8 months ago

Michuzi

WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingra Januari Makamba amesema watawasiliana na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuangalia namna ya kupandisha hadhi Muungano kupitia mtaala wa somo la uraia ambalo linafundishwa shuleni.
Januari Makamba amesema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo moja ya swali liliuliza kuna mkakati gani wa kuwa na mtaala wa somo la Munungano ambalo litajikita kuelezea kwa kina...

 

9 months ago

BBCSwahili

Serikali ya muungano wa vyama yashindikana Italia

Mazungumzo ya muungano wa vyama nchini Italia yameshindikana,hivyo kuiacha nchi ikitakiwa kufanya uchaguzi mpya ama kuwa na serikali ya mpito hadi mwishoni mwa mwaka huu.

 

9 months ago

Michuzi

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA WAADHIMISHA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANZANIA

 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akikata keki ya sherehe ya Muungano na Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt. Adel Al Jubail.
Ubalozi wa Tanzania nchini uliadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanzania mjini Riyadh kwa sherehe iliyojumuisha jumuiya wa wanadiplomasia, Watanzania na Wanadiaspora waishio nchini Saudi Arabia. Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza(kulia) akizungumza jambo na Naibu Gavana wa Jiji la Riyadh Dkt....

 

9 months ago

Michuzi

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA ULIVYADHIMISHA SIKU YA MUUNGANO

Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akimpokea Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Tanzania iliyofanyika jijini New Delhi tarehe 26 Aprili 2018.  Mhe. Baraka Luvanda (kulia), Balozi wa Tanzania nchini India akiwa katika mazungumzo na Mhe. Shri Vijay Goel, Waziri wa Nchi, Masuala ya Bunge na Takwimu wa India kabla ya kuanza rasmi kwa hafla ya kuadhimisha Siku ya Muungano wa Tanzania. ...

 

9 months ago

BBCSwahili

Mitaa ilivyo katika maadhimisho ya Muungano Tanzania

Tazama picha za maeneo tofuati nchini Tanzania asubuhi hii wakati taifa hilo linaadhimisha miaka 54 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana

 

9 months ago

Michuzi

WANAFUNZI WA TANZANIA WANAOSOMA CHUO KIKUU CHA SHARDA INDIA WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO


Na Emmanuel Masaka, Globu ya jamii
WANAFUNZI wa kitanzania wasoma katika Chuo kikuu cha Sharda nchini India jana Aprili 26 wamesherekea Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hiyo ni katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano.
Sherehe hiyo imefanyika kupitia kampuni ya Global Education link inayohusika na masomo ya elimu ya juu nje ya nchi ambapo wanafunzi wa kitanzania wanaosoma katika chuo hicho kupitia kampuni ya Gobal Education link ya nchini Tanzania sambamba na viongozi na...

 

9 months ago

Michuzi

Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya waadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akiwakaribisha wageni waalikwa katika ufunguzi wa siku ya Tanzania ambayo huadhimishwa tarehe 26 Aprili siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hafla ya maadhimisho hayo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta Jijini Nairobi, Kenya.  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Ababu Namwamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar akihutubia wageni...

 

9 months ago

Michuzi

SHEREHE YA MCHAPALO YA KUSHEREHEKEA MIAKA 54 YA MUUNGANO YAFANA WASHINGTON, DC

Balozi Mhe. Wilson Masilingi akisoma hotuba yake.aliyelezea mambo mbalimbali ikiwemo kuitangaza Tanzania katika maswala ya utalii ikiwemo uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani. Katika hotuba hiyo Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliongelea jinsi ya nchi ya Tanzania ilivyokua na amani na salama kwa watalii kwenda Tanzania kwenda kujionea vivutio mbalimbali na katika kuimarisha utalii, Serikali ya awamu ya tano chini ya Rasi Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amenunu ndege sita za usafiri...

 

9 months ago

Zanzibar 24

JPM aahidi kushirikiana na Dkt. Shein kulinda Muungano

Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi wa Tanzania  kuulinda muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa gharama  yoyote  kwa kushirikiana  kwa hali na mali na  Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein.

Amesema  serikali  hizo hazitamvumilia  mtu yoyote  awe wa ndani ya nchi au nje ya nchi  mwenye nia ya  kutaka kujaribu kuuvunja muungano  kwani serikali zote zipo imara katika kulinda  na kutunza amani inayotokana  na uwepo wa...

 

9 months ago

Malunde

UVCCM KIGOMA,BODABODA WAENZI MUUNGANO KWA MCHEZO...DC JENERALI GAGUTI AFUNGUKA


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti amewapongeza vijana wa Kigoma kwa kitendo walichokifanya cha kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26 kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi na bodaboda bila kujali itikadi za vyama vyao.

Pongezi hizo alizitoa jana mara baada ya mchezo huo uliofanyika katika viwanja vya Kawawa Manispaa ya Kigoma Ujiji, wakati akitoa zawadi kwa washindi  ambapo vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM waliibuka...

 

9 months ago

Malunde

MAGUFULI : YEYOTE ATAKAYEJARIBU KUUCHEZEA MUUNGANO TUTAMSHUGHULIKIA VIKALI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu yeyote ataye jaribu kuuchezea muungano atashughulikiwa vikali hata kama atakuwa nje ya nchi.

Ameyasema hayo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo amesema kuwa kuna watu ambao hawapendi muungano uwepo lakini watu hao ni wa kupuuzwa.

Amesema kuwa muungano ni kitu kikubwa cha kujivunia hivyo Watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na...

 

9 months ago

Michuzi

RAIS DKT. MAGUFULI AWAONGOZA MAELFU YA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZILIZOFANYIKA MKOANI DODOMA

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kwenda kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la...

 


Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani