(Yesterday)

Malunde

MBUNGE MSUKUMA : WANASIASA WASHUGHULIKIWE...HATA WATU WA CCM WAMEPOTEA WENGI TU

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amevitaka vyombo vya dola kuwashughulia watu wanaodaiwa kuwa wakorofi hasa wanasiasa, kwa kuwaweka ndani ili kurekebisha tabia zao.

Msukuma alitoa wito huo juzi Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hoja katika Wizara ya Katiba na Sheria.

“Sisi kama wabunge tunaotunga sheria tuviachie vyombo vifanye kazi yake, wanaosema kuna watu wamepotea hata watu wa CCM wamepotea wengi tu, wamechinjwa Kibiti wengi tu na hatukupiga kelele tumeviachia vyombo...

 

2 days ago

MwanaHALISI

ACT, CCM wameendelea kuparuana juu ya ripoti ya CAG

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeeleza kuwa uchambuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) juu ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kimepotosha na kimewaahaada watanzania juu ya upotevu wa Sh. 1.5 trilioni. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Katibu Itikadi na Uenezi, Ado Shaibu amesema msimamo CCM ndio msimamo wa serikali kutokana na kuwa hicho ndicho ...

 

2 days ago

Michuzi

CCM DAR YASHAURI WALIOZIBA NJIA ZA MAJI WAONDOLEWE, YATOA POLE KWA WALIOPOTEZA NDUGU KWASABABU YA MVUA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam kimetoa pole kwa familia ambazo zimepoteza ndugu zao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku kikitoa ushauri kwa Serikali kuwaondoa waliojenga kwenye njia za maji kwa lengo la kupunguza maafa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Cylivia Katekamba amewaambia leo waandishi wa habari kuwa chama hicho kinatoa pole kwa wote ambao wamefikwa na maafa na kuomba wenye uwezo wa kusaidia walioathrika na mvua hizo...

 

3 days ago

Malunde

HAJI MANARA : WOTE NI MAKADA WA CCM LAKINI MIMI NI MAARUFU KULIKO HUMPREY POLEPOLE

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameweka wazi kuwa yeye ni maarufu zaidi nchini Tanzania kuliko Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole.

Haji Manara amesema kuwa yeye ni kada mzuri wa CCM na Polepole anafanya kazi kama yake lakini hana jina kubwa kumzidi yeye kutokana na historia ya maisha yake na chama hicho.

Manara amedai kuwa CCM ndio chama kilichomsomesha nje ya nchi kuhusu masuala ya propaganda na ameshawahi kuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es salaam miaka ya...

 

3 days ago

Michuzi

CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kimesema Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe(ACT-Wazalendo) ni mpotoshaji mkubwa na vyombo vya kisheria vinastahili kumchukulia hatua.
Kimesema Ziito kupotosha kuwa kuna fedha Sh.Trilioni 1.5 za Serikali zimeibiwa si kweli na kwamba wameipitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) hakuna fedha ambayo imepota au kuibiwa na kiasi ambacho kimetajwa kwenye...

 

5 days ago

MwanaHALISI

CCM wamtelekeza Mzee Makamba

JANUARY Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira ametoa madai mazito kwa chama chake, kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtelekeza baba yake Mzee Yusuph Makamba akiwa mgonjwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Makamba ameandika ujumbe huyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akielezea hali ya baba yake ...

 

1 week ago

Michuzi

HALMASHAURI MANISPAA KIGAMBONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ILANI YA CCM

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bi. Kate Kamba ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa utekelezaji wa Ilani wa chama cha Mapinduzi na kusema kuwa ameiona thamani ya fedha katika miradi yote aliyoitembelea hivyo mshikamano uliopo uendelezwe. 
Amayezungumza hayo jana mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi aliyoifanya Manispaaa ya Kigamboni yenye lengo la kuona ni naman gani Ilani ya Chama inatekelezwa. 
Akizungumza na watumishi na wananchi wanao shiriki kusimamia miradi Bi.Kamba amesema...

 

1 week ago

Malunde

MBUNGE WA CCM APIGA MAGOTI BUNGENI DODOMA


Mbunge wa Ileje (CCM) Janeth Mbene amepiga magoti bungeni na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kupeleka maendeleo kwenye wilaya yake anayodai ilisahaulika.
Mbene amefanya kitendo hicho leo bungeni Aprili 13,2018 wakati akichangia bajeti ya ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Mara baada ya kuruhusiwa kuchangia bajeti hiyo, Mbene amesema wilaya ya Ileje ni ya miaka mingi lakini ilikuwa haina barabara ya lami lakini katika Serikali Awamu ya Tano, barabara imejengwa.
Katika kuonyesha kuwa...

 

1 week ago

Malunde

KATIBU WA CCM AMNYWESHA SUMU YA PANYA MTOTO WA MCHEPUKO KUNUSURU NDOA YAKE SHINYANGA

Mtoto wa miezi miwili jina limehifadhiwa mkazi wa Kitongoji cha Unyanyembe kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga  amenusurika kufa baada ya kunyeshwa sumu ya panya na baba yake mzazi Edson Timotheo Damiani (37) kwa kile kilichoelezwa ni kutaka kuficha siri ili mkewe asijue kama amezaa mtoto mwingine nje ya ndoa. 

Akielezea tukio leo Aprili 12,2018 Mama mzazi wa mtoto huyo Maria Shija amesema lilitokea Mach 24 mwaka huu majira ya saa tatu usiku ambapo baba wa mtoto huyo alikwenda nyumbani kwa...

 

1 week ago

CCM Blog

CCM Blog: MAGAZETI YA NDANI NA NJE YA TANZANIA, LEO APRILI 12, 2018

Mdau asante kwa kuperuzi magazeti ya leo katika Blog hii, wewe ni mtu muhimu sana sana kwa uwepo na ustawi wa Blog hii mahiri, endelea kufanya hivi siku zote, ukiwa na maoni andika hapo chini utupostie nasi tutayasoma na kuyafanyia kazi na kama yatahusu wengi pia tutawafikishia. Tunakutakia siku njema. ADMN

 

1 week ago

CCM Blog

ZIARA YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM KATE KAMBA, KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MANISPAA YA TEMEKE

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akizungumza na Viongozi wa CCM na Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Temeke jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba akizungumza na wana CCM alipowasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Temeke kuanza ziara ya kukagua utekelezaji Ilani ya Chama katika Wilaya hiyo
 Viongozi...

 

2 weeks ago

MwanaHALISI

Mbunge wa CCM aikaba serikali

MBUNGE wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) ameihoji serikali na kutaka ieleze ni lini itaana ujenzi wa kituo cha polisi na nyumba za askari. Anaripoti Dany Tibason … (endelea). Nkamia aliihoji serikali leo bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa kutaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga kituo cha polisi wilayani chemba pamoja ...

 

2 weeks ago

CCM Blog

KINANA AONGOZA VIONGOZI WA CCM MAOMBOLEZO YA WINNIE MADIKIZELA MANDELA.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Dkt Gaudensia Kabaka (MCC) akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke...

 

2 weeks ago

Michuzi

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA AHIMIZA VIJANA KUWA NA NIDHAMU

Na Elissa ShundaWAZAZI nchini wameombwa kudumisha nidhamu katika maisha wanayoishi ili vijana wao pia ambao ndiyo viongozi wajao katika ngazi mbalimbali waige mifano mizuri ya kitabia na kiuongozi kutoka kwao ili waje kuwa viongozi bora na si bora kiongozi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Dk.Edmund Mndolwa wakati akizungumza na wanachama wa Jumuiya hiyo na wananchi waliohudhuria  Maadhimisho ya wiki ya wazazi.

Ambayo kitaifa...

 

2 weeks ago

Michuzi

WAZAZI CCM PWANI WATOA DAMU,WACHANGIA UJENZI SHULE YA MSINGI AMANI

Na Elisa Shunda, BagamoyoJUMUIYA ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani imeadhimisha siku ya wazazi kwa mkoa huo kwa kuchangia kutoa damu chupa 120 na kutoa mifuko 50 ya simenti,mabati 100 na matofali 200 vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu na Laki Saba na Hamsini kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi Amani Voda iliyopo Mbwewe wilayani Bagamoyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa mkoa na wilaya waliohudhuria katika maadhimisho hayo wamesema kuwa jukumu...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani