(Yesterday)

Michuzi

RC Gambo Azindua Mradi wa Utaoji Mitego kwa Wanyamapori (De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti ,Jijini Arusha

 Ugawaji wa Vyeti kwa wadau wa Utalii katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya Serengeti iliyofanyika katika Hoteli ya Four Points by Sheraton Arusha (zamani The Arusha Hotel)  tarehe 14:10:2017, Jijini Arusha. Mdau wa Utalii akipokea Cheti cha Ushiriki katika uzinduzi wa mradi wa Utoaji Mitego kwa Wanyamapori (FZS Serengeti Conservation Programme De -Snaring Project) kwa Mbuga ya Wanyama ya...

 

(Yesterday)

Michuzi

Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa FC, Wilbert Molandi mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya 12 mfululizo. anayeshuhudia ni mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary. Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa Queens, Zuhura Abdinoor mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya...

 

2 days ago

Michuzi

TAMASHA LA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA ARUSHA KURINDIMA KESHO


Na Woinde Shizza,Arusha
Tamasha la waandishi wa habari, kanda ya kaskazini, linatarajiwa kufanyika jumapili, octobar 15 katika uwanja wa General Tyre ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Katika tamasha hilo, ambalo litashirikisha wanahabari zaidi ya 500, kutoka mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro,limedhaminiwa na shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kampuni ya vinywaji...

 

4 days ago

Michuzi

KITUO CHA POLISI MOROMBO KUPUNGUZA MSONGAMANO “CENTRAL” ARUSHA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akiongoza askari kuhamisha udongo "Kifusi" toka kwenye msingi wa ujenzi wa nyumba za Polisi na kupeleka kwenye mtaro.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Ujenzi wa kituo kidogo cha Polisi cha Morombo kilichopo kata ya Murieti halmashauri ya Jiji la Arusha  huenda ukawa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambalo linakuwa kwa kasi kibiashara na ongezeko la  idadi ya watu.
 Uwepo wa kituo hicho utawezesha kusogeza...

 

4 days ago

Michuzi

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA KARATU WATIA FORA, ZAIDI YA WANANCHI 1200 KUSAJILIWA KWA SIKU

Si kwa idadi hii ya watu iliyofurika katika Wilaya ya Karatu Kata ya Rhotia ambako Usajili wa Wananchi Vitambulisho vya Taifa unaendelea.
Kwa mujibu wa Afisa Usajili Wilaya ya Karatu Bi. Rehema Ngomuo takribani wananchi 1200 wamekuwa wakisajiliwa kwa siku na wengine kushindwa kuwasajili na kulazimika kurejea makwao tayari kwa siku inayofuata bila manung’uniko wala ulalamishi; kutokana na umati mkubwa wa wananchi kufurika kwenye vituo vya Usajili kupata huduma hiyo.
Diwani wa Kata hiyo Bwana...

 

6 days ago

Michuzi

DC ARUSHA MJINI AWATAKA WANANCHI KUJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA

 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Fabian Daqqaro amewataka wananchi wa wilaya ya Arusha Mjini Kuchangamkia zoezi la Uandikishwaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambalo linaendelea katika kata tatu za Wilaya hiyo. Akizungumza katika kipindi cha Goodmorning Tanzania kinachorushwa na kituo cha Matangazo cha Redio cha Redio 5 Arusha Daqqaro, amesema kuwa zoezi hili lina manufaa makubwa kwa wananchi na watanzania kwa ujumla lakini pia vitambulisho hivyo vitawawezesha watanzania kutambulika kila...

 

6 days ago

Michuzi

MAHAKAMA KUU ARUSHA YAMALIZA MASHAURI YALIYOSAJILIWA JANUARI MPAKA AGOSTI MWAKA HUU

Na Lydia Churi- Mahakama, Arusha
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imefanikiwa kusikiliza na kumaliza kwa zaidi ya asilimia 90 ya mashauri yaliyofunguliwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Mhe. Angelo Rumisha, jumla ya mashauri 737 kati ya 805 yaliyosajiliwa kuanzia mwezi Januari hadi Agosti 2017, yamemalizika.

Alisema haya ni mafanikio ya kuridhisha kwa Mahakama Kuu kanda ya Arusha ambapo kila...

 

6 days ago

Michuzi

TANGA CEMENT YATOA MIFUKO ELFU MOJA YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI NYUMBA ZA POLISI ARUSHA

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani hapa, limepokea jumla ya tani hamsini sawa na mifuko elfu moja ya Saruji yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na Mbili na Laki Tano toka kampuni ya Saruji yaTanga (Tanga Cement) ili ziweze kusaidia ujenzi wa nyumba za Askari wa Jeshi hilo ambalo hivi karibuni walipatwa na majanga ya moto yaliyosababisha nyumba za familia 13 kuungua na kuteketeza karibu kila kitu. Akipokea shehena hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi...

 

1 week ago

Michuzi

ARUSHA WAANZA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAANZA KWA KISHINDO

Wananchi wa Kata za Themi, Sekei na Sombetini Wilaya ya Arusha mjini leo wameanza zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa kishindo; huku baadhi wakihangaika huku na huko kutoa nakala ya viambatisho vyao ili kujisajili kwa wakati.
Akizungumza katika Usajili huo Afisa Usajili wa Wilaya hiyo Bi. Juliet amesema wamepanga kukamilisha usajili wa Kata hizo ndani ya siku 9; na kwamba wananchi wote wanaoishi katika Kata hizo kujitokeza kwa wingi ili wasajiliwe.
Misururu ya wananchi imeonekana katika...

 

2 weeks ago

Michuzi

WANAWAKE HALMASHAURI YA ARUSHA WATAKIWA KUTUMIA JUKWAA LA WANAWAKE KAMA CHACHU YA MAENDELEO

Wanawake wa halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wametakiwa kutumia jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kama chachu ya maendeleo yao na wanawake wote ndani na nje ya halmashauri hiyo kwa kukaa pamoja ili kujengeana uwezo na kushirikisha fursa za maendeleo. 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Halmashauri ya Arusha Katibu Tawala wilaya ya Arumeru Timoth Mzava kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru amesema kuwa lengo la serikali kuanzisha majukwaa hayo ni kuwakutanisha...

 

2 weeks ago

Michuzi

MKOA WA ARUSHA WAJIZATITI KUKAMILISHA ZOEZI LA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqarro ameuhakikishia Uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) dhamira waliyonayo ya kuhakikisha wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea waishio mkoani humo hususani katika Wilaya ya Arusha wanasajiliwa Vitambulisho vya Taifa kwa wakati uliopangwa.
Kauli hiyo ameitoa leo alipokutana na uongozi wa Mamlaka, kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kuendesha zoezi hilo ambalo litaanza rasmi katika Wilaya hiyo Ijumaa Kata za Sekei,...

 

2 weeks ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UZINDUZI WA MAKUMBUSHO MPYA YA OLDUVAI - NGORONGORO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye bonde la Ngorongoro kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi na kutunza mazingira ya bonde hilo ili liwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Makamu wa Rais aliyasema hayo leo wakati wa ufunguzi rasmi wa Makumbusho mapya ya Olduvai - Ngorongoro. Katika ufunguzi huo Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya kuzindua tovuti maalum kuhusu masuala ya utalii katika bonde la...

 

2 weeks ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AWASILI NGORONGORO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mabinti wa Kimasai waliojitokeza wakati wa mapokezi kwenye lango la kuingia kwenye hifadhi ya Ngorongoro ambapo anategemewa kuzindua Makumbusho Mpya ya Olduvai kesho tarehe 3, Oktoba 2017. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoka kwa Msaidizi Mkuu wa Lango Bw. Mansuet...

 

2 weeks ago

Michuzi

PRECISION AIR YAANZA SAFARI RASMI ZA SERENGETI KUPITIA ARUSHA

SHIRIKA la ndege la Precision Air (PW) jana lilizindua safari zake za Serengeti mkoani Mara, kupitia Uwanja wa Ndege wa Arusha.
Uwepo wa safari hizo za ndege utasaidia usafirishaji wa watalii kutoka nchi mbalimbali duniani na ndani ya Tanzania kutembelea hifadhi ya Serengeti kirahisi jambo ambalo litachangia ukuaji wa uchumi nchini.
Pichani juu ni Wafanyakazi wa Ndege ya PrecisionAir na abiria  wakishuka katika Ndege kwenye Uwanja wa Seronera jana walipozind Wafanyakazi wa Ndege ya...

 

2 weeks ago

Michuzi

TPB YAFUNGUA TAWI JIPYA MTO WA MBU – ARUSHA


Benki ya TPB imeendelea kusogeza huduma zao karibu zaidi na wateja kwa kufungua tawi jipya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha.

Lengo la kufungua tawi hilo ni kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi na wao kupata fursa ya kutoa huduma kwenye mazingira bora na ya kisasa zaidi, ili wakazi wa mkoa huo waendelea kufaidika na huduma bora zenye gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua tawi hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya alisema ...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani