4 weeks ago

Michuzi

SERIKALI YAZUIA UCHIMBAJI KWENYE MTO MUHUWESI TUNDURU

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ya vito wilayani Tunduru wakati alipotembelea eneo la Mto Muhuwesi.
Serikali imezuia shughuli za uchimbaji wa madini ya vito kwenye Mto Muhuwesi wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma hadi hapo taarifa za kitaalamu zitakapotolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la tathmini na ukaguzi.
Agizo hilo limetolewa hivi karibuni wilayani humo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter...

 

1 month ago

Ippmedia

Viongozi 4 wa chama cha SACCOS ya walimu Mbinga mbaroni kwa ubadhirifu wa Mil.500.

Vurugu zimeibuka mkutanoni wakati viongozi wanne wa chama cha ushirika cha SACCOS ya walimu Mbinga mkoani Ruvuma wakikamatwa na polisi mkutanoni baada ya kutuhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500.

Day n Time: Jumapili saa 2:00 usikuStation: ITV

 

1 month ago

Michuzi

POSHO ZA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WILAYA YA MBINGA MILIONI 47 KATIKA VIKAO VYA BAJETI, WAMEAMUA ZIENDE KUMALIZIA MILADI

Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, wameamua kutochukua posho zao za vikao viwili vya bajeti ambazo ni shilingi milioni 47, badala yake ziende zikatumike kumalizia miradi ya maendeleo ambayo imesimama katika halmashauri hiyo. Kwa undani wa habari hii hii hapa video yake.

 

1 month ago

Mwananchi

Madiwani watimua watumishi wanne Mbinga

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mbinga Vijijini limewafukuza kazi watumishi wanne na kumvua madaraka mtumishi mmoja.

 

2 months ago

Channelten

Wagonjwa hatarini hospitali ya Tunduru Wajisaidia kwenye ndoo na vichakakani

Wagonjwa katika hospittali ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wodi ya wanawake wanajisaidia kwenye ndoo na vichaka kutokana na matundu ya vyoo kujaa kinyesi huku watunzaji wa wagonjwa wakilazimishwa kufua mashuka ya hospitali kwa mikono.

Hofu ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko imetanda kwa wagonjwa katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru choo kinachotumika na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wanawake kuziba kwa kinyesi kwa zaidi ya wiki moja hali inayowafanya wagonjwa kujisaidia kwenye...

 

2 months ago

Michuzi

wilaya ya Mbinga yawataka wananchi kutunza chakula cha ziada

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Mhe. Consimas Mshenyi (pichani) amewataka wananchi wilayani humo kuhakikisha wanatunza ziada ya chakula walichonacho kutokana na hali ya mvua kutoridhisha  licha ya kusema hakuna njaa katika wilaya yake.


Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari kuhusu hali ya chakula katika wilaya hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema mpaka sasa vituo vya hifadhi ya chakula wilayani hapo vina zaidi ya tani 300 huku ziada kutoka kwa wananchi ikiwa ni tani 10,000 za mahindi huku mchele...

 

3 months ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA MGODI WA MAKAA YA MAWE YA NGAKA WILAYA YA MBINGA MKONI RUVUMA

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe unavyofanywa nakampuni ya Tancoul katika mgodi wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga  kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la maendeleo la taifa NDC Dr Samuel Nyantahe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mkaa wa mawe ulivyoWaziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Ruvama Mhandisi Mahenge pamoja naviongozi mbalimbali walipokuwa wanatemmbelea mgodi wa Ngaka Picha na Chris Mfinanga

KUSOMA...

 

3 months ago

Michuzi

MHASIBU WA KIJIJI TUNDURU MBARONI KWA KUKATAA KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI

Mhasibu wa kijiji cha Huria mkoani wilaya ya Tunduru atiwa mbaroni kwa kukataa kusoma mapato na matumizi ya kijiji. Kwa undani wa habari angalia video yake.

 

3 months ago

Michuzi

SERIKALI WILAYANI TUNDURU YATOA MASAA 48 WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI KUONDOKA KATIKA DARAJA LA MUHUWESI

Daraja la mto wa MUHUWESI ambalo wachimbaji wadogowadogo wanafanya kazi hiyo ya kuchimba madini hali ambayo itapelekea kubomoka kwa daraja hiloSehemu ambayo wachimbaji hawa wanachimbaBaadhi ya wachimbaji(Habari na Ruvuma Tv)

 

3 months ago

Habarileo

Halmashauri Mbinga yapima viwanja 70,000

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imekamilisha kazi ya kuainisha maeneo mbalimbali kwa ajili ya makazi, maeneo ya wazi na kutenga maeneo kwa ajili ya huduma muhimu za kijamii.

 

4 months ago

Michuzi

DC WILAYA YA TUNDURU AELEZA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUTOKOMEZA MIMBA MASHULENI KATIKA WILAYA YAKE SEHEMU YA PILI.


MKUU wa wilaya ya Tunduru JUMA HOMELA  aelezea mpango wa mahakama ya kutembea aliyoianzisha katika wilaya yake ya TUNDURU jinsi ulivyoleta mafanikio , katika kupunuza utoro mashuleni na mimba mashuleni. Attachments area Preview YouTube video RUVUMA TV@ SEHEMU YA PILI TUNDURU yafanikiwa kupunguza mimba kwa wanafunzi RUVUMA TV@ SEHEMU YA PILI TUNDURU yafanikiwa kupunguza mimba kwa wanafunzi

 

4 months ago

Michuzi

DC TUNDURU JUMA HOMELA AELEZA MAFANIKIO YA MPANGO WA KUTOKOMEZA MIMBA MASHULENI KATIKA WILAYA YAKE SEHEMU YA KWANZA.

MKUU wa wilaya ya Tunduru JUMA HOMELA akizungumza na mwandishi wa RUVUMA TV on line ambaye hayupo pichani mafanikio ya kupambana na utoro mashuleni pamoja na kutokomeza mimba mashuleni. Kwa undani wa habari hii bonyeza hiyo video.
RUVUMA TV@TUNDURU yafanikiwa kupunguza mimba kwa wanafunzi

 

4 months ago

Michuzi

WAKULIMA WA ZAO LA KORSHO TUNDURU WANUFAIKA NA BEI MPYA YA ZAO HILO

 http://3.bp.blogspot.com/-Ja9gYTH8Zw8/UoetfpR-U-I/AAAAAAACWMk/zcdGDbWBI9k/s1600/IMG_4156.jpgWAKULIMA wa korosho Wilaya ya Tunduru, wameondokana na umasikini kutokana na kupata soko la uhakika baada ya Kampuni ya Namela General Trade kushinda zabuni ya kununua zao hilo wakulima kwa bei ya Sh 3,757 kwa kilo, ikizishinda kampuni nyingine saba.
Hadi kufikia Novemba 14, kulikuwa na zaidi ya tani 541 zilizoingizwa katika ghala la Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru (Tancu) ambako kampuni hiyo ilipewa kununua korosho tani 400 huku Kampuni ya Machinga iliyoshinda nafasi ya...

 

4 months ago

Michuzi

BANK YA NMB YAKABIDHI VITANDA ,MAGODORO NA MADAWATI TUNDURU

 Meneja wa Bank ya NMB kanda ya kusini Bi Lilian Mwinula akikabidhi vitanda tisa ,magodoro tisa kwa mkuu wa wilaya ya tunduru Juma Homera kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa hospital ya Wilaya ya Tunduru.-------------------------------- Bank ya NMB tawi la TUNDURU mkoani RUVUMA imekabidhi msaada wa vitanda 9 na magodoro 9 katika hospital ya wilaya ya tunduru pamoja na madawati 50 katika shule ya msingi majengo iliyopo mjini tunduru vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi, ikiwa ni...

 

5 months ago

Habarileo

Mbinga washauriwa kuchangia elimu

WADAU wa elimu wilayani Mbinga, mkoa wa Ruvuma, wameshauriwa kuendelea kuchangia katika sekta hiyo ili watoto wasome katika mazingira mazuri na kufanya vyema katika masomo yao.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani