3 days ago

Zanzibar 24

Lowassa afunguka kuhusiana na vuguvugu la kuhama vyama

Waziri mkuu mstaafu na aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa ametoa ya moyoni kuhusiana na hili la wanachama waandamizi kuhama kutoka chama kimoja na kwenda kingine.

Lowassa amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa “Hatuwezi kugombana na kuchukiana kwasababu ya kuhama vyama na wala tusikubali kubaguliwa hivyo, sisi ni Watanzania kwanza.”

Aidha Mhe. Lowassa amesisitiza kuwa anaamini mabadiliko ya kweli yatatoka nje ya CCM.

Mapema...

 

3 days ago

Malunde

UMESIKIA KUHUSU LOWASSA NAYE KUREJEA CCM??....BASI SOMA HAPA
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Lowassa amesema amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," amesema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema . 

Amesema uongo mwingine ambao...

 

3 days ago

MwanaHALISI

Lowassa akanusha kuomba kurejea CCM

EDWARD Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, anaandika Faki Sosi. Lowassa amesema amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo. “Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM,” ...

 

1 week ago

Malunde

LOWASSA : MHESHIMIWA RAIS KWA HESHIMA ZOTE AKUBALI MJADALA WA KATIBA MPYA

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemtumia ‘salamu’ Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwamba gharama za kuandaa Katiba Mpya si kubwa ukilinganisha na mahitaji ya Watanzania.

Akihutubia mamia ya watu katika viwanja vya Soko Kuu la Kwa Mromboo jijini Arusha juzi, Lowassa alimsihi Rais John Magufuli kuruhusu mjadala wa Katiba Mpya kwa kuwa ndiyo kiu ya Watanzania kwa sasa.

“Wananchi wamesema Rais Magufuli aruhusu mjadala wa Katiba Mpya, lakini waziri mkuu wake amesema ni gharama sana mimi nasema...

 

1 week ago

CHADEMA Blog

Lowassa: CCM waliiba kura na sasa ninaomba serikali ya umoja wa vyama.

Aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa amependekeza kuwepo na katiba Mpya inayowezesha uundwaji wa serikali inayojumuisha vyama vyote vya siasa tofauti na sasa ambapo mshindi ndiye pekee anayeunda serikali. Edward Lowassa ameyasema hayo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa tiketi ya CHADEMA katika kata ya Moita katika

 

2 weeks ago

Malunde

LOWASSA,MBOWE KUONGOZA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA UDIWANI CHADEMA

Viongozi wa juu wa Chadema , Freeman Mbowe na Edward Lowassa wataongoza kampeni za uchaguzi mdogo wa nafasi za udiwani kwenye kata 43.

Chama hicho kimeunda Kamati za Kitaifa 10, zitakazoongeza nguvu, hamasa na mikakati ya kampeni za uchaguzi wa marudio kwenye nafasi hizo kuanzia kesho hadi siku ya uchaguzi.

Timu hizo ambazo zitafanya kazi kwa kushirikiana na kamati zingine za hamasa katika ngazi za kanda, mikoa, majimbo, kata na matawi katika maeneo yenye uchaguzi huo, zitaongozwa na...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Habar Picha : Walicho zungumza Nyalandu na Lowassa

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Mh. Lazaro Nyalandu jana alimtembelea Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kuimarisha umoja kwa vyama vya upinzani nchini. “Mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema asante kutufungulia mlango,” alisema Nyalandu katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Lowassa jana jioni. Aidha Mh. Nyalandu ametumia mtandao wake wa kijamii kuweka...

 

2 weeks ago

Malunde

PICHA ZAIDI ZA NYALANDU ALIVYOJITAMBULISHA KWA LOWASSA MARA BAADA YA KUHAMIA CHADEMA

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu jana alimtembelea Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha.
“Mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema asante kutufungulia mlango,” alisema Nyalandu katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Lowassa jana jioni.


 

2 weeks ago

Malunde

LAZARO NYALANDU AMTEMBELEA LOWASSA OFISINI KWAKE

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amemtembelea Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Nyalandu aliyejiondoa CCM wiki iliyopita leo Jumanne Novemba 7,2017 amemshukuru Lowassa kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM.

“Mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema asante kutufungulia mlango,” amesema Nyalandu katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Lowassa.


Kwa upande wake,...

 

3 weeks ago

Malunde

LUSINDE AMCHANA NYALANDU KUHAMIA CHADEMA...AMPA MAKAVU LOWASSA


Kada Maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma Livingstone Joseph Lusinde amewasihi Watanzania kumpuuza Mwanasiasa Lazaro Nyalandu ambaye juzi ametangaza kujivua nyadhifa zake zote katika CCM ikiwemo ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa kile alichodai Serikali kukigandamiza Chama na CCM kupoteza mwelekeo.


Lusinde amesema Bw. Lazaro Nyalandu hakuwahi kunyimwa nafasi yoyote ya kutoa maoni yake ama dukuduku zake...

 

4 weeks ago

Malunde

LOWASSA ACHEKELEA NYALANDU KUIPIGA CHINI CCM ... 'TUMELAMBA DUME'


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM.


Akionyesha kuwa na furaha leo Jumatatu wakati akiongea, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”.

Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango.

Dakika chache tangu Nyalandu aombe...

 

1 month ago

Malunde

LOWASSA AMTEMBELEA TUNDU LISSU KENYA


Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo Oktoba 24 amemtembelea na kumjulia hali Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya.

Katika safari hiyo, Lowassa alikuwa ameandamana na mke wake, Mama Reginal Lowassa na wameonekana kwenye picha wakiwa na furaha na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Viongozi mbalimbali wa chama hicho wamekuwa wakiendelea kumtembelea na...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Lowassa awa mgeni Nairobi kwa Tundu Lissu

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa amekwenda nchini Nairobi Kenya akiwa na mke wake Mama Regina Lowassa kumjulia hali Mh. Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

The post Lowassa awa mgeni Nairobi kwa Tundu Lissu appeared first on Zanzibar24.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani