(Today) 1 hour ago

Mwanaspoti

Simba yaitia aibu Yanga Dar

KITENDO cha Yanga kusajili wachezaji wa gharama kubwa kutoka nje ya nchi kimewaponza kwani katika kikosi cha Taifa Stars sasa kuna mchezaji mmoja tu anayeanza kati ya wachezaji wanne walioitwa.

 

(Today) 5 hours ago

Michuzi

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA TASWE YAANZA KWA KISHINDO UKUMBI WA CARDINAL RUGAMBWA OYSTERBAY, DAR ES SALAAM

Maonyesho ya Kimataifa ya Ushirika wa akinamama wajasiliamali wa Tanzania (TASWE) yameanza kwa kishindo leo katika ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oysterbay. Akizungumza kwa juu ya maonyesho hayo, mwenyekiti na mwanzilishi wa Taswe Saccos, Bi Anna Matinde alisema "Maonyesho haya yamekuwa na hamasa kubwa wafanyabiashara na bidhaa kutoka Comorro, Afrika Mashariki na mikoa mbalimbali nchi zinapatikana hapa kwa wingi na kwa bei nafuu. "Tunawakaribisha wote mje mkutane na wafanyabiashara hawa pamoja...

 

(Today) 11 hours ago

Bongo5

Nay wa Mitego ahamishiwa kituo cha kati cha polisi Dar

Rapper Nay wa Mitego amehamishiwa katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kutoka Mvomero, Morogoro alikokuwa ameshikiliwa na polisi kuanzia asubuhi ya Jumapili, March 26.

Taarifa hiyo imetolewa na mwanasheria maaarufu nchini, Peter Kibatala.

Rapper huyo yupo matatani baada ya kuachia wimbo mpya uitwao Wapo unaikosoa vikali serikali ya Rais Dkt John Magufuli.

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za...

 

(Yesterday)

Channelten

Zoezi la Bomoa Bomoa lahamia Gerezani Kariakoo

BOMOA BOMOA

Zoezi la bomoa bomoa la waliojenga ndani ya mita 30 kupisha ujenzi wa reli ya kisasa leo limehamia eneo la Kariakoo Gerezani jijini Dar es salaam, ambapo majengo kadhaa yamevunjwa,ikiwemo kituo cha mafuta lakini pia wafanyabiashara wa soko la Kibasila wamepewa masaa mawili kuondoka.

Katika eneo hilo la soko la Kariakoo wafanyabiashara hao walionekana kuchanganyikiwa kutokana na taarifa ya kuwataka kuondoka katika kipindi cha saa mbili ikizingatiwa wengi wao walikuwa wamepumzika majumbani...

 

(Yesterday)

Michuzi

SPIKA JOB NDUGAI NA WAJUMBE WA KAMATI ZA BUNGE ZA BAJETI NA NISHATI NA MADINI WATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akimpa muhtasari Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ambaye ameongoza wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na Kamati ya Bajeti bandari ya Dar es salaam kujionea makontena yenye shehena ya mchanga kutoka migodini iliyokuwa imezuiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa agizo la serikali leo Machi 26, 2017Sehemu ya  makontena yenye shehena ya mchanga...

 

(Yesterday)

TheCitizen

Dar RC stays, Nape out and we’re very unhappy

It has been a week of fast moving developments and headlines (again) largely focused on the same person as it has been the case for some time now. It is like we are transfixed on this one individual and even when headlines seem to move on to another trending matter, it doesn’t stay so for long.

 

2 days ago

Malunde

MAKONTENA MENGINE 262 YA MCHANGA WA DHAHABU YAKAMATWA DAR

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binfasi ya TICTS.

Kubainika kwa makontena hayo kumekuja siku tatu tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli...

 

2 days ago

Bongo5

Mbwana Samatta anamiliki mijengo sita Dar

Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.

Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile...

 

2 days ago

CCM Blog

HAFLA YA KUAPISHWA MAWAZIRI, MABALOZI, KATIBU MKUU NA KAMISHNA IKULU DAR ES SALAAM

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri Mpya wa Habari, Utamaduni, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

2 days ago

Michuzi

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI AKUTANA NA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI NA UJUMBE WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

NIS1Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha Balozi wa Ujerumani Nchini, Egon Kochanke na ujumbe wake, wawekezaji kutoka Denmark na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha mbolea Kilwa mkoani Lindi. NIS2Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania...

 

2 days ago

Michuzi

PAC YATEMBELEA MRADI WA NYUMBA ZA WATUMISHI BUNJU B ZILIZOJENGWA NA TBA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma (PAC) imetembelea miradi ya ujenzi wa nyumbaza watumishi zilizojengwa na Wakala wa Majengo (TBA) .
Kamati hiyo imeitaka TBA kuendelea kubuni miradi ya nyumba kwa gharama nafuu ili watumishi waweze kupata nyumba hizo kutokana na viwango vyao.

Akizungumza wa wakati wa Kutembelea miradi ya TBA Bunju B, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC , Joseph Kasunga, amesema kuwa mradi ni ya gharama...

 

2 days ago

CCM Blog

MD KAYOMBO AKAGUA ENEO LITAKLOTUMIKA KWA AJILI YA MAONESHO YA NANENANE LA MANISPAA YA UBUNGO LILILOPO MKOANI MOROGORO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Shamba litakaloandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane lililopo Mkoani Morogoro

Na Mathias Canal, Morogoro
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amefanya ukaguzi wa eneo kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) ili kujiridhisha na kutoa maelekezo ya maandalizi kwa kufyeka majani yaliyopo katika eneo la JKT Mtaa wa Nanenane ikiwa ni hatua za ufanisi kwa ajili ya...

 

2 days ago

Mwanaspoti

Samatta kumbe halali Mbagala bwana!

WADAU na mashabiki wengi wa soka huwa wanajiuliza swali hili kuwa straika Mbwana Samatta anapokuja nchini kupumzika huwa anaishi wapi, Mbagala nyumbani kwao au sehemu nyingine kama wanavyofanya mastaa wa Ulaya.

 

2 days ago

CHADEMA Blog

CHADEMA mkoa wa Dar es Salaam, tunaunga mkono msimamo wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF)

Chadema Mkoa wa Dar Es salaam,Tunaunga Mkono Msimamo wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Kwakutokufanya kazi na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Ndugu Paul Makonda vile vile Tunalipongeza Jukwaa hilo Kwa kumtangaza Mkuu huyo wa Mkoa kama Adui wa Uhuru wa vyombo vya habari Nchini.Vyombo vya habari vinapaswa kuendelea kuwa imara na kusimama kwenye Misingi yao pasipo kuogopa ama kupokea vitisho

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani