4 days ago

Michuzi

Miili ya Askari JWTZ Kurejeshwa Nchini


 

6 days ago

Zanzibar 24

Wanajeshi wa JWTZ waliouawa Congo waagwa

Miili ya askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imeagwa tayari kwa kurejeshwa nchini.

Askari hao walikuwa kwenye operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN). Habari zilizopatikana zilisema miili ya askari hao iliagwa jana.

JWTZ katika taarifa kwa umma juzi iliwataja askari hao kuwa ni Koplo Maselino Paschal Fubusi na Praiveti Venance Moses Chimboni. Taarifa ilisema askari wengine 12 walijeruhiwa katika...

 

3 weeks ago

Michuzi

Dkt. Harrison Mwakyembe awapongeza JWTZ katika Uhifadhi wa Kumbukumbu za Kitaifa.

Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuhifadhi vema kumbukumbu za Mashujaa wa Tanzania waliopigana vita na kusaidia ukombozi katika baadhi ya nchi za jirani ikiwemo nchi ya Msumbiji.
Pongezi hizo amezitoa leo Mkoani Mtwara wakati alipotembelea maeneo ya kumbukumbu ya Kitaifa ambapo kwa Mkoani hapo ametembelea eneo la Mashujaa lililopo Nailendele lengo likiwa ni kujionea maeneo...

 

4 weeks ago

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA 422 WA JWTZ JIJINI ARUSHAaru1aru2IMGS0864
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride  katika sherehe ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba 23, 2017. (PICHA NA IKULU)
IMGS0869
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride  katika sherehe ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya 422 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Septemba...

 

4 weeks ago

Channelten

Rais Magufuli atunuku kamisheni Kwa Maafisa wapya 422 wa JWTZ

sx

Rais John Pombe Magufuli amewatunuku kamisheni maafisa wapya wa jeshi la ulinzi la Tanzania kundi la sitini na moja la mwaka 2016 huku akitumia nafasi hiyo kuwahutubia wananchi waliofika katika sherehe hizo ambapo ametoa nafasi elfu tatu za ajira kwa askari wa JKT kuajiriwa katika jeshi la ulinzi la wananchi.

Jumla ya Maafisa 422 kati yao wakiwemo wanawake 32 na wanaume 390 wametunukiwa kamisheni ambapo baadhi yao ni kutoka chuo cha mafunzo ya kijeshi TMA Monduli na chuo cha kijeshi cha...

 

4 weeks ago

Malunde

JWTZ YATOA TAARIFA KUHUSU MWANAJESHI ALIYEUAWA CONGO


Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa mwili wa marehemu Praiveti Mussa Jumanne Muryery ambaye ameuawa nchini DRC akiwa katika jukumu la Ulinzi wa Amani, utaagwa kwa heshima tarehe 25 Septemba 2017 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florens M. Turuka ataongoza katika kuuaga mwili wa Marehemu.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu...

 

4 weeks ago

Channelten

Ulinzi na usalama wa mitandaoni, Askari 21 wa JWTZ wahitimu mafunzo DIT

policetechnology

Serikali imeahidi kuendelea kuimarisha vitengo vyake vya ulinzi na usalama wa mitandao, ili kuwajengea watendaji wake uwezo wa kupambana na changamoto zitokanazo na maendeleo ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano TEHEMA.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Birigedia Jenerali Yohana Mabongo amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya ulinzi na usalama wa mitandao, yaliyoendeshwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam DIT, kwa...

 

4 weeks ago

Michuzi

JWTZ LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LA UJENZI WA UKUTA MERERANI-SIMANJIRO MKOANI MANYARA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ laanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano.Helikopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuyo akitua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja....

 

4 weeks ago

Channelten

Ujenzi wa Uzio Machimbo ya Mererani, Rais Magufuli aliagiza JWTZ kujenga uzio mara moja

m (24)

Rais John Pombe Magufuli ameliagiza jeshi la wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na Suma JKT kuanza mara moja ujenzi wa uzio katika eneo lote la machimbo ya Madini ya Tanzanite lililopo mji mdogo wa Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara ili kudhibiti wizi na uuzaji holela wa madini ya Tanzanite.

Akiwa ameongozana na waziri wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa na viongozi wengine wa serikali, wataalamu na wanasiasa katika mji mdogo wa mererani wakati wa uzinduzi...

 

4 weeks ago

Malunde

ASKARI WA JWTZ AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WAASI WA CONGO

Askari wa jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) aliyefahamika kwa jina la Praiveti Mussa Jumanne Muryery ameuawa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi akiwa kwenye ulinzi wa Amani nchini DRC Congo.

Kwa mujibu wa taarifa ya (JWTZ) inasema kuwa askari wake huyo alifariki Septemba 17, 2017 na kufuatia shambulio hilo Umoja wa Mataifa umeunda bodi ya uchunguzi kuchunguza tukio hilo

 

4 weeks ago

Zanzibar 24

Askari wa JWTZ auawa kwa risasi huko DRC Congo

Askari wa jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) aliyefahamika kwa jina la Praivate Mussa Jumanne Muryery ameuawa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi akiwa kwenye ulinzi wa Amani nchini DRC Congo

Kwa mujibu wa taarifa ya (JWTZ) inasema kuwa askari wake huyo alifariki Septemba 17, 2017 na kufuatia shambulio hilo Umoja wa Mataifa umeunda bodi ya uchunguzi kuchunguza tukio hilo.

The post Askari wa JWTZ auawa kwa risasi huko DRC Congo appeared first on Zanzibar24.

 

1 month ago

MwanaHALISI

JWTZ yaunda kikosi maalum kusaka silaha

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Husein Mwinyi ameliambia Bunge kuwa kwa sasa kimeundwa kikosi kazi kwa ajili ya kusaka silaha za kivita ambazo zinatumiwa na watu wenye nia mbaya, anaandika Dany Tibason. Dk.Mwinyi ametoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Chambani,Yusufu Salim Husein(CUF). Katika swali la ...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani