(Today) 50 minutes ago

Michuzi

Mkurugenzi SBL afanya mazungumzo na maofisa Idara ya Uhamiaji

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie, jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

“Tukiwa kama kampuni inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla, tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie

SBL imeajiri...

 

2 days ago

Malunde

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Machi, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Lieberman Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Noah Gal Gendler, viongozi wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe....

 

2 days ago

Michuzi

RAIS MAGUFULI, WAZIRI WA ULINZI WA ISRAEL WAFANYA MAZUNGUMZO IKULU


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na ujumbe kutoka nchini Israel...

 

4 days ago

Michuzi

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA JIJINI DAR

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na balozi wa Italia nchini Tanzania Roberto Mengoni masuala mbalimbali ya uushirikiano baina ya Itali na Wizara ya mambo ya Ndani.Maongezi hayo yamefanyika leo katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam.

 

5 days ago

Michuzi

MWAKILISHI BENKI YA DUNIA AFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI MKUU,ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MRADI MABORESHO WA HUDUMA ZA KIMAHAKAMA

Na Mary Gwera, Mahakama
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Miradi ya Utawala Bora kutoka Benki ya Dunia (WB), Bi. Nicola Smithers ameipongeza Mahakama kwa utekelezaji wake wa Mradi wa Maboresho wa huduma za Kimahakama.
Bi. Smithers aliyasema hayo mapema Machi 19, alipokutana na Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam ambapo alipata nafasi ya kuongea na Mhe. Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama akiwemo Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wa Mahakama ya...

 

5 days ago

Michuzi

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI WAKUU WA KIWANDA CHA BIA TANZANIA BREWERIES LIMITED (TBL) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Ricardo Tadeu Rais wa Kampuni ya Anheuser-Busch InBev katika ukanda wa Afrika ambao ni Wanahisa wakuu wa Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Ltd kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango kabla ya kuanza kikao chake na Rais wa Kampuni ya...

 

6 days ago

BBCSwahili

Mkurugenzi wa FBI aliyefutwa kazi 'amwaga mtama' kuhusu mazungumzo na Trump

Naibu mkurugenzi wa zamani katika shirika la ujasusi nchini Marekani FBI Andrew McCabe ametoa barua kuhusu mazungumzo aliyokuwa nayo na rais wa Marekani Donald Trump

 

2 weeks ago

CCM Blog

SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO NA BHART AIRTEL

IKULU, DAR ES SALAAM
Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza rasmi leo tarehe 12 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo kamati iliyoundwa na Rais Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wake Mukesh Bhavnani.

Mazungumzo hayo yanalengo la kufikia...

 

2 weeks ago

Michuzi

SERIKALI YAANZA RASMI MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA BHARTI AIRTEL JUU YA UMILIKI WA AIRTEL TANZANIA

 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa  kampuni ya Bharti Bi. Tina Uneken-van de Vreede akiwa ameongozana na mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo Bw. Mukesh Bhavnani pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano walipowasili kwa ajili ya kuanza rasmi kwa mazungumzo kati ya Serikali na kampuni hiyo kwa lengo la kufikia makubaliano yatayokuwa na tija kwa pande zote mbili kuhusu umiliki wa Airtel Tanzania...

 

2 weeks ago

BBCSwahili

Trump: Mazungumzo na Korea Kaskazini yatakuwa makubwa kwa dunia

Lakini amesema ataacha mazungumzo hayo kwa haraka ikiwa hayataangazia suala la kuharibu silaha za nyuklia

 

2 weeks ago

Malunde

RAILA ODINGA NA RAIS KENYATTA WAFANYA MAZUNGUMZO YA KUFANYA KAZI PAMOJA

Kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Kenya uliofanyika October 2017, na kuleta mkanganyiko mkubwa wa kisiasa nchini humo, Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani wa NASA Raila Odinga leo March 9, 2018 wamekutana rasmi na kuzungumza.

Viongozi hao wamekutana na kuzungumza kuhusu kuacha tofauti zao za kisiasa na kutanguliza maslahi ya wananchi wa nchi hiyo kwanza kwa kufanya kazi pamoja kurudisha amani.

“Maisha yetu ya baadaye hayawezi kupimwa kwa Uchaguzi Mkuu unaofuata bali...

 

2 weeks ago

VOASwahili

Kenyatta, Odinga wafanya mazungumzo

Rais wa Kenya na kiongozi wa upinzani nchini Kenya kwa pamoja wameahidi kuanza mchakato wa kutafuta suluhu baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.

 

3 weeks ago

VOASwahili

Olympic yafungua mazungumzo kati ya Seoul, Pyongyang

Ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Korea Kaskazini Moon Jae-in umeripotiwa kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un Jumatatu.

 

3 weeks ago

Michuzi

WIZARA ZA UJENZI ZANZIBAR, TANZANIA BARA ZAFANYA MAZUNGUMZO ZANZIBAR

 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji, Mustafa Aboud Jumbe akisisitiza jambo katika Mkutano wa mashirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji(SMZ) na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi (SMT) uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Zanzibar. Kushoto ni  Katibu Mkuu  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(SMT), Dkt. Leornard Chamuriho. Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Mkutano wa mashirikiano kati ya Wizara ya...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani