(Today) 19 hours ago

Michuzi

WANANCHI WAJITOLEA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA PANGANI MJINI KIBAHA

 Wakazi mbalimbali kutoka mitaa ya kata ya Pangani, Kibaha Mjini wakionekana pichani kujitolea katika nguvu kazi kujenga shule ya sekondari ya Pangani Msaidizi wa mbunge wa jimbo la Mjini Kibaha ,Method Mselewa (aliyeshika tofali) akiwaunga mkono wakazi wa kata ya Pangani ,katika zoezi la kujitolea kujenga shule ya sekondari. Picha na Mwamvua Mwinyi.

 

3 days ago

Michuzi

UJENZI WA DARAJA LA PANGANI HUKO KIBAHA KUTUMIA MIL.100

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
UJENZI wa daraja litakalounganisha kata ya Pangani ,Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo umeanza ambapo hadi kukamilika kwake utatumia zaidi ya sh. milioni 100.
Akizungumza na wananchi kwenye eneo la ujenzi Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi alisema, tayari ujenzi umeanza na wameshaweka mawe ambayo yatatumika kama kitako cha daraja kwa kutumia waya ili kuzuia mmomonyoko.Alieleza, mawe yanayotakiwa ni malori 100 na nyaya hizo kwa ajili ya kuweka...

 

4 days ago

Michuzi

KAOLE SNAKE PARK YAIPIGA TAFU UMISETA NA UMITASHUMITA BAGAMOYO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kaole Snake Park, Kauthar Kihuhe(kushoto) akikabidhi msaada wa Jezi kwa Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Bagamoyo, Danny Mporere zenye thamani ya Shilingi milioni moja na laki mbili(1200,000) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika kituo hicho cha utalii wa ndani kilichopo Bagamoyo mwishoni mwa wiki.Kulia ni Afisa Utamaduni Wilaya ya Bagamoyo, Stellah Moshi na Afisa michezo Wilaya ya Bagamoyo, Vedastus Mziba KITUO cha Utalii wa ndani...

 

4 days ago

Michuzi

UJENZI WA DARAJA LA PANGANI HUKO KIBAHA KUGHARIMU MIL.100

Sura ya kivuko cha miti kinachotumika kuvuka wakazi wa kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo ambapo kwasasa ujenzi wa daraja umeanza utakaogharimu mil.100. Diwani wa kata ya Pangani Agustino Mdachi (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi kuhusu ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo. Ujenzi wa daraja linalounganisha kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha na Mpiji Magohe wilaya ya Ubungo, umeanza...

 

2 weeks ago

Michuzi

AFRIKA ZINDUKA BAGAMOYO PLAYERS YATIKISA KIGODA CHA NYERERE

Na Sophia Mtakasimba (TaSUBa).
Mchezo wa kuigiza wa jukwaani unaofahamika kwa jina la Afrika zinduka, umetikisa tamasha la kumi la kigoda cha Mwalimu Nyerere lililoendelea  katika ukumbi wa Nkuruma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.


Mchezo huo uliobeba ujumbe wa namna  Bara la Afrika linavyoteseka na umasikini mkubwa ile hali  lina utajiri mkubwa wa mali asili , ardhi na madini umetungwa , umeongozwa na kuchezwa na Kikundi cha “Bagamoyo Players” cha Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo...

 

3 weeks ago

Michuzi

HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY


Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imekosa mashine ya X-RAY ,hali inayosababisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila.

Akizungumza na Michuzi blog, Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo ameeleza ujenzi wa hospitali ya Mkamba unaendelea vizuri hadi sasa nyumba ya mganga, chumba cha upasuaji, maabara na wodi ya wazazi zipo katika hatua nzuri na hii ni kwa...

 

3 weeks ago

Michuzi

KLABU YA ROTARY DAR NORTH KUTEKELEZA MRADI WA MAJI SAFI KISIJU WILAYANI MKURANGA


Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam North imeanza kutekeleza mradi wenye lengo la kupeleka maji safi katika kata ya Kisiju, wilaya ya Mkuranga- Mkoa wa Pwani.Mradi huo unaoitwa Aquaplus unafadhiliwa na klabu ya Rotary Dar North ya Dar es Salaam Tanzania, klabu za Rotary za Milano nchini Italia, shirika lisilo la kiserikali la MLFM la nchini Italia na mfuko wa Rotary.

Kata ya Kisiju- Pwani iko katika fukwe ya wilaya ya Mkuranga na inajishughulisha na uvuvi na pia hakuna upatikanaji rahisi wa...

 

4 weeks ago

The Standard

Kenya-Tanzania plans road linking Malindi and Bagamoyo


The Standard
Kenya-Tanzania plans road linking Malindi and Bagamoyo
The Standard
NAIROBI, KENYA: The start of a mega road project connecting Kenyan and Tanzanian coastal towns faces delay as Kenya drags its feet in moving the project forward. The two countries plan to build a 412km road between Malindi and Bagamoyo that is expected ...

 

1 month ago

AllAfrica.Com

Tanzania: Road Accident Claims 26 Lives in Mkuranga


Tanzania: Road Accident Claims 26 Lives in Mkuranga
AllAfrica.com
At least 26 people have died and other 10 injured after a passenger Toyota Hiace and a truck carrying salt from southern regions of the country were involved in a head-on collision. The accident occurred on the night of Saturday, March 24 at Kitonga ...

 

1 month ago

Michuzi

17 WATAMBULIWA KATI YA 26 WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKURANGA

Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga  WATU 17 kati ya 26 waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Mkuranga Mkoani Pwani ,wametambuliwa majina yao ambapo hatua inayoendelea ni kuwakabidhi kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi. Aidha watu wengine 10 waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa matibabu.  Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK (pichani) inayofanya safari zake Kimanzichana -...

 

1 month ago

Michuzi

WATU 26 wamefariki dunia na wengine kumi kujeruhiwa ajali iliyotokea Mkuranga Mkoani Pwani .

Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.676 DGK inayofanya safari zake Kimanzichana - Mbagala Rangi na gari nyingine aina ya Lori.Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia machi 25 mwaka huu katika eneo la Kitonga kata ya Mwalusembe wilaya ya Mkuranga.Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Stephen Mwandambo alisema amepokea maiti 25 na majeruhi 10 ambapo majeruhi mmoja alifariki njiani akipelekwa...

 

1 month ago

Michuzi

DC KIBAHA AZINDUA CHUO CHA VETA KUWASAIDIA VIJANA WA VIJIJINI

KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda  hatimaye  kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani limeamua kujenga chuo cha ufundi stadi (VETA) kwa lengo la kuwawezesha  vijana wanaotoka katika maeneo ya vijijini ili waweze kujifunza fani mbali mbali ambazo zitawasaidia kupata ujuzi na kuanzisha viwanda vidogovidogo na kujiajiri wao wenyewe.
Kauli hiyo ilitolewa na  Askofu...

 

1 month ago

Michuzi

MJUMBE BARAZA KUU UVCCM PWANI AAHIDI KUSHUGHULIKIA MGOGORO HIFADHI ZA BAHARI MAFIA

Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao,akizungumza na wajumbe wa baraza la UVCCM wa Wilaya ya Mafia kuhusu kupeleka sehemu husika mgogoro wa wananchi na hifadhi ya bahari pamoja na kuwahimiza wanakipigania chama kishinde uchaguzi ujaowa serikali za mitaa. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Makwiro na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki.Picha Zote na Elisa Shunda.Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa...

 

2 months ago

Michuzi

DC WA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AAHIDI NEEMA KWA KINAMAMA WILAYANI HUMO

MKUU wa Wilaya ya Kibaha Bi Assumpter Mshama amewaahidi kina mama wajasiriamali wa Wilaya ya Kibaha kuwa atazungumza na uongozi wa Halmashauri ya Mji  ili itengwe  siku na eneo maalum  kwa ajili ya kufanya maonyesho  ya bidhaa wanazozitengeneza ikiwa ni katika kupambana na  changamoto ya ukosefu wa masoko ya kuuzia bidhaa hizo.Mshama amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake  duniani  Kibaha Mkoa wa Pwani, amewataka wanawake kujiamini, kushikamana  na kuachana...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani