6 days ago

Michuzi

TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA

Na Veronica Kazimoto, Geita.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesajili jumla ya wafanyabiashara wapya 600 katika kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyofanyika mkoani Geita ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Menenja wa TRA mkoani hapa James Jilala ameishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa...

 

1 week ago

Malunde

BABU WA MIAKA 69 AOA BINTI WA MIAKA 13 GEITA


Mzee John Mkubila akizungumza juu ya suala la kumuoa Binti wa miaka kumi na tatu wakati alipokuwa amekamatwa na jeshi la polisi jamii.***Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mzee  wa miaka sitini na tisa (69) kwa kosa la kumuoa binti mwenye umri wa miaka 13 ambaye mkazi wa kitongoji cha Rwenge kijiji cha Bugalama.

Mzee John Mkubila ambaye ni mkazi wa mtaa wa mwembeni kata ya Nyankumbu mjini Geita amekiri kumuoa binti huyo kwa makubaliano ya mzazi wa binti huyo kuwa awe anamsaidia kazi...

 

2 weeks ago

Michuzi

WANANCHI MKOANI GEITA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPATA ELIMU YA MLIPAKODI

Na Veronica KazimotoWafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita wamejitokeza kwa wingi kupata elimu ya mlipakodi inayoambatana na usajili wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na kupatiwa makadirio ya kodi kwa wafanyabiashara mbalimbali.
Akizungumza baada ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wa Wilaya ya Bukombe na Mbogwe wakati wa Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi inayoendelea mkoani hapa, Afisa Kodi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Maternus...

 

2 weeks ago

Michuzi

MKUU WA MKOA GEITA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE KAMPENI YA ELIMU KWA MLIPAKODI

Na Veronica Kazimoto-Geita
Wito umetolewa kwa wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita kujitokeza kwa wingi katika Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko, changamoto, maoni pamoja na kupata elimu ya masuala ya kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Geita, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa, wafanyabishara na wananchi watumie fursa ya kampeni hii itakayomalizika...

 

2 weeks ago

Michuzi

MAAFISA UGANI WAKABIDHIWA PIKI PIKI GEITA TC

Na Joel Maduka,Geita.
Halmashauri ya Mji wa Geita imetoa pikipiki nne(4) kwa Maafisa kilimo wa Kata ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuwatembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na wakulima katika maeneo yao.
Akikabidhi pikipiki hizo,mapema jana katika Ofisi za Halmashauri ya Mji Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Halmashauri hiyo kupitia viongozi wake kwa kuona umuhimu wa kununua pikipiki hizo ili ziweze kuwasaidia wataalam wa kilimo kutekeleza majukumu...

 

2 weeks ago

Michuzi

WAKULIMA KUNUFAIKA NA KILIMO CHA PAMBA GEITA

Na Joel Maduka,Geita
Serikali imewahakikishia mazingira yaliyo salama wakulima wa zao la pamba ikiwa ni pamoja na kununuliwa kwa zao hilo bila ya kukopwa kwa msimu wa pamba ambao unatarajia kuanza tarehe 1 Mei mwaka huu .
Hayo yameelezwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru , Charles Kabeho wakati akifungua mradi wa zao la pamba katika kijiji cha Nyamalimbe Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo alisema serikali imejipanga kuhakikisha mkulima wa pamba mwaka huu ananufaika na zao hilo.
“...

 

3 weeks ago

Michuzi

WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI GEITA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo, Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2,...

 

3 weeks ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AELEKEA GEITA KATIKA SHEREHE ZA KUWASHA MWENGE WA UHURU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Aprili 1, 2018 akiwa njiani kuelekea Geita ambako Aprili 2, 2018 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuwasha Mwenge wa Uhuru. Kulia ni mkewe Mama Mary Majaliwa.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Aprili 1, 2018 akiwa njiani kwenda Geita ambako Aprili 2 , 2018...

 

3 weeks ago

Michuzi

UJIO TAMASHA LA PASAKA MWANZA WAMFURAHISHA MBUNGE MABULA WA NYAMAGANA


*Awaomba wakazi Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi,asema ni fursa kwa wanamuziki wa Injili

Na Ripota Wetu,Globu ya jamiii

MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana ,Mwanza Stanslaus Mabula ameeleza kufurahishwa ha ujio wa Tamasha la Pasaka 2018 ambalo kwa mara ya kwanza linafanyika Jijini humo.

Ambapo amesema hiyo ni fursa kubwa kwa wasanii wa nyimbo za Injili katika Mkoa huo ambao una vipaji vingi vya waimbaji.

Akizungumza mapema leo na Michuzi Blog jijini Mwanza,Mabula amesema kutokana na ujio wa...

 

4 weeks ago

Malunde

MLIPUKO WAUA WACHINA WAWILI WAKICHIMBA DHAHABU GEITA

Raia wawili wa China wamefariki dunia na mlipuko wakati wakipasua mwamba kwa ajili ya kuchimba dhahabu katika mgodi unaomilikiwa na Mayala Ngweso, uliopo kijiji cha Nyamtondo wilayani Geita.

Akizungumza leo Jumanne Machi 27, 2018, kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba chanzo ni uzembe baada ya Wachina hao kulipua mwamba bila kuchukua tahadhari.

Amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Li Shaobin (44) na Qian Zhaorang (49) na kwamba,...

 

4 weeks ago

Michuzi

MBUNGE NYAMAGANA AWEKA MIKAKATI YA KUIBUA,KUENDELEZA MPIRA WA WAVU

Na Zainabu Nyamka,Globu ya jamii
MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana  Stanlaus Mabula ameweka mkakati wa kuibua, kukuza na kuendeleza mpira wa wavu ili  uwe ajira. 
Mabula amebainisha haya  leo kwenye uzinduzi wa Mpira wa Wavu wenye jina la Mrajam Volleyball Championship inayohusisha  vikosi nane kutokea Mwanza, Zanzibar, Manyara, Mara,  Shinyanga na kilele chake kuwa Machi 25/mwaka huu.
Akiwakilishwa na Ahmed Misanga kwa niaba yake amesema mbunge wa Nyamagana amefarijika michuano hiyo kuja kufanyikia...

 

1 month ago

AllAfrica.Com

Tanzania: Gold Miners Call for Geita Common Market


Tanzania: Gold Miners Call for Geita Common Market
AllAfrica.com
Geita — Artisanal gold miners in Geita Region have calling for the government to construct another market in the region in order to curb smuggling. They aired their views when speaking with officials of the opinion gathering committee, which was ...

 

1 month ago

Michuzi

WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU GEITA

Na Joel Maduka,Geita
Mkoa wa Geita unatarajia kunufaika na mradi kabambe wa usambazaji umeme vijijini REA awamu ya Tatu kwa kuongeza shughuli za kiuchumi kwa wananchi kutokana na vitongoji 220, vijiji 372 na Kata 499 ambazo zinatarajia kunuifaika na Nishati ya Umeme.
Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi REA meneja wa TANESCO Mkoani Geita Joachim Ruweta amesema Mradi huo kwa mzunguko wa kwanza utaunganisha wateja wapatao 12,944 na hivyo kukamilika kwa Mradi huo utafanya umeme...

 

1 month ago

Malunde

WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI..WATELEKEZA MWILI WA MAREHEMU KWENYE KITANDA CHA MWENYEKITI WA MTAA GEITA


Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Nyakabale wilayani Geita wametelekeza mwili wa marehemu nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa huo, Elias Ndarawa.

Ndarawa anatuhumiwa kutoshughulikia tukio la Zacharia Shaban kupigwa na polisi jamii hadi kufa.
Wananchi hao waliubeba mwili wa Zacharia na kuulaza kwenye kitanda cha mwenyekiti huyo.
Majaliwa Shaban ambaye ni ndugu wa marehemu Zacharia amesema leo Machi 12,2018 kwamba nduguye alipigwa Machi 5,2018 akiwa eneo la Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM) akiokota mabaki ya...

 

1 month ago

Michuzi

DC Nyamagana aipongeza Airtel na kusisitiza uaminifu kwa mawakala wa mitandao ya simu

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha ameipongeza Artel Tanzania kwa juhudi zake za kupeleka huduma kwa wateja huku pia akitoa onyo kwa Mawakala wa Mitandao ya simu kuacha hila na udanganyifu kwa wateja ili kujenga imani ya mitandao hiyo kwa Jamii.
Bi Tesha amebainisha hayo wakati akifungua moja ya maduka ya kisasa ya kutolea huduma ya kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel eneo la Nyegezi,jirani na kituo cha mabasi yaendayo maeneo mbalimbali nchini. “Wananchi wetu...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani