3 days ago

RFI

Mbowe: Lissu anaendelea vizuri na huenda akaruhusiwa kuondoka hospitali wiki ijayo

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ameondolewa katika chumba mahututi, na huenda akaruhusiwa kwenda nyumbani wiki ijayo, kwa mujibu watu wa karibu yake.

 

3 days ago

Zanzibar 24

“Tundu Lissu kutolewa Hospitali wiki inayo fuata” Mbowe

Mbowe amewaambia wanahabari kwamba kwa mujibu wa madaktari, hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu imeimarika hivyo wakati wowote kuanzia wiki ijayo anaweza kutolewa hospitali.

“Bw Lissu ametolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuwekwa katika wodi ya kawaida huku akiwa na uwezo kamili wa kuongea na kutembea kwa kutumia kiti cha magurudumu,” alifafanua Mbowe. Hata hivyo, Chadema imesema kuwa, kwa kuhofia usalama wa Lissu, kwa sasa hawatamrudisha nchini Tanzania.

“‘Kwa sababu...

 

4 days ago

BBCSwahili

Mbowe: Tundu Lissu kutoka hospitali wiki ijayo

Mwenyekiti wa chama cha upinzani Tanzania, Chadema Freeman Mbowe amewaambia wanahabari kwamba Tundu Lissu anategemea kutolewa hospitalini wiki ijayo

 

4 days ago

Zanzibar 24

Mbowe- Matibabu ya awamu ya tatu ya Tundu Lissu yatafanyika nje ya nchi

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki  mh. Tundu Lissu sasa imezidi kuimarika na kusema atasafirishwa kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.

Mbowe amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya chama hicho, alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya Tundu Lissu na kusema mpaka sasa Mbunge huyo anaendelea vizuri na kudai amefanyiwa upasuaji mara 17.

“Tundu Lissu...

 

1 week ago

CHADEMA Blog

KAULI YA MWENYEKITI WA CHADEMA MHE FREEMAN MBOWE BAADA YA KAULI YA KARDINALI PENGO KUHUSU SUALA LA KATIBA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo kuhusu mchakato wa Katiba imewasikitisha.Wakati Mbowe akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maadili, amani na haki za binadamu kwa jamii ya madhehebu ya dini zote Tanzania, Askofu William Mwamalanga amemshauri Rais John Magufuli kuufufua

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Taarifa ya Bunge baada ya kuchukuwa gari ya kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe

Taarifa iliyotolewa na Bunge jana Alhamisi imesema kuwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe hajanyang’anywa gari kama inavyosemekana na badala yake gari hilo limechukuliwa na bunge na limerudishwa nchini ili dereva afuate utaratibu wa kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi. Bunge limesema ni kweli gari lenye namba ya usajili STL 4587 aina ya Toyota Prado limetengwa maalumu kwa ajili ya kumuhudumia Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika kutekeleza majukumu...

 

3 weeks ago

Malunde

BUNGE LATOA UFAFANUZI KUHUSU GARI LA MBOWE

Ofisi ya Bunge imesema Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe hajanyang’anywa gari.

Taarifa iliyotolewa na Bunge jana Alhamisi imesema kilichotokea ni kwamba, gari hilo limerudishwa nchini ili dereva afuate utaratibu wa kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi.

Mbowe yuko Nairobi nchini Kenya ambako Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anaendelea na matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Bunge...

 

3 weeks ago

Malunde

MBOWE ANYANG'ANYWA GARI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimesikitishwa na hatua ya uongozi wa Bunge la Tanzania ya kulichukua gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe alilokuwa akilitumia kwa shughuli za matibabu ya Tundu Lissu jijini Nairobi.
Chadema imesema Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai, aliamuru gari hilo lipelekwe Nairobi kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa chama hicho
Lissu ambaye pia Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS),...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Hemedi Ali- Freeman Mbowe anyang’anywa gari

Mkuu wa idara ya Uenezi CHADEMA, Hemedi Ali amefunguka na kusema gari ambayo Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alipewa na Bunge kwa ajili ya mizunguko mbalimbali ambayo pia ilikuwa akiitumia Nairobi kwenye matibabu ya Lissu imenyang’anywa na Bunge

Akiongea kutokea Nairobi, Hemedi Ali amesema kuwa haoni dhamira ya dhati ya Bunge hilo kusema lipo tayari kumtibu Tundu Lissu ikiwa wamepokonya gari ambayo Kiongozi wa Kambi rasmi Bungeni alikuwa akiitumia kwenda na kurudi Nairobi kwenye matibabu...

 

3 weeks ago

MwanaHALISI

Spika Ndugai apora gari la Mbowe

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Bunge la Tanzania limeamuru kurudishwa nchini gari linalosaidia kumhudumia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) aliyelazwa nchini Kenya akipatiwa matibabu ya majeraha ya risasi aliyoyapata aliposhambuliwa na watu wasiojulikana mjini Dodoma Sptemba 7 mwaka huu, anaandika Mwandishi Wetu. Gari hilo linatumiwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ...

 

4 weeks ago

Malunde

OFISI YA BUNGE YAMJIBU MBOWE KUHUSU MILIONI 43 ZA WABUNGE KWA AJILI YA TUNDU LISSU

Ofisi ya Bunge imesema fedha zilizochangwa na wabunge Sh.43 milioni kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu zimetumwa katika akaunti ya Hospitali ya Nairobi anakopatiwa matibabu.

Bunge limetoa taarifa kwa umma leo Ijumaa saa chache baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kueleza fedha hizo hazijatumwa.

Katika taarifa hiyo, Bunge limesema fedha hizo zimetumwa Septemba 20 kupitia Benki ya Barclays,...

 

4 weeks ago

Malunde

MBOWE AISHANGAA SERIKALI KUTAKA KUMTIBU TUNDU LISSU

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemshangaa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuwa Serikali iko tayari kumtibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu popote duniani.

Mbowe ametoa mshangao huo leo Ijumaa alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matibabu ya Lissu yanayoendelea jijini Nairobi.

Amesema wakati walipoamua kumpeleka Lissu jijini Nairobi, Waziri Ummy alikuwepo lakini walitaka Lissu apelekwe Muhimbili.

Mbowe amesema wanachama, watu mbalimbali wamechangia matibabu ya Lissu ikiwa ni hata...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani