3 days ago

Ippmedia

Mashamba ya bangi yenye ukubwa wa zaidi ya ekari mia moja na ishirini yakamatwa wilayani Tarime

Vyombo vya dola katika kanda maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara kwa kushirikiana na watendaji mbalimbali wa serikali wilayani Tarime,vimendelea na oparesheni kali ya kupambana na kilimo cha zao haramu la bangi na kufanikiwa kukamata mashamba yenye ukubwa wa zaidi ya ekali 120 ambayo yamelimwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kisha kufyekwa na kuteketezwa kwa moto.

Day n Time: Alhamisi Saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

4 days ago

Bongo Movies

Ostazi Juma na Musoma Anajifunza Nini Kwa Fella, Tale na Sallam Sk?

KUNA watu wamepata umaarufu katika namna ya kuchekesha kidogo. Unamkumbuka yule aliyejiita Mganga wa Diamond? Katika namna isiyotarajiwa, eti ghafla na yeye akawa maarufu tena maarufu sana. Kila eneo akasifika. Kuanzia kwenye blog, magazeti hata katika baadhi ya vipindi vya televisheni akawa anatajwa kila wakati. Ila sasa yuko wapi? Yale maneno na ahadi alizotoa juu ya Diamond ziko wapi? Diamond bado anashikilia usukani wa Bongo Fleva huku yeye akiwa taabani.

Ostazi Juma na Musoma

Kama...

 

3 weeks ago

MillardAyo

VIDEO: Ni kweli Wanawake Tarime bado wanapenda kupigwa na Mume?

Mapenzi ni Mubashara na huu ndio mwezi wake ambapo kilele cha siku ya Wapendanao ni February 14 ambapo kwenye kuisubiria siku yenyewe, AyoTV inatembeza camera yake kwenye kona mbalimbali za Tanzania. Siungi mkono kitendo cha mtu yeyote kupigwa iwe Mwanamke au Mwanaume lakini tumekua tukisikia kwamba Wanawake wa kikurya kutoka Mara huwa wanalazimisha kupigwa na Waume […]

The post VIDEO: Ni kweli Wanawake Tarime bado wanapenda kupigwa na Mume? appeared first on millardayo.com.

 

3 weeks ago

Channelten

Polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya imefanikiwa kuteketeza mashamba makubwa ya bangi

Polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya imefanikiwa kuteketeza mashamba makubwa ya bangi pamoja na nyumba zinazotumiwa kama sehemu ya maficho na wakulima wa zao hilo haramu huku ikifanikiwa kukamata zana mbalimbali za kilimo zilizokuwa zikitumiwa na wakulima wa bangi huko katika kijiji cha Wegita wilayani Tarime mkoani Mara.

Msako mkali unaoendeshwa na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Tarime unabaini nyumba zilizotumika kama maficho ya wahalifu hao pamoja na mashamba makubwa ya bangi...

 

3 weeks ago

Michuzi

MKURUGENZI AMVUA MADARAKA MWALIMU MKUU WA BUNDA B KWA UDAGANYIFU.

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Janeth Mayanja amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunda B, Bw. Laurent Agustino kwa tuhuma za kushiriki kusaidia mwanafunzi mmoja kufanya udanganyifu katika mtihani wa darasa la nne.
Mwalimu huyo anatuhumiwa kumruhusu mwanafunzi wa darasa la tano kufanyia mtihani wa mwanafunzi wa darasa nne kwa lengo la kumsaidia mwanafunzi huyo ambaye hajui kusoma wala kuandika ili aweze kufaulu.
Mkurugenzi huyo...

 

4 weeks ago

Malunde

MUUGUZI WA HOSPITALI YA WILAYA AFARIKI AKICHOTA MAJI TARIME

MUUGUZI wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Magreth Anatoly (57), amefariki dunia kwa shinikizo la damu wakati alipokuwa akisomba maji kutoka kwenye tangi la lori lililokuwa limepeleka maji katika hospitali hiyo, ambayo imekumbwa na ukosefu mkubwa wa maji.
Mfanyabiashara na kada wa CCM, Peter Zakaria amejitolea kutoa lori lake lenye tangi la maji kupeleka maji katika hospitali hiyo pamoja na Magereza wilayani hapa.
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo ya wilaya, Calvin Mwasha amethibitisha...

 

4 weeks ago

Habarileo

Bunda kutumia bil 39/- kwa miradi ya maendeleo

HALMASHAURI ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, kwa mwaka wa fedha 2017/2018, inatarajia kutumia Sh 39,015,963,943, kwa ajili ya uendeshaji wa halmashauri na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo, kutoka kwenye vyanzo vyake yenyewe na ruzuku kutoka Serikali Kuu.

 

1 month ago

TheCitizen

Tarime approves Sh29b for 2017/18 fiscal year

District councillors have approved Sh29 billion for the 2017/18 fiscal year. Acting chairman Bashir Abdalah said yesterday that they were set to collect over Sh1 billion from internal sources.

 

2 months ago

MillardAyo

Jamaa aliyemtahiri mwanawe kwa kisu kortini Bunda

amtahiri

Kila asubuhi Millard Ayo atazisogeza karibu yako habari zote kubwa kutoka kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania ambapo huwa naziweka kwenye page ya Twitter ya @millardayo na kwenye Youtube ya millardayo bila kusahau millardayo.com. Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii ya kwenye gazeti la Habari leo yenye kichwa cha habari […]

The post Jamaa aliyemtahiri mwanawe kwa kisu kortini Bunda appeared first on millardayo.com.

 

2 months ago

AllAfrica.Com

Tanzania: Tarime Town Council Head of Human Resources Department Suspended for Inefficiency


Tanzania: Tarime Town Council Head of Human Resources Department Suspended for Inefficiency
AllAfrica.com
Tarime — Tarime Town Council Director, Mr Elias Ntiruhungwa, has suspended the council's head of human resources department, Mr Jeveryson Kaguna and a nursing officer of Tarime District Hospital, Kegosa Nega, for underperformance. "I am suspending ...

 

2 months ago

Habarileo

Debe la mahindi 20,000/- Bunda

WAKAZI wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, ambapo sasa bei ya mahindi imepanda. Bei hiyo imetoka sh 14,500 kwa debe moja la mahindi hadi sh 20,000, mtama sh 10,000 hadi sh 17,500, udaga umetoka sh 12,500 hadi sh 17,500 huku ulezi ukifikia sh 30,000 kwa debe.

 

2 months ago

Ippmedia

Jeshi la polisi lakamata Mangariba 11 kwa tuhuma za ukeketaji wilayani Tarime

Jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya mkoani Mara, limefanikiwa kuwakamata mangariba kumi na moja wilayani Tarime kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uwakeketaji watoto wa kike zaidi ya 800 katika wilaya ya Tarime kinyume cha sheria.

Day n Time: jumapili saa 2:00 usikuStation: ITV

 

2 months ago

Michuzi

SIHABA NKINGA AKUTANA NA WAZEE WA KOO TANO WILAYANI TARIME

Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wazee wa Kimila kutoka Koo Tano Mkoani Mara wamemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuwawezesha kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.

Akiongea wakati walipokutana na Katibu Mkuu aliyepo Wilayani Tarime Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo...

 

2 months ago

Michuzi

TANZIA: MAZISHI YA BIBI CATHERINE MARWA (89) YAFANYIKA KENYAMANYORI TARIME MKOANI MARA.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Tarime mkoani Mara, akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu, bibi Catherine Seba Marwa (89). Mazishi yamefanyika hii leo katika Kata ya Kenyamanyori wilayani Tarime.Na BMGNdugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa marehemuMtoto wa marehemu (kushoto) akiwa na shemeji yake, wakiweka shadaViongozi wa dini wakiweka mashada Marehemu, bibi Catherine Seba Marwa (89), enzi za uhai wake. Mola aipumzishe roho ya marehemu, mahala pema, peponi,...

 

2 months ago

Michuzi

MASHINDANO YA MITUMBWI MUSOMA VIJIJINI YAMALIZIKA

Mashindano ya Mitumbwi Musoma Vijiji yaliyoshirikisha Kata 12 yamemalizika kwa Kata ya Etaro kuibuka na ushindi na hivyo kujinyakulia fedha tasilimu milioni moja pamoja na kombe.
Mashindano hayo yaliandaliwa hivi karibuni na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ajili ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 ambapo washindi wa pili ambao ni Kata ya Nyakatende walijinyakulia shilingi 750,000 na washindi wa tatu ambao ni Kata ya Suguti kujinyakulia shilingi 500,000 na...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani