(Yesterday)

Channelten

Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali Manyoni Mkoani Singida imeleta madhara makubwa

Screen Shot 2017-01-20 at 4.29.16 PM

MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kunyesha wilayani Manyoni, Mkoani Singida imeleta madhara makubwa katika Vijiji vya Makasuku na Chibumagwa, wilayani humo na kusababisha nyumba na majengo 107 kuezuliwa na upepo, huku mengine yakibomoka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo GEOFREY MWAMBE amefahamishwa kuwa Mtu mmoja ametajwa kufariki dunia na watu wengine wanne kujeruhiwa wakati wa tukio hilo lililotokea juzi majira ya saa...

 

1 week ago

Dewji Blog

DC Manyoni awatia mbaroni watu watatu kwa kuruhusu ndugu yao kuoa mwanafunzi

Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Geoffrey Mwambe amefanikiwa kuzuia msichana mwenye umri wa miaka 14 (jina tunalo) kuolewa na ameagiza arejeshwe mara moja shuleni kuendelea na masomo yake.

Mtoto huyo aliachishwa shule mwaka juzi 2015 akiwa darasa la sita katika shule ya msingi Idodiandole halmashauri ya Itigi wilaya ya Manyoni.

Imeelezwa kwamba mtoto huyo aliachishwa shule kutokana na tatizo la ugonjwa wa kifafa lakini miezi mitatu baada ya kuachishwa shule, mchakato wa kuozeshwa...

 

3 weeks ago

Michuzi

JAFO AFANYA ZIARA WILAYA MANYONI MKOANI SINGIDA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara katika halmashauri mpya yaItigi na Manyoni huku akibaini uwepo wa changamoto mbalimbali hususanupungufu wa dawa katika Kituo cha Afya Itigi na Hospitali ya wilaya yaManyoni mkoani Singida.
Akizungumza katika ziara hiyo, Jafo amesema mara baada ya kutembeleaHalmashauri hizo amebaini changamoto za dawa katika kituo cha afyaItigi pamoja na vifaa katika chumba cha mama huku akisema...

 

2 months ago

Michuzi

MKUU WA MKOA WA SINGIDA AIPONGEZA HOSPITALI YA KIOMBOI, IRAMBA KUPEWA HADHI YA MBILI NA KUHIMIZA IPATE NYOTA TATU

Na Grace Singida 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameipongeza hospitali ya Kiomboi ambayo ni ya Wilaya ya Iramba kwa kupata hadhi ya nyota mbili kutoka sifuri na kuwahamasisha kuendelea kuboresha utendaji ili kupata hadhi ya nyota tatu.

Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ametoa pongezi hizo alipotembelea hospitali hiyo akiambatana na wageni kutoka shirika la Water Aid International ambalo limefadhili ukarabati wa miundombinu hospitalini hapo kwa shilingi milioni mia...

 

3 months ago

Dewji Blog

DC Manyoni afuta sheria ya kila kijana kuchangia 15,000 kwa ajili ya shughuli za maendeleo

Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida,Geoffrey Mwambe,amefuta rasmi amri yake halali yenye kumbukumbu namba AB/241/01/33  ya septemba 06 mwaka huu,iliyokuwa inatoa uhalali wa kuchangia maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo,ikiwemo mtu mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea,kuchanga shilingi 15,000 kwa mwaka.

Michango mingine ni  shilingi 3,000 kwa ajili ya ushuru wa ng’ombe na punda,wakati shilingi 2,000 ni kwa ajili ya ushuru wa mbuzi na kondoo kwa mwaka.Ushuru na kodi hiyo,ni kwa ajili ya...

 

4 months ago

Mwananchi

Watumishi watano waisoma namba Manyoni

Ni msemo uleule wa kuisoma namba leo umewakumba watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni baada ya kusimamishwa kazi na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Geoffrey Mwambe.

 

4 months ago

Mwananchi

DC Manyoni awatumbua watendaji watatu

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Geofrey Mwambe amewasimamisha watendaji wa vijiji vitatu vya Chikuyu, Msemembo na Rungwa kwa kushindwa kutekeleza majuku yao.

 

4 months ago

Michuzi

MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 800 YAZINDULIWA WILAYANI MANYONI


Daraja la Makutopora linalounganisha Wilaya ya Chemba na Manyoni likiwa limekamilika kujengwa, daraja hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 628,247,000 na kisha kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima. Mbijima amewaasa wananchi wa wilaya zinazounganishwa na daraja hilo kutumia fursa ya uwepo wa barabara na miundombinu  mizuri katika kuboresha maendeleo yao.

mir2
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru George Jackson Mbijima akipita katika daraja la...

 

4 months ago

Mwananchi

Bweni la wasichana lateketea Manyoni

Bweni la Wasichana la Shule ya Sekondari Mwanzi wilayani Manyoni, Mkoa wa Singida, limeteketea kwa moto na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh50 milioni huku wanafunzi 42 wakinusurika.

 

4 months ago

Habarileo

DED Manyoni abanwa amalize kero

KATIBU Tawala wa Mkoa Singida, Dk Angelina Lutambi amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Charles Susi kuzipatia ufumbuzi wa kudumu kero zote zinazowakabili wakazi wa Kambi ya Walemavu na Wazee Wasiojiweza ya Sukamahela wilayani humo.

 

4 months ago

Mwananchi

Watumishi saba waliosimamishwa Iramba warejeshwa

Jumla ya watumishi saba wa halmashauri ya Iramba mkoani Singida waliosimamishwa kazi Februari 26 mwaka huu, wamerejeshwa kazini baada ya Serikali kujiridhisha kuwa hawana hatia dhidi ya tuhuma walizokuwa wakituhumiwa.

 

5 months ago

Dewji Blog

Walimu watakaoshindwa kusimamia madawati Manyoni kukatwa mishahara

MKUU wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida,Geofrey Idelfonce Mwambe,amewaagiza walimu wa shule za msingi na sekondari wahakikishe samani ikiwemo madawati yanatunza vizuri,vinginevyo watakatwa sehemu ya mishahara yao, endapo yataharibika au kuvunjwa.

Mkuu huyo wa wilaya,ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati 100 kwa shule za msingi za Bangayegya na Lulanga za halmashauri ya wilaya ya Itigi.Madawati hayo yametolewa msaada na benki ya NMB tawi la Itigi.

Alisema...

 

6 months ago

Ippmedia

Five people killed in two separate accidents in Manyoni district

Five people died in two separate accidents in Manyoni district Singida region. In one incident a bus belonging to Osaka company knocked over and killed three people while in another an oil tanker crashed into a noah before overturning before causing the deaths of two people.

Day n Time: FRIDAY 8:00 PMStation: CAPITAL TV

 

6 months ago

Dewji Blog

Wilaya ya Manyoni yaongoza Singida kwa uhaba wa vyoo

Halmashauri ya wilaya ya Manyoni (kabla ya kutengwa Itigi kuwa halmashauri),imeongoza mkoani hapa, kwa kuwa na kaya 37,569 ambazo hazina vyoo,sawa na asilimia 61 ya kaya 61,723 za halmashauri hiyo.

Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.John Mwombeki, wakati akitoa taarifa ya huduma mbalimbali za afya mkoani hapa.

Alisema halmashauri hiyo ya Manyoni, ina kaya 9,253 zenye vyoo bora sawa na asilimia 15 na kaya zingine 15,008 zina vyoo vya muda sawa na asilimia 24.

Dk. Mwombeki...

 

6 months ago

Dewji Blog

DC mpya wa Manyoni mkoani Singida, Mwambe Geoffrey, ala kiapo

Mkuu wa mkoa wa Singida Mhansisi, Mathew Mtigumwe (kulia), akimwapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Mwambe Idelphonce Geoffrey. Hafla hiyo ilifanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini humo. Dc Mwambe hakuweza kuhudhurua uapishwaji uliofanywa wiki iliyopita kwa wakuu wengine wa wilaya mkoani Singida, kwa kile kilichodaiwa alikuwa nje ya nchi kikazi.

DC mpya wa Manyoni mkoani Singida, Mwambe Geoffrey

Mkuu wa wilaya ya Manyoni, Mwambe Geoffrey akikabidhiwa nyaraka na RC Singida baada ya kiapo

Mkuu wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe (kulia) akimkabidhi nyaraka zenye miongozo ya...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani