7 days ago

Mwananchi

Watatu wafariki dunia Simanjiro

Watu watatu wakazi wa Kijiji cha Narakauwo Kata ya Loiborsiret, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamefariki dunia kwenye ajali baada gari walilokuwa wamelipanda kuacha njia na pinduka.

 

2 weeks ago

Channelten

Wananchi watoa ya Moyoni Mgawanyiko Soko la Hanang

SOKO HANANG

Wafanyabiashara wa soko dogo la Nangwa wilayani Hanang wameiomba serikali kuwaondoa wafanyabiashara wenzao wanaofanya biashara nje ya soko na kuwapeleka ndani ya soko hilo ili kuwepo usawa katika biashara zao ambapo kwa sasa wanadai wanawazuia wateja kufika sokoni hapo na kuishia njiani kwa waliopo nje ya soko.

Kilio hicho wanakitoa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya hanang chini ya mkuu wa wilaya ySara Msafiri Ally katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika eneo hili...

 

3 weeks ago

Mwananchi

Katibu wa Chadema Simanjiro aachia ngazi

Katibu wa Chadema Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Frank Oleleshwa ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo na kuzua taharuki kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa eneo hilo.

 

4 weeks ago

Mwananchi

Mifugo 4000 yafa kwa ukame Simanjiro

Mifugo zaidi ya 4,000 ya wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imekufa kwa kukosa maji na malisho kutokana na ukame ulioikumba wilaya hiyo.

 

1 month ago

Habarileo

U/Ndege wa kimataifa kujengwa Babati

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imepanga kujenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa katika eneo la Ngungungu – Mamire wilayani Babati mkoani Manyara ili urahisishe mawasiliano kwa mikoa mitano inayozunguka mkoa huo.

 

1 month ago

Habarileo

Majaliwa ataka Babati watunze daraja

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa mji wa Babati na kata za jirani walitunze daraja la Bonga kwa kulinda miundombinu iliyowekwa kwa manufaa yao na nchi.

 

1 month ago

Michuzi

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI NA KUHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI BABATI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati  kuhitimisha  ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Babati wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati kuhutubia mkutano wa hadhara, Februari 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee  wakati alipoingia kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati,...

 

1 month ago

Michuzi

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BABATI

 Baba mmoja mabaye jina lake halikupatikana akiwa amembeba mwanae kwa mtindo wa 'Kangaroo Style' wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza na wanakijiji  wa Singu wilayani  Babati, Februari  21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la daraja la Bonga- Endanachan wilayani Babati,  Februari 22, 2017.  Kulia ni Mkoa wa Manyara, Dkt, Joel Bendera na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi.(Picha na Ofisi ya Waziri...

 

1 month ago

Michuzi

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MBULU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimiana wanakwaya wa Shule ya Sekondari ya Singiland wilayani Mbulu wakati alipowasili kwenye uwanja wa michezo wa Mbulu kuhutubia Mkutano wa hadhara, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Mbulu mkoani Manyara, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

1 month ago

Michuzi

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA YAKE BABATI NA MBULU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sukari na nishati ya kuni inayotengenezwa kwa kutumia makapi ya miwa inayokamuliwa katika kiwanda cha sukari cha Manyara wakati alipotembelea kiwanda hicho Februari 19, 2017. Kuni hizo zina ubora unaofanana na ule wa makaa ya mawe na hutumika zaidi katika mitambo inayotumia nishati ya kuni. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kulia kwa Waziri Mkuu, ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera. Waziri Mkuu, Kassim...

 

1 month ago

Michuzi

MAJALIWA ATETA NA MBUNGE WA SIMANJIRO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Simanjiro, James Ole Milya kwenye Ikulu Ndogo ya Orkesimet wilayani Simanjiro Februari 16, 2017. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia kwaya ya Wamasai wa Simanjiro wakati alipowasili kwenye uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjairo mjini Orkesimet Februari 16, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa...

 

1 month ago

Michuzi

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIMANJIRO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Februari 16, 2017.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya wilaya ya Simanjiro kutoka kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Zephania Chaula baada ya kusomewa taarifa hiyo kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Februari 16, 2017.Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula akisoma...

 

1 month ago

Ippmedia

Wazee wa makabila manne makuu ya wilayani Kiteto wakubaliana kumaliza migogoro ya ardhi

Wazee wa makabila manne makuu ya wilayani Kiteto mkoani Manyara yamemhakikishia waziri mkuu Mhe.Kassimu Majaliwa kwamba hakutakuwa na mapigano yatakayotokana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji mara baada ya kuridhiana kwa kuchinja kondoo na kuku ili kukubaliana kutafuta amani ya kudumu,huku waziri mkuu akiwataka viongozi wa serikali kutatua mgogoro wa mpaka kati ya wilaya za Kiteto na Chemba.

Day n Time: Jumatano Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

1 month ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI KITETO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017. Wananchi wa Kiteto wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto Februari 15, 2017.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka Mzee Mbambire Oloi Kurukur, jani la mti ikiwa ni ishara ya amani ya kukomesha mapigano kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto kabla...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani