4 months ago

Michuzi

MAJAMBAZI NANE NA WAHAMIAJI HARAMU SABA WAKAMATWA MKOA WA PWANI

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani  JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu nane wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utekaji wa gari.  Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni wahamiaji haramu saba kutoka nchi ya Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Tukio hilo lilitokea Juni 4 mwaka huu, katika eneo la Vigwaza ambapo watu wawili waliojifanya wasamaria wema walisimamisha gari hiyo yenye namba za usajili T 311 DHS aina ya Fuso lililokuwa...

 

5 months ago

Malunde

Kimenuka!! POLISI SHINYANGA WAKAMATA SILAHA ZA KIVITA,WAUA MAJAMBAZI WANNE MAKABURINI KAHAMA...ANGALIA PICHA

Watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi eneo la makaburi  ya Kitwana kata ya Busoka tarafa ya Kahama Mjini wilayani Kahama wakati wakijaribu kuwatoroka askari waliokuwa kwenye msako mkali wa kuwatafuta majambazi wanaojihusisha na matukio ya uhalifu katika wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makaburi ya Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama leo Jumatatu Juni 4,2018,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule alisema tukio hilo...

 

5 months ago

BBCSwahili

Meneja wa zamani wa Man City Manuel Pellegrini aporwa na majambazi wenye bunduki

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini ameporwa na majambazi waliokuwa na bunduki nchini Chile.

 

5 months ago

Malunde

WANAODAIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA KWA KUPIGWA MAWE

Watu watatu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wamepigwa mawe hadi kufa na wananchi wa Kijiji cha Bubare Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.

Watuhumiwa hao waliuawa baada ya kuwekewa mtego kutokana na kuwapo taarifa za wao kutaka kuvamia nyumba ya mmoja wa wakazi wa kijiji hicho kwa nia ya kupora fedha za mauzo ya mifugo.

Baadhi ya viongozi wa Serikali ya kijiji waliojaribu kuwazuia wananchi kuwashambulia watuhumiwa hao, walilazimika kutimua mbio kuokoa maisha yao baada ya kugeuziwa kibao na kuanza...

 

6 months ago

Michuzi

POLISI WAUA MAJAMBAZI WANNE WAKATI WAKIJIBIZANA KWA RISASI MKOANI PWANI

Na Mwamvua Mwinyi, KisaraweWATU wanne wanatuhumiwa kuwa majambazi wamefariki dunia baada ya kujibizana risasi na askari polisi ,wakati wakijaribu kufanya tukio la ujambazi katika nyumba ya Juliana Shirinde ambae ni Mhasibu wa kikundi cha vikoba Ushelisheli,wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Aidha jeshi la Polisi mkoani Pwani,limenasa gari ndogo yenye namba za ubalozi ambazo ni namba bandia T 17 CD 220 ambayo ilikuwa inatumiwa na majambazi kufanya uhalifu.
Akitoa taarifa ya tukio hilo la kukamatwa...

 

6 months ago

Malunde

POLISI WAUA MAJAMBAZI WANNE PWANI

Majambazi wanne wameuawa na polisi asubuhi ya leo Ijumaa Aprili 20, wakati wakijaribu kupora Kisarawe mkoani Pwani.
Kabla ya kuuawa yalitokea majibizano ya risasi kati yao na askari Polisi.

Imedaiwa majambazi hao wametokea jijini Dar es Salaam na walikuwa wanatumia gari lenye namba za kibalozi hatua iliyosababisha askari wa usalama barabarani kutowahisi chochote kwani gari hizo sio rahisi kusimamishwa ovyo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani...

 

6 months ago

Malunde

MAJAMBAZI YAVAMIA KANISA KATOLIKI DAR

Majambazi wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora fedha na baadhi ya vifaa vya kuendeshea misa usiku wa kuamkia leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango, Uchumi na Fedha wa parokia hiyo, Arnold Kimanganu amesema kuwa majambazi hao waliwapiga walinzi kabla ya kuingia kanisani.

“Majambazi walivyofika waliwapiga walinzi, tuna walinzi wanne walimshika mlinzi mwenye silaha wakampiga na kumnyang’anya bunduki, kumkamata mwingine...

 

7 months ago

Zanzibar 24

Majambazi wavamia kanisa na kupora vitu vya kufanyia ibada

Majambazi wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora fedha na baadhi ya vifaa vya kuendeshea misa usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango, Uchumi na Fedha wa parokia hiyo, Arnold Kimanganu amesema kuwa majambazi hao waliwapiga walinzi kabla ya kuingia kanisani.

“Majambazi walivyofika waliwapiga walinzi, tuna walinzi wanne walimshika mlinzi mwenye silaha wakampiga na kumnyang’anya...

 

7 months ago

Zanzibar 24

Majambazi wavunja kanisa na kupora mali Dar es Salaam

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Usiku wa kuamkia leo April 5, 2018 kuna Majambazi wamevamia na kuvunja kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam, na kupora fedha za sadaka zilizokusanywa tangu sikukuu za pasaka mpaka sasa na vifaa vya kuendeshea misa.

“Ni vibaka wameingia hapo kanisani na kuiba pesa na baadhi ya vitu, pesa ambazo zilikuwa za sadaka tangu sikukuu, ila thamani yake bado...

 

7 months ago

BBCSwahili

Majambazi wamvamia na kujaribu kumkata miguu mwanariadha wa Afrika Kusini kwa msumeno

Mwanariadha nchini Afrika kusini nusra akatwe miguu kabisa aliposhambuliwa na kundi la wanaume alipokuwa anafanya mazoezi Jumanne alfajiri.

 

8 months ago

Zanzibar 24

Mtu mmoja auawa na watatu kujeruhiwa baada ya majambazi kuvamia kwenye machimbo ya dhahabu

Watu watatu  wanaosadikiwa  kuwa ni majambazi wamevamia machimbo ya madini ya   dhahabu  ya Ifumile  Kijiji  cha  Isumamilomo   Wilaya ya  Mpanda na kumuua mchimbaji   mmoja kwa  kumpiga   risasi ya tumbo  kwa  kutumia    bunduki aina ya AK 47 na kujeruhi wengine watatu.

Pia wanadaiwa kupora  dhahabu yenye uzito wa zaidi  ya   gramu 650, fedha  taslimu Sh. milioni 1.5 na   mashine  mbili za kutafutia  dhahabu.

Kamanda  wa    Polisi Mkoa  wa  Katavi,  Damas  Nyanda,  alitoa taarifa hizo jana...

 

8 months ago

BBCSwahili

Majambazi wavamia kituo cha polisi na kuwaua polisi 5 Afrika Kusini

Washukiwa wanaaminiwa kupora mashine ya kutoa pesa muda mfupi kabla ya kuvamia kituo cha polisi

 

9 months ago

Malunde

Picha : POLISI KATAVI WAUA MAJAMBAZI WAWILI,KUKAMATA WATATU WAKIWA NA SILAHA ZA KIVITA


Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi wakati majambazi hao wakijibizana risasi na askari polisi majibishano ya risasi baina yao na askari polisi na wahifadhi ya taifa ya Katavi katika kijiji cha Kapalamsenga wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Pamoja na kuua majambazi hao majambazi wengine watatu kati ya watuhumiwa hao watano wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa wakiwa na silaha nzito tatu na magazine tano risasi 16 na vipande vinne ...

 

9 months ago

Zanzibar 24

Afisa kilimo auawa na majambazi wakati wakivamia duka la mfanyabiashara Shinyanga

Afisa kilimo kata ya Bukene – Didia wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ndonho mwenye umri wa miaka 32, ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliokuwa wanavamia duka la Juma Mnyesi miaka 47 katika kijiji na kata ya Didia wilayani humo. Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema mauaji hayo yametokea jana Januari 23,2018 saa mbili na dakika 40 usiku katika kijiji cha Didia, kata ya Didia, tarafa ya Itwangi, wilaya ya Shinyanga...

 

9 months ago

Malunde

Picha & Video : AFISA KILIMO AUAWA KWA KUPIGWA RISASI MAJAMBAZI YAKIVAMIA DUKA LA MFANYABIASHARA DIDIA SHINYANGA


Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Edward Ndonho (32) ambaye ni afisa kilimo kata ya Bukene - Didia wilaya ya Shinyanga Vijijini ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliokuwa wanavamia duka la Juma Mnyesi (47) katika kijiji na kata ya Didia wilayani humo.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule aliyefika eneo la tukio,amesema mauaji hayo yametokea jana Januari 23,2018 saa mbili na dakika 40 usiku katika kijiji cha Didia, kata ya Didia, tarafa ya Itwangi, wilaya...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani