10 months ago

Michuzi

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATENDAJI WAKUU KUTOKA BOT, MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA NA UMOJA WA WACHIMBAJI MADINI TANZANIA


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia AcksonSpika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu kutoka Benki kuu ya Tanzania...

 

10 months ago

Michuzi

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MADINI NA KUZINDUA MAABARA YA KISASA YA MADINI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa 38 wa Mawaziri wa Madini  kutoka nchi wananchama wa Ukanda wa  Maziwa Makuu kwenye   Kituo cha Utafiti  na uendelezaji wa sekta ya Madini, Kundichi jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Meneja wa Maabara ya Kemia na Mazingira wa Kituo cha Utafiti na Uendelezaji wa Sekta  ya Madini, Bw.  Charles Butete baada ya kuzindua maabara hiyo , kunduchi jijini...

 

10 months ago

Michuzi

MAHAKAMA YAELEZWA JALADA HALISI KESI VIGOGO WA UTHAMINI MADINI NA ALMASI WA SERIKALI LIPO KWA DPP

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada halisi la kesi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya almasi wa Serikali lipo kwa Mkurugenzi wa mashtaka ( DPP).
Wakili wa Serikali Esterzia Wilson ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja mahakamani hapo kwa kutajwa.Amedai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na jalada halisi lipo kwa DPP, hivyo akaomba tarehe...

 

11 months ago

Michuzi

WATAALAMU WA MADINI NCHINI WAJIFUNZA UZOEFU KUTOKA AUSTRALIA

Na Veronica Simba – Dodoma
Wataalam mbalimbali kutoka sekta ya madini nchini wameshiriki warsha maalum iliyotolewa na wataalamu kutoka Australia, kwa lengo la kujifunza uzoefu kutoka nchi hiyo ambayo imepiga hatua kubwa katika sekta husika. Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko alifungua rasmi warsha hiyo ya siku mbili, Juni 4 jijini Dodoma na kusema kuwa Tanzania inahitaji kujifunza zaidi kutoka nchi zilizofanikiwa katika sekta ya madini kama Australia, ili iweze kukuza zaidi mchango wake...

 

11 months ago

Michuzi

WALINZI 10 WA KAMPUNI YA ULINZI YA KK KORTINI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA WIZI WA MAPIPA 26 YA MAKINIKIA YA MADINI

 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
WALINZI 10 wa kampuni ya ulinzi  ya KK na muendesha foko mmoja wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kula njama na wizi wa mapipa 26 ya makinikia ya madini yenye thamani ya Sh. 1,705,296,434.4.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri, wakili wa Serikali, Patrick Mwita amewataja washtakiwa hao kuwa ni Omar Omar (24), Boniface Mahingu (44), Haji Chalaza (30), Fadhil Kilima (28), Paulo Bigambo (27), Mwema Bakari (37), Israel Yeckonia...

 

11 months ago

Malunde

MBUNGE AMTAKA WAZIRI ALETE SANGOMA KUPATA MADINI YA MASHETANI

Mbunge wa Newala Vijijini Ajali Akibar amemtaka waziri wa madini Anjela Kairuki kwenda Afrika ya Kusini kutafuta waganga wa kienyeji na kuwaleta nchini, ili kuweza kupata madini kwa wingi.
Mbunge Akibar ameyasema hayo leo alipokuwa akichangia hotuba ya Wizara ya Madini Bungeni, na kusema kwamba amesikia kwamba madini yanatokana na mashetani, hivyo ni vyema Waziri akaenda kumleta mganga aje kuagua.
“Siku moja tuliwahi kusikia kwamba mambo ya madini yanatokana na mashetani, sasa hao mashetani...

 

11 months ago

Michuzi

SPIKA NDUGAI AFUNGUA MAONESHO YA MADINI BUNGENI DODOMA

Na Veronica SimbaSpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo Mei 30, amefungua rasmi maonesho ya madini katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma na kuipongeza Wizara ya Madini kwa kuyaandaa.Akitoa hotuba ya ufunguzi, Ndugai alimpongeza Waziri mwenye dhamana, Angellah Kairuki pamoja na watendaji wa Wizara, kwa juhudi kubwa za kutangaza na kulinda rasilimali ya madini hapa nchini. Alisisitiza kuwa, anatumaini juhudi hizo zitaendelezwa ili kuiwezesha sekta husika kuwa na...

 

11 months ago

Michuzi

KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA TANZANITE ONE YAKUBALI KUILIPA SERIKALI FIDIA MARA BAADA YA KUFIKIA MAKUBALIANO Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akitia saini pamoja na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma mara baada ya kufikia makubaliano na  Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Madini ambayo imekubali kulipa fidia kwa Serikali pamoja na mambo mengine ya Kimkataba.  
 Kiongozi wa Kamati ya Majadiliano kwa upande wa Serikali Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akibadilishana hati za Makubaliano na Mkurugenzi wa...

 

11 months ago

Michuzi

DC GAIRO AAGIZA WACHIMBAJI MADINI WASIO NA LESENI KUSIMAMISHA UCHIMBAJI MARA MOJA

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kutembelea sehemu ya migodi inayochibwa kinyemela na wachimbaji wasiokuwa na leseni. Moja ya mashine zilizokutwa eneo la mgodi. Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe amesikitishwa na makampuni ya uchimbaji madini ya viwandani wanaochimba madini mbalimbali Wilayani hapo hasa aina ya Felispar bila leseni. Mhe. Mchembe aliyasema hayo alipotembelea migodi ya Kata ya Rubeho ambapo wachimbaji...

 

11 months ago

VOASwahili

Serikali - Tanzania yafuta leseni za kuhodhi maeneo ya madini

Serikali ya Tanzania imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake wametakiwa kuomba upya wakizingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.

 

11 months ago

Michuzi

UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi  inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya Almasi wa Serikali kuwa hadi kufikia Mei 21 mwaka huu kuhakikisha wanatoa jibu kuhusu hatua ya upelelezi wa kesi hiyo ulipofikia.Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbrad Mashauri baada ya Wakili wa Serikali, Saada Mohammed kudai mahakamani hapo upelelezi wa kesi hiyo bado  haujakamilika na kwamba jalada lipo  kwa...

 

11 months ago

Michuzi

Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote

Greyson Mwase na Asteria Muhozya, MorogoroKatibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema kuwa zoezi la utoaji wa leseni kwa ajili ya utafiti, uchimbaji na biashara ya madini linatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa mara baada ya uanzishwaji wa Tume ya Madini.Profesa Msanjila ameyasema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari  kwenye mkutano wa baraza la kwanza la wafanyakazi wa Wizara ya Madini mjini Morogoro  tarehe 07 Mei, 2018 wenye lengo la kujadili...

 

11 months ago

Michuzi

Biteko apiga marufuku bei holela madini ya ujenzi

Na Greyson Mwase, TangaNaibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amepiga marufuku tabia ya wachimbaji wa madini ya ujenzi ya kushusha bei ya madini hayo kwa ajili ya kuuza kwa wingi, badala ya kufuata bei elekezi iliyowekwa na Serikali  huku wakiwalipa  vibarua kiasi kidogo cha fedha kisichoendana na kazi ngumu wanazofanya.Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo  mapema leo alipofanya ziara katika machimbo ya madini ya ujenzi aina ya kokoto katika eneo la Amboni mkoani Tanga lengo likiwa ni kukagua...

 

11 months ago

Michuzi

WAZIRI KAIRUKI AKABIDHI VIFAA VYA DOLA 350,000 KWA OFISI ZA MADINI ZA KANDA


Na Veronica Simba – DodomaWaziri wa Madini Angellah Kairuki amekabidhi vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani 350,000 kwa Ofisi za Madini za Kanda mbalimbali nchini.Akikabidhi vifaa hivyo kwa Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda hizo, jana Mei 4 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma; Waziri Kairuki aliwataka wahusika kuvitunza kutokana na gharama kubwa iliyotumika kuvinunua.“Serikali imekopa kwa ajili ya kuhakikisha sekta ya madini inaendelezwa ili iweze...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani