9 months ago

Malunde

ASKARI WALIOTUHUMIWA MAUAJI YA AKWILINA WAACHIWA...DPP AFUNGA JALADA

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi.

Hayo ameyasema leo Aprili 20, 2018; Ikulu jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari huku akionya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.

Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki...

 

10 months ago

Malunde

LEMA : SI AJABU UKASIKIA SILAHA ILIYOMUUA AKWILINA IPO NYUMBANI KWA KIONGOZI WA CHADEMA


Machi 30, 2018 Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameongea kuhusu taarifa iliyotolewa na Kamanda wa kanda maalum ya DSM Lazaro Mambosasa kuhusu silaha iliyotumika kumuua Akwilina kuwa bado haijajulikana na wanaendelea na upelelezi.
Lema kupitia akaunti yake ya Twitter ameandikia kuwa ameitafakari kauli ya Mambosasa kuhusu tukio la Akwilina juu ya silaha iliyotumika.
“Nimeitafakari kauli ya Mambosasa inayohusu tukio la Akwilini kuhusu silaha iliyotumika, bila shaka kuna dhambi kubwa...

 

10 months ago

Malunde

Mambosasa: Silaha Iliyomuua Akwilina Haijajulikana, Bado Tunaendelea KuchunguzaKamanda wa Polisi Kanda Maalum jijni Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ameelezea hatua inayoendelea kuchukuliwa juu ya askari polisi sita waliokuwa wameshikiliwa kutokana na kifo cha mwanafunzi wa NIT Akwilina Akwilin, aliyeuawa kwa risasi mapema mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kamanda Mambosasa amesema polisi hao bado wapo kwenye uchunguzi kubaini ni nani anahusika, kwani mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuweza kumbaini.
“Wale...

 

10 months ago

MwanaHALISI

Mbowe, Viongozi Chadema wapewa kesi ya Akwilina

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na viongozi watano wa chama hicho wamesomewa mashtaka nane katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu likiwemo la kufanya maandamano yaliyosababisha kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT), Akwilina Akwiline. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Mbowe na wenzake Dk. Vicent Mashinji, Salum Mwalim, Mchungaji Peter Msigwa, John Mnyika na ...

 

11 months ago

MwanaHALISI

Mbowe aibua mazito risasi ya Akwilina

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kuwa jeshi la Polisi limewajeruhi waandamanaji wa tano wa risasi za moto huku moja ikimpata Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT), Akwilina Akwilini zilizokuwa zikiwalenga wao. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Mbowe amewaambia waandishi wa Habari leo, kuwa Polisi walifyatua risasi za moto ...

 

11 months ago

Ghafla!

University student Akwilina Akwilini shot dead by a police man finally laid to rest


Ghafla!
University student Akwilina Akwilini shot dead by a police man finally laid to rest
Ghafla!
A student, Akwilina Akwilini from the collage of NIT in Tanzania was shot dead on 17th February; by a stray bullet as revealed on social media. Apparently the young lady met her untimely death after the police allegedly shot in the air; to control a ...

 

11 months ago

Malunde

WAZIRI NDALICHAKO AAHIDI KUMSOMESHA MDOGO WAKE AKWILINA

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kumsomesha mdogo wake Akwilina Akwilini, Angela Akwilini ambaye kwa sasa anasoma kidato cha tatu.
Akizungumza leo Februari 23, 2018 baada ya mazishi ya Akwilina aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16, 2018 eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam, Profesa Ndalichako amesema atamsomesha Angela hadi Chuo Kikuu.

 

11 months ago

AllAfrica.Com

Tanzania: Gone Too Soon - Akwilina Laid to Rest


Ghafla!
Tanzania: Gone Too Soon - Akwilina Laid to Rest
AllAfrica.com
Dar es Salaam — The body of Akwilina Akwiline has been laid to rest at her home village of Marangu in Rombo District, Kilimanjaro. The the burial was attended by a lot of top government officials including minister for Education, Science and ...
University student Akwilina Akwilini shot dead by a police man finally laid to restGhafla!

all 5

 

11 months ago

Malunde

KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA WA AKWILINA MKOANI KILIMANJARO

Mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umeshapelekwa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro ambako inafanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu.

Baada ya ibada hiyo ndugu, jamaa, viongozi na watu wa kada mbalimbali watatoa heshima za mwisho na kisha mwili kupelekwa nyumbani kwa ajili ya mazishi yatakayoanza saa saba mchana.

 

11 months ago

Malunde

USALAMA WAIMARISHWA KIJIJI ATAKACHOZIKWA MWANAFUNZI AKWILINA ALIYEPIGWA RISASI


Vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha usalama katika eneo atakalozikwa mwanafunzi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline katika kijiji cha Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Uchunguzi uliofanywa na MCL Digital saa 2:00 hadi saa 4:30 asubuhi leo Ijumaa Februari 23, 2018 umebaini uwapo wa askari wengi wakiwamo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na askari kanzu.
Mbali na askari kanzu, wameonekana maofisa usalama wa Taifa na polisi waliovalia kiraia, wakiwa...

 

11 months ago

Malunde

VIONGOZI MBALIMBALI WAMEANZA KUWASILI MAZISHI YA AKWILINA KILIMANJARO

Viongozi mbalimbali wa Serikali wameanza kuwasili nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini kijiji cha Marangu, Kata ya Marangu Kitowo, Olele mkoani Kilimanjaro.

Mwili wa mwanafunzi huyo aliyeagwa jana katika viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es Salaam umefika kijijini hapa leo Februari 23, 2018 saa 3:30 asubuhi.

Viongozi waliofika mpaka sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Leonard Akwilapo, Mkuu wa Chuo Cha NIT, Profesa...

 

11 months ago

Malunde

MAELFU WAUAGA MWILI AKWILINA DAR, MAZISHI KESHO KILIMANJARO

Mwili wa mwanafunzi aliyepigwa risasi na askari polisi siku ya Ijumaa, Februari 16, Akwilina Akwilini, umeagwa rasmi leo na maelfu ya waombolezaji pamoja na wanafunzi wa chuo cha Usafirishaji, na kisha kuanza safari kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.


Shughuli ya kuaga mwili huo imefanyika leo mchana  katika viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), huku pia baadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali na watu maarufu wakihudhuria tukio hilo, lililowaacha mamia na machozi ya...

 

11 months ago

Malunde

WANAFUNZI WA CHUO CHA NIT WABEBA MABANGO YENYE UJUMBE MZITO WAKIMUAGA AKWILINA

Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwemo ya kumtaka waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kujiuzulu.


Ibada hiyo imefanyika leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali.

Waombolezaji hao walinyanyua mabango hayo baada ya waziri wa Elimu,...

 

11 months ago

MwanaHALISI

Akwilina aagwa, wanafunzi watoa neno zito kwa serikali

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo, Prof. Joyce Ndalichako amesutwa na wanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) baada ya kutaka kuwatetea wauaji wa Akwilina Akwilini. Anaripoti Mwandishi Wetu …. (endelea). Tukio hilo limetokea leo Alhamisi Viwanja vya NIT, Mabibo jijini Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Akwilina, aliyeuwawa kwa risasi “iliyorushwa na ...

 

11 months ago

Malunde

Picha : MATUKIO YALIYOJIRI BAADA YA MWILI WA AKWILINA KUWASILI KATIKA CHUO CHA NIT

Vilio, simanzi na kupoteza fahamu kwa baadhi ya wanafunzi ni baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.
Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.
Wanafunzi zaidi ya wanne aliokuwa akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama hawaamini baada ya kushuhudia jeneza lenye mwili wake, huku wengine wakipoteza fahamu na kupewa huduma...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani