(Today) 11 hours ago

Michuzi

RC DKT. KEBWE AAGIZA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI GAIRO WAKAMATWE


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-GAIRO. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameliagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo kuwatafuta na kuwakamata watu walioharibu miundo mbinu ya maji ikiwemo kuiba pampu ya maji ya Kijiji cha Italagwe katika Wilaya ya Gairo na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.
 Dkt. Kebwe ametoa agizo mapema leo Mei 24 mwaka huu akiwa katika Kijiji cha Italagwe Kata ya Italagwe, wilayani humo wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kutembelea na kuhimiza...

 

(Yesterday)

Michuzi

SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA MAKAZI YA WATU WENYE UKOMA YA SAMARIA HOMBOLO

Serikali imejipanga kuwajengea Kisima cha kisasa watu wenye mahitaji maalum kitachoweza kuhudumia Kaya 26 zenye jumla ya watu 56 wenye ukoma na wazee katika Kambi ya Samaria Hombolo jijini Dodoma.
Hatua hiyo inakuja mara baada ya wakazi wa kambi ya Samaria kueleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo; ukosefu wa maji salama, changamoto za matibabu kwa kukosa bima za afya, uchakavu wa  magodo kwa ajili ya malazi, uhaba wa chakula cha uhakika.
Changamoto hizo zimeibuliwa wakati ya Ziara ya...

 

(Yesterday)

Malunde

MFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI KAHAMA AFARIKI KWA AJALI YA PIKIPIKI

Rexpirius Vicent enzi za uhai wake
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Kahama (KUWASA) Rexpirius Vicent Ntukigwa (29) ambaye ni mkazi wa Nyahanga mjini Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa anaendesha kuacha njia na kutumbukia mtaroni.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule tukio hilo limetokea jana Mei 23,2018 majira ya saa 12 na dakika 45 asubuhi katika eneo la Five Ways - Nyihogo barabara itokayo...

 

(Yesterday)

Zanzibar 24

Vijana 25 wapelekwa Bagamoyo kujifunza kuvua Samaki katika kina kirefu cha Maji

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea na jitihada za kuwawezesha vijana kwenda kuvua katika bahari kuu ili waweze kunufaika na Rasilimali za Bahari zilizopo.

Akijibu swali katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Chukwani  nje kidogo ya mji wa Zanzibar Naibu Waziri wa Kilimo ,Mali asili Mifugo na Uvuvi Dk. Makame Ali Ussi amesema mpaka sasa jumla ya Vijana 25 tayari wameshapelekwa Bagamoyo kwa kujifunza namna ya Kuvua samaki katika kina kirefu cha Maji.

  Amesema  Zanzibar ni...

 

2 days ago

Michuzi

WAZIRI WA MAJI KAMWELWE ATAHADHARISHA KUWAFUKUZA WAHANDISI

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe ametahadharisha kuwafukuza kazi na kuwashitaki wahandisi wa serikali wanaokosa uzalendo na kuhujumu miradi ya maji katika hatua ya usanifu na usimamizi kwa kupitisha vifaa vilivyo chini ya viwango.
Mhandisi Kamwelwe ametoa tahadhari hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Songwe ya kukagua utekelezaji wa miradi mitatu ya maji ya Iyula na Itaka katika halmashauri ya Mbozi, mradi wa Umwagiliaji Naming’ongo katika halmashauri ya Momba na mradi wa...

 

2 days ago

Zanzibar 24

Watoto watoa mwili wa aliyekufa maji Mtwara

Watoto wawili wenye umri wa miaka 8-12, wameibuka mashujaa baada ya kuokoa mwili wa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mzee Nampwenge aliyekufa na maji, baada ya kuzama kwenye bwawa alipokuwa akiogelea huko Namayanga, Naliendelea mkoani Mtwara.

Mtoto Islam Shaibu

Akizungumza na Eatv mwenyekiti wa mtaa wa Namayanga Ally Salum Nayove amesema ni kweli watoto hao waliotambulika kwa majina ya Faraji Muhibu, na Islam Shaibu, wanaosoma darasa la nne na mwingine la pili...

 

3 days ago

MwanaHALISI

Bwawa la maji kujengwa Morogoro kupunguza uhaba

SERIKALI imekiri kuwa mji wa Manispaa ya Morogoro unakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa maji ya uhakika na kusababisha wananchi kukumbwa na hadha ya ukosefu wa maji. Anaripoti Dany Tibason … (endelea). Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso alipokuwa ajibu swali la nyongeza la mbunge wa ...

 

4 days ago

Michuzi

REHEMA FOUNDATION YAKABIDHI MRADI WA MAJI SHULE YA SEKONDARI ZOGOWALE

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Zogowale ,mjini Kibaha Mkoani Pwani ,wakishangilia kupata huduma ya maji shuleni hapo ,baada ya kujengewa kisima cha kupampu kilichogharimu zaidi ya sh.mil.11 ,(wa katikati)Mkurugenzi wa Rehema Foundation ,Mohammed Cesur.
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
CHANGAMOTO ya maji safi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa shule ya sekondari Zogowale, Mjini Kibaha mkoani Pwani, inabaki historia baada ya kujengewa kisima kirefu cha kupampu, kilichogharimu zaidi ya sh....

 

5 days ago

Michuzi

DC WA SAME AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MEI 30 MWAKA HUU

MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Senyamule amemtaka mkandarasi wa mradi wa maji Kijiji cha Hedaru kukamilisha mradi huo unaogharimu bilioni 1.18 ifikapo Mei 30 mwaka huu.
Akitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo juzi mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli ni kuona mwanamke anatua ndoo kichwani kwa kupata huduma ya maji .
Alisema mradi huo umelenga kufikia vijiji...

 

1 week ago

Michuzi

Ubalozi Kuwait wakabidhi kisima cha maji nambari 63 katika Chuo cha Ufundi cha Yombo kwa wanafunzi walemavu

 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem hivi karibuni alizindua kisima cha maji safi na salama nambari 63 katika Chuo cha Ufundi cha Yombo kwa wanafunzi walemavu kilichopo Jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo ambao ulishuhudiwa na mwakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Josephine Lyungi, Kaimu Mkuu wa Chuo, Bi. Maryam, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiwalani, Emannuel pamoja na walimu na wanafunzi. 
Huu ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait unaofahamika kwa jina la “KISIMA CHA MAJI...

 

1 week ago

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA UWEKEZAJI CHA JWTZ NA VIWANDA VYA MAJI NA USHONAJI VYA SUMA JKT MGULANI JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu wakifunua pazia kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee...

 

1 week ago

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA UWEKEZAJI CHA JWTZ NA VIWANDA VYA MAJI NA USHONAJI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo  na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Hussein Mwinyi,  Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu alipowasili kuzindua kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam leo Mei 17, 2018. Kituo kicho kina viwanda vya ushonaji na maji ya kunywa pamoja na Shule ya Sekondari ya Jitegemee na Ukumbi wa...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Mtoto afariki baada ya nyumba yao kujaa maji Unguja

Mtoto mmoja afariki baada kutumbukia ndani ya maji kufuatia nyumba yao kujaa maji na kufurika.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 za usiku huku mvua ikiemdelea kunyesha huko Mtoni Kidatu Wilaya ya Magharib A Unguja.

Baadhi ya Mashuhuda walioshuhudia tukia hilo wamesema kuwa maji yalikuwa yanaingia ndani kwa kasi na kujaa ambapo milango ilikua haifunguki wakati walipokua wakijihami kukaa juu ya dari mtoto huyo alimponyoka kwa yule ambae aliemshika na hatimae kuzidiwa na maji.

“Yule mtoto...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Waziri afunguka sababu 4, tatizo la maji Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imeomba kulitafutia ufumbuzi  wa haraka tatizo la maji ambalo linawakabili baadhi ya wananchi wa Zanzibar  ili  kuwaondolea usumbufu  hususa wanawake na watoto katika  kipindi  cha mwezi mtukufu wa ramadhani.

Akizungumza na Zanzibar24  Mwakilishi wa Viti maalum Mkoa wa kaskazini Pemba kundi la vijana   Viwe Khamis Abdalla amesema  bado kuna shehia katika mkoa wake zinakabiliwa na tatizo la maji kwa muda mrefu licha ya yeye kujitahidi kuwaomba mamlaka...

 

1 week ago

Malunde

WANAFUNZI WAFA MAJI BAADA YA KIVUKO KUZAMA PWANI

Wanafunzi wawili wamekufa maji baada ya kivuko walichokuwa wakitumia kuzama katika eneo la Chulwi wilayani Mkuranga mkoani Pwani, huku watu wazima 10 wakiokolewa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Ali Hengo aliye eneo la tukio amesema wanafunzi hao walikuwa wakivuka kwenye kivuko ambacho sio rasmi wanachokitumia kila siku kwa ajili ya kwenda shuleni huku wakiwa na wananchi wengine, ambacho ndiyo kimezama na kusababisha vifo hivyo.
"Kuna watu walikuwa wakivuka pamoja na wanafunzi sasa wakazama,...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani