2 weeks ago

VOASwahili

Bunge la Marekani lailazimisha Facebook kuthibitisha udhibiti wa siri

Wabunge wa Marekani wakiwa Washington walimbana kwa maswali magumu Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg wiki hii wakitaka aeleze jinsi kampuni yake ilivyokuwa ikitunza taarifa na siri za watumiaji wa mtandao wake.

 

1 month ago

VOASwahili

Soko la Facebook latetereka kwa kupoteza uaminifu

Pamoja na mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerbag kuomba msamaha kutokana na kupoteza uaminifu kitu kilichowakera watu zaidi ya milioni 50 duniani, soko lake la hisa limeonyesha kutetereka.

 

1 month ago

BBCSwahili

Thamani ya facebook yashuka kwa $58bn kufuatia kashfa

Mtandao huo wa kijamii ulikabiliwa na hisia kali kutoka kwa wanasiasa , wawekezaji na wateja wake kufuatia kashfa ya data

 

1 month ago

Malunde

MMILIKI WA FACEBOOK MARK ZUCKERBERG AOMBA RADHI WATEJA WAKE

Mwanzilishi wa mtandao maarufu duniani wa Facebook, Mark Zuckerberg, kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica, inayotuhumiwa kuingilia data za watumiaji milioni 50 wa  mtandao huo, ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa.
Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zuckerberg bila kuomba radhi kwa kile kilichotokea, amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa wala kudukuliwa...

 

1 month ago

Michuzi

MMILIKI MTANDAO WA FACEBOOK AWAOMBA RADHI WATEJ A WAKE


ZUCKERBERG AFUNGUKA SAKATA  LA FACEBOOK.
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
MWANZILISHI  na mmiliki wa mtandao wa Facebook  Mark Zuckerberg ameibuka na kuomba msamaha kwa wateja wake baada ya sakata la kudukuliwa kwa data za watumiaji  zaidi ya milioni 50 wa mtandao huo na kampuni ya taarifa na takwimu ya Cambridge Analytica. 
Kashfa hiyo imeipa hasara ya zaidi ya bilioni 45 kwa siku mbili kutokana na hofu na upotoshaji uliotokea kwa watumiaji wake. Zuckerberg amehaidi uaminifu na umakini zaidi...

 

1 month ago

RFI

Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg aomba radhi kwa watumiaji wake

Mkurugenzi mkuu na mmliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg amevunja ukimya juma hili kuhusu kashfa iliyoikumba kampuni yake ambapo ameomba radhi kutokana na "kuvunja uaminifu" na weteja wake zaidi ya bilioni moja na kuapa kutorudia makosa yaliyojitokeza.

 

1 month ago

Zanzibar 24

Mmiliki wa Facebook aomba radhi kutokana na kashfa ya Cambridge Analytica

Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kashfa ya Cambridge Analytica,ameibuka na kudai kwamba wamefanya makosa. Analytica inatuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.

Katika ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Facebook Zuckerberg amesema kitendo hicho kimewavunjia uaminifu. Hivyo kutokana na hali hiyo ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibwa kwa taarifa za watumiaji wake.

AmesemaThe CEO said:...

 

1 month ago

BBCSwahili

Njia za kulinda data na maelezo muhimu kukuhusu katika Facebook

Ni nini ambacho wateja wanaweza kufanya ili kudhibiti data yao mbali kutoa kiwango cha ujumbe utakaosambazwa?

 

1 month ago

BBCSwahili

Cambridge Analytica yadaiwa kutumia maelezo ya watu Facebook kuwafaa wanasiasa

Kampuni hiyo inashutumiwa kutumia data binafsi za wafuasi wa Facebook milioni 50 kushawishi wakati wa uchaguzi wa urais mwaka 2016

 

2 months ago

BBCSwahili

Akamatwa baada ya kutekeleza mauaji katika Facebook live

Maafisa wa polisi kaskazini mwa Carolina wanasema kuwa mtu mmoja alipigwa risasi hadi kufa alipokuwa akijichukua kanda ya video ya moja kwa moja katika mtandao wa facebook Live

 

3 months ago

BBCSwahili

Ukurasa wa Facebook unaoeneza chuki dhidi ya vijana wa dini ya kiislamu umefungwa

Ukurasa mmoja wa Facebook unaoeneza chuki kwa kuwataka watu wa dini ya kihindi wawawinde vijana 102 wa dini ya kiislamu

 

3 months ago

Malunde

MWALIMU MBARONI KWA KUTUKANA FACEBOOK

JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkolani, Deogratius Kisandu, akidaiwa kutumia lugha ya matusi, kejeli na kudhalilisha katika ukurasa wake wa Facebook.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema Kisandu alikamatwa jana baada ya kuwepo taarifa kuhusu kuonekana ujumbe wa matusi na lugha zisizofaa katika ukurasa wake wa Facebook.
Alisema walimfuatilia mtuhumiwa na kumkamata akiwa na simu yake...

 

3 months ago

Malunde

FACEBOOK YATANGAZA KUBORESHA HABARI ZAKE

Mmiliki wa facebook Mark Zuckerbag

Kampuni ya facebook imetangaza kuwa imebadili kampuni inayoipa habari, ili kukabiliana na kile ilichotaja kama habari za uzushi na za kupotosha.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo ya facebook, Mark Zuckerberg, amesema mtandao wake sasa utakuwa ukiwauliza matumiaji wake ni vyanzo vipi vya habari wanaamini zaidi na hivyo kuwapa nafasi ya kwanza.
Waandishi wa habari wanasema kuwa kampuni hiyo ya facebook ambayo ina zaidi ya watumiaji bilioni mbili, inataka...

 

3 months ago

BBCSwahili

Facebook kutumia utafiti ili kuboresha habari zake

Kampuni ya facebook imetangaza kuwa imebadili kampuni inayoipa habari, ili kukabiliana na kile ilichotaja kama habari za uzushi na za kupotosha

 

3 months ago

BBCSwahili

Picha ya Selfie kwenye Facebook yasababisha muuaji kupatikana Canada

Brittney Gargol alipatikana amenyongwa karibu na Saskatoon, Saskatchewan, huku mkanda wa Antoine ukiwa kando na mwili wake.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani