6 days ago

Malunde

Picha: AGPAHI YAKUTANISHA VIJANA 230 KUTOKA KISHAPU NA MANISPAA YA SHINYANGA KWENYE BONANZA LA MICHEZO


Vijana 230 kutoka halmashauri za wilaya ya Kishapu na Manispaa ya Shinyanga wamekutana katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Bonanza hilo limefadhiliwa na Mfuko wa Kusaidia watoto wa Uingereza ( Children’s Investment Fund Foundation UK- (CIFF) limefanyika Jumamosi Agosti 12,2017 katika uwanja wa shule ya msingi...

 

1 week ago

Malunde

MTOTO AFARIKI KWA KULIWA NA FISI KISHAPU - SHINYANGA


Mtoto aliyejulikana kwa jina la Katambi Masunga mwenye umri wa miaka mitano amefariki dunia baada ya kuliwa na fisi katika Kitongoji cha Mwabuli kijiji Mwamadulu kata ya Lagana wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa Agosti 8,2017 kuamkia Agosti 9,2017 baada ya fisi kuvamia katika familia aliyokuwa anaishi motto huyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,mtoto huyo mwenye ulemavu wa viungo akiwa na mtoto mwenzake wakicheza nyumbani kwao majira ya saa...

 

1 week ago

Michuzi

Kaya 6019 katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu kunufaika na fedha za TASAF

Sehemu ya walengwa wa kaya maskini wakiwa katika zoezi la kupokea ruzuku kijij cha Mwigumbi.
Na Robert Hokororo.
Kaya  6019 katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, zinatarajia kunufaika na fedha sh. milioni 204.6 zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) awamu ya tatu. Hayo yamebainishwa na Mratibu wa TASAF wilayani humo, Sospeter Nyamuhanga ofisini kwake wakati akizungumzia zoezi la uhawilishaji fedha hizo linalotarajiwa kuvifikia jumla ya vijiji 78.
Alisema kuwa...

 

2 weeks ago

Channelten

Serikali yawaonya waalimu wanaowapa mimba wanafunzi huko Meatu

maxresdefault-1

Serikali imesema itawafukuza kazi walimu na kuhakikisha wanafungwa jela miaka 30, endapo watabainika kuwashawishi wanafunzi kufanya nao mapenzi jambo ambalo ni kinyume na sheria za nchi.

Akizungumza na wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari, Mwandoya iliyopo wilayani Meatu mkoani Simiyu, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amesema adhabu hiyo haita ishia kwa walimu, kwani hadi wazazi nao watawajibishwa.

Mpina amesema hayo baada ya kupokea taarifa...

 

2 weeks ago

MwanaHALISI

Serikali yawapigia debe maskini Kahama

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela amewataka wananchi wa kijiji cha Iyenze kata Iyenze  wilayani  Kahama mkoani Shinyanga kuhakikisha wanawasaidia wanzeo wasiojiweza kwa kuwalipia  Bima ya Afya iliyoboreshwa(CHF), anaandika Mwandishi Wetu. Kijiji  hicho kina kaya 1177 wakati 7932 na idadi ya watu wanafikia zaidi ya 7000 kwa mujibu wa sensa ya  mwaka 2012. ...

 

3 weeks ago

Michuzi

BARAZA LA MADIWANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA WAPONGEZWA KWA HATUA YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KWA UFANISI PAMOJA NA CHANGAMOTO ZA UHABA WA FEDHA

Na Robert Hokororo
Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imepongezwa kwa hatua yake ya utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi pamoja na changamoto za uhaba wa fedha.

Pongezi hizo zimetolewa leo na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Boniphace Butondo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kupokea taarifa za kata kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka.Butondo alisema miradi hiyo imetekelezwa kwa kiwango kizuri pamoja na changamoto ya uhaba wa...

 

3 weeks ago

Mwananchi

NBC yafungua klabu ya wafanyabiashara Kahama

Benki ya NBC imezindua Klabu ya Biashara mjini Kahama ili kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara biashara wadogo na kati.

 

3 weeks ago

Michuzi

NBC Yazindua Klabu ya Biashara mjini Kahama

 Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mjini Kahama, Shinyanga jana. Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Katikati ni mmoja wa wateja, Salum Selemani na Joshua John (kulia), Ofisa Masoko wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kutoka ofisi ya Mwanza. Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza na...

 

4 weeks ago

Michuzi

KAMATI YA FEDHA KISHAPU YAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Na Robert Hokororo
Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango halmashauri ya wilaya ya Kishapu imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata za Lagana, Itilima na Talaga. Katika ziara hiyo wajumbe hao pamoja na wataalamu kutoka halmashauri walitembelea maendeleo ya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Mwadulu iliyopo kata ya Lagana.
Wakiwa eneo hilo wajumbe hao kupitia kwa mwenyekiti wa halmashauri, Boniphace Butondo walipongeza juhudi za uongozi wa shule hiyo...

 

1 month ago

Malunde

MAOFISA UGANI WA WILAYA YA BUKOMBE WATAKIWA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA KILIMO


Mkuu wa wilaya ya Bukombe,. Joseph Maganga (kulia), akizungumza na maofisa Ugani wa Wilaya hiyo kwenye mafunzo ya kilimo cha mazao ya Mihogo,Pambana Viazi lishe yaliyoandaliwa na Tume yaTaifa yaSayansi na Teknolojia(COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia OFAB. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya hiyo, Zacharia Bwile na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Baraka Maganga.
Mshauri wa Jukwaa la Masuala ya Bioteknolojia (OFAB) Dk. Nicholaus Nyange, akitoa mada kuhusu...

 

1 month ago

TheCitizen

Precision Air announces start of scheduled Kahama flights Sept 5

Precision Air Services Plc will start flying to Kahama on September 5, the company announced on Monday.

 

1 month ago

Malunde

Picha & Sauti: MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAISLAM WA AHMADIYYA KANDA YA ZIWA WAFANYIKA KAHAMA SHINYANGA


Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa (Ahmadiyya Muslim Jamaat Kanda ya ziwa) leo Jumapili Julai 9,2017 imefanya mkutano wa mwaka wa Jumuiya hiyo kwa mwaka 2017.
Mkutano huo umefanyika katika Msikiti wa Ahmadiyya Muslim Jamaat Tz Masjid Fath uliopo katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa huo.
Akizungumza...

 

1 month ago

Channelten

Mkandarasi atakiwa kujisalimisha, Agizo la DC Kahama kwa kampuni ya Chengdu

MIMI

Serikali wilayani kahama, Mkoani Shinyanga, imeagiza kujisalimisha kwenye vyombo vya Usalama, Mkadarasi wa Kampuni ya CHENGDU INTERNATIONAL, iliyokuwa ikitekeleza ujenzi wa soko la kimaitafa la mazao ya nafaka katika halmashauri ya mji huo, kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria, kufuatia kuutekeleza mradi wa ujenzi wa soko hilo, kwa zaidi ya miaka (4) mine sasa.

Agizo hilo la serikali limetolewa na mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya...

 

2 months ago

Malunde

Picha: WATU WATATU WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA WIZI WA PIKIPIKI KAHAMA



Wananchi waliojichukulia sheria mkononi leo wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki. 

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yamefanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa leo majira ya saa nne asubuhi.
Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani