(Yesterday)

Malunde

ZITTO KABWE AIJIBU CHADEMA KUHUSU KUMSIFIA RAIS MAGUFULI

Na Regina MkondeMbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewajibu baadhi ya watu wanaomkosoa na kumuita msaliti kutokana na kitendo cha kumsifia Rais John Magufuli alipokuwa ziarani jimboni humo.

Zitto alijibu mapigo hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kigoma Mjini, ambapo alisema asingeweza kumkosoa Rais Magufuli wakati ule kwa kuwa alikuwa mgeni jimboni kwake, pia alikuwa anafanya shughuli za maendeleo ya wananchi wa jimboni...

 

1 day ago

Malunde

MADIWANI WATATU WA CHADEMA WAJIUZULU NA KUTIMKIA CCM HAI KILIMANJARO

Wakati Wimbi la Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kujiunga na Chama cha Mpinduzi (CCM) likiwa limepamba moto mkoani Arusha, majirani zao wa Kilimanjaro nao wameanza kutimka kwa kile wanachodai kuwa ni kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Mapema leo mchana Julai 26, 2017, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewapokea madiwani watatu kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai ambao wametangaza kujiuzulu nyadhifa zao na kujiunga CCM.

Madiwani...

 

1 day ago

MwanaHALISI

Wanachama 54 Chadema wambwaga OCD wa Geita

MAWAKILI wanaowatetea wanachama 54 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), wameshinda pingamizi la Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Geita, Mponjoli Mwabulambo, katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya kufanya mkutano wa ndani kinyume cha Sheria, anaandika Irene David. Wiki mbili zilizopita wanachama hao walikamatwa na kupelekwa polisi na hatimaye kufikishwa mahakamani ambapo OCD aliwakatalia ...

 

2 days ago

Mwananchi

Diwani wa tisa Chadema ajiuzulu mkoani Arusha

Madiwani wa Chadema wameendelea kukihama chama hicho kwa kile wanachodai ni katika kuunga mkono utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

 

4 days ago

TheCitizen

Chadema condemns arbitrary arrests of its leaders

Opposition Chadema has condemned arbitrary arrests of its leaders and the prevention of political meetings by the state.

 

4 days ago

Zanzibar 24

Bendera za CHADEMA zamponza mbunge wa Mbozi

Mbunge wa Mbozi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Pascal Haonga ameitwa na Jeshi la Polisi kutokana na bendera za chama chake kupepea kwa wingi katika mji wa Mlowo wilayani Mbozi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange alimuita mbunge huyo na kumhoji kutokana na bendera hizo kupeperushwa kwa wingi wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili katika eneo hilo ili kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

Pascal Haonga amesema kuwa...

 

4 days ago

Michuzi

MBUNGE VITI MAALUMU CHADEMA ASAIDIA UJENZI MWANZA

Na Judith Ferdinand wa BMG, MwanzaMbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani Mwanza Mhe. Susan  Maselle, ametoa shilingi milioni moja ili kuchangia ujenzi wa darasa la awali (chekechea) katika shule ya msingi Nyerere, Kata ya Igoma Jijini Mwanza.Mhe. Maselle alitoa fedha hizo jana katika harambee ya kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika katika ukumbi wa Agape Lodge katika mtaa wa Nyerere Kata ya Igoma.Alisema pamoja na juhudi za serikali kuboresha elimu,...

 

5 days ago

MwanaHALISI

Chadema kumburuza DC Chemba mahakamani

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Chemba, Dodoma, umejipanga kwenda mahakamani kumfungulia kesi Mkuu wa Wilaya hiyo Samson Odunga, anaandika Dany Tibason. Kusudio la kwenda mahakamani kumfungulia keshi linatokana na madai ya kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji cha Chemka, Hussein Katikilo (Chadema) bila sababu za msingi. Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Chemba, ...

 

7 days ago

Malunde

KATIBU MKUU WA CHADEMA DK. VICENT MASHINJI MATATANI TENA

Katibu Mkuu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Vicent Mashinji, amejikuta matatizoni tena, baada ya kuachiwa kwa dhamana mkoani Ruvuma jana.

Muda mfupi baada ya kuachiwa, Dk. Mashinji aliwekwa chini ya ulinzi na kutakiwa kuripoti ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ili ahojiwe kuhusu kauli yake ya ‘ngedere kulinda shamba’ aliyoitoa kwenye mkutano wa ndani siku chache zilizopita.
Mmoja wa mawakili wanaomtetea kiongozi huyo, Barbabas Pombona, alisema mteja wake alihojiwa...

 

1 week ago

Mwananchi

Mbunge Chadema aanza ziara Katavi

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi kwa tiketi ya Chadema  Rhoda Kunchela ameanza ziara ya mkoa mzima wa Katavi kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi wake.

 

1 week ago

Mwananchi

Mbunge Chadema ahojiwa kwa kufanya kampeni za 2020

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Kunti Majala  amesafirishwa chini ya ulinzi wa polisi leo kutoka Chemba hadi ofisi za polisi mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa akidaiwa kuanza kampeni za uchaguzi mkuu ujao mapema.

 

1 week ago

Channelten

Viongozi 9 Chadema wafikishwa mahakamani, Watakiwa kujibu mashitaka ya kufanya mkusanyiko bila kibali

IMG_8558

Viongozi tisa wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwemo katibu mkuu wa chama hicho taifa,Dokta vicent Mashinji na mbunge wa viti maalum Zubeda Sakuro, wamefikishwa katika mahakama ya mkoa wa Ruvuma, kujibu mashitaka mawili yanayowakabili,ambapo julay 15 mwaka huu wakiwa wilaya ya nyasa mkoani Ruvuma , inadaiwa walifanya mkusanyiko bila kibali.

Kwa upande wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kesi hiyo imesimamiwa na wakili wa serikali Renatus Mkude ameiambia mahakama hiyo kuwa...

 

1 week ago

MwanaHALISI

Polisi walikoroga Ruvuma, wazuia vikao vya ndani vya Chadema

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limekizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya mikutano ya ndani, anaandika Irene David. Katazo hilo limekuja siku chache baada ya viongozi waandamizi wa chama waliokuwa mkoani humo akiwamo Katibu Mkuu, Vicent Mashinji kushikiliwa na vyombo vya usalama kwa madai kwamba wanatumia lugha za kashfa na matusi kwa viongozi wa ...

 

1 week ago

Malunde

MGHIRA AANZA KUWAVAA WAPINZANI,ASEMA LOWASSA KUHAMIA CHADEMA NI UFISADI WA KISIASAMkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa njia aliyoitumia aliyekuwa mgombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu uliopita kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ilikuwa ni aina fulani ya ufisadi wa kisiasa.
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifanya mahojiano na Gazeti la Mwananchi ambapo amesema kuwa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema njia aliyoitumia ilikuwa ni aina mojawapo ya ufisadi kwakuwa hakupitishwa na...

 

1 week ago

Mwananchi

Mghwira: Lowassa kuhamia Chadema ufisadi wa kisiasa

Moto wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 ulishazimika lakini kuna kila dalili kwamba majivu yake bado hayajapoa na moja ya dalili za kuwapo kwa hali ya uvuguvugu ni kauli ya hivi karibuni ya Anna Mghwira dhidi ya Edward Lowassa kwamba njia aliyotumia kugombea urais ilikuwa ni aina nyingine ya ufisadi.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani