2 weeks ago

Michuzi

MADIWANI WA CCM WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI JIMBO LA HAI WAKABIDHIWA VYETI


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .
MSIMAMIZI wa uchaguzi katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro , Ndugu Yohana Sintoo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika kata tatu zilizokuwa hazina uwakilishi limekamilika salama na kuwapata viongozi watakaowawakilisha wananchi kwenye kata husika.


Ndg Sintoo ameyasema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani wateule watatu walioshinda  kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 26 mwaka huu.


“Ndugu zangu mtakumbuka kuwa mwishoni mwa...

 

3 weeks ago

Malunde

ALIYETAJWA KUFARIKI DUNIA AJALI YA NDEGE ARUSHA, YUPO HAI

Mfanyakazi wa hoteli za kitalii za andBeyond Serengeti, Moses Muhina aliyetajwa kuwa ni miongoni mwa abiria waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Shirika la Coastal Aviation, imebainika alibadili ndege muda mfupi kabla ya safari ili kuwahi kazini.

Muhina ambaye ni mwongozaji watalii katika hoteli hiyo, alikuwa aondoke na ndege ya Coastal Aviation saa nne asubuhi lakini viongozi wa hoteli walimbadilishia ndege, hivyo aliondoka na Air Exel iliyofika salama Serengeti.

Akizungumza na gazeti...

 

1 month ago

Bongo Movies

Hussein Machozi Nusura Azikwe Hai

Msanii wa Bongo Fleva ambaye aliwahi kucheza soka kabla ya kuanza kung’ara kupitia nyimbo zake za Full Shangwe, Utaipenda, Kafia Gheto na nyingine, Hussein Machozi naye yaliwahi kumkuta makubwa.


Mbali na muziki, lakini ni mmoja kati ya wasanii ambao wana vipaji vya kucheza soka. Machozi anafunguka kuhusiana na tukio ambalo hatalisahau katika maisha yake:
“Kuna siku nikiwa mkoani Kagera katika uwanja wa mazoezi wa Kagera, wakati huo nilikuwa nikiichezea Kagera Sugar B, tulikuwa tunafanya...

 

2 months ago

BBCSwahili

Waliomuingiza mtu mweusi katika jeneza akiwa hai wafungwa Afrika Kusini

Wakulima wawili wa Afrika Kusini waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza akiwa hai wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela

 

2 months ago

Michuzi

VITAMBULISHO VYA TAIFA VYAKUSANYA MAELFU YA WANANCHI WA KATA MASAMA MASHARIKI WILAYA YA HAI –KILIMANJARO

ZOEZI la Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoani Kilimanjaro limechukua sura mpya baada ya wananchi kuendelea kuhamasika na kufurika kwa wingi kwenye vituo vya Usajili kujisajili.
wananchi wa Kata ya Masama Mashariki Wilaya ya Hai ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa katika kituo cha Usajili kilichopo kwenye kijiji cha Mbweera, Mboreny, Sonu, Ngira na Sawe. Zoezi katika Kata hiyo litamalizika Jumatano 18/10/2017 kabla ya kuhamia Kata za Masama Magharibi na Kata ya Kia. 
Zoezi...

 

2 months ago

Michuzi

MAHAKAMA YATOA AMRI NG’OMBE WALIOTAIFISHWA KUPIGWA MNADA NA MWANDISHI MAALUM - MWANGA

NG’OMBE waliotaifishwa na serikali katika wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wamatarjiwa kupigwa mnada kufuatia uamuzi wa mahakama.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, wakati alipokwenda kukagua lindo la ng’ombe hao, jana eneo la Mgagao, wilayani Mwanga, walikohifadhiwa.
“Kufuatia uamuzi wa mahakama, ng’ombe hawa watauzwa kwa njia ya mnada siku ya Ijumaa, Oktoba 20, mwaka huu, kutokana na hali za ng’ombe hawa kutokuwa nzuri”, alisema.
Aliongeza, “Tayari mahakama...

 

2 months ago

Channelten

Operesheni ya kusaka Mifugo, Waziri aendesha operesheni kali Mwanga

MIFUGO MPINA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameendesha operesheni kubwa ya kusaka mifugo iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria katika Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuonya kuwa kazi hiyo inayoendelea isihusishwe na ushirikiano mwema uliopo baina ya Tanzania na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema watu watakaokamatwa katika operesheni hiyo watashughughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi kama wahalifu wengine na kueleza kuwa muda wa siku 7 alioutoa kwa mifugo yote...

 

2 months ago

Channelten

Wachimbaji watatu wafukiwa na Kifusi, Mmoja aokolewa akiwa hai

WACHIMBAJI

Wachimbaji watatu wamefukiwa na kifusi cha Udongo katika Machimbo yasiyo rasmi katika Kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita,huku mmoja akiokolewa akiwa hai na wawili wakifariki dunia.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Lwamgasa Samweli Shosha amesema tukio la kwanza limetokea oktoba 9 majira ya usiku ambapo Mchimbaji Emanuel Dimba(30)alifukiwa na kifusi wakati akiwa ndani ya duara amelala na la pili oktoba 10 likimhusisha Fikiri Paul(27)mkazi wa kijiji cha Mlanda Wilayani Chato mkoani Geita...

 

2 months ago

BBCSwahili

Syria waweka hai matumaini ya Kombe la Dunia

Omar Al Somah alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti dakika za mwisho na kuweka hai matumaini ya Syria kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 kwa kutoka sare ya 1-1 na Australia.

 

3 months ago

Michuzi

WAKULIMA WILAYANI HAI WASIFU MRADI WA N2AFRICA KWA MBEGU BORA ZA MAZAO YA MAHARAGE

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Wakulima wadogo katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro wameipongeza Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo ya (IITA) yenye makao makuu yake nchini Nigeria kwa teknolojia walizoanzisha za kutafiti wadudu waharibifu na aina mpya ya mbegu za maharagwe aina ya Jesca, Lyamungo 90 na Uyole njano wanazozitoa kwa wakulima.

Wakulima hao wamesema kuwa mbegu hizo zimepelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya mbogamboga jamii ya mikunde...

 

3 months ago

CHADEMA Blog

MAELEZO YA MBUNGE WA ROMBO MHESHIMIWA JOSEPH SELASINI KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA TUNDU LISSU

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari."Hao watu walipoona hawashuki

 

3 months ago

BBCSwahili

Huenda kiongozi wa Islamic State bado yuko hai

Mwezi Juni Urusi ilisema kuwa kulikwa na uwezekano kuwa Baghdad, alikuwa ameuawa mapema kwenye shambulizi la angani mjini Raqqa

 

4 months ago

Michuzi

PROFESA NDALICHAKO AVUTIWA NA KITUO CHA MAFUNZO KWA VITENDO CHA KIKULETWA WILAYANI HAI

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kushoto) akifurahia madhari ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme,kulia ni Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika.Picha kwa hisani ya ATCWaziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akifurahia madhari ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Kituo cha kuzalisha umeme cha...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani