(Today) 1 hour ago

Michuzi

DKT. MOLLEL ASHINDA UBUNGE SIHA MKOANI KILIMANJARO

Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia mgombea wake Dkt Godwin Mollel kimeshinda kiti cha ubunge katika jimbo la Siha baada ya kupata kura 25,611 sawa na asilimia 80 akimshinda mpinzani wake Elvis Mosi (Chadema) aliyepata kura 5,905 sawa na asilimia 18.5.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Cheti cha uthibitisho kwa kuchaguliwa kwake,Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo Valerian Juwal amesema mgombea Tumsifueli Mwanry (CUF)  amepata kura 274 sawa na asilimia 0.9 huku mgombea wake chama cha Sauti ya...

 

(Yesterday)

Michuzi

POLISI NA CRDB WATOA ELIMU KWA WANANCHI MKOANI LINDI JUU YA WIZI KATIKA MITANDAO

 Jeshi la Polisi kitengo cha Polisi Jamii kutoka Polisi Makao Makuu Dar es salaam likiongozwa na Naibu Kamishina wa Polisi  DCP Ahmada Khamis, pamoja na Maafisa kutoka Bank ya CRDB wametoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha katika  mitandao na matumizi salama ya huduma mbalimbali za kibank. Naibu Kamishina wa Polisi  DCP Ahmada Khamis akitoa  elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi Wilaya ya Ruangwa kata ya Nkowe  juu wa wizi wa fedha...

 

2 days ago

Michuzi

MAHAKAMA YAANZA UJENZI WA MAHAKAMA TATU MKOANI GEITA

Na Lydia Churi-Geita.
Katika kutekeleza dhamira yake ya kuboresha huduma za Mahakama na kusogeza huduma hizo karibu zaidi na wananchi, Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imeanza rasmi ujenzi wa majengo matatu ya Mahakama katika mkoa wa Geita pamoja na wilaya zake za Bukombe na Chato.
Ujenzi wa Mahakama hizi ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2015/16 hadi 2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao ulianza...

 

3 days ago

Michuzi

MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA MAJENGO YA MAHAKAMA MKOANI MARA

Pichani ni muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Robanda lililopo Serengeti wilayani Mugumu, jengo hili lilijengwa kwa nguvu za wananchi na kumaliziwa na Mahakama ya Tanzania lilikabidhiwa rasmi tayari kwa matumizi Januari 26, 2018, uwepo wa jengo hili utasaidia kuwapunguzia wananchi aza ya kusafiri kilomita zipatazo 40 kwenda Mahakama ya Mwanzo Serengeti kutafuta haki zao.Maafisa Tawala wa Mahakama mkoani Mara wakionyesha baadhi ya ofisi za jengo hilo; hapo ni sehemu ya ukumbi wa...

 

3 days ago

Michuzi

KWANDIKWA AKAGUA MIRADI YA UJENZI MKOANI TANGA

Diwani wa Kata ya Mombo, Halima Mussa akizungumza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (wa pili kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya sekta ya ujenzi ikiwemo barabara katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Mombo ikiwemo stendi ya Mombo jana Jumatano Februari 14, 2018. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen NgonyanNaibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (katikati) akiongozwa na Mbunge wa Korogwe Vijijini,...

 

5 days ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAJUMUISHO YA ZIARA YAKE MKOANI IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Iringa kushirikiana ili kuweza Kuwasaidia wananchi.Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kutoa majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais alitembelea wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi ambako kote alishiriki shughuli za kimaendeleo ikiwa kuzindua Vituo vya Afya Kising’a wilaya Iringa, Jengo la Utawala na Madarasa katika Shule ya ...

 

5 days ago

Malunde

MENEJA OFISI YA TAKWIMU MWANZA GOODLUCK LYIMO AAINISHA IDADI YA KAYA ZANAZOFANYIWA UTAFITI WA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI 2018/2019 MKOANI MWANZA

Meneja wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mkoani Mwanza, Goodluck Lyimo amebainisha idadi ya kaya zinazofanyiwa zoezi la utafiti wa Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara 2017/2018 mkoani Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, meneja huyo amelima kuwa, zoezi hilo linahusisha jumla ya kaya 408 mkoani Mwanza ambapo tayari Kaya 68 zimekamilisha mahojiano, Kaya 30 zinaendelea na mahojiano na kwamba hadi kufikia februari 28 mwaka huu Kaya 98 zitakuwa zimekamilisha mahojiano hayo. 

"Zoezi hili...

 

6 days ago

Michuzi

MRADI ORIO MUARUBAINI TATIZO LA UMEME MKOANI KATAVI

 NA SAMIA CHANDE, KATAVI.

Mradi wa Orio uliotekelezwa kwa ushirikiano wa  Serikali ya Uholanzi na Tanzania  kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umesaidia kujenga kituo cha kuzalisha umeme chenye uwezo wa Megawati 2.5 ambazo zimesaidia  kumaliza tatizo la umeme Wilaya ya  Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Meneja wa TANESCO Mkoani  Katavi, Mhandisi Julius Sabu, kituo hicho kimesaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo, na kutoa umeme wa uhakika na wenye...

 

1 week ago

Michuzi

WILAYA YA TUNDURU YAPIGWA JEKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA NAKAYAYA MKOANI RUVUMA

 Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Juma Homera kulia, akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 25 kutoka kwa  meneja mawasiliano wa Shirika la maendeleo la Petroli Nchini(TPDC) Marie Msellemu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya wilayani humo. Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera katikati na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya  hiyo Chiza Malando kulia,wakifurahia mfano wa Hundi ya shilingi milioni 25  iliyotolewa na Shirikala maendeleo ya Petroli...

 

1 week ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS KATIKA SIKU YA PILI WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo mkoani Iringa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah akisoma taarifa ya wilaya yake mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati ziara ya Makamu wa Rais wilayani Kilolo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa...

 

1 week ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya siku nne mkoani Iringa ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo na kuzindua mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania – REGROW.

Mara baada ya kuwasili mkoani Iringa , Makamu wa Rais alifungua wodi mpya katika Zahanati ya Kising’a ambapo aliwaomba wananchi wote wajiunge na mfuko wa bima ya Afya ili waweze kunufaika na huduma bora za afya.“niwaombe sana...

 

1 week ago

Michuzi

TANZIA: Mfanyabiashara maarufu mkoani Kigoma, Carole P. Mtei afariki dunia

Mfanyabiashara maarufu mkoani Kigoma, Carole P. Mtei amefariki tarehe 04/02/2018 katika hospitali ya Rabininsia, Tegeta jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa ykimsumbua. 

Mwili wa Marehemu Mtei unatarajiwa kuagwa leo Alhamisi 08/02/2018 katika Hospitali ya Lugalo na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwao Marangu, Moshi kwa Mazishi yatakayofanyika siku ya Jumamosi 10/02/2018. habari ziwafikie Ndugu, Jamaa na Marafiki wote wa Familia ya Mtei popote pale...

 

2 weeks ago

Michuzi

JESHI LA ZIMAMOTO MKOANI ARUSHA LAMUUNGA MKONO JPM

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Arusha limemkabidhi vifaa vya kuzimia moto (fire extenguisher’s) sita mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya nyumba za polisi zilizojengwa mkoani humo.
Akikabidhi vifaa hivyo kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamanda, Kennedy Komba amesema Jeshi hilo lina wajibu wa kuhakikisha ujenzi wa nyumba za makazi unazingatia vigezo vyote vya usalama, wao...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani