2 days ago

VOASwahili

Chadema yataka wanachama wake wafikishwe mahakamani

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa polisi wamekuwa wakiwasumbua wanachama wao na hakuna hatua yoyote ya kuwafikisha mahakamani inayochukuliwa.

 

3 days ago

MwanaHALISI

IGP, DCI ‘wamkimbia’ Nondo mahakamani Dar

WAKATI Mwenyekiti wa Mtandao wa Wananfunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo akipandishwa kizimbani leo asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam nayo imeanza kusikiliza kesi ya Nondo dhidi ya Serikali, akidai haki ya uwakilishi pamoja na dhamana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). Mawakili wa Mtandao wa Watetezi ...

 

4 days ago

Zanzibar 24

Abdul Nondo kufikishwa mahakamani leo

Wakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini TSNP  Jebra Kambole leo Machi 21, 2018  amesema kuwa Abdul Nondo atasomewa mashtaka huko mkoani Iringa asubuhi hii Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi.

 “Watanzania taarifa zilizonifikia hivi punde kutoka kwa vyanzo vya kuaminika huku tukisubiri kesi yetu kuitwa mbele ya Jaji SAMEJI Mahakama Kuu DSM, kijana Abdul Nondo yupo Iringa akisubiri kusomewa mashtaka mkoani humo” Wakili Kambole.

Mnamo Machi 6, 2018 Abdul Nondo alipotea...

 

5 days ago

Malunde

HAKIMU AAGIZA NABII TITO AFIKISHWE MAHAKAMANI

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha ameagiza Tito Machibya (Nabii Tito) kufikishwa mahakamani ili kuendelea na kesi yake au apate maelezo kamili ya kwanini mtuhumiwa huyo hafikishwi mahakamani.

Hakimu Karayemaha ametoa maagizo hayo leo Machi 19, 2018 baada ya kuelezwa kuwa Nabii Tito hakufikishwa mahakamani kwa kuwa bado anaendelea kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa akili unaomkabili kwenye kituo cha magonjwa ya akili Hospitali ya Mirembe mkoani hapa.

Nabii...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Watu 18 wapandishwa Mahakamani kwa tuhuma ya kupatikana na Dawa za Kulevya Unguja

Waliopandishwa Mahakamani kwakupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroin ni pamoja na Suleiman Maulid Mussa mwenye umri wa miaka 30 na Mukrim Khamis mwenye umri wa miaka 23 wote wakaazi wa Mbuzini Mwalim Khamis Juma mwenye umri wa miaka 30 mkaazi wa Michezani , Muhammed Mahmoud Machano mwenye umri wa miaka39 mkaazi wa meli sita mwera na Ali Suleiman Ali mwenye umri wa miaka 40 mkaazi wa miembeni.

Wengine ni Rehani Rajab Rished mwenyeumri wa miaka 26 mkaazi wa Mkaazi wa Kwahani na na...

 

1 week ago

Malunde

WAFUASI WA CHADEMA WALIOKAMATWA MSIBANI WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Wafuasi zaidi ya 10 wa Chadema waliokamatwa wakiwa nyumbani kwa mwanachama mwenzao kuhani msiba wanatarajiwa kupandishwa kizimbani muda mfupi ujao.

Watu hao, leo Machi 14, 2018 tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza na kuwekwa katika mahabusu mahakamani hapo kusubiri kukamilika kwa taratibu za kimahakama ili wasomewe mashtaka dhidi yao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi watu hao walikamatwa eneo la Mabatini Machi 13, 20018 baada ya kutokea...

 

2 weeks ago

RFI

Tanzania: Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari yapingwa Mahakamani

Wanahabari na wanaharakati nchini Tanzania wamekwenda Mahakamani kupinga Sheria ya Huduma ya vyombo vya Habari  kwa kile wanachosema, itatishia uhuru wa wanahabari nchini humo.

 

2 weeks ago

Malunde

POLISI : NONDO ALIJITEKA,ALIKWENDA IRINGA KWA MPENZI WAKE....ATAFIKISHWA MAHAKAMANI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo na kujiteka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Machi 13, 2018 Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema Nondo ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi kuhusu taarifa za kutekwa kwa Abdul...

 

2 weeks ago

Michuzi

MAKALA YA SHERIA: KUPOTELEWA NA NYARAKA INAYOHITAJIKA MAHAKAMANI KAMA USHAHIDI

Na Bashir Yakub.
Inaweza kuwa nyaraka muhimu kama hati ya nyumba, mkataba wa mauziano au mkataba mwingine wowote, wosia, kadi ya gari au ya mashine yoyote,hati ya kusimamia mirathi, cheti cha ndoa au vyeti vinginevyo, na nyaraka nyingine mbalimbali.
Nyaraka hii inaweza kuwa inatakiwa sehemu muhimu kama mahakamani ili kuthibitisha shauri au kesi yako. Na inaweza ikawa ni nyaraka ambayo kuwepo kwake ndio kushinda kwako na kutokuwepo kwake ndio kushindwa kwako.
Pamoja na umuhimu wa nyaraka hii...

 

2 weeks ago

Malunde

ALIYETAJA ORODHA YA WATU 10 HATARI ZAIDI KWA USALAMA WA TAIFA TANZANIA KUBURUZWA MAHAKAMANI

Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi amefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria Cyprian Musiba kwa kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika tarehe 25 Februari, 2018.

Barua hiyo iliyotolewa na Mwanasheria wa Maria Sarungi, Benedict Alex Ishabakaki imeeleza kuwa mteja wake alitajwa na gazeti la Tanzanite toleo Namba 50 lililotoka...

 

2 weeks ago

Malunde

AFISA WA TRA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA

Ofisa Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Joyce Amon amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtaka la kushawishi rushwa.

Wakili wa Serikali, Sophia Nyanda alisema jana Ijumaa Machi 9, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Adelf Sachore kuwa Desemba 12, 2017 katika eneo la Gerezani Kariakoo Wilaya ya Ilala mshtakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa TRA kama Ofisa Msaidizi wa Kodi alishawishi rushwa ya Sh800,000 kutoka kwa Antelo Sanga ili asiweze kumwandikia cheti cha...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Ofisa Msaidizi wa TRA afikishwa mahakamani kwa kushawishi rushwa ya Sh800,000

Ofisa Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Joyce Amon amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtaka la kushawishi rushwa.

Wakili wa Serikali, Sophia Nyanda amesema leo Ijumaa Machi 9, 2018  mbele ya Hakimu Mkazi  Adelf Sachore kuwa  Desemba 12, 2017  katika eneo la Gerezani Kariakoo Wilaya ya Ilala mshtakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa TRA kama Ofisa Msaidizi wa Kodi alishawishi rushwa ya Sh800,000 kutoka kwa Antelo Sanga ili asiweze kumwandikia cheti cha...

 

3 weeks ago

Malunde

MAVUNDE AAGIZA KUFIKISHWA MAHAKAMANI WAAJIRI 6,907 WALIOSHINDWA KUJISAJILI WCF


SERIKALI imesema haitabadili msimamo wake wa kuwapeleka mahakamani waajiri wote ambaobado hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikiaKazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amewaambia waandishi wa habari leo Machi 6, 2018 jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri ametoa tamko hilo wakati wa ziara yake ya kushtukiza aliyoifanya wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekelkezatakwa hilo la Kisheria...

 

3 weeks ago

BBCSwahili

Magavana na wabunge wa Kenya waliopoteza viti vyao mahakamani

Katika orodha ya magavana waliopoteza viti vyao baada ya wapinzani wao kupeleka kesi katika Mahakama Kuu; wa kwanza alikuwa Bwana Martin Wambora, Gavana wa kaunti ya Embu.

 

3 weeks ago

Malunde

JINSI MLIPUKO WA TRANSFOMA ULIVYOZUA KIZAA ZAA MAHAKAMANI DAR

Shughuli katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zilisimama kwa muda baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme katika transfoma ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) iliyopo katika eneo la mahakama hiyo.

Trasfoma hiyo imelipuka na kusababisha nyaya mbili kushika moto na kuzua hofu miongoni mwa watu waliokuwa mahakamani hapo, kuanza kukimbia hovyo.

Tukio hilo limetokea asubuhi Machi 1, 2018 wakati kesi mbalimbali zikiendelea kusikilizwa.

Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Dar es Salaam, Gasto Kanyairita...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani