6 months ago

BBCSwahili

Mtaalamu bingwa wa afya ya akili kutoka Tanzania kutuzwa Marekani

Mtaalam bingwa wa kukabiliana na matatizo ya kiakili na mtafiti kutoka Tanzania Profesa Sylvia Kaaya ni miongoni mwa watu sita ambao watatuzwa shahada ya heshima na chuo cha Marekani cha Dartmouth.

 

6 months ago

Michuzi

Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

Dar es Salaam. Muogeleaji wa Tanzania, Natalia Ladha ametamba kufanya vyema katika mashindano ya kuogelea ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya jimbo la Florida nchini Marekani yajulikanayo kwa jina la Florida Gold Coast Junior Olympic.
Natalia aliondoka nchini jana tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Martin County Juni 16 ambapo atajiunga na waogeleaji wa klabu ya Swimfast.
Muogeleaji huyo ambaye ni nyota kwa waogeleaji wa Tanzania wenye umri kati ya miaka...

 

6 months ago

Michuzi

MAAFISA UUGUZI CHUO KIKUU CHA NEW YORK NCHINI MAREKANI KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KATIKA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WAGONJWA

Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimkabidhi zawadi ya kinyago Afisa Muuguzi wa Chuo Kikuu cha New York cha nchini Marekani Linda Herrmann wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Maafisa uuguzi wawili kutoka chuo hicho walifika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

 

6 months ago

VOASwahili

Trump atamualika Kim Marekani kama mkutano wao utaleta matunda

Rais wa Marekani, Donald Trump alisema alhamis kwamba atamualika kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong Un kuja Marekani kama mkutano ujao wa kihistoria na kiongozi huyo utakuwa na mafanikio. Kwa upande mwingine, alisema yuko tayari kujiondoa kwenye mkutano ikiwa mambo hayatakua sawa. Rais Trump alikutana kwa saa mbili na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe huko White House siku ya alhamis chini ya wiki moja kabla ya mkutano wake wa kilele na Kim Jong Un huko Singapore. Mkutano huo na Korea...

 

6 months ago

VOASwahili

Marekani yakanusha madai ya Sudan Kusini

Balozi mpya wa Marekani kwa Sudan Kusini amekanusha shutuma ambazo zimetolewa na utawala wa Kiir kwamba Marekani inataka mabadiliko ya uongozi nchini Sudan Kusini.

 

6 months ago

BBCSwahili

Mwanamume aumwa na kichwa cha nyoka Texas, Marekani

Mwanamume mmoja katika jimbo ya Texas, Marekani nusura afe baada ya kuumwa na kichwa cha nyoka ambaye alikuwa amemkata na kumuua.

 

6 months ago

VOASwahili

Marekani inatofautiana kupunguza wanajeshi wake Afrika

Waatalamu wa kijeshi wa Marekani wanatofautiana juu ya mipango ya awali ya kupunguza idadi ya operesheni maalum za jeshi la Marekani  barani Afrika. Gazeti la New York Times liliripoti kwanza juu ya mpango huo mapema mwezi June ikieleza kwamba kupunguzwa operesheni maalum kutaweza kupunguza idadi ya makomando wanaofanya kazi katika bara hilo kutoka 1,200 hadi kufikia 700 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Maafisa wa kijeshi wameiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba ingawa maafisa wa...

 

6 months ago

BBCSwahili

Loris Karius: Kipa wa Liverpool atumwa kwa madaktari Marekani

Mlinda lango wa Liverpool Loris Karius alitumwa kwa madaktari wataalamu nchini Marekani baada yake kuwasiliana na klabu hiyo akiwa likizoni Marekani.

 

6 months ago

VOASwahili

Trump asema amewapiku marais wengine wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku ya 500 katika madaraka Jumatatu, akitangaza kuwa “wengi wanaamini” kwamba ameweza kutekeleza mambo mengi zaidi kuliko rais wengine wa Marekani.

 

6 months ago

Michuzi

MISSY TEMEKE NA MUMEWE WAFUTARISHA HILTON HOTEL, ROCKVILLE, MARYALAND, MAREKANI

Missy T (kati) akiwa na Loveness Mamuya (kushoto) na Shamis siku ya Ijumaa June 1, 2018 katika hotel ya Hilton iliyopo Rockville, Maryland siku Missy Temeke na mumewe Mohamed Matope walipofutarisha. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production kwa udhamini wa Kilimanjaro studio.Wageni waliofika kwenye futariiliyoandaliwa na Missy T na mumewe Mohamed Matope siku ya Ijumaa June 1, 2018 katika hotel ya Hilton iliyopo Rockville, Maryland nchini Marekani.Wageni waalikwa wakipata futari siku ya...

 

6 months ago

BBCSwahili

Mgogoro wa visiwa vya China Kusini: China yasema matamshi ya Marekani ni ya 'kijinga'

Beijing inasema kuwa ina haki ya kupeleka majeshi na silaha 'katika himaya yake' baada ya Marekani kuishutumu kwa kuwatishia majirani zake.

 

6 months ago

BBCSwahili

Mhubiri awaomba waumini wamnunulie ndege yake ya nne Marekani

Jesse Duplantis amesema Mungu amemwambia anunue ndege aina ya Falcoln 7X ambayo inagharimu $54m (£41m).

 

6 months ago

RFI

Marekani, Saudi Arabia kushiriki maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam

Nchi zaidi ya 30 ikiwemo Marekani na Saudi Arabia zinatarajiwa kushiriki maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam yanayopangwa kuanza Juni 28 hadi julai 13 mwaka huu.

 

6 months ago

Michuzi

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWA MFUKO WA DHARURA WA RAIS WA MAREKANI WA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI (PEPFAR)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani