(Yesterday)

Zanzibar 24

CHADEMA wapigwa na chini Kesi ya Benjamini Sitta

Mahakama Hakimu mkazi Kisutu yamthibitisha Benjamini Sitta kuwa Meya halali wa Manispaa ya Kinondoni. hatua hiyo imetoliwa baada ya kushinda kesi iliyofunguliwa dhidi yake kuhusiana na matokeo ya uchaguzi.

Mnamo mwezi Oktoba, 2016 chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kupinga ushindi wa Benjamini Sitta kuwa Meya wa Kinondoni.

Baada ya uthibitisho huo Benjamimi Sitta ataanza kazi zake za umeya atazopangiwa.

The post CHADEMA...

 

(Yesterday)

Mwananchi

Mahakama Kisutu yafuta kesi ya umeya Kinondoni

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi  ya matokeo ya umeya wa Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

 

(Yesterday)

Mtanzania

MAHAKAMA YATAKA UPELELEZI KESI YA PEDESHEE NDAMA UKAMILIKE

Gavel-300dpi-Small

Na Kulwa Mzee -Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeutaka upande wa Jamhuri kukamilisha haraka upelelezi katika kesi ya  kughushi, kutakatisha fedha na  kujipatia Dola za Marekani 540,390 kwa udanganyifu inayomkabili mfanyabiashara Ndama Shabani Hussein, maarufu kama Pedeshee Ndama Mtoto wa Ng’ombe (44).

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa, alisema hayo jana baada ya Wakili wa Serikali, Leonard Challo kudai mahakamani wakati kesi ilikuwa...

 

1 day ago

Habarileo

Kesi ya ‘Ndama mtoto wa Ng’ombe’ yaahirishwa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kesi ya utakatishaji fedha ya Sh bilioni 1.8 inayomkabili mfanyabiashara Ndama Hussein (44) maarufu kama ‘Ndama mtoto wa Ng’ombe’, hadi Januari 24 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

 

1 day ago

Mwananchi

Mawakili wa Lema waomba kesi ipelekwe Mahakama ya Katiba

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amepandishwa kizimbani akikabiliwa na kesi mbili; ya kutoa lugha ya kuudhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kuhamasisha maandamano ya Ukuta ambayo mawakili wake wameomba ipelekwe Mahakama ya Katiba.

 

1 day ago

Mwananchi

Mahakama yataka upelelezi wa kesi ya ‘Ndama mtoto wa ng’ombe’ ukamilishwe haraka

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa ameuagiza upande wa mshtaka katika kesi ya  kughushi, kutakatisha fedha na  kujipatia dola za Marekani 540,390 kwa njia ya udanganyifu inayomkabili  Mfanyabiashara maarufu wa jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto wa Ng'ombe(44) kukamilisha upelelezi haraka.

 

2 days ago

Bongo5

Kaimu Jaji Mkuu aahidi kusajili kesi katika mfumo wa kielektroniki

Kaimu Jaji Mkuu, Pro Ibrahim Hamis Juma ameeleza mikakati yake ya kufanya mabadiliko katika mahakama ikiwemo kesi kusajiliwa katika mfumo wa kielektroniki ili kuwezesha haki.

Jaji huyo ameyaeleza hayo Jumatano hii baada ya kuapishwa na Rais wa Jammhuri ya Muuungano wa Tanzania kuwa Kaimu Jaji mkuu wa Tanzania. “Mimi lengo ni kuhakikisha kesi zinasajiliwa zinakuwa katika mtindo wa kielektroniki ili kuwezesha haki iweze kupatikana kwa haraka na kuwa na uwazi zaidi ya ilivyo sasa,” alisema...

 

2 days ago

Mtanzania

MAWAKILI WAOMBA KESI YA LEMA IHAMISHIWE MAHAKAMA KUU

Pg 2

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) na mkewe Neema Lema, wakiwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana kwa kesi ya uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

 

Na JANETH MUSHI -ARUSHA

MAWAKILI wanaomtetea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) katika kesi ya kuhamasisha watu kukusanyika na kufanya maandamano kinyume cha sheria, wameomba shauri hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu mbele ya jopo la majaji watatu kutokana na kuwapo kwa masuala ya...

 

2 days ago

Habarileo

Kesi ya Lissu kuendelea siku ya Wapendanao

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeahirisha kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) hadi Februari 14, mwaka huu, baada ya shahidi wa upande wa mashitaka kupata dharura ya kikazi.

 

2 days ago

Mwananchi

Kesi ya Lissu kusikilizwa Siku ya Wapendanao

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Februari 14, mwaka huu itaendelea kuisikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

 

2 days ago

Mtanzania

KESI NYINGINE YA KUPINGA SHERIA MPYA YA HABARI YAFUNGULIWA MWANZA

Karsan

Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan

Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na Kampuni ya Hali Halisi Publishers leo wamefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza wakidai ufafanuzi wa Mahakama juu ya sheria mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kukiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18.

Mlalamikaji mkuu katika kesi hiyo ni UTPC akishirikiana na Hali Halisi Publishers ambapo tayari kesi hiyo imekwishafunguliwa na...

 

3 days ago

MwanaHALISI

Kesi ya wahariri Mawio, Lissu yaahirishwa, kusikilizwa kesho

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imehairisha usikilizwaji wa awali wa kesi ya uchochozi inayowakabili wahariri wa gazeti la Mawio, mbunge wa Chadema na mchapishaji wa magazeti, anaandika Faki Sosi. Kuahirishwa kwa kesi hiyo kunatokana na upande wa mashitaka kutokamilisha maelezo ya awali. Imeahirishwa hadi kesho . Wanaokabiliwa na keshi hiyo ni Simon ...

 

3 days ago

Mtanzania

RC WA ARUSHA MRISHO GAMBO KUWA SHAHIDI WA KWANZA KESI YA LEMA

Lema na mkeweMkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo anatarajiwa kuwa Shahidi wa kwanza katika kesi namba 351 ya mwaka jana inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mke wake Neema Lema.

Mbele ya Hakimu Nestory Barro wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, katika kesi hiyo ya uchochezi Lema na mkewe wanadaiwa kutoa kauli za kukashifu dhidi ya Gambo ambapo leo watuhumiwa hao wamesomewa hoja za awali za shitaka linalowabili.

Lema alikuwa akitetewa na Wakili John Mallya na Sheck Mfinanga,huku Serikali...

 

4 days ago

Mwananchi

Upelelezi kesi ya Mkurugenzi Jamii Forums bado

Upelelezi wa kesi ya kuwa na anuani za tovuti ambazo hazijasajiliwa nchini inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence  Melo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haujakamilika.

 

4 days ago

Mwananchi

Kesi ya Malkia wa Pembe za Ndovu yakwama

Kesi  ya uhujumu uchumi kwa  kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo yenye thamani ya Sh 5.4 bilioni inayomkabili raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66) na wenzake wawili imeshindikana tena kuanza kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa mashtaka  kwa sababu hakimu yupo likizo.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani