1 month ago

Zanzibar 24

Sailors yachupa hadi nafasi ya pili baada ya kuwapa kichapo polisi, kmkm hoi kwa mafunzo, boys mzigoni leoo

Timu ya Black Sailors “Mabaharia Weusi” wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya kuichapa Polisi bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa jioni ya jana kwenye uwanja wa Amaan. Bao pekee la Sailors limefungwa na Hassan Said “Kilahe” dakika ya 29 na kuwafanya sasa wakamate nafasi ya pili kwenye msimamo  baada ya kufikisha alama 12 sawa sawa na JKU ambao pia wana points 12 tofauti ya mabao ya kushinda na kufungwa huku KVZ wakiongoza ligi hiyo...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Sailors yachapwa na zimamoto, boys yaanza ligi

Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo saa 8 za mchana Jang’ombe Boys waliichapa Charawe mabao 4-2. Mabao ya Boys yamefungwa na Khamis Mussa (Rais) dakika ya 3, 9, na 21 (Hat-trick) na bao la nne likifungwa na Hafidh Bariki (Fii) dakika ya 83 huku mabao ya Charawe yakiwekwa nyavuni na Ulimwengu Edimundi dakika ya 66 na Yussuf Mkubwa dakika ya 68. Saa 10 za Jioni Black Sailors ikachezea kichapo cha mabao 2-1...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Khamis Mussa rais wa boys apiga hat-trick

Mshambuliaji wa timu ya Jang’ombe Boys Khamis Mussa (Rais) amefanikiwa kuondoka na mpira uwanjani baada ya kufunga mabao 3  yani Hat trick. Amefunga mabao hayo wakati Boys walipoipiga Charawe mabao 4-2 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa mchana wa leo katika Uwanja wa Amaan. Rais amefunga mabao hayo katika dakika ya 3, 9, na 21  na bao la nne likifungwa na Hafidh Bariki (Fii) dakika ya 83 huku mabao ya Charawe yakiwekwa nyavuni na Ulimwengu Edimundi...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Boys hoi kwa kilimani City, Sailors yaimaliza Charawe

Timu ya Jang’ombe Boys imeendelea kufanya vibaya katika ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na Kilimani city mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan.

Bao pekee la City limefungwa na Baraka Mashango dakika ya 19.

Mapema saa 8 za mchana Kiwanjani hapo Black Sailors wakaendelea na ari yao ya ushindi baada ya kuifunga Charawe mabao 2-1.

Mabao ya Sailors yamefungwa na Mustafa Hamad “Mboma” dakika ya 43 na Maulid Dhamiri wa Charawe alijifunga mwenyewe...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Boys kama Taifa, yabanwa na Chuoni leo

Mzunguko wa tatu wa ligi kuu soka Zanzibar Kanda ya Unguja umehitimishwa jioni ya leo kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan kati ya Jang’ombe Boys na Chuoni ambao wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0.

 

Kwa matokeo hayo Boys amefikisha alama 2 baada ya kucheza michezo mitatu kwa kwenda sare miwili na kufungwa mmoja wakati Chuoni amejikusanyia alama 4 baada ya kushinda mmoja, sare mmoja na kufungwa mmoja.

 

Mzunguko wa nne wa ligi hiyo utaanza Ijumaa Oktoba 27 katika...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Jan’gombe Boys hoi kwa Black Sailors

Mzunguko wa pili wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja umemalizika jioni ya leo ambapo timu ya Black Sailors (Mabaharia Weusi) wameichapa Jang’ombe Boys bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Amaan.

Bao pekee la Sailors lililopeleka furaha kwa kocha wao Juma Awadh limefungwa na Abbas Peter John dakika ya 75 ya mchezo huo.

Mzunguko wa tatu wa ligi hiyo utaanza Jumamosi ya Oktoba 21 saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Amaan kati ya Mafunzo na Taifa ya Jang’ombe na saa 10:00 za...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Charawe hoi yapigwa 4-0 na Kipanga, KMKM yawatia adabu Kilimani City, kesho Sailors na Boys

Timu ya Kipanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mnene baada ya kuichapa Charawe mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliopigwa saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan.

Mabao ya Kipanga mawili yamefungwa na Nassor Ali dakika ya 9 na 47 huku mabao mengine yakiwekwa nyavuni na Talib Hamad dakika ya 30 na Daud Nyerere dakika ya 87.

Saa 10 za jioni uwanjani hapo ulipigwa mchezo mwengine ambapo Timu ya Mabaharia wa KMKM imefanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu baada...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Ligi Kuu Zanzibar yaanza kwa kishindo, JKU raha raha, Boys na KMKM hakuna mbabe

Ligi kuu soka Visiwani Zanzibar kanda ya Unguja imeanza rasmi leo kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.

 

Mapema saa 8 za mchana Mabingwa watetezi wa ligi hiyo JKU wameanza vyema baada ya kuichapa Mafunzo bao 1-0 kwa bao lililofungwa na Ali Haji Said (Zege) dakika ya 44.

 

Mchezo mwengine uliopigwa kiwanjani hapo majira ya saa 10 za jioni Jang’ombe boys na KMKM wakaenda sare ya kufungana bao 1-1.

 

KMKM ndio wa kwanza kufunga bao kupitia Salum Akida dakika ya 5 ambapo bao la...

 

3 months ago

Channelten

Mchezaji wa Serengeti Boys afuzu majaribio Esperance ya Tunisia

43

Mchezaji wa Serengeti Boys afuzu majaribio Esperance ya Tunisia

Mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, Yohana Oscar Nkomola amefuzu majaribio katika klabu ya Esperance ya Tunisia na sasa anatarajiwa kusaini mkataba.

Nkomola alikuwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki fainali za vijana Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon.

CHANZO : CRI KISWAHILI

Share on: WhatsApp

The post Mchezaji wa Serengeti Boys afuzu majaribio Esperance ya Tunisia appeared first on...

 

3 months ago

Zanzibar 24

Picha; Jang’ombe boys wakifanya Usafi hospitali ya Kidongo chekundu

Mapema leo asubuhi wapenda michezo wa Jang’ombe boys wamejitokeza kufanya usafi wa mazingira katika hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo Chekundu Mjini Unguja.

The post Picha; Jang’ombe boys wakifanya Usafi hospitali ya Kidongo chekundu appeared first on Zanzibar24.

 

5 months ago

Mwanaspoti

Mngeta Rangers, City Boys zafanya kweli

Mngeta Rangers FC imeanza kwa  kishindo mashindano ya Rwakatare Cup 2017 baada ya kuisambaratisha Bodaboda Itongoa  FC kwa mabao 5-1 katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo.

 

5 months ago

Zanzibar 24

Boys wampa jezi shabiki mtoto wa timu hiyo

Kijana Abdulrahman Khatib, shabiki wa Jang’ombe Boys aliyeonekana amevaa fulana iliyoandikwa ‘I love Jang’ombe Boys’ huku akijimilikisha namba 13, amepewa jezi rasmi za timu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na katibu wa Jang’ombe Boys, Alawi Haidar Foum, imesema dogo huyo pia amepewa madaftari, begi la shule na fedha taslimu shilingi elfu thelathini.

Kundi la mashabiki wa Jang’ombe Boys, FRIENDS OF BOYS, limebeba majukumu mawili ya kumsaidia dogo huyo

1. Kumlipia kiingilia kwenye mechi zote za...

 

5 months ago

Mwananchi

Kamusoko, kipa Serengeti Boys wasaini Yanga

Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba mpya wa miaka miwili kiungo Mzimbabwe, Thaban Kamusoko huku pia ikimsajili kipa wa Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili.

 

5 months ago

Mwanaspoti

Kipa Serengeti Boys aitwa Taifa Stars

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemuita kikosini aliyekuwa  kipa wa timu ya taifa ya vijana 'Serengeti Boys', Ramadhan  Kabwili katika maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) dhidi ya Rwanda, Jumamosi hii.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani