(Today) 3 hours ago

Zanzibar 24

Hukumu ya kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwanasheria Mkuu kusomwa Machi 8

Hukumu ya kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Jeshi la Polisi kuhusu matumizi mabaya ya Sheria ya Makosa ya Mtandao kusomwa tarehe 8 Machi.
Hukumu hiyo itasomwa Mahakama Kuu, mbele ya Mtukufu Jaji Kitusi baada ya kushindikana kusomwa tarehe 22 Februari.
Kampuni ya Jamii Media ambao ni waendeshaji wa mtandao wa JamiiForums na FikraPevu walifungua kesi ya Kikatiba kutaka vifungu vya 32 na 38 vya Sheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya.
Kwa kudai yakwamba Vifungu...

 

(Today) 3 hours ago

Habarileo

Wema Sepetu ahudhuria kesi ya Mbowe

MSANII nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amehudhuria kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.

 

(Yesterday)

Mwananchi

Askofu Mokiwa aomba kesi imalizwe nje ya mahakama

Aliyekuwa  Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Valentino Mokiwa katika kesi ya madai aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akipinga kustaafishwa kwa lazima anaomba wamalizane  nje ya mahakama.

 

(Yesterday)

Habarileo

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam,  Dk. Valentino Mokiwa, afungua kesi

ALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam,  Dk. Valentino Mokiwa, amefungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akiiomba itengue uamuzi wa kuvuliwa uaskofu na kumtangaza kuwa askofu.

 

(Yesterday)

Zanzibar 24

Mkea wa Bilionea Marehemu Msuya ashikiliwa tena na jeshi la polisi kwa kesi ya mauaji

Jeshi la Polisi limewakamata mke wa bilionea marehemu Msuya, Miriam Mrita na mwenzake R. Muyela muda mfupi baada ya Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwaachia huru.

Mjane huyo aliwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji ya wifi yake (Mdogo wa mume wake), marehemu Anathe Msuya aliyechinjwa kinyama Mei 25, 2016 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni.

 

The post Mkea wa Bilionea Marehemu Msuya ashikiliwa tena na jeshi la polisi kwa kesi ya mauaji appeared first on Zanzibar24.

 

(Yesterday)

Mwananchi

Mahakama yatupa rufaa ya kupinga kesi ya uchaguzi jimbo la Longido

Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha.

 

2 days ago

Dewji Blog

Hukumu Kesi ya Kikatiba Sheria ya Makosa ya Mtandao ‘Kuzungumkuti’

Hukumu ya kesi ya Kikatiba namba 9 ya mwaka 2016 iliyofunguliwa mwaka jana na Kampuni ya Jamii Media ikipinga baadhi ya vifungu vya sheria ya makosa ya mtandao kwa kile kuingilia uhuru wa maoni na kujieleza wa wananchi imeshindwa kusoma huku kukiwa hakuna sababu zilizotajwa.

Akizungumza eneo la Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam Wakili wa Jamii Media, Benedict Ishebakaki Alex alisema awali walipata wito wa mahakama kuwa hukumu ya kesi yao ilikuwa isomwe leo lakini wamefika mahakamani na...

 

2 days ago

Bongo5

Kesi ya Wema Sepetu upelelezi haujakamilika, imeahirishwa mpaka Machi 15

Malkia wa filamu Wema Sepetu Jumatano hii alirudi Mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana kwenye sakata la dawa za kulevya.

Wema Sepetu akiwa na Martin Kadinda

Kesi hiyo imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kusema upelelezi haujakamilika hivyo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa 15 March 2017.

Muigizaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao walitajwa kwenye list ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda yawatuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Katika upelelezi wa awali...

 

2 days ago

Michuzi

KESI YA WEMA SEPETU KUTAJWA TENA MACHI 15 2017.

.Msanii Wema Sepetu akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kesi yake ya kuahirishwa hadi March 15 mwaka huu.Kesi hiyo imeaihirishwa na Hakimu Mkazi Thomas Simna baada ya wakili wa Serikali Constantine Kakula kuieleza mahakama kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika

 

2 days ago

Zanzibar 24

Upelelezi kesi ya mkurugenzi wa Jamii Forums wakamilika

Upelelezi wa kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Jamii Media Limited, Maxence Melo (40), umekamilika.

 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, baada ya upande wa mashitaka kuomba muda wa kujipanga zaidi ili kusoma maelezo ya awali ya mshitakiwa.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mohammed Salum amedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya...

 

2 days ago

Bongo5

Upelelezi kesi ya bosi wa Jamii Forums wakamilika

Upelelezi wa kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Jamii Media Limited, Maxence Melo (40), umekamilika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, baada ya upande wa mashitaka kuomba muda wa kujipanga zaidi ili kusoma maelezo ya awali ya mshitakiwa.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mohammed Salum amedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya...

 

3 days ago

Habarileo

Wahimizwa mbinu za kisasa kesi za usafirishaji binadamu

MAOFISA wa upelelezi katika Jeshi la Polisi , mahakimu na waendesha mashitaka wametakiwa kutumia mbinu za kisasa za kupeleleza, kuendesha na kusikiliza kesi dhidi ya biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

 

3 days ago

Habarileo

Upelelezi kesi ya bosi Jamii Forum wakamilika

UPELELEZI wa kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Jamii Media Limited, Maxence Melo (40), umekamilika.

 

3 days ago

Michuzi

KATIBU WA SEKRETARIETI YA KITAIFA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU NCHINI AWATAKA WANASHERIA KUONGEZA KASI USIKILIZAJI KESI ZA BIASHARA HIYO HARAMU

Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Wizara hiyo ambapo yalitolewa kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka (hawapo pichani) kwa kupewa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani