1 day ago

VOASwahili

Uhuru aadhimisha Kumbukumbu ya Kenyatta kwa kuhimiza mshikamano

Rais Uhuru Kenyatta ameeleza tofauti za kisiasa kuwa ni msingi wa demokrasia ya Kenya, lakini ameonya kuwa kuhitilafiana katika maoni kusitumike kugawa nchi.

 

4 days ago

Channelten

Uchaguzi Kenya, Upinzani wawasilisha pingamizi la kupinga ushindi wa Kenyatta

_97028565_raila

Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance NASA umewasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti.

Mawakili wa muungano huo wamewasilisha nyaraka za kesi hiyo na ushahidi katika Mahakama ya Juu mjini Nairobi takriban saa moja na nusu kabla ya muda unaoruhusu pingamizi kumalizika, ambapo wakiwasilisha nyaraka za ushahidi zenye kurasa 9,000.

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa Ijumaa wiki...

 

5 days ago

RFI

NASA wawasilisha kesi mahakamani dhidi ya ushindi wa Kenyatta

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umewasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya juu Jijini Nairobi.

 

5 days ago

Zanzibar 24

Dondoo muhimu za kesi ya kupinga ushindi wa Kenyatta

Agosti 18: Siku ya mwisho ya kuwasilsiha kesi Agosti 20: Siku ya mwisho ya kuwasilisha nyaraka za kesi kwa wanaofaa kujibu kesi Agosti 24: Siku ya mwisho kwa wanaofaa kujibu kesi kuwasilisha majibu Septemba 1: Siku ya mwisho kwa Mahakama ya Juu kutoa uamuzi.

Uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kesi hiyo ni wa mwisho. kwa mujibu wa Katiba ya kenya, iwapo mahakama hiyo itaidhinisha ushindi wa Bw Kenyatta kiongozi huyo ataapishwa kuongoza kwa muhula mwingine tarehe 12 Septemba, siku saba baada ya...

 

5 days ago

VOASwahili

Hatimaye NASA yawasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Kenyatta

Muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Ijumaa usiku uliwasilisha malalamishi kwenye mahakama ya juu, kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta uliotangazwa wiki moja iliyopita na tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC.

 

5 days ago

BBCSwahili

Odinga kuwasilisha kesi kupinga ushindi wa Kenyatta leo

Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance leo unatarajiwa kuwasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

 

6 days ago

BBCSwahili

Mbunge amtaka Magufuli kumuiga Kenyatta na kuruhusu maandamano

Mbunge wa Arusha mjini nchini Tanzania amemtaka raisMagufuli kumuiga mwenzake Uhuru Kenyatta kupitia kuwaruhusu wapinzani wake wa kisiasa kufanya siasa zao bila vikwazo.

 

6 days ago

RFI

NASA kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta mahakamani

Katika makala haya leo , utasikia maoni ya wasikilizaji kuhusu uamuzi wa muungano wa upinzani nchini Kenya  NASA  kwenda mahakamani dhidi ya ushindi wa rais Uhuru Kenyatta

 

1 week ago

RFI

Odinga kupinga ushindi wa rais Kenyatta katika Mahakama ya Juu

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA Raila Odinga, ametangaza kwenda katika Mahakama ya Juu kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta, baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika wiki iliyopita.  

 

1 week ago

BBCSwahili

Uchaguzi Kenya 2017: Odinga kupinga ushindi wa Kenyatta mahakamani

Raila Odinga ametangaza kwamba muungano wake wa National Super Alliance utawasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.

 

1 week ago

RFI

Raila Odinga kutoa tamko la uelekeo wa NASA baada ya kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ameahirisha kutangaza mwelekeo wake na wa muungano wake wa NASA, baada ya kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta aliyetangazwa wiki iliyopita. Odinga alitarajiwa kuwahotubia wafuasi wake hapo jana lakini muungano wa NASA, umesema kuwa tangazo hilo sasa litafanyika hii leo jumatano. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 72, ameendelea kusisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda Uchaguzi huo, na kura zake ziliibiwa.

 

1 week ago

BBCSwahili

Marekani yampongeza Kenyatta kwa kuchaguliwa muhula wa pili

Marekani imewapongeza watu wa Kenya kufutia kumalizika kwa uchaguzi mkuu kwa njia ya amani, na pia kumpongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

 

1 week ago

Zanzibar 24

Rais Kenyatta aruhusu maandamano ya amani kwa wanaopinga ushindi wake

Rais Uhuru Kenyatta amewaruhusu Wakenya kufanya maandamano ya amani kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8,2017. Kenyatta amewataka polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa na badala yake wawape ulinzi waandamanaji hao wakati wa maandamano ya amani na yanayoruhusiwa kisheria kwa watu ambao hawafurahii matokeo ya uchaguzi uliopita. Rais Kenyatta aliyasema hayo jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo wakati akiwa Jengo la Harambee...

 

1 week ago

Malunde

RAIS UHURU KENYATTA ARUHUSU WANAOPINGA USHINDI WAKE WAANDAMANE....AMEWATAKA POLISI WAWAPE ULINZI

Rais Uhuru Kenyatta huenda akaingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia kwa marais wa Afrika kwa kuamua kuruhusu maandamano ya amani kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8,2017.

Kenyatta amewataka polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa na badala yake wawape ulinzi wakati wa maandamano hayo ya amani na yanayoruhusiwa kisheria kwa watu ambao hawafurahii matokeo ya uchaguzi uliopita.

Rais Kenyatta alisema hayo jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa wagombea walioshindwa...

 

1 week ago

VOASwahili

Kenyatta awashauri wasioridhishwa na matokeo kwenda mahakamani

Rais mteule Uhuru Kenyatta ametaka wale wote walioshindwa uchaguzi na kutoridhishwa na matokeo wachukue hatua za kikatiba kupata haki yao.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani