(Yesterday)

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA MAWAZIRI CHA mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi TANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam, Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali na kampuni washirika wa mradi huo...

 

(Yesterday)

Mwananchi

Ndesamburo ataka Tanga iwe ngome ya Chadema

Mgombea uenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Philemon Ndesamburo amesema Tanga inahitaji nguvu zake za ziada kuhakikisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vinashinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

 

3 days ago

Michuzi

MAHAKAMA KUU TANGA YAWEKA MIKAKATI KUONDOSHA MASHAURI KWA WAKATI

Na Lydia Churi- Mahakama, Tanga.
Mahakama Kuu Kanda ya Tanga inakusudia kuwanunulia Mahakimu wake 67 kompyuta Mpakato (Laptops) ili kurahisisha kazi zao na kuondosha mashauri kwa wakati katika Mahakama mbambali za mkoa wa Tanga.
Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga, Afisa Utumishi wa Kanda hiyo, Bwana Farid Mnyamike amesema kompyuta hizo zitawasaidia waheshimiwa Mahakimu katika kuandika hukumu ili wananchi waweze kupati haki kwa wakati.Alisema katika kanda yake,...

 

3 days ago

Mwananchi

Mbowe atoa somo kwa CUF, kujenga ngome ya Chadema Tanga

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema mgawanyiko uliopo baina ya madiwani wa CUF katika Halmashauri ya Jiji la Tanga utachelewesha maendeleo ya wananchi.

 

4 days ago

Mwananchi

January atoa agizo zito Korogwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amewaagiza wakazi wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, kuvilinda vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

 

6 days ago

Michuzi

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA KAZI NZURI YA TPSC TAWI LA TANGA

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Mwaine Ismail Nchemba (Viti Maalum ) Tabora akifafanua jambo wakati kamati yake ilipozuru tawi la Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) tawi la Tanga leo asubuhi.Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dk.Henry Mambo akifurahia jambo wakati wakiwasilisha taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa waliotembelea Chuo hicho tawi la Tanga leo asubuhi Wanakwaya wa Chuo...

 

1 week ago

Michuzi

RC SHIGELLA AWAPIGA MSASA MAKATIBU TAWALA MKOANI TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, amesema Utafiti mpya wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi kwa kutumia mfumo wa (CD4T-cell count) utasaidia kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
Amesema Utafiti huo utaangazia pia kuwepo kwa Viashria vya Usugu wa dawa, kiwango cha maambukizo ya Kaswende na homa ya Ini kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.
Amesema Tafiti tatu zilizotangulia zimekuwa zikiwahusiha wananchi wenye umri wa miaka 15 hadi 49 tofauti na utafiti wa mwaka 2016/ 2017 ambao ni wa kipekee...

 

1 week ago

Habarileo

Tanga Uwasa wafundisha matumizi lazima ya maji

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) imewataka wateja wake kuwa waangalifu katika matumizi ya majisafi hata kama wana uwezo wa kuyalipia na kuhakikisha wanajiwekea utaratibu mzuri wa kuyatumia kwa ufanisi ili kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima.

 

1 week ago

Michuzi

TANGA UWASA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA.

Mtaalamu wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Ramadhani Nyambuka akisistiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma kwa mteja wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji Machi 22 mwaka huuAfisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo Afisa Ankra wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa...

 

2 weeks ago

Michuzi

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AENDELEA KUTATUA KERO ZA WANANCHI JIMBONI KWAKE,AKABIDHI BAISKELI KWA MLEMAVU

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF),Alhaj Mussa Mbaruku akiendeseha baiskeli hiyo kabla ya kumkabidhi mkazi wa Makorora Mbwana Hamisi leo kwa ajili ya matumizi yake kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Makorora Ally Kivurande 
Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF), Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na wananchi wa Makorora Jijini Tanga leo wakati wa Hafla ya Makabidhiano hayoMbunge wa Jimbo la Tanga(CUF),Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi Baiskeli Mlemavu wa miguu Mbwana Hamisi Mkazi wa Makorora...

 

2 weeks ago

Michuzi

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA AMUANGUKIA WAZIRI MWIJAGE

MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi CUF Alhaj Mussa Mbaruku amemuomba Waziri wa Viwanda na biashara Charles Mwijage kuingilia kati ucheleweshawajiwa wa cheti cha ubora wa viwango unaotolewa na shirika hilo la TBS na kusababisha zaidi ya watumishi 300 kupoteza ajira baada ya  kiwanda hicho kufungwa.

Ameyazungumza hayo jana baada ya siku kadhaa kutolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa shirika hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kupoteza ajira kwa zaidi ya watumishi 300...

 

2 weeks ago

Michuzi

TAASISI YA USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE (UDI) YACHANGIA MAENDELEO WILAYANI LUSHOTO

 Wanafunzi wa shule ya secondari viti kata ya shume wilayani Lushoto wakipokea mifuko ya saruji yenye thamani ya shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo kutoka kwa taasisi ya USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE (UDI) ikiwa ni katika kuchangia juhudi za Mh. Mbunge wa Mlalo mh. Rashid Shangazi za kuleta maendeleo jimboni hapo. Diwani wa kata ya Vuga wilayani Lushoto mh. Dhahabu jumaa akipokea miche ya miti kutoka kwa taasisi ya USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE , ikiwa ni juhudi za...

 

2 weeks ago

Michuzi

TANGA UWASA INAHITAJI BILIONI 15 KUTEKELEZA MPANGO WA KUSAFISHA MAJITAKA

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka katika Jiji la Tanga (Tanga-Uwasa), linahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusafisha majitaka yaweze kutumika kwa shughulinyingine za kibinadamu ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.

Akizungumza katika semina kwa wanahabari Jijini hapa Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Injinia Joshua Mgeyekwa, alisema kutokana na kuzaliza kiasi cha mita za ujazo zipatazo 2,700, wameonelea wayasafishe kwa kujenga mfumo utakaosaidia maji hayo...

 

2 weeks ago

Michuzi

Wanawake wa Tanga Cement waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kufanya mazoezi na kupima afya.


Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Diana Malambugi (wa pili kulia), Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Nje wa Kampuni hiyo, Mtanga Noor (kulia), pamoja na baadhi ya wanawawake wafanyakazi wa Kampuni ya Saruji Tanga pamoja na wake wa wafanyakazi, wakishiriki mbio za pole pole kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani zilizoanza eneo la Kange na kumalizikia katika kiwanda cha kampuni hiyo, Pongwe, nje kidogo ya mji wa Tanga juzi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,...

 

2 weeks ago

CCM Blog

WANAFUNZI WA S/SEK KATA YA PANGANI WATEMBEA KM 34 AMA KUTUMIA PIKIPIKI SH.10,000

Mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka,akizungumza jambo katika ziara yake kata ya Pangani .(picha na Mwamvua Mwinyi) Baadhi ya wakazi wa kata ya Pangani,wakisikiliza jambo katika ziara ya mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha, Silvestry Koka kwenye kata hiyo. Diwani wa kata ya Pangani,Agustino Mdachi akizungumza na wananchi wa kata hiyo kwenye ziara ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mji,Silvestry Koka aliyoifanya katika kata hiyo.
Na Mwamvua Mwinyi,KibahaWANAFUNZI wa shule ya sekondari ya...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani