4 days ago

Michuzi

FIFA: Mkutano wao hawataki Mtu zaidi ya viongozi wa TFF na Waandishi 10 tu

 

1 week ago

MillardAyo

Deus Kaseke na Shaban Dihile wamefungiwa na TFF leo

Mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho la soka Tanzania TFF Efram August leo ametangaza kuwa mchezaji wa Singida United Deus Kaseke na mchezaji wa Green Warriors Shaban Dihile wamefungiwa mechi tatu kila mmoja na faini ya Tsh laki 5. VideoMAGOLI: Yanga vs Majimaji FC Feb 14 2018, Full Time 4-1

 

1 week ago

Michuzi

Serikali na TFF yakutana na Wahariri wa Michezo kujadili Maandalizi ya Ujio wa Rais wa FIFA na CAF

 Mjumbe wa CAF na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Leodger Tenga (katikati) akizungumza na Wahariri wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali nchini (hawapo pichani) kuhusu mambo ambayo uongozi wa FIFA utapenda kujua katika soka la Tanzania ambapo moja wapo ni Maendeleo ya Soka la Wanawake,Kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe na Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa...

 

2 weeks ago

Michuzi

KAMATI YA NIDHAMU TFF YAMFUNGIA JUMA NYOSO, KUKOSA MECHI TANO

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza kumfungia  Juma Nyoso wa Kagera Sugar kwa kosa la kupiga shabiki baada ya mchezo kati ya timu yake dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.
Akitolea ufafanuzi hukumu hiyo, Ofisa habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kamati ya nidhamu iliketi na kujadili masuala mbalimbali ya nidhamu ikiwemo suala la beki wa timu ya Kagera Juma Nyoso kumpiga shabiki wakati wa mchezo wao...

 

3 weeks ago

Michuzi

VIGOGO TFF KUHUDHURIA MKUTANO MKUU CAF

Na Agness Francis, Globu ya Jamii VIONGOZI wa tatu wa ngazi za juu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) wanatarajia kuhudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika(CAF).
Taarifa ya TFF iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam imesema mkutano huo utafanyika Februari 2 mwaka huu nchini Morocco.
Imesema viongozi watakaohudhuria ni Rais wa Bodi ya Ligi ya Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia, Makamu wa Rais wa TFF Michael  Wambura na Kaimu  mkuu wa Bodi hiyo Kidao...

 

3 weeks ago

Michuzi

KAMATI YA MAADILI TFF YAMUADHIBU MJUMBE BODI YA LIGI

Na Agness Francis Globu ya jamii.
KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungulia mashitaka Mwenyekiti wa Abajalo FC na Mjumbe wa Bodi ya Ligi Edgar Chibula kwa tuhuma ya kuikashifu na kuidhalilisha Kamati ya Bodi ya Ligi ya TFF katika vyombo vya  Habari ambapo ni kinyume na sheria. 
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Ofisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amesema kuwa  Chibura alishitakiwa Februari 28 mwaka huu kwa kosa la  kuzungumza maneno yasiofaa kwa...

 

4 weeks ago

Zanzibar 24

Juma Nyoso ashtakiwa kamati ya nidhamu ya TFF

Afisa Mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura leo Januari 27, 2018 amesema kufuatia  mchezaji Juma Nyosso wa Kagera Sugar kumpiga shabiki kamati hiyo imepitia ripoti ya kamishna wa mchezo huo namba 112 kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba SC na kubaini kuwa tukio hilo ni la kinidhamu hivyo kulifikisha sehemu husika.

”Kamati imepitia ripoti ya kamishna na imeonesha kuwa kulikuwa na tukio ambapo mchezaji wa Kagera Sugar Juma Nyosso alimpiga ngumi shabiki hivyo suala hilo...

 

1 month ago

Michuzi

TFF:KAMATI YA MAADILI YAPITIA SHAURI LA WATUHUMIWA WA KUGHUSHI NA UDANGANYIFU WA MAPATO.

Kamati ya Maadili iliyokutana Januari 18, 2018 imepitia shauri lililowasilishwa na Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF wakiwatuhumu viongozi wanne kwa makosa ya kughushi na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC na Simba uliochezwa Disemba 30,2017.
Shauri la kwanza lililomuhusu Katibu msaidizi wa Ndanda Ndugu Selemani Kachele,Kamati imegundua kuwa mtuhumiwa aliitwa wakati wa kuhesabu mapato kuthibitisha deni dhidi ya Ndanda lenye thamani ya...

 

1 month ago

Michuzi

SERIKALI YATOA TAMKO SAFARI YA SIMBU, YAWAONYA TFF

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SERIKALI imetoa tamko kuhusu ushiriki wa mwanariadha Alphonce Simbu katika mashindani ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika April mwaka huu.
Mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika Gold Coast nchini Australia, ambapo Serikali na Kamati ya Olimpiki Taifa (TOC) walipokea barua kutoka kwa Simbu ya kuomba ashiriki mashindano ya London Marathon ambayo ni makubwa zaidi kuliko ya Jumuiya ya Madola. Simbu ambaye ni mshindi wa tatu wa London Marathon...

 

1 month ago

Michuzi

CAF YATEUA WANNE TFF KUSIMAMIA MECHI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limepitisha majina manne ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwa makamishna wa michezo mbalimbali inayoandaliwa na CAF.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizotoa Makamishna wanne ambayo ni idadi ya juu hakuna nchi iliyozidisha idadi hiyo ambayo ni kwa kipindi cha kutokea mwaka 2018 mpaka 2020.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF waliopata nafasi hiyo ni Makamu wa Rais Michael Wambura,Ahmed ...

 

1 month ago

Michuzi

RAIS WA TFF WALLACE KARIA AOMBOLEZA KIFO CHA OMARY KAPERA:


Kufuatia kifo cha beki wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Omary Kapera (wa tatu toka kulia) ,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha beki huyo wa zamani. Rais Karia akitoa salamu za rambirambi amesema ni masikitiko makubwa kumpoteza mmoja wa wachezaji wa zamani aliyeitumikia pia timu ya taifa. "Nimeshtushwa na taarifa hizo za kifo cha Kapera hasa ikichukuliwa bado tupo kwenye majonzi ya kumpoteza...

 

2 months ago

Michuzi

MAAMUZI YA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF

Kamati ya nidhamu iliyokutana Januari 1, 2018 ilipitia ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 na ule kati ya Azam Fc na Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017.

Kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons,Meneja wa timu ya Tanzania Prisons Erasto Ntabahani alipelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu kwa kosa la kumshambulia muamuzi wa akiba,kamati imejiridhisha kuwa Ntabahani alimshambulia kwa...

 

2 months ago

Michuzi

KAMATI YA MASHINDANO TFF YAIPA USHIND PRISONS NA JKT RUVU KOMBE LA FA

Kikao cha kamati ya Mashindano kilichokutana Desemba 29, 2017 kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujadili mchezo namba 31 na 32 uliohusisha timu za Abajalo FC dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya na ule kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) iliyokuwa ifanyike Desemba 20, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru na Chamazi.

Kamati ilikaa na kupitia taarifa mbalimbali za michezo hiyo.
Kamati kupitia kanuni ya 24 kifungu cha (1) katika mchezo kati...

 

2 months ago

Malunde

MWAKYEMBE ATOA MAAGIZO MAZITO TFF

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka TFF kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayohusu michezo ya ligi daraja la kwanza, kati ya Dodoma FC vs Alliance na Pamba vs Biashara.

Sakata la maamuzi yasiyo ya haki katika michezo ya Dodoma FC dhidi Alliance ya Mwanza na Pamba ya Mwanza dhidi Biashara ya Musoma ndio limefanya Waziri mwenye dhamana ya michezo kutoa agizo hilo kwa shirikisho ili kuhakikisha utata huo unamalizika.

Katika taarifa yake Waziri Mwakyembe...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani