefikishwa kwenye kamati hiyo kwa masuala ya kimaadili.
Shauri hilo la Wambura limefikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.
Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomuhusu Wambura ikiwa ni uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa mwaka 2015.
Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili baadaye leo na ana hiyari ya kufika kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo,kutuma kwa maandishi,kuleta mashahidi au kutuma muwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi.
Makosa anayoshtakiwa Wambura ni1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013
2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)

AMMY NINJE KOCHA NGORONGORO HEROESKOCHA Ammy Ninje ameteuliwa kuwa Kocha wa muda wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes)
Ninje atakiongoza kikosi hicho kwakuwa Kim Poulsen na Oscar Mirambo wamebaki na majukumu na kikosi cha Timu ya Taifa chini ya miaka 16 Serengeti Boys kinachojiandaa na mashindano ya Cecafa yatakayoanza Aprili 1-15,2018 nchini Burundi.
Kocha Ninje atakiongoza kikosi cha Ngorongoro Heroes kuanzia kwenye mechi zake za Kirafiki za Kimataifa dhidi ya Morocco Machi 17,2018,dhidi ya Msumbuji Machi 21,2018 na mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Vijana chini ya miaka 20 dhidi ya DR Congo zote zikichezwa Uwanja wa Taifa.
Mshindi kati ya Tanzania na DR Congo atakwenda kucheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa mwezi Mei.
Awali Ninje alikuwa kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya wakubwa Taifa Stars ambapo pia alikuwa kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyofanyika nchini Kenya.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF.

1 week ago

Zanzibar 24

Kiongozi wa TFF akumbwa na tuhuma nzito

Makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Michael Richard Wambura, ameingia matatani kwa tuhuma za kupokea pesa kinyume na taratibu za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine ya kinidhamu.

Wambura amefikishwa mbele ya Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF ambayo inakutana leo Jumatano Machi 14, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala lake.

Makosa matatu ya Wambura yatakayojadiliwa na kamati leo ni kupokea fedha za shirikisho malipo yasiyo halali, kughushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.

Wambura ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye soka la Tanzania ikiwemo klabu ya Simba na Chama cha soka mkoa wa Mara, alichaguliwa kuwa makamu wa Rais kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Dodoma mwaka jana.

The post Kiongozi wa TFF akumbwa na tuhuma nzito appeared first on Zanzibar24.

2 weeks ago

Michuzi

Kumbilamoto afunga michezo ya mpira wa pete ya mkoa wa Dar es Salaam

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Vingunguti ambayo imeingia fainali katika michezo ya mpira wa pete ya mkoa wa Dar es Salaam iliyoratibiwa na (CHANEDA) kwa ajili ya kupata timu wawakilishi wa mkoa huu.  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua Timu ya Mpira wa pete ya Mbagala ambapo timu hiyo nayo ilifika hatua ya fainali kwa ajili ya kupata mshinddi atakaye wakilisha Mkoa wa Dar es Salaam katika Mashindano ya Afrika Mashariki.  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na Timu zote mbili kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali kw atimu zilizoshiriki ligi ya mkoa wa Dar es Salaam Timu za Mchezo wa mpira wa Pete kwa wanaume zikimenyana wakati wa mchezo wa fainali ya mkoa wa Dar es SalaamMashabiki wakifatilia michezo fainali ya mpira wa pete wa Wanaume kwa mkoa wa Dar es Salaam.

(Today) 55 minutes ago

Michuzi

Mkurugenzi SBL afanya mazungumzo na maofisa Idara ya Uhamiaji

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

“Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie

SBL imeajiri...

(Today) 55 minutes ago

Bongo Movies

Ebitoke Afunguka Mapya Kuhusu Mahusianao yake na Ben Pol

Msanii wa vichekesho bongo ambaye inasemekana yupo kwenye mahusiano na msanii Ben Pol, amesema kipindi mahusiano yao yalipoonekana yamekufa, ukweli ni kwamba penzi hilo halikufa isipokuwa Ben Pol alimtuliza ili asiyaweke sana kwenye mitandao.

Akizungumza na mwandishi wa EATV.TV, Ebitoke amesema baada ya kulalamika kuwa Ben Pol hapokei simu zake na hamjali, Ben Pol alimuomba yaishe na aache kuyaweka kwenye mitandao na vyombo vya habari, kwani ni jambo ambalo sio zuri sana kwao.

“Watu...

(Yesterday)

Michuzi

TUKUTANE COVENTRY JUMAMOSI TAREHE 05/05/2018, MKUTANO MKUU WA PILI (AGM – 2018) – JUMUIYA YA WATANZANIA UK NA IRELAND KASKAZINI.


Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania UK na Northern Ireland inapenda kuwatangazia Wanachama wake na Watanzania wote wanaoishi nchini Uingereza, Wales, Scotland na Ireland ya Kaskazini (Ireland)kuwa Mkutano Mkuu wa Pili (AGM – 2018) Utafanyika katika Jiji la Coventry hapa nchini UingerezaAnuani – ST. MARY & ST BENNEDICT                 52A RAGLAN STREET                 COVENTRY –  CV1 5QFKuanzia saa tano asubuhi hadi saa kumi na moja Jioni, Ajenda kuu kubuni mikakati Zaidi kwa maendeleo ya...

(Yesterday)

VOASwahili

Mamilioni waandamana kutaka udhibiti wa bunduki Marekani

Mamilioni ya watuwaliandamana katika miji mbalimbali ulimwenguni kote siku ya Jumamosi kushinikiza mageuzi katika sheria zinzohusu umiliki wa bunduki.

(Yesterday)

BBC

Cricketer charged with ball-tampering

Australia's Cameron Bancroft admits he tampered with the ball against South Africa - and captain Steve Smith says he knew in advance.

(Yesterday)

Michuzi

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA ‘TERMINAL III’ DAR ES SALAAM


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya...

(Yesterday)

Michuzi

WAZIRI MKUU AWATAKA VIJANA WAFANYE KAZI KWA BIDII NA MAARIFA

*Asisitiza kwamba kazi ndiyo msingi wa maendeleo 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wafanye kazi kwa bidii na maarifa kwa sababu kazi ndiyo msingi wa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Pia amewasihi wananchi wanaoishi katika maeneo ya mipakani wahakikishe suala la kulinda mipaka hiyo linapewa kipaumbele ili kuimarisha amani na utulivu nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wananchi alipowasili katika uwanja wa ndege wa...

(Yesterday)

Michuzi

TCCIA NA AZANIA BANK ZAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA DAR ES SALAAM

 Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, akitoa mada katika mkutano huo. Wadau. Kaimu Meneja Huduma na Uwezeshaji Brella, Bosco Gadi, akitoa mada katika mkutano huo.Mwakilishi kutoka UWURA, Mr. Keneth akitoa mada. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group Ltd, Ali Mfuruki akizungumza katika mkutano huo.

 Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja, akizungumza katika mkutano huo. Maofisa wa Benki ya Azania wakiwa wamepozi kwa picha kabla ya kuanza kwa mkutano...

(Yesterday)

MwanaHALISI

Mipango ya Jaji Mutungi, Lipumba kumng’oa Maalimu Seif yafichuka

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa Msajili wa vyama siasa nchini Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi yake Profesa Ibrahimu Lipumba wamepanga njama ya kukisambatisha chama hiko pamoja na kumfukuza Katibu mkuu huyo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Maalimu Seif ameyasema hayo leo alipokutana na wanachama ...

(Yesterday)

Update Kenya (Blog)

How Raila recued Jirongo from poverty in 2017


Update Kenya (blog)
How Raila recued Jirongo from poverty in 2017
Update Kenya (blog)
Former Presidential candidate Cyrus Jirongo has revealed that NASA leader Raila Odinga helped him secure a job in Tanzania. According to Jirongo, he was abandoned by top Jubilee leadership and Raila is the one that came to his rescue. Jirongo said that ...

and more »

(Yesterday)

Michuzi

WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA

Na Mwandishi MaalumJumla wa wagonjwa wa akili 55 waliokuwa  wametenda makosa mbalimbali yakiwamo ya jinai wakiwa na  ugonjwa wa akili, wameachiwa huru baada ya mahakama kutowatia hatiani.Hayo yameelezwa leo  mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi ( Mb) wakati alipokuwa akiwasilisha  Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara Katiba na Sheria na Taasisi zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.  Kamati hiyo ilikuwa nchini ya ...

(Yesterday)

Michuzi

UBALOZI WA KUWAIT NA TAASISI YA DORIS MOLLEL WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WATOTO NJITI, HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA, DODOMA

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaseem Al Najem (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika, sehemu ya vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti, vilivyotolewa na Ubalozi wa Kuwait kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki, mjini Dodoma. Wengine pichani ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi...

(Yesterday)

Citizen TV (Press Release)

Jirongo urges support for Raila-Uhuru unity deal


Citizen TV (press release)
Jirongo urges support for Raila-Uhuru unity deal
Citizen TV (press release)
According to him, those from Western Kenya can now look forward to better services from the national government. He applauded Raila Odinga for accepting to meet president Kenyatta saying the move will give the country a chance to have an all-inclusive ...
How Raila recued Jirongo from poverty in 2017Update Kenya (blog)

all 4 news articles »

(Yesterday)

BBCSwahili

Umoja na amani ya Tanzania viko hatarini;Maaskofu wa kilutheri waonya

Maaskofu wa KKKT waorodhesha mambo yanayohatarisha

(Yesterday)

Malunde

FISSOO : TANZANIA NI YA PILI BARANI AFRIKA KWA UZALISHAJI WA FILAMU


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo amewataka Watanzania kutumia vizuri fursa za masoko ya filamu kwa ajili ya kujiingizia kipato kwa sababu Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa filamu barani Afrika ikitanguliwa na Nigeria.

Akizungumza Machi 23,2018 wakati wa uzinduzi wa Filamu ya "Laana ya Mke" katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema  ni lazima waigizaji watumie fursa zinazotengenezwa na...

(Yesterday)

BBC

Moses earns Nigeria victory as Morocco and Tunisia also win

Chelsea winger Victor Moses earns Nigeria a win as Morocco and Tunisia also win their World Cup warm-up matches.

(Yesterday)

CBS Minnesota / WCCO

Despite Threats Facing Our World, Chimp Expert Jane Goodall Sees Hope


CBS Minnesota / WCCO
Despite Threats Facing Our World, Chimp Expert Jane Goodall Sees Hope
CBS Minnesota / WCCO
The world's leading expert on chimpanzees and a proponent of conservation is in Minnesota this weekend. The 83-year-old spoke to a full house on the University of Minnesota campus Friday night as part of her spring lecture tour. She began with her ...

and more »

(Yesterday)

Michuzi

MAADHIMISHO YA SIKU YA USONJI KUFANYIKA KESHO

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Wazazi wanapaswa kuwapa nguvu, moyo na kupata haki ya elimu kwani wao pia wanauwezo wa kufanya kazi mbalimbali katika jamii  hivyo katika matembezi hayo yatasaidia kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye Usonji(Autism) kuonekana wanaweza na wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi  wa shule za Almuntazir Mohammad Ladack amesema lengo  la maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye Usonji...

(Yesterday)

VOASwahili

Fatma Karume apata ridhaa ya Tundu Lissu

Uchaguzi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) wa nafasi ya urais unatarajiwa kufanyika April 14, 2018, na wakili wa kujitegemea Fatma Karume amesema Jumamosi ana baraka zote za Rais wa chama hicho Tundu Lissu.

(Yesterday)

Malunde

NAPE NNAUYE AKUMBUSHIA ALIVYONUSURIKA KUPIGWA RISASI


 Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amezungumzia tukio la kutishiwa bastola wakati akitaka kuzungumza na waandishi wa habari nje ya Hoteli ya Protea lililotokea baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Nape amekumbushia tukio hilo la Machi 23, 2017 na kuandika, “mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo Mwenyezi Mungu aliniokoa na mdomo wa bunduki wa wanyama wasiopenda haki! Mungu mkubwa, mbegu ya haki haifi.”

Katika...

Mpenzi wako akikuonyesha visa vya kukuchoka nawe bado unampenda,je, utaendelea kumganda au...

Mpenzi wako akikuonyesha visa vya kukuchoka nawe bado unampenda,je, utaendelea kumganda au utamuacha aende zake!? Toa maoni yako

 

Tazama Video yangu mpya “ANAWEZA” bonyeza link hiyo hapo...

Tazama Video yangu mpya “ANAWEZA” bonyeza link hiyo hapo 👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽👇🏽 👉🏽https://youtu.be/RBeBx890Xpg Pia Subscribe kwenye YouTube channel ya Lady Jaydee kuona nyingine nyingi #Anaweza

 

LIVE: PEKENYO LA HABARI SUBSCRIBE | Masanja TV | For more Gospel Updates:...

LIVE: PEKENYO LA HABARI SUBSCRIBE | Masanja TV | For more Gospel Updates: 👇 👇 https://www.youtube.com/channel/UCmKRCC5AXn1Hb0ClJx8iZ2w?sub_confirmation=1

 

(Yesterday)

Michuzi

TCCIA NA AZANIA BANK ZAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA DAR ES SALAAM

 Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, akitoa mada katika mkutano huo. Wadau. Kaimu Meneja Huduma na Uwezeshaji Brella, Bosco Gadi, akitoa mada katika mkutano huo.Mwakilishi kutoka UWURA, Mr. Keneth akitoa mada. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Infotech Investment Group Ltd, Ali Mfuruki akizungumza katika mkutano huo.

 Rais wa TCCIA, Ndibalema Mayanja, akizungumza katika mkutano huo. Maofisa wa Benki ya Azania wakiwa wamepozi kwa picha kabla ya kuanza kwa mkutano uliondaliwa na TCCIA kwa ajili ya wafanyabiashara kuchangamkia fursa zilizopo katika uwekezaji.  Mkutano huo ulidhaminiwa na benki hiyo. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


2 days ago

CCM Blog

MPANGO WA PAMOJA WA TANZANIA NA CHINA KATIKA KUONGEZA UZALISHAJI WA TIJA WA ZAO LA MAHINDI MKOANI MOROGORO WAZINDULIWA

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin, akimuonyesha Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, moja ya picha katika Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini, katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji hicho. Mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro na Chuo hicho Kikuu cha Kilimo cha China. Nyuma yao ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro.
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, akisalimiana na Profesa Wu Jiu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji  cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.  
 Wasanii akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi,  jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.
 Balozi wa Tanzania hapa nchini Wang Ke akisaini kitabu ca wageni alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba moani Morogoro. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa mkoa huo Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe (mwenye gauni la bluu) na Regina Chonjo wakiselebuka muziki na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho mkoani Morogoro. 
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
 Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. 
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.
 Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho cha Mtego wa Simba.
 Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akipongezwa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo baada ya hotuba yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya gairo Siriel Mchembe  
 Benjamin Amos akizungumza wati wa uzinduzi wa kwanza wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China. uzinduzi huo ulienda pamoja na uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.
 Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China waakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya uzinduzi wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo hicho
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo na Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (kulia) wakijiandaa kufungua mabango yenye maelezo, wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke wakifurahi baada ya kufanya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakionyeshana bango lenye maelezo baada ya kuzindua jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.
Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Cha China na Viongozi wa mkoani Morogoro baada ya uzinduzi wa Mradi wa pamoja  wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

2 days ago

BBCSwahili

Trump kuiongezea ushuru wa forodha China

Rais Donald Trump ametangaza mpango wa wa ongezeko la ushuru wa forodha kwa bidhaa za China,hali hiyo inatarajiwa kuongeza vita vya vikali vya kibiashara

2 days ago

Michuzi

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAO, YASEMA HAKUNA TATIZO KATIKA LUKU

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco)limekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii  inayodai kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia Machi 25 hadi Aprili 5 mwaka huu.
Taarifa hiyo ya kutunga inadai kutokana na hali hiyo wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.
Tanesco kupitia Ofisi ya Uhusiano imesema taarifa hizo si za kweli na uzushi wenye nia ya kupotosha umma kwani haijatokea taarifa yoyote kuhusu hitilafu katika mifumo ya manunuzi ya LUKU.
"Ikumbukwe kwamba taarifa kutoka Tanesco hazitolewi na mtu binafsi bali ofisi ya uhusiano iliyo chini idara ya Mkurugenzi Mtendaji ambayo ni msimamizi wa utoaji taarifa za shirika hili,"imesema taarifa ya Tanesco.
Imewaomba wateja wote wa Tanesco waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote ."Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida."

2 days ago

Michuzi

MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI DAR WAHOJI KUHUSU FEDHA ZINAZOTOLEWA NA KARIAKOO


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
BARAZA la Madiwani wa Jiji la  Dar es Salaam limeomba kufahamu kiasi cha fedha kinachopatikana katika Soko la Kariakoo maana wamechoshwa na kauli ya kwamba soko hilo linaendeshwa kwa hasara.
Baadhi ya madiwani hao wamekiambia kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji hilo leo jijini Dar es Salaam wamesema Jiji linamiliki soko kwa asilimia 51.Diwani wa Kata ya Mbezi Humphrey Sambo amekiomba kikao hicho kupata taarifa za mapato ya soko hilo kwani kwa mtazamo wa kawaida wamedai fedha inayopatikana ni nyingi lakini wao wanaambiwa linaendeshwa kwa hasara.
"Tufuatilie ili kujua nini ambacho kinaendelea katika Soko la Kariakoo kwani nimechoka kusikia kila siku wanapata hasara lakini watu wanakwenda kazini," amesema.Amefafanua kwa kuwa Jiji linahisa ya asilimia 51 ni vema ikajulikana kinachopatikana na mgao wa Jiji ni kiasi gani.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Tabata Patrick Asenga amesema soko la Kariakoo si kweli linapata hasara kwani hata vizimba vya biashara vilivyopo kodi yake ni Sh.300,000 hadi Sh.400,000.Amesema ni vema Jiji likatoa kauli ya kuwaita wanaosimamia soko hilo ili waeleze kuhusu soko hilo na kwamba hakubaliani na kauli ya soko kuendeshwa kwa hasara.
Kutokana na maelezo hayo ya madiwani,Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amemuomba Mkurugenzi wa Jiji hilo kuyafanyia kazi na kwenye kikao kijacho majibu yatolewe."Mkurugenzi wa Jiji naomba ukae na menejimenti yao  kushughulikia suala hili kwanza na  na menejimenti yake na baada ya hapo taarifa itolewe," amesema.Mstahki Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiongoza kikao cha robo ya pili ya baraza la madiwani leo, kushoto ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana.

3 days ago

BBCSwahili

Trump atarajiwa kutangaza vikwazo dhidi ya China baada ya uchunguzi

The White House says its investigation finds that China encourages the theft or transfer of intellectual property.

3 days ago

AllAfrica.Com

21 Mar

East Africa: World Bank Report Says Climate Change to Hit East Africa Hard


East Africa: World Bank Report Says Climate Change to Hit East Africa Hard
AllAfrica.com
Climate change across East Africa could see more than 10 million people forced to move by 2050, according to a new World Bank report. The hardest hit could be the coastal regions of Kenya and Tanzania, but the report says that any areas suffering from ...

and more »

5 days ago

Michuzi

MWAKILISHI BENKI YA DUNIA AFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI MKUU,ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MRADI MABORESHO WA HUDUMA ZA KIMAHAKAMA

Na Mary Gwera, Mahakama
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Nicola Smithers ameipongeza Mahakama kwa utekelezaji wake wa Mradi wa Maboresho wa huduma za Kimahakama.
Bi. Smithers aliyasema hayo mapema Machi 19, alipokutana na Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam ambapo alipata nafasi ya kuongea na Mhe. Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama akiwemo Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
“Nimefurahishwa na maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya huduma za Mahakama unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, hususani katika eneo la uondoshaji wa mlundikano wa mashauri,” alisema Bi. Smithers
Akimkaribisha ofisini kwake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahimu Juma alimueleza Bi. Smithers juu ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama ya Tanzania yote yakiwalenga wananchi ambao ndio wateja wa Mahakama.
“Miongoni mwa maeneo ambayo tunayoendelea kupambana nayo ili kurejesha imani ya wananchi kwa Mahakama ni pamoja na Rushwa, katika hili tmefanya jitihada kadhaa ikiwa ni pamoja na kusambaza mabango ‘posters’ yenye ujumbe wa kupinga rushwa na kuyasambaza katika ofisi za Mahakama kote nchini pamoja na kusambaza simu za kuwawezesha wananchi wenye malalamiko kutuma meseji ili malalamiko yao yaweze kufanyiwa kazi,” alieleza Mhe. Jaji Mkuu.Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Nicola Smithers akisaini Kitabu cha Wageni pindi alipowasili ofisini kwa Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahimu Juma akiongea jambo na Mgeni wake Bi. Nicola Smithers ambaye ni Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB).Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga (wa pili kushoto) akichangia jambo katika Mazungumzo hayo, wa kwanza kushoto ni Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati, wa pili kulia ni Meneja kutoka Benki ya Dunia-Tanzania, Bw. Dennis Biseko.Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati (wa kwanza kushoto) akichangia jamboMeneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Nicola Smithers akizungumza jambo.Mkuu wa Kitengo cha Maboresho-Mahakama, Mhe. Zahra Maruma akiwa katika mazungumzo hayo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

5 days ago

Malunde

TIGO TANZANIA NA UBER WAUNGANA KULETA OFA MPYA, MURUA KWA WATEJA WA DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akipeana mikono na Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado mara baada ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo na kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana. ***
Dar es Salaam, 19 Machi, 2018. Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeingia katika makubaliano ya kipekee na kampuni ya kiteknologia ya Uber. Kuanzia leo, wateja wote wa Tigo watatumia huduma za Uber App bure! Makubaliano haya ya aina yake yatawafaidi watumiaji wa huduma za usafiri za Uber pamoja na madereva waliojiunga na mfumo huo. 

“Tigo ni nembo pana ya biashara katika soko la Tanzania na tuna wajibu wa kuzindua njia bora zaidi kwa wateja kujumuika katika maisha yanayowazingira. Makubaliano haya na Uber yanaboresha bidhaa na huduma ambazo wateja wetu wanafurahia katika maisha yao ya kila siku,” Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema. 
Naye Alfred Msemo, Mkurugenzi wa Uber alisema, “Tunafurahia makubaliano haya na Tigo yatakayowawezesha watumiaji na madereva wa huduma za Uber waliojisajili na mtandao wa Tigo kutumia huduma ya Uber App bure kwenye simu zao za mkononi bila tozo lolote la gharama za data. Uber ni mfumo wa simu za kisasa unaowezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kubonyeza kitufe tu! Lengo kuu la Uber ni kuwezesha usafiri salama, wa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kila mtu, kila sehemu. Makubaliano haya yatawahamasisha maelfu ya wakaazi wa Dar es Salaam ambao wamejisajili na mtandao wa Tigo kutumia Uber App kwa ajili ya huduma za usafiri jijini Dar es Salaam,’ Msemo alibainisha. 

5 days ago

Michuzi

TIGO TANZANIA NA UBER WAUNGANA KULETA OFA MPYA KWA WATEJA WA DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari(wa pili kushoto) akipeana mikono na Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado(wa pili kulia) mara baada ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo na kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeingia katika makubaliano ya kipekee na kampuni ya kiteknologia ya Uber. Kuanzia leo, wateja wote wa Tigo watatumia huduma za Uber App bure! Makubaliano haya ya aina yake yatawafaidi watumiaji wa huduma za usafiri za Uber pamoja na madereva waliojiunga na mfumo huo. 

“Tigo ni nembo pana ya biashara katika soko la Tanzania na tuna wajibu wa kuzindua njia bora zaidi kwa wateja kujumuika katika maisha yanayowazingira. Makubaliano haya na Uber yanaboresha bidhaa na huduma ambazo wateja wetu wanafurahia katika maisha yao ya kila siku,” Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema. Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza katika hafla ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure, iliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo, Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado pamoja na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed.

Naye Alfred Msemo, Mkurugenzi wa Uber alisema, “Tunafurahia makubaliano haya na Tigo yatakayowawezesha watumiaji na madereva wa huduma za Uber waliojisajili na mtandao wa Tigo kutumia huduma ya Uber App bure kwenye simu zao za mkononi bila tozo lolote la gharama za data. 

Uber ni mfumo wa simu za kisasa unaowezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kubonyeza kitufe tu! Lengo kuu la Uber ni kuwezesha usafiri salama, wa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kila mtu, kila sehemu. Makubaliano haya yatawahamasisha maelfu ya wakaazi wa Dar es Salaam ambao wamejisajili na mtandao wa Tigo kutumia Uber App kwa ajili ya huduma za usafiri jijini Dar es Salaam,’ Msemo alibainisha. Kampuni hizi mbili zitashirikiana katika bidhaa na promosheni zitakazoboresha huduma kwa wateja wa sasa na wa siku zijazo. Tigo na Uber nchini Tanzania wanatarajia kutangaza ofa zaidi kabambe zitakazowawezesha wateja kufurahia huduma za Uber jijini Dar es Salaam ambapo huduma za Uber zinapatikana kwa sasa. 

1 week ago

Michuzi

BENKI YA CRDB YAJITOSA KUKISAIDIA CHAMA CHA MAAFISA HABARI,MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI (TAGCO)

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .
BENKI ya CRDB imeahidi kuendelea kukisaidia Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikali na kwamba kufanya hivyo kutasaidia upatikanaji wa taarifa zilizo sahihi na kwa wakati sahihi.
Hayo yameelezwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu wakati akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa (AICC) jijini Arusha ,sambamba na mkutano mkuu wa chama hicho (TAGCO) 
"Benki ya CRDB tunaamini "with right information" ambao hawa ni haki yao kuifikisha kwa wananchi ambao watakuwa aware nini kinaendelea,sio tu katika kutangaza nafasi za kazi kama baadhi ya watu wanavyofikiria ,pia wanahusika katika kutangaza Zabuni zilizopo,nafasi za Maendeleo,Nafasi za uwekezaji na sSehemu gani hasa unaweza kuwekeza kwa ajili ya maendeleo."alisema Semunyu.
Amesema Maafisa Habari wa taasisi za Serikali ndio daraja la kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi na kwamba kupitia kwao kila kinachofanyika ndani ya Serikali kitwafikia wananchi kwa njia na wakati sahihi.
"Kama alivyosema Msemaji Mkuu wa Serikali kwamba kuna tofaui kubwa ya kufikisha habari na kufikisha habari sahihi,kwa hiyo daraja hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa halipati heshima stahiki sasa litapa heshima."alisema Semunyu..
Meneja UhusiaNo wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.Washiriki wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB ,Godwin Semunyu wakati wa mkutano huo. kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TAGCO,Pascal Shelutete,Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu na mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamadunina Michezo,Susan Mlawa.Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo.Meneja Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada juu ya mfumo maalumu wa kadi za kielektroniki maarufu kama Credit Card ,huduma ambayo inatolewaa na Benki ya CRDB.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

1 week ago

Malunde

BASI LAZAMA KWENYE MTO WENYE VIBOKO SERENGETI


Basi la kampuni ya Kimotco lililokuwa linatoka Musoma, kwenda Arusha, kupitia Mugumu, limezama katika mto wenye viboko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Mhifadhi mkuu wa Hifadhi hiyo William Mwakilema amethibitisha kupata taarifa ya tukio hilo leo Machi 16,2018.

Mwakilema amesema hakuna majeruhi wala vifo na kuwa abiria wote wako juu ya basi.
“Jitihada za kuwaokoa mmoja mmoja zinaendelea. Baada ya kusombwa na maji abiria wote wako juu ya basi maana halikuzama lote, jitihada za kuwaokoa zinaendelea mpaka sasa zaidi ya abiria wanne wametolewa,"amesema bila kutaja idadi ya abiria wote.
Kamanda wa Polisi mkoa Mara, Jafari Mohamed hakuweza kupatikana kwa njia ya simu, hata hivyo polisi wilayani Serengeti wamesema wameshatoa taarifa kituo kidogo cha cha polisi Seronera kufuatilia.

Mmoja wa mawakala wa kampuni hiyo Neema Kegocha amekiri kupata taarifa na kudai wanatafuta usafiri wa kwenda eneo la tukio.
Na Anthony Mayunga, Mwananchi

1 week ago

ITWeb Africa

16 Mar

Tanzania govt, Bharti Airtel go head-to-head over Airtel Tanzania


ITWeb Africa
Tanzania govt, Bharti Airtel go head-to-head over Airtel Tanzania
ITWeb Africa
Talks have started between the Tanzanian government and India's Bharti Airtel over the ownership of Airtel Tanzania. The Tanzanian government has initiated a move to repossess Airtel Tanzania at the directive of President John Magufuli over claims that ...
Tanzanian journalist recounts his midnight flight from assassinsMail & Guardian

all 2 news articles »

1 week ago

Michuzi

Waziri Mwakyembe akutana na Balozi wa China na Balozi wa Umoja wa Ulaya


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. WANG KE alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika. Mratibu wa programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma (kushoto) pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Habari wakifuatilia majadiliano ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) na Balozi wa China nchini walipokutana kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia kitabu alichopewa na balozi wa China nchini Mhe. WANG KE (kushoto) baada ya kufanya mazungumzo yanayohusu masuala ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer wakiangalia moja ya historia iliyoifadhiwa ya harakati za ukombozi wa Bara la Afrika baada ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimuonyesha Bolozi wa Umoja wa Ulaya (wapili kushoto) Mhe. Roeland Van de Greer pikipiki zilizotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika. Kulia ni Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi MdumaPicha na: Genofeva Matemu - WHUSM

1 week ago

Michuzi

MUWSA,NMB WAZINDUA MALIPO YA ANKARA ZA MAJI NJIA YA NMB MOBILE.

 Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba(Wa Pili kutoka kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Malipo ya Ankara za Maji kwa njia ya NMB Mobile leo,uzinduzi ulioenda sambamba na uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji kwa mkoa wa Kilimanjaro.Wengine toka kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Michael Mwandezi,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA) Joyce Msiru,akifuatiwa na Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kishosha. Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliifanyika leo katika viwanja jirani na ofisi za MUWSA. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akitoa taarifa juu ya utoaji wa Huduma ya Maji kwa mgeni rasmi ,Kippi Warioba katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro. Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Emanuel Kishosha akitoa maelezo kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba wakati wa maadhimisho ya wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa malipo ya Ankara za Maji kwa njia ya NMB Mobile. Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha Mti katika eneo la chanzo cha Maji cha Kaloleni.Jumla ya ya miti 500/imeoteshwa katika eneo hilo ikiwa ni msaada uliotolewa na taasisi ya Kilimanjaro Project. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akiotesha mti katika eneo la chanzo cha Maji cha Kaloleni Mara baada ya kuzindua wiki ya Maji mkoa wa Kilimanjaro ikibeba kauli mbiu ya "hifadhi maji na mfumo Wa kiikologia kwa maendeleo ya jamii" Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya Maji ,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akikagua baadhi ya mabanda ya maonesho yaliyopo katika viwanja vilivyopo jirani na ofisi za MUWSA.

1 week ago

Michuzi

Mawakala wa Tigo Pesa Wajinyakulia Mamilioni

Kampuni inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao, Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya Tigo Pesa leo imewazawadia wakala wake mamilioni ya pesa kwa utendaji wao mzuri.
Wakala RBB RBB ya Sinza, Dar es Salaam ilijishindia TZS 10 millioni kutoka Tigo Pesa, huku Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar akijinyakulia zawadi ya pili ya TZS 5 millioni katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo. ‘Nilishinda zawadi ya kanda katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba kwa hiyo nafurahi kuwa uwekezaji na juhudi nilizofanya katika kipindi hiki vimeniwezesha kutangazwa kama mojawapo wa washindi wa kitaifa,’ Khatib alisema.
Pamoja na zawadi hizio kwa washindi wa kitaifa, Tigo pia ilitoa zawadi nane za TSH 3 millioni na TZS 2 millioni kwa mawakala bora kutoka kila kanda nchini. Pia zawadi za bonasi zilitolewa kwa mawakala wote waliofikia malengo waliowekewa katika kipindi cha promosheni hiyo.
Mojelwa Mlinga wa Ukonga, Dar es Salaam aliyeibuka kama wakala bora wa kanda ya Pwani na kujinyakulia kitita cha TZS 3 milioni alisema kuwa atatumia hela alizoshinda kuboresha mtaji wake wa biashara. ‘Nilishinda zawadi ya pili kitaifa katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba na nilikuwa natarajia kushinda zawadi ya kwanza kitaifa, ila nashukuru kuwa nimefanikiwa kupata zawadi ya kanda,’ alisema. Robert Butambele (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Sinza, Dar es salaam akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni kumi kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Butembele aliibuka mshindi wa kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge. Said Khatib (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Mkunazini, Zanzibar akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni tano kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo - Hussein Sayed (wa tatu kulia). Khatib aliibuka mshindi wa pili kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa - Restituta Kedmond (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo - Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge. Baadhi ya mawakala mbali mbali walioshinda zawadi katika promosheni ya mawakala wa Tigo pesa iliyoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo. Hii ilikuwa baada ya kupokea zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam leo. Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

1 week ago

Michuzi

HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI

 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akikabidhi Msaada wa Vitanda 4o na Magodoro 40 kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe kwaajili ya hospitali ya mwananyamala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusheherekea siku ya Mwanamke duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8. Benki hii imetoa vitanda na magodoro kwaajili ya wodi ya akina mama katika hospitali hiyo. Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda 40 na magodoro 40 katika hospitali ya Mwananyamarla jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe na kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe akishukuru kwa Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda  kwa kuiona hospitali ya Mwananyamala kwa kuwa kunahospitali nyingi"Tunashukuru Mchango wenu sana Mungu awabariki ."kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda na Kulia ni Mkuu wa matawi ya Kanda Elizabeth Mayengo.
BENKI  ya Exim Tanzania leo imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa Mwananyamala, jijini Dar es Salaamkwa kuwa Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika hospitali ya Mwananyamala wakiongozwa na wafanyakazi wanawake wa Benki ya Exim kwenye hospitali hiyo jengo la utawala  katika hospitali hiyo ukipokelewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala Dk. Khadija Shebe.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Matawi ya benki ya Exim, Agnes Kaganda amesema “Katika kuadhimisha sherehe za wanawake mwezi huu, Benki ya Exim inatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii na kwenye ukuaji wa uchumi. Msingi wa mpango wetu huu wa mwaka mzima wa kujali jamii ni kuelewa kiasi gani wanawake ni muhimu katika jamii".
Benki imejitolea kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 kwa kusaidia wanawake kwa kuboresha huduma za uzazi katika sekta ya afya. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa ya kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu na sisi tumejizatiti kwenye mpango huu."
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa wanawake nchini. Aliongezea kwa kusema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii .”KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

2 weeks ago

Telecompaper

13 Mar

Tanzania begins talks with Bharti Airtel over ownership of local unit


Mobile World Live
Tanzania begins talks with Bharti Airtel over ownership of local unit
Telecompaper
Tanzanian officials have began talks with Bharti Airtel to discuss the disputed ownership of Airtel Tanzania, Bloomberg reported citing presidency officials. The company requested the proceedings after a government investigation into the ownership of ...
Airtel seeks accord on Tanzania business ownershipMobile World Live

all 3 news articles »

2 weeks ago

AllAfrica.Com

13 Mar

Tanzania: Govt Starts Talks With Bharti Airtel


Tanzania: Govt Starts Talks With Bharti Airtel
AllAfrica.com
Dar Es Salaaam — Talks between the government and Bharti Airtel with regard to the ownership of Airtel Tanzania commenced on Monday, March 12. The negotiation team from Tanzania is led by Minister of Constitution and Legal affairs Professor ...

and more »

(Yesterday)

Bongo Movies

Esther Kiama yupo kwenye maombi mazito kusaka mtoto wa kike

MDADA anayefanya kazi ya kuigiza kwenye filamu za Kibongo, Ester Kiama amesema kuwa sasa hivi yuko kwenye mfungo wa Kwaresima kwa ajili ya maombi maalum ya kutafuta mtoto wa kike.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Ester aliweka wazi kuwa, anatamani sana mtoto na kwa sababu tayari ana mtoto wa kiume, anahitaji kupata wa kike na ndio maana yuko kwenye mfungo maalumu wa siku 40 kwa ajili ya maombi hayo.

“Katika kipindi hiki cha Kwaresima na mimi nimefunga na kuomba, ombi langu kwa Mwenyezi Mungu ni la kutaka kupata mtoto wa kike maana ndilo hitaji langu. Ndiyo maana nimejitahidi kufunga kuanzia mwanzo mpaka nimalize 40,” alisema Ester.

Tazama nyimbo mpya ya abdukiba hapa–>>https://bit.ly/2pBebz8

1 day ago

Malunde

DIAMOND ATINGA OFISI ZA BASATA KIMYAKIMYA KUYAMALIZA
Msanii wa muziki, Diamond Platnumz Ijumaa hii amefanya mazungumzo ya siri na Baraza la Sanaa Taifa ‘Basata’ ikiwa ni siku chache toka aingie kwenye majibizano na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo “African Beauty” ametua viwanja vya basata majira ya nchana akiwa na meneja wake, Sallam SK. Hata hivyo baada ya kufanya mazungumzo hakuweza kuzungumza chochote juu ya nini kilitokea.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Basata zinadai muimbaji huyo alifika katika taasisi hiyo ya malezi ya wasanii kwaajili ya kuzungumza na viongozi hao juu ya kauli zake ambazo amekuwa akizitoa juu ya Naibu waziri huyo.
Hata hivyo Basata hawajatoa taarifa yoyote juu ya kikao hicho cha siri ambacho kilichukua masaa kadhaa.
Wadau wa mambo wanadai huwenda muimbaji huyo alikwenda Basata kwaajili ya kuamba radhi juu ya mambo yanayoendelea.
Mapema wiki hii muimbaji huyo wakati anahojiwa na kituo cha redio cha Times FM aliitupia lawama Basata pamoja na Naibu waziri huyo baada ya kufungia nyimbo 15 za wasanii wa bongofleva zikiwemo zake mbili.
Kauli hizo zilimfanya Waziri wa Habari, Dk Mwakyembe kutoa kauli yake na kudai kwamba ameshtushwa na kauli za muimbaji huyo juu ya waziri.

1 day ago

Malunde

AGPAHI YAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE MUHEZA


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto  akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya  kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy  machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa  akimpongeza na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara  baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita  na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala
****SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya Ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya  kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy  machine).
Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa  mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa  sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika  ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.
Mkurugenzi mtendaji  wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua  mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa  wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya  Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao  katika vifaa tiba.
"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu  katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema  Mwakyusa.
Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza  atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza (Muheza DDH) ili ianze  kazi.
"Nalishukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali  ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.
Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya  alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalumu ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo.
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

2 days ago

Michuzi

SHIRIKA LA AGPAHI LAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE KWA WILAYANI MUHEZA

SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy machine).

Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika vifaa tiba.

"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema Mwakyusa.Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza( Muheza DDH) ili ianze kazi.

Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.

Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

2 days ago

Michuzi

MAKONDA AWAITA OFISINI KWAKE WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO

RC Paul Makonda

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  amewataka wanawake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto wafike ofisini  Jumatatu ya  Aprili 9 kwa lengo la  kupatiwa msaada wa kisheria.
Taarifa ya Makonda kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana amesema jopo la wataalamu wa sheria, maofisa ustawi wa jamii na askari Polisi kutoka dawati la jinsia wamejipanga ipasavyo kuwahudumia na kuhakikisha mzazi mwenza anatoa fedha kwa ajili ya matunzo ya mtoto.
"Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.Ewe mwanamke huu si wakati wa kulia wala kuteseka kwani Serikali yako itasimama na wewe hadi upate haki yako," amesema Makonda.

2 days ago

Bongo Movies

DIAMOND PLATNUMZ: SIOGOPI Kwenda Jela Labda UNIUWE

EXCLUSIVE INTERVIEW NA DIAMOND PLATNUMZ KWA MARA YA KWANZA TIMES FM BAADA YA KUTOKA TU KENYA, KAONGEA MENGI SANA KUHUSU BEEF NA MEDIA, ZARI, ALBUM YAKE, WEMA, ALIKIBA, KUFUNGIWA NYIMBO NK. Msanii Diamond aeleza kwanini alifanya performance kwa mara ya kwanza nje Nairobi,kenya. Diamond alieleza kuwa kwenye performance yake ilikuwa na changamoto nyingi na nchi yetu haijaweza kuwezeshwa katika sanaa. Pia alisema sababu nyingine ya kufanya performance yake huko nairobi ni kwaajili kuonesha kuwa bongo fleva imekuwa. DIAMOND ametangaza NDOA Mwaka Huu na pia kuwa hana beef na mtu yeyote, amesema kuwa ni watu tu wanatengeneza skendo mbalimbali kuleta utata.

bofya “PLAY” kutazama

Diamond alieleza pia kwa jinsi gani amekwazika alivyo fungiwa nyimbo yake bila sababu na bali kulipia codi nyimbo zake.

Bofya PLAY kutazama

2 days ago

Malunde

TCRA YAWALIMA BARUA TIMES FM...KIPINDI CHA DIAMOND KUMPONDA NAIBU WAZIRI SHONZA

Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kimetakiwa kuwasilisha kipindi cha mahojiano waliyofanya na mwanamuziki Diamond Platinumz kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mkurugenzi wa Times FM, Amani Misana amesema kuwa amepokea barua ya kuwataka wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi, 19, 2018 na kwamba leo wametekeleza agizo hilo.
“Tumepokea barua na tumefanya yale tuliyoagizwa ikiwamo kuwasilisha kipindi chote,” amesema kwa ufupi Misana.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema suala la kituo hicho kupewa barua ni la kiutawala zaidi na mamlaka hiyo haipo kwenye kitengo chake isipokuwa kama tayari barua imefika, wakati wa kutolewa uamuzi vyombo vya habari vitaalikwa.
Mwanamuziki Diamond alizua mjadala baada ya kuzungumzia suala la nyimbo za wasanii kufungiwa akimlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutowatendea haki wasanii.
Diamond hakuishia katika mahojiano hayo yaliyoongoza na mtangazaji Omary Tambwe, Machi 20 kupitia mtandao wa Twitter alimjibu naibu waziri huyo akisema ametumia njia hizo kumjibu kwa kuwa naye alitumia hizo hizo.
Hata hivyo, jana mamlaka za Serikali ikiwamo Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe walimshukia mwanamuziki huyo wakisema amefanya makosa kumshambulia naibu waziri kwa kuwa uamuzi anaotoa siyo wake binafsi.

2 days ago

Michuzi

Kifo cha Mwalimu Mponda wa TaSUBa chaigusa Serikali

Na Anitha Jonas – WHUSMSerikali imetoa  pole kwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kwa kumpoteza Mwalimu mahiri John Mponda aliyekuwa balozi  wa tasnia ya Sanaa nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza katika ibada ya kumuaga marehemu huyo iliyofanyika katika Chuo cha TaSUBa Wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kumuaga kwani anatarajiwa kuzikwa kijiji cha Mbalizi Mkoani Mbeya.

“Tunatambua mchango wa Mwalimu John Mponda katika tansia ya sanaa nchini na kupitia wanafunzi waliyopita katika mikono yake pamoja na vikundi vya vijana alivyovianzisha ambavyo amekuwa akivifundisha kazi za sanaa, hakika tumempoteza mtu makini,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza  katika msiba huo Mheshimiwa Shonza  aliwasihi wasanii waliyopata mafunzo kutoka kwa mwalimu huyo kuwa mabalozi  kwa wasanii wenzao na kuwashauri misingi iliyobora katika katika kukuza na kuendeleza kazi za sanaa. Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha TaSUBa Dkt.Herbert Makoye alisema kuwa marehemu mwalimu Mponda ameondoka katika kipindi walichokuwa wanamuhitaji sana kwani kwasasa taasisi hiyo ipo katika maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la Bagamoyo ambalo nilakimataifa na hufanyika kila mwaka na yeye  alikuwa mratibu na mpaka mauti yanamfika alikuwa akiwa shughulikia maandalizi hayo.  “Kwa hakika msiba huu ni pigo kwa taasisi yetu na mwalimu huyu alikuwa kiungo miongoni mwetu na alifanya kazi yake kwa weledi na kujituma alikuwa ni mtu aliyeipenda kazi yake ,’’alisema Dkt.Makoye.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mkufunzi wa Sanaa katika Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) marehemu Mwl. John Mponda leo  kabla ya ibada ya kumuaga kwa ajili ya safari ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika Mbalizi mjini Mbeya.

3 days ago

Michuzi

UAMUZI MAOMBI YA DHAMANA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYAKAZI MSTAAFU WA TAZAMA KUJULIKANA APRILI 5 MWAKA HUU

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamiiMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema uamuzi wa maombi ya dhamana katika kesi  ya kuhujumu uchumi inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(Tazama),  Samwel Nyakirang'ani(63) na wenzake sita, kujulikana Aprili 5, mwaka huu.
Uamuzi huo ambao ulitakiwa kutolewa leo, umeahirishwa kwa sababu Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema bado hajamaliza kuuandaa kutokana na kuwa na majukumu ya kikazi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wakili wa utetezi, Kusalika Augostine kuwasilisha maombi mahakamani hapo akidai wateja wake wanahitaji kupata dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhaminika.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Nyangi Mataro( 54) mwalimu wa shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni, mfanyabaishara, Farijia Ahmed (39) mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias b(39) mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus (25) mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko (40) mkazi wa Tungi Kasirati na Hunry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni nq Audai Ismail
washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta ya  dizeli, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.
Ilidaiwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka (TPA).
Inadaiwa walijiunganishia mafuta hayo kutoka katika bomba la rangi ya silva lenye upana wa inchi 24 ambalo halishiki kutu.
katika shtaka la kuharibu miundo mbinu, ilidaiwa,  kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa walitoboa na kuharibu bomba la mafuta ya dizel lenye upana wa inchi 24, ambalo lilikuwa likitumika kufirisha mafuta,  mali ya (TPA).
Aidha washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la mafuta mazito( Crude oil) lenye upana wa Inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya (TPA)

3 days ago

Zanzibar 24

Ebitoke aweka wazi tuhuma za kutembea na mume wa Mamaa Ashura

Mchekeshaji kutoka kundi la Timamu, Ebitoke amejibu tuhuma kuwa amekuwa akitoka kimapenzi na mume wa Mamaa Ashura.
Muigizaji huyo amesema kuwa tuhuma hizo hazina ukweli wowote ni stori tu za kupikwa.

“Kwa wale wanaosema mimi nimempindua si kweli wakati yupo tumemficha sehemu, tutamleta,” Ebitoke ameiambia Bongo5.

“Mama Ashura yupo na anaendelea na mambo mengine, atarudi kama mwanzo na wataendelea kumuona ila sasa hivi hayupo kidogo, kuna mambo ambayo anayafanya,” ameongeza.

Hapo awali kulikuwa na taarifa kuwa baada ya Ebitoke kuanza kutoka kimapenzi na mume wa Mamaa Ashura ndipo kumepelekea muigizaji huyo kutoonekana tena katika kundi hilo.

The post Ebitoke aweka wazi tuhuma za kutembea na mume wa Mamaa Ashura appeared first on Zanzibar24.

3 days ago

Michuzi

USHAHIDI WA DAKTARI KUHUSU SABABU ZA KIFO .


Na Bashir Yakub.


Unaweza kuwa wewe, ndugu yako,rafiki au  jamaa yako ameunganishwa katika kesi ya mauaji. Aghalabu, daktari anasubiriwa kutoa ushahidi mahakamani kuhusu sababu za kifo cha marehemu.
 Na ni ushahidi huo wa daktari utakaokuondoa katika kesi  hiyo ya mauaji au utakuingiza katika kesi hiyo na hivyo kutiwa hatiani na kuadhibiwa.


Lakini sio daktari tu bali wenye kesi wote ambao ushahidi wake unahitaji mtaalam(expert) kuthibitisha mfano mkemia, mtaalam wa muandiko na sahihi, mtaalam wa biashara , mtaalam wa DNA  nk.


1.USHAHIDI WA DAKTARI.


Kifungu chac 47 cha Sheria ya Ushahidi kinaruhusu kutumika na kukubalika kwa ushahidi wa mtaalam( expert). Mtaalam ni pamoja na daktari.


2. MAMBO  6  MUHIMU UNAYOTAKIWA KUJUA.

A ).  Kabla daktari au mtaalam mwingine yoyote hajaanza kutoa ushahidi wake ni ni muhimu sana athibitishe kwa ushahidi kuwa yeye ni mtaalam kweli (expert) kwa hicho anachotaka kutolea ushahidi. Usikubali akaanza  kueleza kabla ya kuthibitisha utaalam.Mtake athibitishe hilo kwanza.


Utaalam unathibitishwa kwa taaluma(professional). Kama ni daktari na mtaalam wa eneo fulani la tiba ,mfano mifupa, moyo, nk, aoneshe cheti cha taaluma katika eneo hilo. Halikadhalika kwa wataalam wengine nao wanatakiwa kufanya hivyo. Kama hawezi kuthibitisha hilo basi hiyo ni faida kwako kwakuwa ushahidi wake ni wa kutia shaka.


Na hapo haijalishi mtaalamu(expert) huyo ameletwa na nani. Awe ameletwa na polisi, PCCB, au idara nyingine yoyote. Msimamo huu ulitolewa na mahakama  katika kesi ya MUHAMMED AHMED V 
REPUBLIC(1957)E.A. C.A 523.

B ). Daktari au shahidi yoyote mtaalam, asiwe tu mtaalam wa vyeti, bali awe mwenye ujuzi wa uzoefu wa kazi husika. Kwa mfano, daktari au mtaalam ambaye amemaliza chuo, ana cheti lakini hajaajiriwa wala kuwahi kuifanyia kazi taaluma yake popote hawezi kuitwa mtaalam mwenye uwezo(competence) wa kutoa ushahidi wa kitaalam.

                    KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com


3 days ago

Zanzibar 24

Waziri wa afya Z’bar azindua bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi zanzibar (ZFDA)

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umetakiwa kuendeleza juhudi za kuleta ufanisi katika majukumu yake ili kuzidi kujenga imani na kupata sifa za kimataifa.

Sifa hizo zitaepelekea Wadau kutoka nje ya Zanzibar kuja kujifunza namna Wakala huo unavyofanya kazi za kulinda na kuimarisha afya ya jamii kwa maslahi mapana ya taifa.

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed ameyasema hayo wakati akizindua Bodi ya Ushauri wa Wakala huo  katika ofisi za ZFDA Mombasa mjini Zanzibar.

Amesema kinachohitajika katika Wakala huo ni kujiamini na kusimamia sheria ambazo zimewekwa kwa ajili ya kumlinda mtumiaji.

Amewasisitiza Watendaji wa ZFDA kuzikamata na kuziangamiza bidhaa zote zisizokidhi viwango hadaharani na kwa mujibu wa Idadi waliyoitangaza ili kuondoa tuhuma ambazo baadhi ya wananchi huzitoa.

amesema yapo madai kwamba wanakamata bidhaa lakini wanapoziteketeza  wananchi hawapewi taarifa kamili ya ueteketezwaji huo hivyo akasisitiza taarifa kutolewa kwa uzito wake.

Amewanasihi kuwa wanakabiliwa na majukumu kubwa ya kuhakikisha Vyakula, Dawa na Vipodozi vinavyoingizwa vinakuwa katika hali ya ubora ili kuepuka jukumu kwa maslahi yao ya hapa duniani na kesho mbele ya Mungu.

“Mnajukumu kubwa mbele ya Mungu mkiruhusu mali na bidhaa mbovu mtaenda kuwajibika siku ya malipo”aliwanasihi Waziri wa Afya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya ZFDA Mayasa Ally Salim amesema utaratibu wa udhibiti unafanywa kupitia idara nne za wakala zikiwemo Idara ya usalama wa chakula, Idara ya Dawa Vipondozi na bidhaa za tiba, Idara ya Huduma za maabara na Idara ya human a wakala.

Amesema kazi kubwa ya ZFDA ni kulinda na kuimarisha afya ya jamii kwa kusimamia udhibiti wa bidhaa za chakula, Dawa, Vipodozi, Vifaa Tiba na Vitendanishi kupitia usajili, ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara.

Awali akimkaribisha mgeni Rasmi Mkurugenzi wa ZFDA Burhan Othman  Simai alimuhakikishia kuwa Idara yake ipo tayari kufua kila ushauri ambao utazidikuleta ufanisi kwa kazi yake.

Wakati huo huo ZFDA ilipokea Msaada wa Gari mbili zenye thamani ya Shilingi Milioni 150  kutoka Mfuko wa Kimatifa wa Global Foundation ambazo zitatumika kwa ajili ya kufuatilia usajili,ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara kwa Unguja na Pemba.

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 21.03.2018

The post Waziri wa afya Z’bar azindua bodi ya ushauri ya wakala wa chakula dawa na vipodozi zanzibar (ZFDA) appeared first on Zanzibar24.

3 days ago

Malunde

TCRA,MWAKYEMBE KUKOMAA NA DIAMOND 'SHERIA NI YA WOTE BILA KUJALI UMAARUFU WA MTU'


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia mahojiano ya mwanamuziki Nasseb Abdul maarufu Diamond aliyoyafanya katika kituo cha Redio cha Times jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Machi 21, 2018 Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka hiyo, Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo wanachokisimamia.

Katika mahojiano hayo, Diamond alimjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutokana na Serikali kuzifungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Kisaka amefafanua kuwa kiutaratibu wao wanaangalia zaidi chombo ambacho wamekipa leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine.

Amesema suala hilo kwa sasa linafanyiwa kazi na kamati ya maudhui na kuahidi kulitolea ufafanuzi siku za hivi karibuni akiwataka wananchi kuwa na subira.

Wakati TCRA ikisema hivyo, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema amesikitishwa na matamshi ya Diamond kuhusu kufungiwa kwa nyimbo hizo aliyoyatoa katika kipindi hicho.

“Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo za wasanii wawili kwa kukiuka maadili yalifanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa Shonza ambaye analaumiwa na Diamond,” amesema.

“Diamond atambue kuwa Serikali ina taratibu zake na maamuzi ya naibu waziri ni ya wizara. Kama vikao na wasanii tumefanya vingi sana, lakini Diamond hakuwahi kuhudhuria vikao hivyo, si wajibu wa Serikali kumfanyia kikao cha peke yake.”

Amesisitiza, “Sheria ni ya watu wote bila kujali umaarufu au nafasi ya mtu katika jamii, hivyo msanii Diamond anapaswa kutii sheria na mamlaka zilizowekwa.”

Dk Mwakyembe ameeleza kuwa sio busara kwa Diamond kushindana na Serikali na endapo ana ushauri wowote ni vyema akawasilisha kwa njia sahihi, lakini si kumshambulia naibu waziri kwa dharau na kejeli kama alivyofanya.

“Diamond kwa mafanikio aliyoyapata katika muziki, anatarajiwa kuwa mfano bora kwa wanamuziki wenzake. Napenda kuwakumbusha wasanii wote kwamba sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine,” amesema.

“Pamoja na kuwa na kipaji hicho, wasanii wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia tasnia ya sanaa kama ilivyo kwa tasnia nyingine.”

Na Nasra Abdallah, Mwananchi

4 days ago

Malunde

DC AAGIZA POLEPOLE AKAMATWE KWA KUUZA DAWA

Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango ameliagiza jeshi la polisi katika wilaya hiyo kumkamata na kumfikisha mahakamani Mganga wa zahanati ya Kibanga wilayani humo Ruiz Polepole.
Mkuu wa Wilaya huyo ametoa agizo hilo kufuatia wananchi wa kijiji cha Kibangu kutega mtego ambao ulimnasa Mganga huyo wa zahanati ya Kibanga akiuza dawa zinazotolewa na Serikali ambazo zinapaswa kutolewa bure. 
Aidha upelelezi ukikamilika mganga huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo za kuuza dawa za serikali kinyume na utaratibu wa serikali.

4 days ago

Zanzibar 24

Saba wauawa kwa ajali ya Gari Kigoma

Watu saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania katika Mlima wa Kasagamba kijiji cha Mkongoro barabara ya kutoka Manyovu wilaya ya Kigoma Vijijini kuelekea mkoani Kigoma. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Maltini Otieno amesema ajali hiyo imetokea leo Machi 21,2018 majira ya saa tatu asubuhi. Amesema gari aina ya Scania lori yenye namba T741AAB  ilianguka na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Siri Hamis (43) mwenyeji wa Singida pamoja na utingo wake aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Saidi (23) mkazi wa Manyoni. Kamanda Otieno amesema katika gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne mmoja mwanamke na wa tatu wanaume ambapo wote walifariki na majina yao hayakufahamika. Aidha amesema ajali hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Eliakimu Samsoni (15 )aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea shuleni na gari hilo kumgonga akiwa anatembea. Amesema chanzo cha ajari hiyo ni dereva kushindwa kuimudu gari kwenye mteremko mkali na kusababisha gari hiyo kutelemka kwa mwendo mkali na kumshinda dereva huyo na kusababisha vifo hivyo. Kamanda Otieno amewaomba madereva kuzingatia sheria za barabarani na kuhakikisha gari za mizigo hazibebi abiria ili kunusuru vifo vitokanavyo na ajali na kuhakikisha wanazingatia alama za barabarani.

The post Saba wauawa kwa ajali ya Gari Kigoma appeared first on Zanzibar24.

4 days ago

Malunde

LE MUTUZ NAYE AMTOLEA UVIVU NAIBU WAZIRI SHONZA SAKATA LA DIAMOND

Wakati BASATA wakimtuhumu Diamond kulewa na umaarufu na kufanya abishane na Naibu waziri ambaye anawakilisha Serikali, bado huko katika mitandao ya kijamii watu wamezidi kuonyesha hisia zao juu ya jambo hilo kwa kudai kuwa Naibu waziri anatafuta kiki kwa lengo la Kumshusha Diamond.

Mwanahabari na Blogger, Le Mutuz ameibuka na kudai kwa Naibu Waziri amekuwa akitumiwa na watu wenye chuki kubwa na muziki wa Diamond ili kuua muziki wake na sio vinginevyo.

Le Mutuz anasema kuwa huu ulikuwa ni wakati wa serikali kuona mchango wa Diamond hasa baada ya kuchaguliwa kwenda kufanya show ya ufunguzi wa kombe la Dunia. 

Lemutuz ambaye amesema kuwa pamoja na kwamba Mh Juliana Shonza ni mwana CCM mwenzake lakini anaona kabisa katika hili la kuwafungia na kubishana na Diamond katika mitandao ya kijamii hawezi kunyamaza kimya.

Hata hivyo Lemutuz amemhusisha Julana Shonza na moja ya kiongozi wa kituo fulani cha radio “MUNGU MTU” ambacho hajakitaja na kusema kuwa wamekuwa wakishirikiana ili kumtua Diamond katika nafasi kubwa ya mafanikio ya kimuziki aliyonayo.

4 days ago

Malunde

BASATA WADAI DIAMOND KAITUKANA SERIKALI KUMJIBU NAIBU WAZIRI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond amefanya makosa kumjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akifananisha kitendo hicho na kuitukana Serikali.

Diamond Platnumz na naibu waziri huyo waliingia katika vita ya maneno baada ya Serikali kufungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Mngereza amesema Diamond anapaswa kuelewa kwamba maneno machafu anayoyatoa dhidi ya waziri huyo ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo hata ukienda katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni.

Mngereza amesema wamesikitishwa na kauli ya Diamond na kusisitiza kwamba ni vyema akafuata taratibu katika kulalamikia suala hilo ikiwemo kuandika barua kama alivyomuelekeza Waziri Shonza.

Ameongeza kuwa si lazima msanii aandikiwe barua pale anapokosa kama ambavyo Diamond ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter, kwamba Shonza angemwandikia barua kabla ya kumfungia.

Amebainisha kuwa si kila mwanamuziki anayefanya makosa huwa anaandikiwa barua.

Katika malalamiko yake, Diamond amesema naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka kufungia nyimbo na pia kutowaandikia barua rasmi ndio maana ameamua kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.

Jana Waziri Shonza alisema hawezi kujibizana na Diamond kwa sababu alichofanya si maamuzi yake binafsi na kwamba kama anaona ameonewa apeleke malalamiko yake kwa maandishi.

4 days ago

Malunde

HAJI MANARA AINGILIA KATI SAKATA LA DIAMOND NA NAIBU WAZIRI SHONZA

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amefunguka na kumkingia kifua msanii Diamond na wenzake ambao wamekuwa wakitetea haki zo kwa Naibu waziri ambae ameibuka na sera ya kuwafungia wasanii kwa madai kuwa wanaimba nyimbo zisozokuwa na maadili katika jamii.

Hivi karibun Diamond aliongea katika media moja na kusema kuwa hata kama atatakiwa kulala jela kwa sababu ya muziki basi atafanya ilimradi kutetea haki ya muziki kwa sababu watu wanaofungia muziki huo hawajui historia ya muziki wala msanii wanaemfungia.

Haji Manara amesema kuwa pamoja na kwamba wasanii wanaweza kuwa wamefanya kosa lakini wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la pili na kwa upande wa Diamond ni msanii mkubwa mbaye amekuwa akiiwakilisha nchi katika mambo mbalimbali.
"Ngoja na mimi nispitwe na hili..inawezekana kuwa kama binadamu anaweza kuwa amekosea , lakini inabidi tutambua kuhusu muziki wa kisasa na soko lake linataka nini..by the way diamond na wenzie tunawatumia sana katika maswala ya kijamii na hata kampeni zetu za kisiasa,na huyu ni brand kubwa ,,,walau tufanye staha kidogo na tujitaidi tupende vya kwetu.

NB.mimi napenda muziki mzuri sina cha timu wala cha baba yake na timu….hawakawii wabongo. @diamondplatinumz"

Trending News

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani