5 days ago

Michuzi

AGPAHI YATOA MAFUNZO YA HUDUMA ZA KISAIKOLOJIA KWA WAHUDUMU WA VITUO VYA TIBA NA MATUNZO MWANZA

Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limeendesha mafunzo kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii wanaosaidia kazi katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) vilivyopo katika halmashauri za wilaya mkoani Mwanza. 
Mafunzo hayo ya siku tano yanayokutanisha wahudumu wa jamii kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba, Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana yanafanyika kuanzia...

 

5 days ago

Michuzi

DIAMOND,HAMISA MOBETO WAFUNGA JALADA MATUNZO YA MTOTO

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
HATIMAYE jalada la kesi ya madai ya matunzo ya mtoto lililofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto na Mwanamitindo maarufu nchini, Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuziki, Naseeb Abdull 'Diamond Platinumz' limefungwa rasmi.
Akizunguma leo na waandishi wa habari baada ya kutoka mahakamani Diamond amesema, walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ili upande wa Ustawi wa Jamii na Mahakama ziwe sawa ili kesho na kesho kutwa...

 

5 days ago

Malunde

Picha : AGPAHI YATOA MAFUNZO YA HUDUMA ZA KISAIKOLOJIA KWA WAHUDUMU WA VITUO VYA TIBA NA MATUNZO MWANZA


Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza Dk. Pius Masele.***Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limeendesha mafunzo kuhusu msaada na huduma za kisaikolojia kwa wahudumu wa jamii wanaosaidia kazi katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) vilivyopo katika halmashauri za wilaya mkoani Mwanza.
Mafunzo hayo ya siku tano yanayokutanisha wahudumu wa jamii kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela,Kwimba,...

 

4 weeks ago

Malunde

Picha : AGPAHI YAKABIDHI KOMPYUTA 46 KWA AJILI YA VITUO VYA TIBA NA MATUNZO KWA WATU WANAOISHI NA VVU MKOA WA MARA


Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi kompyuta 46 zenye thamani ya shilingi milioni 70.2 zitakazotumika katika vituo vya tiba na matunzo (CTC) kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwenye halmashauri za wilaya mkoani Mara.
Shirika hilo limekabidhi kompyuta hizo siku ya Jumatatu, Januari 22, 2018 kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Nyanda katika ukumbi wa mikutano wa Mwembeni uliopo katika Manispaa ya Musoma.
Akizungumza wakati wa...

 

3 months ago

Michuzi

Mahakama yatupilia mbali maombi ya matunzo ya mtoto dhidi ya Mwanamuziki Diamond Platnum


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Diamond Platnum.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 10/2017 na Hakimu Devotha Kisoka wa mahakama hiyo.

Hakimu Devotha alitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika kutokana na msanii Diamond kuwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto.

Katika pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakamani hapo anadai...

 

3 months ago

Michuzi

Uamuzi kesi ya matunzo ya mtoto dhidi ya msanii Diamond kutolewa kesho.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesho Novemba 10, 2017 inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya kesi ya matunzo ya mtoto iliyofunguliwa na mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya msanii maarufu nchini, Nassib Abdul au Diamond Platinum.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi, Devotha Kisoka upande wa Watoto.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote husika kutokana na.msanii Diamond kuwasilisha pingamizi kupinga kesi hiyo kwa madai kuwa...

 

4 months ago

Malunde

DIAMOND PLATNUMZ ADAI HANA UWEZO WA KUMLIPA HAMISA MOBETO MILIONI 5 ZA MATUNZO YA MTOTO

Msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana uwezo wa kumlipa Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.

Diamond amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo ya mtoto.

Katika majibu yake Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa kulipwa kwa mwezi kwa ajili ya...

 

4 months ago

Malunde

ASKARI WA FFU AMUUA KWA RISASI MZAZI MWENZAKE MZOZO WA MATUNZO YA MTOTO

Polisi wilayani Babati mkoani Manyara inamshikilia askari wa jeshi hilo Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Cosmas James akituhumiwa kumuua mzazi mwenzake, Regina Daniel (23) kwa kumpiga risasi nne.

Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa ni mzozo ulitokea Regina alipomfuata James lindoni kudai fedha za matumizi ya mtoto.

Akithibitisha tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Longinus Tibishubwamu amesema lilitokea mjini Babati Ijumaa Oktoba 27,2017 saa 12:30 jioni.

Amesema askari huyo...

 

4 months ago

Bongo Movies

Diamond Kupandishwa Kizimbani Kisa Matunzo ya Mtoto kwa Hamisa Mobeto

Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.

Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mabetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.

Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.

Wakili Zulu akizungumza na Gazeti la Mwananchi leo Alhamisi amesema...

 

5 months ago

Zanzibar 24

Wazee walia na afya zao kwa kukosa matunzo bora

Jumuiya ya wazee Zanzibar na wastaafu  wameiyomba serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kuongeza juhudi na  kuwasaidia wazee hasa katika huduma za afya pamoja na kuwawezesha kiuchumi.

Waandishi wa habari waliohudhuria

Wakitoa taarifa kwa waandishi wa habari  juu ya maadhimisho ya siku ya wazee dunia inayotarajiwa kufanyika oktoba mosi  wamesema bado wazee wengi Zanzibar wanakabiliwa na matatizo ya kiafya,kukosa malenzi bora licha ya  jumuiya hizo ...

 

8 months ago

Mwanaspoti

Banka: Niyonzima anahitaji matunzo

NYOTA wa zamani wa Taifa Stars, Mohammed Banka amesema kama Simba itafanikiwa kumsainisha kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kutoka Yanga, basi viongozi wajue namna ya kumtunza.

 

11 months ago

Michuzi

MAKALA YA SHERIA: JE SHERIA INASEMAJE KUHUSU MKE KUTOA MATUNZO KWA MME WAKE


NA  BASHIR  YAKUB -

Je  nani  anawajibu  wa  kumtunza  mwenzake  kati  ya  wanandoa.  Je  ni  mme,  je  ni  mke   au  ni  wote .  Sheria  inasemaje  kuhusu  hili. Kwa  kuanza  tu  ni  kuwa  suala  matunzo  kwa  wanandoa  ni  la  kisheria. Matunzo  sio  hisani,zawadi  au  upendeleo  maalum  bali  ni  wajibu  uliozaliwa  na  sheria.
Sheria  ya  Ndoa  iliyofanyiwa  marekebisho  mwaka  2010 ,  sura  ya  29 imeweka  bayana  habari  nzima  ya  matunzo  baina  ya  wanandoa. Niseme  mapema  tu  kuwa...

 

11 months ago

Michuzi

JE MWISHO WA KUTOA MATUNZO YA MTOTO NI MIAKA MINGAPI ?.

Na  Bashir  Yakub.
Matunzo  ya  mtoto  hasa  kwa  wazazi  waliotengana  ni  pamoja na  chakula,  makazi,  mavazi,  elimu,  pamoja  na  malezi  bora. Wazazi  wote  kwa  pamoja  yaani  baba  na  mama  wanao wajibu   kila  mmoja  kwa  nafasi  yake kuchangia  katika   matunzo  ya  mtoto.


Aidha  makala  haya  kupitia Sheria  ya  Mtoto ,Na. 21  ya  2009   yatajibu  ikiwa  suala  kutoa  matunzo  ya  mtoto  ni  la  milele  au  linao  muda  maalum.  Lakini  kabla ya  hayo  tutizame  nani  ana ...

 

11 months ago

Michuzi

JE BABA ANATAKIWA KUTOA SHILINGI NGAPI ZA MATUNZO YA MTOTO ?

Image result for MATUNZO YA MTOTO
Na Bashir YakubWazazi  wanapokuwa  wametengana  matunzo  ya mtoto  ni  jambo  jingine  linaloleta    faraka  kubwa. Nani  anawajibu  wa  kutoa  matunzo  ya mtoto,  na  matunzo  yenyewe  ni  kiasi  gani  hubaki  kuwa  kiini  cha  ugomvi.


Wapo  wanaotoa  lakini  anayepewa  anasema  anapewa  kidogo.  Anayetoa  naye  anasema  natoa  kidogo  kwasababu  sina. Huyu  naye  anauliza  kama  huna  kwanini  ulizaa. Mambo  kama  hayo  na mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo.


Basi  katika  kupitia ...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani