4 days ago

Michuzi

MWANAFUNZI UDOM ANAOMBA MSAADA WA MASOMO

MWANAFUNZI wa Shahada ya Sheria mwaka wa Kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Amaniel Furahini(21) ameiomba serikali na watanzania kumsaidia kulipa ada ili aweze kuendelea na masomo yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Mwanafunzi huyo amesema amekuwa akisoma katika mazingira magumu kutokana na kukosa ada huku akidai kuwa wazazi wake hawana uwezo wa kumsomesha kwa kuwa ni wakulima wanaotegemea mvua za msimu wilayani Same.

Amesema alipochaguliwa kujiunga na ...

 

5 days ago

Malunde

ASKARI AFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI KWENYE KITUO CHA POLISI TABORA


ASKARI Polisi wa Kituo Kidogo cha Lukula katika Kata ya Kitunda wilayani Sikonge, mkoani Tabora Je basa Charles amekamatwa na jeshi hilo akituhumiwa kukutwa na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwele akifanya mapenzi kituoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Machi 15, mwaka huu, Diwani wa Kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkoani Tabora, Mbwana Seif alisema askari huyo walimfanyia mtego na mzazi wa mwanafunzi Farida Juma kituoni hapo kwa muda wa siku tatu na kufanikiwa...

 

1 week ago

Michuzi

POLISI DAR WABAINI MWANAFUNZI ALIYEDAI KUTEKWA KUMBE ALIKUWA KWA MPENZI WAKE

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

*Mambosasa asema watamchukulia hatua za kisheria, atoa onyo kali
Na Said Mwishehe, Globu ya jamiiKAMANDA wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Abdul Nondo(24), aliyedai kutekwa  na watu wasiojulikna siku za karibuni uchunguzi wao umebaini kumbe alikwenda kwa mpenzi wake mkoani Iringa.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mambosasa amefafanua Machi 6 mwaka huu ,kuanzia...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Uchunguzi wa Polisi umekamilika sakata la Mwanafunzi kupotea na kuonekana Iringa

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa ufafanuzi kuhusu kile kinachoitwa kutekwa kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Nchini TSNP, Abdul Nondo.

Akizungumza na Wandishi wa Habari Kamanda wa polisi  Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mnamo Machi 7, mwaka huu walipokea taarifa kutoka kwa wenzao wa Iringa ambapo walithibitisha kupatikana kwa mwanafunzi huyo akiwa mzima huku akiwa hajaripoti kituo chochote cha Polisi.

Mambosasa amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kwa...

 

2 weeks ago

Michuzi

MWENYEKITI UWT AMZUNGUMZIA MWANAFUNZI CHUO KIKUU DAR ANAYEDAI AMETEKWA


*Amtaka aache kutafuta kiki kwa staili hiyo,awapa somo vijana wa kitanzania

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) Gaudentia Kabaka amewataka vijana wote nchini kuacha tabia ya kuichafua Serikali kwa kujifanya wanatekwa kwani madhara yake ni makubwa.
Amesema vijana wa kitanzania wanatakiwa kusoma kwa bidii ili waweze kuisaidia nchi yao katika kuleta maendeleo badala ya kutafuta kiki za kitoto.
Kabaka ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumzia madai ya...

 

2 weeks ago

Malunde

MWANAFUNZI WA UDSM ANAYEDAIWA KUTEKWA NA WASIOJULIKANA AFIKISHWA POLISI


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akizungumza
MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amefikishwa makao makuu ya Polisi Mkoa wa Iringa Mjini Iringa kwa mahojiano zaidi wakati jeshi hilo likiendelea na uchunguzi wa taarifa zake za kutekwa na watu wasiojulikana mapema wiki hii.

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu wa kitivo cha Siasa na Utawala cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha Jumanne usiku akiwa jijini Dar...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Polisi wazungumzia sakata la Mwanafunzi kupotea na kupatikana Iringa

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limeeleza kuwa limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama Mwenyekiti wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omari Nondo alikuwa ametekwa au la ili liweze kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akiongea na waandishi wa habari ameeleza kuwa bado uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea ili waweze kubaini kama ni kweli ametekwa na kuwakamata wahusika kwa ajili ya kuwachukulia hatua zaidi za...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Mwanafunzi aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha apatikana

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) aliyeripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.

Imeelezwa kuwa, Nondo alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo hilo kuwa hapo ni wapi? Wenyeji hao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa katika kituo cha polisi kilichopo...

 

2 weeks ago

BBCSwahili

Mwanafunzi aliyetekwa apatikana akiwa hajitambui

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana

 

2 weeks ago

Michuzi

KAMPUNI YAMPA BAISKELI MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA ILI ATIMIZE NDOTO YAKE

Na Mwandishi wetuKAMPUNI ya D&G Export Company Ltd inayojishughulisha na ununuzi wa mazao na utunzaji wa korosho wilayani Tunduru na Liwale imeamua kumsaidia baiskeli ya magurudumu matatu mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Msingi Kichangani Shaibu Mpoto.
Mwanafunzi huyo alishindwa kuendelea na masomo yake baada ya kupata ugonjwa  wa kupooza miguu, miaka minne iliyopita jambo ambalo lilimfanya kuwa na wakati mgumu kuendelea na masomo lakini  kupatikana kwa baiskeli hiyo kutarudisha ndoto...

 

3 weeks ago

BBCSwahili

Mauaji ya Baraka: Shirika lataka ukweli kuhusu mauaji ya mwanafunzi Manzania Baraka Naferi Afrika Kusini

Wanachama wa Shirika la Africa Diaspora Forum wamefanya mandamano nchini Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi hiyo na serikali ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa Tanzania mwezi jana.

 

3 weeks ago

VOASwahili

Mwanafunzi auwawa kikatili Afrika Kusini

Mwanafunzi wa Tanzania aliyekuwa akisoma nchini Afrika Kusini ameuwawa kikatili Ijumaa nchini humo.

 

3 weeks ago

Malunde

MWANAFUNZI WA KITANZANIA AFARIKI KWA KUGONGWA GARI NA WASIOJULIKANA AFRIKA KUSINI


Mwanafunzi wa Kitanzania aliyekuwa akisoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ), Afrika Kusini, Baraka Nafari amefariki dunia kwa kugongwa na gari na watu wasiojulikana akitokea katika matembezi ya usiku.

Uwezo Edward, ambaye ni binamu wa Baraka anayeishi Afrika Kusini amesema hana uhakika iwapo ndugu yake alikuwa na adui au ugomvi na mtu, lakini mazingira ya kifo chake yana utata.
Akizungumza na MCL Digital leo Machi 2, 2018, Edward amesema Baraka ataagwa Jumanne...

 

3 weeks ago

Malunde

Breaking : MWANAFUNZI KIONGOZI WA CHUO KIKUU APIGWA RISASI

Kifo cha Mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini Kenya kimezuaa shutuma mpya za mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi nchini humo.


Ripoti zinasema Evans Njoroge, mwanafunzi ambaye alikua kiongozi Chuo kikuu cha Meru nchini humo, aliuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa polisi.
Mwandishi wa BBC, Ferdinand Omondi anasema pichaza mwili wa kijana huyo, damu yake ikionekana imetapakaa kote, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku raia wa Kenya wakighadhabishwa na kile...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Mfanyakazi wa Bunge atuhumiwa kutaka kumlawiti Mwanafunzi

Mwanafunzi wa chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya amemfungulia mashtaka mfanyakazi wa Bunge la nchi hiyo, kwa kutaka kumlawiti.

Mfanyakazi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake, ametajwa kutaka kumlawiti mwanafunzi wa kiume, kwenye maeneo ya ofisi za bunge.

Kwenye maelezo yake mwanafunzi huyo amesema kwamba afisa huyo alimfuata na kumwambia yeye ni Afisa wa Polisi, na kumchukua mpaka ndani ya majengo ya bunge, na kuanza kumfanyia vitendo hivyo...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani