(Today) 7 hours ago

Malunde

TUNDU LISSU : MSAJILI MUTUNGI AMEKUWA BUBU NA KIZIWI ASIYESIKIA WALA KUKEMEA UONEVU DHIDI YA VYAMA VYA SIASA

Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu amefunguka na kumtaka Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mtungi kujitafakari, kwani amedai kuwa Jaji huyo amekuwa ni mpofu kwa mambo mabaya wanayofanyiwa watu wa upinzani nchini.

Lissu amesema hayo kufuatia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuwaandikia barua CHADEMA ambayo anadai inatuhuma mbalimbali pamoja na vitisho mbalimbali

"Nimesoma barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, yenye tuhuma na vitisho vingi...

 

(Yesterday)

MwanaHALISI

Tundu Lissu amvaa Jaji Mutungi, ampa neno zito

MWANASHERIA wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi aache vitisho vya kuitisha chama cha Chadema na anatakiwa kujitafakari kwanza mwenyewe. Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji kwa matibabu, ameandika waraka wake kumjibu Jaji Mutungi kufuatiwa barua yake aliyoiandikia Chadema ya kukituhumu chama hicho kufanya ...

 

(Yesterday)

Zanzibar 24

Tundu Lissu aeleza hali ya afya yake inavyo endelea kwa sasa huko nchini Ubelgiji

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia hali ya afya yake akisema kwa sasa anachoweza kukifanya ni kusimama peke yake na ili atembee anahitaji msaada wa magongo.

Lissu ambaye pia ni rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) anayeendelea na matibabu ya viungo katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji alisema hayo jana alipozungumza na Mwananchi.

“Mie naendelea vizuri na kwa sasa ninaweza kusimama kidogo tu. Sijaanza kutembea bila magongo,”...

 

2 weeks ago

Malunde

ZITTO KABWE AMTEMBELEA TUNDU LISSU UBELGIJI

Mbunge Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe amemtembelea Tundu Lissu nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu ya viungo na saikolojia tangu Januari 7, 2018.
Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki anapata matibabu hayo baada ya kushambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 akiwa nje ya makazi yake mjini Dodoma. 
Awali mbunge huyo alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Dodoma siku hiyohiyo kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi alikotobiwa hadi Januari 6, 2018 alipohamishiwa...

 

2 weeks ago

Malunde

WABUNGE WAVUTANA MATIBABU YA TUNDU LISSUMbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amehoji sababu za Bunge kutogharamia matibabu ya Tundu Lissu aliyepo nchini Ubelgiji tangu Januari 7, 2018 akipatiwa tiba ya mazoezi.


Lema ametoa kauli hiyo leo Februari 8, 2018 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za Bunge za Utawala na Serikali za Mitaa, Katiba na Sheria na Sheria Ndogo.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 akiwa ndani ya gari...

 

3 weeks ago

Malunde

MAOFISA WA JUMUIYA YA ULAYA (EU) WAMTEMBELEA TUNDU LISSU
Maofisa watatu wa Jumuiya ya Ulaya (EU) leo Februari 5,2018 wamemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Lissu alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30, Septemba 7 mwaka jana na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alilazwa hadi Januari 6,2018 alipohamishiwa Ubelgiji katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, anakoendelea na matibabu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari...

 

3 weeks ago

Malunde

TUNDU LISSU AMLILIA KINGUNGE

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka.

Akizungumza leo Februari 2, 2018 ameanza kwa kusema “namtakia mapumziko mema.”

Amesema Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na alionyesha ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia kuhudhuriwa kutokana na mazingira yalivyokuwa.

“Ni mmoja wa wazee walioonyesha ujasiri mkubwa katika mazingira ya siasa za Tanzania yalivyokuwa,...

 

3 weeks ago

Malunde

MSAIDIZI WA LISSU : MAHAKAMA SIYO SEHEMU YA MAJARIBIO..WATENDAJI WOTE WAIHESHIMU

Makamu wa Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Godwin Ngwilimi amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania pamoja na watendaji wote wa sheria kuiheshimu mahakama kwani ni sehemu ambayo ukienda mwishowe haki inapatikana.
Akizungumza jana wakati alipokuwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ambapo ameonya mahakama zisitumike kuonea watu wengine huku akikazia kuwa mahakama haipaswi kuwa sehemu ya majaribio kwani siyo maabara.
"Msiruhusu hata mara moja kwani mnalindwa na Katiba. Msimamie hayo...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Familia ya Tundu lissu yailalamikia Bunge

Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa. Msemaji wa familia ya Lissu, wakili Alute Mughwai, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa miezi ni mitano sasa Lissu hajapata stahiki zake kimatibabu kama Mbunge. “Tumemaliza miezi mitano tangu kutokea kwa tukio la kushambuliwa kwa Lissu na Bunge kama taasisi limeshindwa kutoa fedha za matibabu kwa...

 

3 weeks ago

Malunde

FAMILIA YA TUNDU LISSU YALIA NA BUNGE


Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa.

Lissu amelazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Luvein nchini Ubelgiji tangu mapema mwezi huu baada ya kutibiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa miezi minne.

Msemaji wa familia ya Lissu, wakili Alute Mughwai, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa miezi ni mitano sasa Lissu hajapata stahiki...

 

4 weeks ago

MwanaHALISI

Vigogo 600 wamtembelea Lissu hospitali

JUMLA ya wageni 617 walimtembelea kumjulia hali Tundu Lissu akiwa kitandani ndani ya Hospitali ya Nairobi, Kenya alimokuwa akipatiwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Lissu alilazwa kwa miezi minne- kuanzia Septemba 7, mwaka jana hadi Januari 6, mwaka huu. Idadi hiyo ni baada ya watu kuruhusiwa kumuona na kumsalimia Lissu akiwa kitandani kuanzia Novemba, ...

 

4 weeks ago

MwanaHALISI

Lissu: Kiburi cha Mbowe kimeniokoa

UAMUZI wa kumsafirisha haraka Tundu Lissu, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kwenda Nairobi, Kenya kwa matibabu, kuliokoa maisha yake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Aliyesimama kidete kuhakikisha Lissu anasafirishwa kwenye Nairobi kwa matibabu zaidi ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.  “Pamoja na jitihada zote za madaktari wa Hospitali ...

 

4 weeks ago

Malunde

SAED KUBENEA : SALUM MWALIMU NDIYE TUNDU LISSU MDOGO

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Kanda ya Pwani amefunguka na kusema mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni kupitia CHADEMA, Salum Mwalimu kuwa ni mtu makini na ndiye Lissu mdogo ambaye anastaili kwenda Bungeni.
Kubenea amesema hayo leo Januari 27, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha.
Kubenea amesisitiza kuwa mgombea huyo ni kati ya watu makini...

 

1 month ago

CHADEMA Blog

HALI YA TUNDU LISSU INAENDELEA KUIMARIKA

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa TLS, Mhe Tundu Lisu akiwa nchini Ubelgiji anapoendelea na matibabu na mazoezi ya kuimarisha viungo, huku akiwa ameweza kutembea mwenyewe kwa kutumia gongo na hali yake kuzidi kuimarika zaidi.

 

1 month ago

Zanzibar 24

Vicent Lissu azungumzia hali ya Tundu Lissu nchini Ubelgiji

Ndugu wa Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, ambaye anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji, Vicenti Mughwai alisema jana kuwa afya ya kaka yake Lisu  inazidi kuimarika na sasa anaweza kufanya mambo mengi mwenyewe ikiwamo kwenda kuoga na kutembea kwa kutumia magongo. Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), alipelekwa Ubelgiji Januari 7, mwaka huu, akitokea Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu tangu Septemba 7, mwaka jana...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani