1 day ago

Michuzi

DC MUFINDI ASISITIZA MPANGO WA CHAKULA CHA MCHANA KWA WANAFUNZI.

Na Ofisa Habari Mufindi  Serikali Wilayani Mufindi Imewataka wajumbe wa kamati za Shule na viongozi wa Serikali za vijiji kwa kushirikiana na wazazi, kutekeleza mpango wa utoaji chakula cha mchana kwa wanafunzi wanapokua shuleni kwa lengo la kuongeza ufanisi wakati wa kujifunza na kuleta matokeo chanya.  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi iliyofanyika Kata ya Nyololo Wilayani...

 

4 days ago

Mwanaspoti

Wachezaji 80 wataka kusajiliwa Njombe Mji

Zaidi ya wachezaji 80 walioachwa na timu zao zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini na nje ya nchi wamejitokeza kutaka kusajili wa Klabu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe baada kutangaa kufanya usajili.

 

4 days ago

Michuzi

MAMIA YA WANANCHI WAJITOKEZA KUJISAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WILAYA YA MUFINDI


Wananchi wa Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wamejitokeza kwa wingi kusajili Vitambulisho vya Taifa kufuatia maelekezo ya Mkuu wa mkoa huo Mhe. Amina Masenza ambaye amejizatiti kuweka historia ya kuwa mkoa wa kwanza kwa wananchi wake kuwa na Vitambulisho vya Taifa; baada ya kufanikisha kwa asilimia kubwa zoezi la kuwasajili Watumishi wa Umma lililofanyika nchi nzima.

Kwa kuanza; zoezi la Usajili kwa mkoa wa Iringa limeanza katika Wilaya ya Mufindi ambapo zaidi ya wananchi 70,000...

 

5 days ago

Channelten

Kero ya daraja Miaka 7 Kilolo Idete Iringa

DARAJA LA IRINGA

ZAIDI ya kaya 600 zenye watu 2000 katika kijiji cha Kiwalamo kata ya Idete katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa zinatarajia kunufaika na ujenzi wa daraja la mto Lukosi linalounganisha kijiji hicho na maeneo ya jirani ambalo limekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo kwa takribani miaka 6 baada ya serikali wilayani humo kutenga kiasi cha shilingi milioni 239 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.

 

Hili ndio daraja katika mto Lukosi ambalo linaunganisha kijiji cha...

 

2 weeks ago

Channelten

Mbegu bora zao la mahindi, Wakulima Mufindi watakiwa kuunda vikundi

SAM_0652

WAKULIMA wa zao la Mahindi katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vidogo vidogo , ili waweze kupata mbegu kwa gharama nafuu, lakini pia kuwa na shamba darasa.

Taarifa ya Rose Chapewa kutoka Mufindi Mkoani Iringa inafafanua zaidiÖ.

Meneja wa kampuni inayozalisha mbegu za mahindi aina ya Pana Mikoa ya Nyanda za juu kusini Tolio Mafie , ametoa ushauri huu kwa wakulima wa zao la mahindi katika vijiji vya Malangali na kitelewasi Wilayani Mufindi, akiwataka...

 

2 weeks ago

Channelten

Vijana katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wana nafasi nzuri zaidi ya kuondokana na changamoto ya umasikini

download

IMEELEZWA kuwa vijana katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wana nafasi nzuri zaidi ya kuondokana na changamoto ya umasikini wa kipato ikilinganishwa na vijana wenzao katika maeneo mengine nchini kutokana na wilaya hiyo kuwa na maeneo mengi yaanayofaa kwa kilimo cha mbogamboga na matunda msimu mzima wa kilimo.

Vionjo ktk wimbo huo wa msanii Prof Jay wa ‘KAZI KAZI’ vinakumbusha umuhimu wa vijana kufanya kazi. Vijana ni nguvu kazi muhimu nchini lakini upo ushahidi ktk sehemu nyingi nchini wa...

 

2 weeks ago

Michuzi

WANANCHI KILOLO MKOANI IRINGA WATAKIWA KUUZA MAZAO YAO KWA VIPIMO SAHIHI

 Mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  mkoani  Iringa  Asia  Abdalah  akiwataka  wananchi wa  kijiji  cha Irindi na Magana  kata ya  Mahenge  kuachana na uuzaji mazao kwa  vipimo batiliMkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  Asia Abdalah  akiwahutubia  wananchi  mwenye   kilembe  cha madoa mekundu ni meneja  wa  vipimo  mkoa wa Iringa Zainabu Kafungo. Kwa taarifa kamili BOFYA...

 

2 weeks ago

Michuzi

MUFINDI YAENDELEA KUTEKELEZA SERA YA KUWA NA ZAHANATI KILA KIJIJI.

Na Afisa Habari MufindiHalmashauri ya Wilaya ya Maufindi imeendelea kutekeleza sera ya serikali ya kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati kwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye  zahanati za Vijiji vinne kati ya vitano zilizopo kata ya Ihalimba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi umetekelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Festo Mgina, Diwani wa kata Ihalimba Mh. Award Mahanga sanjari na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri Prof. Riziki...

 

3 weeks ago

Michuzi

WAKULIMA WA KIJIJI CHA IPILIMA WILAYANI MUFINDI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA SHAMBA DARASA KUTOKA YARA TANZANIA

Aidan Timos (pichani kulia) ni mkulima wa mahindi na nyanya kutoka kijiji cha Ipilimo, wilayani Mufindi mkoani Iringa. Aidan amekuwa mkulima mashururi aliefanikiwa kubadili kilimo chake cha mazoea na kwenda kwenye kilimo cha biashara baada ya kupata elimu ya lishe linganifu ya mimea kutoka Yara Tanzania Ltd miaka miwili iliyopita. 
Kutokana na jitihada zake kwenye kilimo, wanakijiji walimteua kuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho. Mwanzoni mwa msimu huu wa mahindi, Timos aliwakaribisha Yara...

 

4 weeks ago

Channelten

Mbio za Mwenge Kilolo Iringa, wakulima washauriwa hili

FB_IMG_1466382718514

WAKULIMA katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wameshauriwa kuanzisha viwanda vidogo katika ngazi za vijiji ili kuongeza thamani ya mazao yao kwa kuyasindika badala ya kuendelea na mazoea ya kuyapeleka sokoni yakiwa hayajasindikwa.

Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ki-Taifa Bw. Amour Hamad Amour wakati wa ziara ya kukimbiza mwenge wilayani Kilolo ambapo umezindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi 8 ya maendeleo yenye jumla ya shilingi million 14.9...

 

4 weeks ago

Channelten

Hatarini kwa njaa Wangingíombe mkoani Njombe

 

Njombe.8

WANANCHI wa tarafa ya Wangingíombe iliyopo katika wilaya ya Wangingíombe mkoani Njombe wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na baa la njaa kufuatia upungufu wa mvua katika msimu huu wa kilimo uliosababishwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira ikiwemo vyanzo vya maji.

Wananchi hao ktk tarafa hiyo ambao walipata fursa ya kuongea mbele ya timu ya kikosi kazi maalumu cha ki-taifa kilichoundwa na makamu wa rais samiah suluhu Hassan kwa lengo la kunusuru mto ruaha mkuu wamesema hali ya...

 

1 month ago

Channelten

Uharibifu chanzo cha maji hifadhi ya Kitulo, Kikosi Kazi Maalumu cha Ki-Taifa Mguu kwa mguu mkoani Njombe

KITULO

Kilimo cha viazi na ufugaji pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo katika Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe vimetajwa kuwa moja ya sababu zinazochangia kwa kiasi kikubwa kuharibu vyanzo vya maji katika hifadhi hiyo ambavyo baadhi yake vinatiririsha maji yake kwenye mfumo wa ikolojia ya bonde la mto Ruaha Mkuu.

Kikosi Kazi Maalu cha Ki-Taifa kinabisha hodi mkoani Njombe katika wilaya ya Makete ambayo takwimu zinatuambia wilaya hii ina jumla ya vyanzo vya maji 742 ambavyo baadhi...

 

1 month ago

Channelten

Kilimo cha miti wilayani Mufindi kimeshika kasi ya ajabu inayopelekea Upandaji Miti hovyo

153

 

IMEELEZWA kuwa kasi kubwa ya upandaji wa miti usiozingatia uhifadhi wa mazingira unaofanywa na  wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ni moja ya sababu inayochangia uharibifu wa vyanzo vya maji katika maeneo mengi wilayani humo ikiwemo baadhi ya mito ambayo inatiririsha maji yake kwenye mto Ruaha mkuu.

Kilimo cha miti wilayani Mufindi kimeshika kasi ya ajabu. Wakati agizo la serikali kupanda miti milioni 1 na nusu kwa mwaka kwa kila wilaya, mwaka jana pekee wilaya...

 

1 month ago

TheCitizen

From Njombe with ‘Mdindifu’ drink

It rained cats and dogs, as the old saying goes. But we still had one task to undertake before seriously embarking on our road trip from Makambako to Morogoro on our way back to Arusha.

 

1 month ago

Channelten

JESHI la Polisi wilayani Mufindi linawashikilia watu wawili wakazi wa kijiji cha Ihanganatwa kwa tuhuma za kujihusisha na kilimo cha bangi

IMG_20170406_142352

JESHI la Polisi wilayani Mufindi mkoani Iringa linawashikilia watu wawli wakazi wa kijiji cha Ihanganatwa kata ya Maduma kwa tuhuma za kujihusisha na kilimo cha bangi.

cha zaidi ya vitalu vitatu hali inayosababisha kuendelea kusambaza madawa ya kulevya katika kijiji chao.

Akizungumza wakatia wa zoezi la uteketezaji wa madawa hayo ya kulevya aina ya bangi, mkuu wa wilaya ya Mufindi Bw. Jumuhuri William amesema zoezi hilo ni endelevu na amewataka wananchi ambao wanaojihusisha na kilimo hicho...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani