3 days ago

Bongo Movies

Barnaba: Bado nampenda mke wangu

KUNA wasanii na wanamuziki. Wasanii ni wale ambao wanaweza kuifanya kazi yao kuwa sanaa na kuwapatia fedha. Kwenye kuimba wanaweza kuwa siyo wazuri sana.

Wanamuziki ni wale wanaojua kuimba. Wanafahamu ala za muziki, wanatengeneza mahadhi ya muziki wenyewe na kuimba kwa mvuto wa kipekee.

Kwa wale wa Bongo Fleva, kuna mtu anaitwa Barnaba. Huyu ni mwanamuziki. Anajua muziki kuliko kitu kingine chochote.

Amewahi kutamba na vibao kadhaa kama Wrongo Number, Magumegume, Lover Boy na...

 

6 days ago

Zanzibar 24

Picha: Mke wa rais wa zanzibar mama shein akabidhi msaada wa vyarahani zanzibar

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika sherehe ya upokeaji msaada wa Vyarahani uliotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kwa kikundi cha Ushirika wa akina Mama (SIRI MOYONI) Unguja Ukuu Kae pwani Wilaya ya Kati Unguja.

 

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kulia akipeana mikono ikiwa ni ishara ya kupokelewa na Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Maudline Cyrus Castico mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Ushirika wa akina Mama (SIRI...

 

2 weeks ago

VOASwahili

Kuishi pamoja kama mke na mume licha ya mmoja kuwa ameathirika na HIV inawezekana. Tazama hii

Mume na mke walioamua kuishi pamoja licha ya mmoja wa kuwa na maambukizi ya HIV. Amina Chombo kutoka Mombasa anasimulia zaidi.

 

2 weeks ago

BBCSwahili

Jay-Z akiri hajakuwa mwaminifu kwa mke wake Beyonce

Mwanamuziki wa rap Jay -Z amekiri kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine akiwa bado kwenye ndoa yake na Beyonce.

 

2 weeks ago

Malunde

MKESHA WA THE WORSHIPPERS NIGHT 2017 KUFANYIKA IJUMAA HII KATIKA UKUMBI WA UPANGA CCC


WAKAZI WA DAR ES SALAAAM MKO TAYARI? The worshippers night 2017 - USIKU WA WAMUABUDUO ni usiku wa kusifu na kuabudu ambapo watu wote wa Dar es salaaam tutakutana katika ukumbi wa CCC UPANGA JIJINI DAR E SALAAAM, Ni siku ya ijumaaa hii tarehe 1.12.2017 kuanzia saa 2 kamili usiku.


Mkesha huu unawaunganisha watu wote wa madhehebu yote. Mkesha huu utapambwa na choir na waimbaji mbalimbali kama vile
Kwaya ya uinjilisti KIJITONYAMAAIC CHANG'OMBEMTBC PRAISE AND WORSHIP TEAMIFM TAFESMSASANI PRAISE AND...

 

3 weeks ago

Malunde

MKE WA KAFULILA : MUME WANGU KAINGIA KWENYE KUNDI LA WANASIASA WASIO NA MSIMAMO
Mke wa aliyewahi kuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, Jesca Kishoa, amemtaja mumewe kuwa ni mtu aliyeingia kundi la wanasiasa wasio na msimamo.
Kishoya amesema wakati wote mumewe amekuwa na msimamo usioyumba lakini anashangazwa kaingia katika mtego mbovu.
"Bado naamini kuwa Chadema ni mahali sahihi kabisa ambapo siwezi kufikiri siku moja nitatoka, hivyo siyumbi kwa hilo na wanaonipigia simu watambue hilo," amesema Kishoya
Amesema taarifa za mumewe kujiondoa Chadema amezipata kupitia...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Mke wa Tundu Lissu afunguka mazito

Mke wa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema angependa kuwajua watu waliomshambulia mumewe, aliyewaamuru wafanye shambulio hilo na sababu za kufanya uovu huo. Mke huyo ambaye pia ni wakili, Alicia Magabe anasema kuwafahamu watu hao ni muhimu kwa kuwa familia haijui kwa sasa watu hao wanatafakari na kupanga kitu gani baada ya jaribio la kwanza la kumuua kushindikana. Lissu, alishambuliwa na watu wasiojulikana Septemba 7 akiwa ndani ya gari lililokuwa limewasili kwenye...

 

3 weeks ago

Malunde

MKE WA TUNDU LISSU AFUNGUKA MAZITO KUHUSU WALIOMSHAMBULIA MMEWE
Mke wa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema angependa kuwajua watu waliomshambulia mumewe, aliyewaamuru wafanye shambulio hilo na sababu za kufanya uovu huo.

Mke huyo ambaye pia ni wakili, Alicia Magabe anasema kuwafahamu watu hao ni muhimu kwa kuwa familia haijui kwa sasa watu hao wanatafakari na kupanga kitu gani baada ya jaribio la kwanza la kumuua kushindikana.

Lissu, mmoja wa wanasiasa wasio na hofu kusema lolote wanaloliamini, alishambuliwa na watu wasiojulikana...

 

3 weeks ago

Malunde

MKE WA MGOMBEA UDIWANI CHADEMA AMUOMBEA KURA MMEWE ALIYEKO MAHABUBU
 Mke wa mgombea udiwani Kata ya Mhandu (Chadema), Godfrey Misana amelazimika kupanda jukwaani kumwombea kura mume wake aliye mahabusu kutokana na kukabiliwa na shtaka la kujeruhi.
Katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika leo Jumapili Novemba 19,2017 katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu, mwanamama huyo, Rose aliitwa jukwaani na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kuomba kura kwa ajili ya mume wake. 
Rose aliwaomba wakazi wa kata ya Mhandu kumpa kura mume wake ili aweze...

 

4 weeks ago

BBCSwahili

Rais Mugabe amtunuku shahada mke wa Jenerali aliyemzuia

Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe, akiwemo mke wa jenerali aliyemzuia siku ya Jumatano

 

1 month ago

Malunde

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MKE WAKE AKIWA KWA MCHEPUKO

Mkazi wa Mtaa wa Kamando katika Kata ya Igunga Mjini wilayani Igunga mkoani Tabora, Masumbuko Stephano (39) amefariki dunia papo hapo baada ya kuchomwa kisu na mkewe Christina Elias (30) kwa wivu wa mapenzi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kamando, Julius Kitundu alisema mauaji hayo yamefanyika Novemba 6, mwaka huu saa 7:15 usiku katika Mtaa wa Kamando. 
Kitundu alidai Stephano alichomwa kisu wakati akiwa kwa hawara yake, Happiness William (28) mkazi wa Mtaa wa Kamando.
Alidai mke wa marehemu...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Beka Flavour aporomosha matusi kisa Mwanamke

Msanii Beka Flavour ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Sikinai’ amefunguka na kuomba radhi kwa Watanzania baada ya kushusha matusi kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya mtu mmoja kumkorofisha juu ya mpenzi wake.

Beka Flavour amesema kuwa yeye kama binadamu alipoona mtu huyo ameandika mambo ambayo hakupendezwa nayo kuhusu mpenzi wake huyo aliamua kumjibu na kwa kuwa alikuwa na hasiri alijikuta ameandika matusi pasipo yeye mwenyewe kutegemea.

 

Matusi aliyoyatupia beka Flavour...

 

1 month ago

Malunde

MKE WA LAZARO NYALANDU,FARAJA KOTA AVUNJA UKIMYA

Faraja Kota ambaye ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza jinsi alivyojawa na hofu baada ya mfululizo wa matukio ya wiki nzima tangu mumewe atangaze kujiondoa ndani ya CCM.
Mwanamke huyo aliyewahi kutwaa taji la Miss Tanzania katika mtandao huo ameandika “If only you knew how terrified I am.” Akimaanisha laiti ungejua ni kiasi gani nimejawa hofu.
Hata hivyo, wafuasi wake katika mtandao huo katika maoni yao wamemtoa hofu huku...

 

1 month ago

Malunde

Makubwa Haya : WAKUTWA WAMEKUFA WAKIFANYA MAPENZI KWENYE TAXI .....MWANAMKE NI MKE WA MTU

Mwili wa mwanamke mmoja aliyeripotiwa kuwa ni mke wa mtu mwenye watoto wanne umekutwa kwenye taxi mjini Lagos, nchini Nigeria ukiwa juu ya kifua cha mwanaume ambaye naye alikuwa ameshakufa. 
Wote wawili wakiwa wamelaliana wakishiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea Jumapili ya wikiendi iliyopita wamesema walikuta gari dogo (Taxi) ikiwa imepaki na ndani kukiwa na watu waliokuwa uchi wakiwa wamelaliana ndipo wakaamua kuchukua uamuzi wa kufungua milango.
Shuhuda...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani