4 days ago

RFI

NASA wawasilisha kesi mahakamani dhidi ya ushindi wa Kenyatta

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umewasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya juu Jijini Nairobi.

 

4 days ago

Zanzibar 24

Dondoo muhimu za kesi ya kupinga ushindi wa Kenyatta

Agosti 18: Siku ya mwisho ya kuwasilsiha kesi Agosti 20: Siku ya mwisho ya kuwasilisha nyaraka za kesi kwa wanaofaa kujibu kesi Agosti 24: Siku ya mwisho kwa wanaofaa kujibu kesi kuwasilisha majibu Septemba 1: Siku ya mwisho kwa Mahakama ya Juu kutoa uamuzi.

Uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kesi hiyo ni wa mwisho. kwa mujibu wa Katiba ya kenya, iwapo mahakama hiyo itaidhinisha ushindi wa Bw Kenyatta kiongozi huyo ataapishwa kuongoza kwa muhula mwingine tarehe 12 Septemba, siku saba baada ya...

 

4 days ago

Michuzi

Breaking nyuzzzz......: Odinga afungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi wa Kenya

Aliyekuwa Mgombea Urais wa Kenya kupitia umoja wa NASA, Raila Odinga hatimaye amefungua kesi katika Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchi hiyo kupinga matokeo ya urais wa Kenya saa 4:30 usiku yaani saa moja na nusu kabla ya deadline ya Saa 6 kamili ya usiku wa leo. Election Petition ina viambatanisho (annexure) vyenye kurasa zaidi 9, 000.

 

4 days ago

VOASwahili

Hatimaye NASA yawasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Kenyatta

Muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Ijumaa usiku uliwasilisha malalamishi kwenye mahakama ya juu, kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta uliotangazwa wiki moja iliyopita na tume ya uchaguzi na mipaka, IEBC.

 

4 days ago

BBCSwahili

Odinga kuwasilisha kesi kupinga ushindi wa Kenyatta leo

Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance leo unatarajiwa kuwasilisha kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

 

4 days ago

Bongo Movies

Uamuzi pingamizi kesi ya Wema kutolewa Agosti 31

Dar es Salaam. Uamuzi wa kupokea au kutopokea kielelezo cha ushahidi cha msokoto mmoja wa bangi na vipisi viwili vya bangi katika kesi inayomkabili mlimbwende wa Tanzania 2006, Wema Sepetu utatolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwisho wa mwezi huu.

Wema Sepetu akiwa na mama yake mahakamani hivi karibuni

Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amesema uamuzi huo ulipaswa autoe leo, lakini bado kuna tafiti anazifanya, hajakamilisha hivyo aliuahirisha hadi Agosti 31,2017.

Hata hivyo, baada ya...

 

5 days ago

Michuzi

Uamuzi wa kesi ya bangi inayomkabili Wema Sepetu wapigwa kalenda

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, imesema uamuzi wa kupokelewa au kutokupokelewa kwa bangi iliyokutwa nyumbani kwa miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili utatolewa Septemba 12.
Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba amesema hayo leo wakati kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Katika kesi hiyo, Wema ambaye pia ni msanii maarufu wa filamu anakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kete mbili za bangi na msokoto mmoja pamoja na...

 

5 days ago

BBCSwahili

Gabriella aombwa kumaliza kesi ya Bi Mugabe nje ya mahakama

Katika mahojiano marefu ya simu na bi Gabriella Engels ambaye amemtuhumu bi Grace Mugabe kwa kumpiga, alitulia na kuonekana kuwa mtu aliyekuwa na wasiwasi mwingi

 

6 days ago

BBCSwahili

Bi Mugabe aomba kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi

Serikali ya Zimbabwe imemuombea mkewe Mugabe kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini , maafisa wa polisi wa taifa hilo wamesema.

 

6 days ago

MwanaHALISI

Kesi ya wabunge CUF Agosti 25

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam itatoa uamuzi tarehe 25 Agosti mwaka huu, wa pingamizi zilizowekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusiana na kesi ya kupinga uteuzi wa wabunge wanane wapya uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoka Chama cha Wananchi (CUF), anaandika Faki Sosi. Msajili wa Mahakama Kuu, Mustapha Siyani, ameeleza leo ...

 

6 days ago

BBCSwahili

Mugabe kuelekea Afrika Kusini kutatua kesi ya mke wake

Msichana wa umri wa miaka 20 amemlaumu mke wake Mugabe, Grace kwa kumpiga kwa kifaa cha umeme wakati wa mzozo kwenye hoteli moja Jumapili jioni

 

6 days ago

Zanzibar 24

Kibatala, Tundu Lissu waukataa ushahidi kesi ya Wema Sepetu

Ushahidi wa kesi inayomkabili  malkia wa filamu Wema Sepetu na wenzake wawili kuhusiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi, bado ni kizaazaa baada ya kuzua mvutano mzito katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam hapo jana.

Wakili wa upande wa washtakiwa Peter Kibatala na Tundu Lisu, wameupinga ushahidi wa vielelezo ambavyo vimefikishwa mahakamani hapo na ofisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu kwa madai kuwa kuna baadhi ya vitu vimeonekana katika ushahidi huo ambapo...

 

1 week ago

Bongo Movies

Kesi ya Wema Sepetu Ngoma Nzito, Ushahidi Wakataliwa

Ushahidi wa kesi ya Wema Sepetu na wenzake wawili ya matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi, umezua mvutano mzito katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam Jumanne hii.

Upande wa washtakiwa ambao unaongozwa na wakili Peter Kibatala na Tundu Lisu, umeupinga ushahidi wa vielelezo ambavyo vimefikishwa mahakamani hapo na ofisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu kwa madai kuwa kuna baadhi ya vitu vimeonekana katika ushahidi huo ambapo mwanzoni havikutajwa.

Moja ya vitu ambavyo...

 

1 week ago

Michuzi

DIWANI WA KATA SAMBASHA ( CCM) AACHIWA KWA DHAMANA DHIDI YA KESI INAYOMKABILI

Na Vero Ignatus.Arusha

Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .

Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).

Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serekali Penina Joakim ...

 

2 weeks ago

Michuzi

MISS TANZANIA SHOSE SINARE ALALAMIKIA WAPELELEZI WA KESI YAO.

 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.Miss Tanzania, Shose  Sinare ameuomba upande wa mashitaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, pamoja na wenzake wawili walete  mawasiliano yanayofanyika kati ya Tanzania na Uingereza juu ya upelelezi dhidi ya kesi yao.
Shose amedai hivyo leo katika  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha, Mbali na Sinare, washitakiwa wengine ni   katika kesi hiyo ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani