4 months ago

Zanzibar 24

Vijana Chakechake wafundwa juu ya dhana ya Diaspora

WAJUMBE wa mabaraza ya Vijana kutoka wilaya nne za Pemba, wakifuatilia hutuba ya Mkuu wa wilaya ya Chakechake Rashid Hadid Rashid, wakati alipokuwa akifungua semina juu ya dhana ya diaspora, semina iliofanyika skuli ya sekondari Madungu mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba) .

 

OFISA wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratib wa wazanzibari wanaoishi nje ya nchi, Ali Ameir Haji, akielezea dhana ya diaspora, kwa wajumbe wa mabaraza ya vijana wa wilaya nne za Pemba, kwenye semina...

 

4 months ago

Zanzibar 24

Mbunge wa Chakechake Pemba aainisha mafanikio ya Ahadi zake

Mbunge wa jimbo la chakechake kisiwani Pemba kwa tiketi  ya chama cha wananchi  CUF  Mh Yussuf Kaiza  Makame amesema kuwa kitendo  bora katika uwongozi ni kuahidi katika maendeleo na kisha kuzitekeleza ahadi kwa wananchi kama ulivyoahidi.

Kauli hiyo aliitoa leo katika ofisi mpya ya mbunge huyo huko chakechake mjini wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali juu ya kutazama vipi kiongozi bora anatakiwa awe kwa wananchi wake pamoja na utekelezaji wa ahadi...

 

4 months ago

Zanzibar 24

Habari Picha: Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba akikabidhi vespa kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya micheweni

Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba Omar Khamis Othman akikabidhi vespa kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini pemba kwa ajili ya urahishaji wa ufatiliaji wa kazi zao.

Vespa hizo zimetolewa kwa mkopo nafuu kwa madiwani hao.

Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman (alie vaa flana manjano) akiangalia Vespa aliowakabidhi Madiwani wa Halmashauri Wilaya ya Micheweni kushoto yake ni Katibu Tawala Mkoa Kaskazin Pemba Ahmed Khalid Abdallah Hafla hiyo iliyo fanyika...

 

4 months ago

Zanzibar 24

SMZ imetenga kiasi hiki, kwa ajili ya utanuzi na kuimarisha huduma za hospital ya Chakechake

 Jumla ya shilingi Millioni mia tatu na hamsini zimetengwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya utanuzi wa Hospitali ya Chakechake ili kuimarisha  huduma za Afya hospitalini hapo.

Akijibu swali la Nyongeza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani Nnje kidogo ya mji wa Zanzibar ,Waziri wa Afya Zanzibar Mahmod Thabit Kombo amesema kujengwa kwa Hospitali hiyo kutawasaidia wagonjwa kuondokana na Usumbufu wanaoupata ikiwemo ukosefu wa sehemu za kupumzikia.

Kukamilika kwa...

 

7 months ago

Zanzibar 24

Vikoba vyanawirisha ndoa Vitongoji Chakechake Pemba

WANAWAKE wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, wamesema kujiunga kwao kwenye vikundi vya kuweka na kukopa, ‘hisa’ ni hatua muhimu kwao kuwasaidia waume zao huduma za kila siku, hasa kwa vile hutokezea siku wanakosa.

Walisema wanaume hawana mkataba na Muumba, kwamba kila siku watakuwa wanakamilisha hudua za ndani ya nyumba, hivyo kuingia kwao kwenye vikundi hivyo vya kuweka hisa, pamoja na mambo mengine, lakini pia ni kuwasaidia wenza wao huduma za lazima.

Wakizungumza...

 

8 months ago

Zanzibar 24

Rais wa Zanzibar aweka jiwe la msingi Skuli mpya ya Chimba Micheweni Pemba

SKULI mpya ya msingi ya shehia ya Chimba wilaya ya Micheweni Pemba, ambayo jana iliwekewa jiwe la msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe: Dk Ali Mohamed Shein, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

WANAFUNZI wa skuli ya Kinowe msingi, waliohudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la skuli mpya ya Chimba wilaya ya Micheweni, ambapo kazi hiyo ilifanywa na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi...

 

9 months ago

Zanzibar 24

Video: CRDB yafungua tawi jipya Chakechake Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wateja wa Benki nyingi hapa nchini ni msongamano wa wateja pamoja na ucheleweshaji huduma na kuitaka Benki ya CRDB kuwa na mikakati katika kupambana na kadhia hiyo.

 Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Chake Chake Pemba, katika sherehe ya ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB likiwa Tawi la 280 ndani ya mtandao wa benki hiyo kutoka matawi 19 iliyokuwa nayo mara tu...

 

9 months ago

Michuzi

DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI JIPYA LA BENKI YA CRDB, CHAKECHAKE KISIWANI PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohanmed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo katika Mji wa Chake chake, kisiwani Pemba, Julai 29, 2017. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha na Mipando wa Zanzibar,...

 

9 months ago

Zanzibar 24

Wakaazi wa Micheweni wapo hatarini kukumbwa na maradhi, Pemba

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba wako hatarini kukumbwa na maradhi mbalimbali ikiwamo ya Nimonia, magonjwa ya kuharisha, surua rubela na mengineyo kutokana na kutokua na uwelewa wa kutosha katika huduma za afya hususan suala zima la chanjo.

Choma chanjo kuepuka maradhi hatari.

Wakizungumza na mwandishi wa habari kwa nyakati tofauti wazazi na walezi wa watoto katika maeneo ya wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini Pemba juu ya ushiriki wao katika kuwapatia...

 

9 months ago

Zanzibar 24

Picha: ZLSC wakiwa kwenye mkutano Wilaya ya Chakechake Pemba

Picha: Sheha wa shehia ya Mgogoni Wilaya ya Chakechake Jimbo la Wawi,  Juma Kombo Hairallwa, akifungua mkutano wa wazi wa kutoa msaada wa kisheria, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Tawi la Pemba na kufanyika Skuli ya Connecting Continent iliopo Mgogoni.

Picha: Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuali yalioulizwa na wananchi wa shehia ya Mgogoni Jimbo la Wawi, Wilaya ya Chakechake, wenye...

 

10 months ago

Zanzibar 24

Zoezi la ugawaji fomu nafasi mbali mbali wilaya ya chakechake Pemba sasa limeanza

JUMUIYA ya Wazazi ya CCM wilaya ya chakechake  mkoa wa kusini Pemba imewataka wanachama wa  jumuiya hiyo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi tofauti za uwongozi ili kukijenga chama hicho hatimae kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kauli hiyo imetolewa jana na katibu wa wazazi wilaya ya chakechake Bikiembe Ramadhan Khamis katika zoezi la ugawaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika jumuia hiyo, zoezi ambalo limeanza rasmin tarehe 2 jully 2017.

Akimkabidhi...

 

11 months ago

Zanzibar 24

Zawa iko mbioni kumaliza kilio cha Hospitali ya chakechake Pemba

Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) tawi la Pemba imesem anaendelea kuboresha  upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika hospitali ya Chake chake ili kuondoa kilio cha muda mrefu hospitalini hapo kutopata huduma hiyo kwa uhakika.

Hayo yamebainishwa leo na Afisa Mdhamini  Wizara ya ardhi mazingira maji na nishati Mh.Juma Bakari Alawi katika uzinduzi wa uchimbaji wa mtaro wenye lengo la kupeleka huduma hiyo katika hospitali ya Chake Chake .

Alawi amesema kuwa ZAWA kupitia wataalamu wake ...

 

11 months ago

Zanzibar 24

Huduma ya Maji yawagawa wakazi wa Mtoni Chakechake Pemba

Wananchi wa na wakaazi wa Mtoni wilaya ya chakechake Mkoa wa kusini Pemba wameitaka mamlaka ya maji Zanzibar ( ZAWA ) kuchukua hatua za haraka ili kutatua mzozo unaoonekana kukua siku hadi siku kutokana na upatikani wa huduma ya wa maji kijijini hapo. Wito huo umetolewa kutokana na pande mbili kijijini hapo Mtoni juu na Mtoni chini kuanza kushikana mashati baada ya Mtoni chini kuunga maji katika bomba iliyotokea Mtoni juu ambapo kila upande kati yao unajiona uko sahihi. Hayo...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Utafiti: Wakaazi wa micheweni Pemba wapo hatarini kwa kutotumia chumvi yenye madini joto

WAKAAZI wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wako hatarini kupata ugonjwa wa goita  pamoja na matatizo ya kuzaa watoto wenye udumavu wa akili  na kuharibu mimba  kwa akina mama baada ya  kubainika  kuwa chumvi yenye madini joto haitumiki ipasavyo  katika Wilaya hiyo.   Mkuu wa kitengo cha Lishe cha Wizara ya Afya Pemba Raya Mkoko amesema kuwa utafiti uliofanywa katika familia 2,685 ni  familia 345 sawa na asilimia kumi na tatu (13%)  ambazo zimebainika kuwa zinatumia chumvi zenye...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Wananchi Chakechake waishi na taka tani 150 kila mwezi

WANANCHI wa mji wa Chakechake kisiwani Pemba, wanaishi na takataka wastani wa tani 150, kati ya tani 450 zinazolishwa kwa mwezi, wakati zinazolewa na baraza la mji huo ni tani 300.

Mji huo wenye wakaazi wastani wa 13,730 kwa siku huzalisha tani kati ya 15 hadi 17 kwa siku, ambapo baraza la mji huo, lenye gari moja ya kuzolea taka, huzoa tani 10 kwa tano tano kila mwendo mmoja kwa gari lao maalumu na kubakisha tani tano kila siku.

Taarifa zinaeleza kuwa, tatizo kubwa lililopo ndani ya baraza...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani