(Yesterday)

Michuzi

UJUMBE KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI(NDC) WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA

Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Balozi Peter Kallaghe(kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt Juma Malewa walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Februari 21, 2018(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dkt Juma Malewa akifanya mazungumzo mafupi na Maafisa Wakufunzi(hawapo pichani)kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania walipofanya...

 

2 weeks ago

CCM Blog

MKUU WA GEREZA LA UKONGA ASTAAFU UTUMISHI WA JESHI AKIHIMIZA KUENDELEZWA VIWANDA VYA MAGEREZA

 Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila , akipunga mkono wa kwaheri  wakati wa hafla ya kumuaga akistaafu utumishi wa jeshi hilo. Hafla hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Steven Mwaisabila (kushoto), akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa hafla ya kumuaga akistaafu utumishi wa jeshi hilo, Hafla hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya Chuo cha Magereza...

 

2 weeks ago

Malunde

MAGEREZA WATAJA SABABU ZA KUMZUI PROFESA JAY KUMUONA SUGU GEREZANI

Mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ jana alizuiwa kumuona mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi pamoja na katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga baada ya kuzuiwa na maofisa wa magereza.

Profesa Jay aliyeambatana na mke wake, Grace Haule walifika jana jijini Mbeya na kwenda gerezani kuwaona Sugu na Masonga ambao wapo mahabusu wakikabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Mkuu wa magereza Mkoa wa Mbeya,...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Askari Magereza 11 wasimamishwa kazi kwa mauaji

Jeshi la Magereza Tanzania limewasimamisha kazi askari wake kumi na moja waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mwanakijiji, Aloyce Makalla (41) wiki iliyopita. Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema askari hao walisimamishwa kazi na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk Juma Malewa juzi. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, John Masunga alithibitisha kusimamishwa kwa askari hao lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi akisisitiza kuwa msemaji wa jeshi hilo ni Kamishna...

 

2 weeks ago

Malunde

ASKARI MAGEREZA 11 WAKUFUKUZWA KAZI TUHUMA ZA KUUA MWANAKIJIJI

Jeshi la Magereza Tanzania limewasimamisha kazi askari wake kumi na moja waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mwanakijiji, Aloyce Makalla (41) wiki iliyopita.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema askari hao walisimamishwa kazi na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk Juma Malewa juzi.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, John Masunga alithibitisha kusimamishwa kwa askari hao lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi akisisitiza kuwa msemaji wa jeshi hilo ni Kamishna...

 

4 weeks ago

Michuzi

RWEGASIRA AIAGIZA TBA KUMALIZA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA KWA WAKATI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (wapili kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza, Mhandisi Khadija Salum, alipokua anamuonyesha Katibu Mkuu huyo maeneo mbalimbali ya ujenzi wa nyumba hizo zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu huyo aliiagiza TBA kumaliza ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano kuanzia sasa.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest...

 

4 weeks ago

Michuzi

RWEGASIRA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (wapili kushoto) akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza, Mhandisi Khadija Salum, alipokua anamuonyesha Katibu Mkuu huyo maeneo mbalimbali ya ujenzi wa nyumba hizo zilizopo Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Moja ya jengo la Makazi ya Askari Magereza likionekana hatua iliyofikia. Nyumba hizo zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam,...

 

1 month ago

Michuzi

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA WATENDAJI WA ASASI YA INTERNATIONAL YOUTH FELLOWSHIP JIJINI DAR

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiteta jambo Ofisini kwake  na Maafisa Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship(IYF), leo Januari 23, 2018 walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambapo Watendaji wa Asasi hiyo wamewalisha mada kuhusu mafunzo yanayolenga mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu mara wamalizapo vifungo magerezani.   Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF),  Jeon Hee yong...

 

1 month ago

Michuzi

KAMISHNA GASTON SANGA AMWAKILISHA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA KUFUNGUA MAFUNZO YA MAAFISA VIUNGANISHI WA UTUNZAJI WA TAKWIMU

Afisa Mradi wa Envirocare , ndugu Antony Mlelwa (Mwenye shati jeupe) akifungua na kumkabidhi kompyuta Afande Kamishna Gaston Sanga huku Mkurugenzi na Meneja Mradi wakishuhudia. Kompyuta hizo zitatumika kuhifadhia Taarifa na Takwimu kwa wataalam wapya wa katika Mradi wa Msaada wa Kisheria Magerezani.Mkurugenzi wa Envirocare Bi Loyce Lema akitoa maelezo mafupi ya historia ya Envirocare kabla ya kumkaribisha Afande Kamishna Gaston Sanga kutoa hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza na kufungua...

 

1 month ago

Michuzi

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA VIONGOZI KUJADILI MASUALA YA JESHI LA MAGEREZA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya Jeshi la Magereza baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk . Juma Malewa.Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ya wizara,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Watu waliovaa sare za askari magereza wavamia baa Dar es salaam

Watu zaidi ya 10 wakiwemo waliovaa sare za askari Magereza wamevamia baa moja iliyopo Keko jijini Dar es salaam, kujeruhi watu huku wakipora mali mbalimbali zikiwemo simu za mkononi na fedha za wateja. Watu hao walivamia baa hiyo  iitwayo Omax jana saa tano usiku na kuanza kuwapiga na kuwapora mali hizo wateja kisha kutokomea gizani. Awali, kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alisema alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi, alisema yuko Kibiti kikazi. Hata hivyo alikiri...

 

2 months ago

Michuzi

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AMEHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2017 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2018 JIJINI MBEYA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Baraza Maalum la kufunga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka mpya 2018. Baraza hilo limehudhuriwa na Maafisa na Askari kutoka vituo mbalimbali vya Magereza Mkoani Mbeya, Chuo cha Magereza Kiwira na Chuo cha Ufundi Mbeya ambapo Baraza hilo limefanyika leo Desemba 31, 2017 katika Viwanja vya Magereza Mkoani Mbeya.Baadhi ya Askari wa kike wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali vya Magereza ya Mkoa wa Mbeya wakisikiliza hotuba ya...

 

2 months ago

Michuzi

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT JUMA MALEWA AWAAGA MAAFISA MAGEREZA TOKA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WALIOKUWA WAKISHIRIKI MAZOEZI YA ULINZI WA AMANI JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kushoto) akiteta jambo na Maafisa wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji toka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Desemba 15, 2017 katika Ukumbi wa Magereza – Recreation, Ukonga Jijini Dares salaam. Maafisa hao walikuwa hapa nchini kushiriki mazoezi ya Kijeshi ya pamoja kuhusu ulinzi wa amani yaliyohusisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yaliyoandaliwa na Jeshi la...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Askari Magereza amsababishia kifo askari mwenziwe kwa kumchapa risasi

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linamshikilia kwa mahojiano askari Magereza wa Gereza la Kisongo jijini Arusha, Koplo Faustine Masanja kwa tuhuma za kumuua mwenzake wakiwa kazini.

Akizungumza na Vyombo vya Habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Desemba 14,2017 majira ya saa 2:00 asubuhi.

Kamanda Mkumbo amesema baada ya Masanja kumjeruhi mwenzake kwa risasi, alipelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu ambako alifariki...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Kamishna Magereza atoa neno kwa wafungwa waliopata msamaha wa Rais

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Juma Malewa amewataka wafungwa waliotolewa kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku ya uhuru, waheshimu mamlaka iliyowatoa na waende wakawe raia wema huko waendako.

Kamishna Malewa amesema anaamini kuwa wafugwa hao walioachiliwa huru kwa msamaha huo wameshajifunza na kujirekebisha na kuwaomba raia wawapokee na kuwatengenezea mazingira ya kuwaingiza katika kazi ili na wao waende sambamba...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani