2 days ago

Michuzi

MASHAMBA YA MPUNGA YA MBARALI NA KAPUNGA YAPEWA ONYO KALI NA KIKOSI KAZI CHA KITAIFA CHA MTO RUAHA.


Kampuni inayojishughukisha na kilimo cha Mpunga ijulikanayo kwa jina la  Highland Estates iliyopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya imepewa agizo na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha kilichoko mkoa wa Mbeya kuwa ndani ya mwezi mmoja wahakikikishe wamesafisha mifereji yote inayozunguka ndani ya shamba lao  kwa kujenga upya miundombinu inayopoteza maji ,  kung'oa magugu maji na nyasi zote zilizoota katika mifereji ya matoleo ya maji ndani ya shamba hilo  kwani inazuia...

 

5 days ago

Michuzi

HALIMASHAURI YA MBARALI YATAKIWA KUWEKA MIFUGO YOTE CHAPA ILI KURAHISISHA UDHIBITI WAKE KATIKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Halimashauri ya Wilaya ya Mbalari imeagizwa kuhakikisha ng’ombe wote wa Wilaya hiyo wanawekewa chapa ili kurahisisha kuweza kujua ng’ombe wote wa Wilaya hiyo. Pia kila mfugaji awe na ng’ombe wasiozidi arobaini tu ili kuweza kuzuia uharibifu wa mazingira uanaosababibshwa na mifugo wengi kupita kiasi. 
Katika maagizo hayo pia Halimashauri ya Wilaya ya Mbarali imetakiwa kushirikiana na Wananchi wake kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuepuka uharibifu mkubwa wa mazingira ...

 

1 week ago

Bongo5

Music: Bebe Cool x Sauti Sol – Mbozi Za Malwa

Msanii Bebe Cool kutoka Uganda na kundi la Saut Sol kutoka Kenya wameachia wimbo unaitwa “Mbozi Za Malwa”.

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!Share on Whatsapp

 

3 weeks ago

MwanaHALISI

Bodi ya Chai Rungwe kuvunjwa

MBUNGE wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda ameitaka Serikali kuvunja bodi ya chai ya Wilaya ya Rungwe kwa sababu wananchi hawana imani na bodi hiyo na haina faida kwao, anaandika Dany Tibason. Mwakagenda alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza ambao ameema wawekezaji wameingizwa kwenye bodi hiyo ambao kimsingi wanajiwekea matakwa yao. “Mfano mmiliki wa ...

 

3 weeks ago

Mwananchi

CCM yamtosa Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Mbozi

Vwawa. Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe, kimemuondolea udhamini Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Erick Ambakisye kwa madai ya kushindwa kuisimamia na kusababisha upotevu wa fedha za umma na upatikanaji wa hati zenye shaka kwa miaka minne mfululizo.

 

1 month ago

Michuzi

PROFESA MWANDOSYA AENDELEA KUTANGAZA KIVUTIO CHA UTALII CHA MATEMA BEACH WILAYANI KYELA MKOA WA MBEYA

 Waziri mstaafu Profesa Mark Mwandosya akiwa ameamka alfajiri na mapema ili kufanya mazoezi na kuzunguka katika ziwa Nyasa hususan kwenye fukwe maarufu na mwanana za Matema wilayani Kyela mkoani Mbeya. Fukwe hizo ni mojawapo ya vivutio vikubwa vya utalii kwa kuwa na mandhari ya kupendeza, samaki wa kila aina pamoja na utengenezaji wa vyungu, magudulia na mitungi vya udongo. Profesa Mwandosya ameiambia Globu ya Jamii kwa njia ya mtandao kwamba Matema Beach pia ni location nzuri sana kwa...

 

1 month ago

Bongo Movies

VIDEO:Mzee Hashim Rungwe Autaka Ukocha wa Taifa Stars

Mwenendo usioridhisha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, umemuibua Mwenyekiti wa chama cha siasa cha Ukombozi wa Umma, (CHAUMMA), Mzee Hashim Rungwe, kutaka yeye ndiyo aitwe kuwa kocha wa timu hiyo.

Mzee Rungwe ambaye alikuwa KIKAANGONI ya EATV, alikutana na swali lililomkumbusha wakati alipowahi kutamka kuwa anahitaji kuwa kocha wa timu, ambapo mzee Rungwe amekiri na kusisitiza kuwa bado anaihitaji nafasi hiyo hata sasa.

“Mimi nina uzoefu, nimecheza mpira, mimi ni mtu wa mpira,...

 

1 month ago

Mwananchi

Wakazi wa Kyela washangilia meli kushushwa Ziwa Nyasa

Hivi karibuni, wakazi wa Kyela Mkoa wa Mbeya, walilipuka kwa kupiga mayowe na shangwe za furaha baada ya meli mbili za mizigo zilizotengenezwa na kampuni ya kizalendo ya Marine Transport Ltd ya jijini Mwanza, kushushwa Ziwa Nyasa, kwa majaribio ya awali baada ya kukamilika kwa asilimia 95.

 

1 month ago

CHADEMA Blog

MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE CHADEMA KYELA AFARIKI DUNIA

Mamia ya Wananchi wa Kyela - Mbeya tarehe 12 Machi, 2017 walikusanyika katika mazishi ya Antony R. Mapunda -Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Kyela na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Butiama kilichopo Kata ya Mbugani katika Mamlaka ya Mji wa Kyela.Marehemu ambaye kipindi cha uhai wake alisifika kwa uongozi uliotukuka na msimamo wake thabiti kwenye mambo mbalimbali ya uongozi na utendaji,

 

1 month ago

Dewji Blog

MO Dewji Foundation kushirikiana na Tulia Trust kujenga vyoo katika Hospitali ya Rungwe

Katika kuendeleza huduma zake kwa jamii, Taasisi ya MO Dewji imeungana kwa pamoja na Taasisi ya Tulia Trust inayomilikiwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson kujenga vyoo katika Hospitali ya Rungwe iliyopo mkoani Mbeya.

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo katika mashindano ya kukimbia ya Tulia Marathon, Mratibu Miradi wa Taasisi wa MO Dewji, Catherine Decker amesema taasisi yao imeamua kushirikiana na Dk. Tulia ili kusaidia kuboresha sekta ya afya ya nchini ambayo kwa sasa...

 

2 months ago

Mwananchi

Changamoto za ardhi Mbarali zitatuliwe, wananchi wanufaike

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla aliunda kamati inayojumuisha watalaamu wa ardhi kuchunguza uhalali wa watu kumiliki zaidi ya eka 100 wilayani Mbarali huku idadi kubwa ya wananchi wakiwa hawana ardhi ya kilimo.

 

2 months ago

Mwananchi

Polisi yawalaza saa 12 wakazi Ushirika, Rungwe

Wakazi wa kijiji cha Ushirika wilayani Rungwe wamelazimika kulala saa 12.00 jioni ya leo baada ya polisi kupiga mabomu ya kuwatawanya vijana wa bodaboda waliokuwa wakilishambulia gari la polisi walipofika kuwasaka watu walioiba mbolea.

 

2 months ago

Michuzi

SAFARI YA BAISKELI KUTOKA MBEYA KWENDA CHUNYA YADUMISHA UTALII WA NDANI NAKUTAMBULISHA RASMI MCHEZO WA BAISKELI MKOANI MBEYA


Safari hii iliandaliwa na Asasi mbili za Uyole Cultural Tourism Enterprises na ELIMISHA kwa ushirikiano na Chama cha waendesha baiskeli Mkoa wa Mbeya na Afisa Utamaduni wa Mkoa Bw.George Mbijima.
Awali, akiongea na wapenzi wa mchezo wa baiskeli,viongozi wa serikali na wanahabariAwali, wakati wa kuwaaga waendesha baiskeli Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Elias Mwasandele amewashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kuwaunga mkono zaidi sana Uyole Cultural Tourism na ELIMISHA kwa kufanikisha...

 

2 months ago

Mwananchi

Mbarali walia gharama kubwa ya kukodi mashamba

Wakulima wilayani Mbarali mkoa wa Mbeya wameiomba Serikali iwasaidie kupunguza gharama za kukodi ardhi ya kilimo kwa madai kuwa zipo juu.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani