(Yesterday)

Michuzi

Mwanri awatangazia kiama wale wanaoshiriki kula ubwabwa na kusherekea ndoa za watoto wadogo

NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametanga kiama kwa watu wote wanaoshiriki kuwaoza watoto wadogo wakiwemo wa Shule kwa kuwakata na kuwafikisha Mahakamani ili waweze kuadhibiwa.
Hatua hiyo inalenga kukomesha mimba na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike ikiwa ni sehemu ya kutetea haki za watoto wa kike kupata elimu kama walivyo wavulana na vile kuokoa maisha yao ambayo yanaweza kupotea wakati wa kijifungua kwa kuwa bado ni wadogo.
Mwanri alitoa amri hiyo jana katika vijiji...

 

2 days ago

Malunde

ALISHTAKI KANISA KWA KUMPA MASHARTI MAGUMU YA KUFUNGA NDOA

Aboneka amesema vijana wengi wananyimwa haki yao kikatiba kufunga ndoaMwanaume mmoja ameshitaki kanisa moja nchini Uganda akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.
Michael Aboneka amepeleka kesi hiyo katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki kanisa la Watoto Church wakati waumini wengine wa kanisa hilo wakiunga mkono taratibu za kanisa lao.
Michael Aboneka amesema kuwa Watoto Church, linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya...

 

2 days ago

Zanzibar 24

Alishitaki Kanisa akipinga masharti yaliyowekwa ili kufunga ndoa

Mwanaume mmoja ameshitaki kanisa moja nchini Uganda akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.

Michael Aboneka amepeleka kesi hiyo katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki kanisa la Watoto Church wakati waumini wengine wa kanisa hilo wakiunga mkono taratibu za kanisa lao.

Michael Aboneka amesema kuwa Watoto Church, linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya kufunga ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka 18 kama katiba...

 

2 days ago

BBCSwahili

Alishtaki kanisa Uganda kwa kumuekea masharti makali ya kufunga ndoa

Michael Aboneka amepeleka kesi katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki kanisa la Watoto Church akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa wa kanisa hilo aanaosema unakwenda kinyume na katiba.

 

4 days ago

Zanzibar 24

Utafiti: Huu ndio umri sahihi wa kufunga ndoa

Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Utah kilichopo nchini Marekani imebainisha kwamba watu ambao wamefunga ndoa kati ya umri wa miaka 28 mpaka 32 wamekuwa na ndoa yenye mafanikio zaidi.

Utafiti huo umebainisha kwamba ndoa ambazo zipo katika hatari ya kuvunjika ni zile ambazo mmoja wa wanandoa ana umri wa chini ya miaka 20 na wale waliofunga ndoa wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 45 na kuongeza kuwa ndoa hizo hazijadumu zaidi ya miaka mitano.

Taarifa za utafiti huo...

 

1 week ago

BBCSwahili

Najuta kufunga ndoa Ramadhani ikiwa karibu

Mwezi mtukufu wa Ramadhani unatajwa kuwa ni mwezi wenye neema ambapo, familia hujumuika kwa pamoja katika swala na chakula

 

1 week ago

Michuzi

SHEIKH WA MKOA DAR ASHAURI WALIOFUNGA NDOA KUELEKEA MWEZI WA RAMADHANI WASIBEZWE, BALI WAPEWE MOYO KWANI NI JAMBO JEMA

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema vijana wa Kiislamu ambao wamefunga ndoa wakati wa kuelekea mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wanatakiwa kupongezwa na kupewa moyo badala ya kuwabeza na kuwakejeli kwa uamuzi wao wa kufunga ndoa.
Sheikh Alhad ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambao umeanza leo kwa waumini wa dini hiyo kuanza kutekeleza moja ya nguzo za Kiislamu.
Hivyo...

 

2 weeks ago

BBCSwahili

Wawili wasio na uwezo wa kusikia na kuzungumza wafunga ndoa Kenya

Kaskazini Mashariki mwa Kenya kumefanyika harusi ya kipekee baada mvulana na msichana walio na ulemavu wa kusikia na kuongea kufunga ndoa.

 

2 weeks ago

BBCSwahili

Kwanini ndoa zinakithiri wakati Ramadhani?

Siku chache zikiwa zimesalia ili kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ndoa za haraka haraka zimekuwa zikishuhudiwa. Kulikoni?

 

2 weeks ago

Malunde

Mapenzi huota Popote!! NDOA YA AINA YAKE YAFUNGWA LINDIBahati Ramadhani akiwa amembeba mumewe Jivunie Mbunda katika harusi yao iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Picha na Jackline Masinde **
Ndoa ya Jivunie Mbunda na Bahati Ramadhani inadhihirisha usemi usemao ‘mapenzi sawa na majani huota popote.”

Wawili hao walifunga ndoa juzi mjini Liwale mkoani Lindi na kuvuta hisia za wengi.

Mbunda (35) mwenye ulemavu uliosababisha kuwa na kimo kifupi alifunga pingu za maisha na Bahati (25), mkazi wa Newala mkoani Mtwara aliyemzidi mumewe urefu kama mara tatu...

 

3 weeks ago

Malunde

SHAMSA FORD AMJIA JUU HARMONIZE KUINGILIA NDOA YAKE

Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Filamu  Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.

Siku ya jana Wolper, Harmonize na Sarah walikuwa kwenye vita kali ya Kwenye mitandao ya kijamii na katika harakati hizo Harmonize alianika orodha nzima ya wanaume ambao Wolper amewahi kujivinjari nao na mmoja kati ya watu hao ni Chidi Mapenzi.

Chidi Mapenzi ni mume halali kabisa...

 

3 weeks ago

BBCSwahili

Raia wa kigeni wanunua ndoa nchini Costa Rica

sababu za raia wa Costa Rica hulipwa pesa na wachina ili kufunga ndoa

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Mwandishi wa vitabu maarufu atangaza kufunga ndoa na mwanaume mwenziwe

Mwandishi vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina ambaye ametangaza wazi kwamba ni mpenzi wa jinsia moja amefichua kwamba atafunga ndoa mwaka ujao.

Mwandishi huyo ambaye alifichua hali yake ya kimapenzi mwaka 2014 siku yake ya kuzaliwa, amesema harusi hiyo itafanyika nchini Afrika Kusini.

“Nilimuomba mpenzi wangu tufunge ndoa wiki mbili zilizopita. Na alikubali, karibu mara moja. Yeye ni raia wa Nigeria. Tutakuwa tunaishi Afrika Kusini ambapo atakuwa anahudhuria masomo mwaka ujao....

 

3 weeks ago

BBCSwahili

Binyavanga Wainaina: Mkenya mpenzi wa jinsia moja kufunga ndoa na raia wa Nigeria

Mwandishi vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina ambaye ametangaza wazi kwamba ni mpenzi wa jinsia moja amefichua kwamba atafunga ndoa mwaka ujao.

 

4 weeks ago

Michuzi

MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI BADO TISHIO RUKWA


Na Anthony Ishengoma-Wizara ya Afya. 
Mkoa wa Rukwa kwasasa huna jumla ya kesi 256 zinazohusiana na mimba kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari na Msingi. 
Akiongea katika Mkutano uliondaliwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na Ofisi ya Mkoa wa Rukwa kwa madereva bodaboda kuhusu mimba na ndoa za utotoni Kaimu KatibuTawala Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Abubakari Kunenge amesema idadi ya kesi hizi imepatikana kwa kipindi cha miezi tisa kwa mwaka 2017/18. 
Aidha Bw....

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani