2 weeks ago

Bongo Movies

Lulu Diva Apokonywa Kila Kitu na Mpenziwe

IMEVUJA! Ukiachana na habari ya kudaiwa kupangishiwa nyumba na kununuliwa gari mpya aina ya Jeep na kigogo, imebainika kuwa msanii huyo amepokonywa kila kitu alichokuwa amepewa na mpenzi wake wa zamani aitwaye Joho.

Hivi karibuni, Lulu Diva aliripotiwa kuwa amepangiwa nyumba na kupewa gari jipya ambapo aliibuka sosi mwingine na kudai kuwa Lulu si mkweli, aliyenunua gari hilo ni mpenzi wake Joho ambaye alikuwa akiishi naye kinyumba kwa takriban miaka mitatu kiasi cha kufikia hatua ya...

 

3 weeks ago

Bongo Movies

VIDEOMPYA: Lulu Diva-amezoea

Msaani Lulu diva kaachia video mpya,inaitwa “amezoea”.

BOFYA PLAY KUITAZAMA

 

3 weeks ago

Michuzi

MWILI WA MAREHEMU LULU SYLVESTER MATTUNDA LEMA WAWASILI KIJIJINI NRONGA KWA MAZISHI

Marehemu Lulu Sylvester Mattunda Lema.Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu, Lulu Sylvester Mattunda Lema mara baada ya kuwasili nyumbani kwao katika Kitongoji cha Nkwelengya, Kijiji cha Nronga, Kata ya Machame Magharibi,Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Januari 25, 2018. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Januari 26, 2018. Sylvester Mattunda Lema (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watoto wake mara baada ya kuwasili Nyumbani kwao katika Kitongoji cha...

 

4 weeks ago

Michuzi

TANZIA: BIBI LULU AKIDA SILVESTER AFARIKI DUNIA

TANZIA: Familia ya Bwana Sylvester Manase Matunda Lema, wa Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000 jijini Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mama yao, Bibi.Lulu Sylvester kilichotokea katika Hospitali ya Agha Khan tarehe 20/01/ 2018 majira ya saa 10;30 alfajiri.
Maandalizi ya mazishi yanafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza mkabala na kituo cha daladala Simu 2000. Mwili utaagwa Jumatano Januari 24, 2018 kuanzia saa 8 mchana Kanisani KKKT Usharika wa Sinza -Kumekucha. 
Mwili wa...

 

4 weeks ago

Bongo Movies

Lulu Diva Afunguka Kuhusu Kufunga Ndoa

BAADA ya staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kufunga ndoa na Uchebe, msanii anayekimbiza na Ngoma ya Give It To Me, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefungukia upande wa maisha yake kwamba acha waoane wao lakini kwake noo!

Akizungumza na Showbiz, Lulu aliyewahi kuwa muuza nyago kwenye video za Kibongo alisema kuwa, hafikirii maisha ya ndoa wala kuwa na uhusiano na staa Bongo kwani atapata presha tu.

“Kama kuoana acha waoane wao lakini kwangu noo! Nimeingia kwenye muziki kwa hiyo...

 

4 weeks ago

Bongo Movies

Alikiba Ashambuliwa na Mashabiki Kisa Lulu

KATIKA kile kilichoonekana kwamba amemkumbuka aliyewahi kuwa mpenzi wake zamani ambaye kwa sasa anatumikia kifungo gerezani, Elizabeth Michael ‘Lulu’, staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba hivi karibuni alishindwakuficha hisia zake na kuweka picha ya mrembo huyo ambapo baadhi ya mashabiki walimshambulia huku wengine wakimpongeza.

Kiba aliweka picha hiyo ya Lulu kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kuandika kitu chochote na kupata mashabiki wengi ambao walianza kuchangia huku wengine wakimnanga...

 

1 month ago

Bongo Movies

Baada ya siku 61 za Lulu gerezani Idriss Sultan kaandika hivi

Kupitia instagram page ya Idris Sultan ameandika ujumbe ambao umewakumbusha wengi tukio la Elizabeth Michael “Lulu” kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Idris Sultan na Elizabeth Michael wamefanya kazi pamoja katika tamthilia ya SARAFU na moja kati ya kipande katika tamthilia hiyo kimeonyesha kuwa Elizabeth Michael ndiye anayemtembelea Idris Sultan gerezani wakati uhalisia wa sasa ni...

 

1 month ago

Bongo Movies

Hatimaye Mashabiki na Wapenzi wa Lulu Kuanza Kumuona

Zikiwa zimepita siku 54 tangu muigizaji wa filamu bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, sasa mashabiki wake wataanza tena kumuona kupitia tamthiliya ya Sarafu inayotarajiwa kuanza kurushwa kuanzia Januari 10 siku ya Jumatano.

Sarafu ni moja ya tamthiliya zitakazoonyeshwa katika king’amuzi cha DSTV kupitia chanel yao ya Maisha Magic Bongo ambapo itakuwa inarushwa siku ya Jumatano na Alhamisi.

Katika tamthiliya hiyo ambayo msimu wake wa kwanza utaenda mpaka...

 

3 months ago

Zanzibar 24

Hii ndio sababu iliyo mfanya mama kanumba kucheka baada ya hukumu ya lulu

Nawashangaa wanaonishangaa mimi kucheka, lakini nawataka wakumbuke kuwa hata mimi nililia mno wakati werngine wakila bata.

Maneno hayo yametamkwa na Flora Mtegoa ambae alikua  Mama wa aliyekuwa mwigizaji mahiri wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba,

Mama Kanumba alisema kuwa, baada ya Lulu kuhukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka miwili kwa kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia, alijikuta akicheka, lakini hakumaanisha kuwa anafurahia Lulu kwenda jela kwa sababu yeye ni Mkristo hivyo...

 

3 months ago

Malunde

PATCHO MWAMBA : LULU HAKUMUUA KANUMBA BALI ALIKUWA SHAHIDI WAKATI ANAKUFA

Mwanamuziki na Muigizaji nchini, Patcho Mwamba ameifungukia kauli ya Mama Kanumba ya kushukuru kitendo cha Muigizaji Lulu kufungwa miaka miwili kwa kosa la kumuua bila kukusudia muigizaji Kanumba na kusema kwamba hakuna haja ya kuendelea na 'beef' kwani hakuna haki inayoweza kumrudisha Kanumba hai.

Patcho ambaye alikuwa muigizaji na rafiki wa karibu na Marehemu Steven Kanumba amesema kwamba Mama kanumba anapaswa kuwa na moyo wa kusamehe kwa sababu binti huyo akimaliza kifungo atarudi mtaani...

 

3 months ago

Bongo Movies

Lulu Awaambia Ndugu Zake Wasikate Rufaa Kilichotokea ni Mipango ya Mungu

Imeelezwa kuwa baada ya msanii Elizabeth Michael kusomewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, aliwaambia ndugu zake wasikate rufaa kwa kuwa kilichotokea ni mipango ya Mungu na yupo tayari kukabiliana nayo.

Msanii wa wa Maigizo Elizabeth Michael akiwa ndani ya chumba cha mahakama kuu jijini Dar .Picha nyingine lulu akipandishwa katika gari ya polisi baada ya kuhukumiwa .Picha na Omary Fungo

Msanii , Muhsin Awadh maarufu Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na mwigizaji huyo katika kipindi...

 

3 months ago

Bongo Movies

Dk Cheni Awafungukia Wanaosema Hukumu ya Lulu Haitoshi

MSANII mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo na mshereheshaji (MC), Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye ni mlezi wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuibuka maneno mengi kwenye mitandao hiyo ambapo watu wengine wanasema Lulu amepewa adhabu ndogo na wengine wakipendekeza angefungwa kwa miaka mitano na kuendelea.

Dk Cheni amewalaumu wasiomtakia mema Lulu akisema mambo yote mabaya yanaweza kumtokea yoyote, kwa hiyo kufurahia jambo baya...

 

3 months ago

Zanzibar 24

Ujumbe aliouandika Afande Sele akimlaumu Kanumba kuhusu Lulu

Baada ya hukumu ya Lulu jana Afande ameandika ujumbe huu ambao uliamsha hisia za wengi… “Nakumbuka vizuri saana mwaka 2006 yaani miaka miwili tu baada ya mimi kushinda taji la ufalme wa rhymes Tz na kukabidhiwa ile gari maridadi sana ya zawadi aina ya toyota sera yenye milango ya kubinuka kama mabawa ya ndege anaejiandaa kuruka….Jumamosi moja ktk mwaka ule nikiwa kwenye ubora wangu wa hali ya juu na ushawishi mkuu kuliko msanii yeyote Tz nilialikwa kutumbuiza Tabata kwenye ukumbi wa Dar West...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani