2 weeks ago

Michuzi

AZAM TV 2: TAARIFA YA HABARI JUNI 5, 2019

 

2 weeks ago

Michuzi

KUTINYU AMFUATA KOCHA VAN DER PLUIJM AZAM FC

Na Agness Francis, Globu ya Jamii
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati  Azam FC imetangaza rasmi kuwa imemsajili  kiungo Tafadzwa Kutinyu mkataba wa mwaka mmoja.
Kiungo huyo atachezea kikosi cha  Azam FC ambacho maskani yake iko Chamazi jijini Dar es Salaam. Mchezaji huyo amekuwa na msimu mzuri tokea ajiunge na Singinda United msimu huu ambaye alitokea katika klabu ya Chicken Inn ya nchini kwao Zimbabwe.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Azam FC Jaffary Iddy amesema mchezaji huyo...

 

3 weeks ago

Michuzi

HIMID MAO MKAMI AAGA RASMI AZAM FC

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Aliyekuwa Nahodha wa Azam FC, Himid Mao Mkami ameiaga rasmi timu hiyo, baada yakupata nafasi kwenda kucheza Soka la kulipwa nchini Misri kwenye Klabu ya Petrojet inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo inayofundishwa na Aliyekuwa Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hassan Shehata.
Himid maarufu kwa jina la Ninja aliyekuwa na Azam FC tangu mwaka 2009, katika ukurasa wake wa Instagram ametumia nafasi hiyo kuaga Benchi la Ufundi, Makocha, Viongozi na Wafanyakazi wote wa...

 

4 weeks ago

Michuzi

MSHAMBULIAJI AZAM AKIRI MAJERAHA YA NYONGA YAMEPUNGUZA KASI ALIYONAYO MSIMU ULIOPITA

Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
MSHAMBULIAJI wa Azam Shaaban Idd, amekiri kuwa nje ya dimba kwa takribani miezi saba akiuguza majeraha ya nyonga kulimwaribia kuendeleza kasi aliyokuwa nayo msimu uliopita.
Shaaban aliweza kuiongoza Azam FC kuichapa Tanzania Prisons mabao 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) akifunga hat-trick na jingine likitupiwa wavuni na kiungo Frank Domayo.
Mara baada ya Shaaban kukosa raundi ya kwanza ya ligi kutokana na majeraha aliyopata...

 

1 month ago

Michuzi

AZAM FC YATAMBA KUIFUNGA PRISON JUMAPILI

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, tayari imeianzia kambi Tanzania Prisons huku benchi la ufundi likijinasibu limejipanga kuendeleza ubabe dhidi ya maafande hao.
Timu hizo zinatarajia kuumana Jumapili hii katika Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1.00 usiku, ukiwa ni mchezo wa raundi ya 29 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa kikosi hicho kimeanza vema maandalizi yake huku akikiri ushindani mkubwa unaoonyeshwa na...

 

1 month ago

Michuzi

AZAM WAKATA TAMAA KUTWAA UBINGWA MSIMU HUU, WAAHIDI KULINDA HESHIMA

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC imepoteza matumaini yake ya kunyakuwa kombe la Ligi Kuu vodacom Tanzania bara msimu huu.
Kwa sasa Azam FC ana michezo 3 iliyobakia mpaka hivi sasa ambayo akishinda yote atanyakuwa pointi 9,miwili ikiwa ni ya Nyumbani na mmoja wa ugenini.
Wanalambalamba hao watawakaribisha wanalizombe Maji maji kutoka mkoani Ruvuma katika dimba la Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam utakaochezwa kesho saa 10...

 

2 months ago

Michuzi

AZAM vs MTIBWA, SASA KUPIGWA SAA 10 JIONI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MCHEZO kati ya Klabu ya Azam FC na Mtibwa Sugar uliotarajiwa kuchezwa saa 8 mchana umefanyiwa mabadiliko ya muda, ambapo sasa utafanyika Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro, kesho Jumamosi saa 10.00 jioni.
Awali mchezo huo ulikuwa ufanyike saa 8.00 mchana, lakini Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeamua kuusogeza hadi jioni kutokana na ratiba ya wadhamini wa matangazo ya televisheni Azam TV kutobana muda huo.
Tayari kikosi cha Azam FC kimewasili mkoani...

 

2 months ago

Michuzi

MWANTIKA AANZA MAZOEZI MEPESI, YAKUBU MOHAMED KWENDA AFRIKA KUSINI KWA UCHUNGUZI ZAIDI- DAKTARI AZAM

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
BEKI wa timu ya Azam Fc David Mwantika, ameanza rasmi mazoezi ya wenzake wiki hii ikiwa baada ya kuugua ghafla uwanjani wiki tatu zilizopita.
Mwantika alipata hitilafu hiyo ya mwili dakika ya 65 wakati Azam FC ikicheza hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Mtibwa Sugar kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Mbagala Zakhem na kuhamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke, na baadaye ya Rufaa ya Muhimbili (MNH).
Baada ya...

 

2 months ago

Michuzi

AZAM WAIOMBA TFF WASOGEZA MBELE MECHI YAO DHIDI YA NJOMBE MJI

Na Agness Fracis,Blogu ya Jamii

UONGOZI wa Azam FC umeomba mchezo wao dhidi ya Njombe Mji usogezwa mbele kutokana na muda mchache waliopumzika baada ya kumalizana na Ruvu Shoting ya Mlandizi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa Azam Jaffary Maganga amesema wameomba mchezo kusogezwa mbele ili kupata nafasi ya kujiandaa ikiwa ni jana wametoka ugenini kucheza na timu ya Ruvu shooting.

"Tumeandika barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania( TFF) kuomba mchezo dhidi ya...

 

2 months ago

Michuzi

NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUCHEZWA APRILI 20 NA 21

Hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inatarajia kuchezwa Aprili 20 na Aprili 21,2018.
Nusu fainali ya Kwanza itachezwa Ijumaa Aprili 20,2018 ikiwakutanisha Stand United ya Shinyanga watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage,Shinyanga saa 10 jioni.
Singida United ya Singida watawakaribisha JKT Tanzania ya Dar es Salaam kwenye nusu fainali ya pili itakayochezwa Uwanja wa namfua Jumamosi Aprili 21,2018 saa 10 jioni.
Washindi kwenye nusu...

 

3 months ago

Michuzi

AZAM KUJIPIMA NGUVU KWA FRANCE RANGERS KABLA YA KUVAANA NA MTIBWA SUGAR

Na Agness Francis Globu ya jamiiKLABU Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC wanawakaribisha France Rangers katika dimba lao la nyumbani kwa ajili ya mchezo wa kirafiki.
France Rangers ni timu ambayo imemaliza msimu huu daraja la kwanza Mkoa wa Dar es Salaam yenye kikosi kizuri na wachezaji walio fiti uwanjani.
Mchezo huo wa kirafiki dhidi ya timu hizo mbili utachezwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi  utakaofanyika kesho Jumamosi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Habari Azam FC...

 

3 months ago

Michuzi

BEKI WA AZAM FC KUELEKEA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BEKI wa kati wa Azam FC, Daniel Amoah, anatarajia kwenda jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya goti Jumatatu ijayo.
Amoah ameshindwa kupona majeraha hayo tokea ayapate Desemba 19, mwaka jana, wakati Azam FC ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania na kuichapa mabao 3-1.
Februari 7 alirejea tena uwanjani na kucheza mechi dhidi ya Simba, Azam FC ikipoteza kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo alijikuta akijitonesha tena hali...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani