1 day ago

MwanaHALISI

Ndugai agomea milioni 43 matibabu ya Lissu.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ametua nchini akitokea nchini Kenya anapomuuguza Mbunge wa Singida Mashariki ( Chadema), Tundu Lissu na kufunguka kwamba Spika Job Ndugai amezuia Sh. milioni 43 zilizochangwa na wabunge kusaidia matibabu huku akivituhumu vyombo vya ulinzi na usalama kwamba vinahusika kumpiga risasi mbunge huyo, anaandika Hellen Sisya. ...

 

2 days ago

Michuzi

SPIKA JOB NDUGAI AHUDHURIA MAZISHI YA FAMILIA YA ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akiongoza viongozi Mbali mbali wa serikali katika misa ya kuaga miili ya familia ya aliekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, uliofanyika leo katika kanisa la Anglikana Tanzania (Dayosisi ya Mpwapwa)iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiweka Shada ya maua katika mazishi ya familia ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg. Gregory George Teu, yaliyofanyika leo katka...

 

4 days ago

Michuzi

SPIKA JOB NDUGAI MGENI RASMI KATIKA KONGAMANO LA MTANDAO WA WANAMAOMBI TANZANIA (APN).

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mchungaji Kelvin Ngaeje wa kanisa la Anglican baada ya kualikwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Mtandao wa wanamaombi Tanzania (APN) uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo kikuu cha St. John kilichopo Mjini Dodoma.Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto)akizungumza wakati akifungua Kongamano la Mtandao wa wanamaombi Tanzania (APN) lililofanyika leo katika ukumbi wa Chuo kikuu cha St. John...

 

1 week ago

Michuzi

SPIKA NDUGAI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE MJINI DODOMA

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Watumishi wa Bunge kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. kulia ni katibu wa Bunge, Dkt. Thomas kashililah, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mhe. Magdalena Sakaya (wa pili kulia) na kushoto ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge, Mhe. Mary Chatanda Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (hayupo kwenye picha) wakati wa kikao...

 

1 week ago

MwanaHALISI

Spika  Ndugai asema usalama Tanzania ni sifuri

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewataka wabunge kuwa makini pindi wawapo majimboni kwao au nje ya jimbo kutokana na hali ya usalama kutokuwa shwari hapa nchini, anaandika Dany Tibason. Ndugai alitoa rai hiyo kwa wabunge muda mfupi baada ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kuahirisha Bunge mjini Dodoma. Ndugai aliwataka wabunge hao kuwa makini muda wote ...

 

1 week ago

Michuzi

SPIKA JOB NDUGAI ATEMBELEWA NA BALOZI WA IRELAND NCHINI

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (katikati) na Mshauri Mwandamizi wa Serikali hiyo, Ndg. Aran Corrington,  pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akimsikiliza Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (katikati) na kulia ni Mshauri mwandamizi wa serikali hiyo, Ndg. Aran Corrington,  pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini...

 

1 week ago

MwanaHALISI

Filamu ya Ndugai na wabunge yaendelea Dodoma

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema  mbunge wa Ubungo Saed  Kubenea hajaitwa kwenye Kamati Ulinzi na Usalama ya Bunge kama mtuhumiwa wa kitu chochote, anaandika Hamis Mguta. Ndugai amesema hayo leo bungeni akieleza kauli iliyotolewa na Mbunge wa  Arusha Mjini,  Godbless Lema akimshtumu Spika kuhusu sababu za kuwaita mbunge Kubenea na Zittp Kabwe ...

 

1 week ago

Michuzi

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA BALOZI WA IRELAND NCHINI

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (katikati) na Mshauri Mwandamizi wa Serikali hiyo, Ndg. Aran Corrington, pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akiagana na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock (kulia) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia)akiagana na...

 

1 week ago

Michuzi

SPIKA JOB NDUGAI ATEMBELEWA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (kushoto) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. katikati ni Mwakilishi Mkazi wa DFID hapa nchini, Ndg. Beth Arthy. Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (katikati) na Mwakilishi Mkazi wa DFID hapa nchini, Ndg. Beth Arthy,  pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini...

 

1 week ago

Malunde

BUNGENI BALAA: SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AMCHIMBA MKWARA MZITO ZITTO KABWE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, amesema ana uwezo wa kumzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuzungumza mpaka mwisho wa bunge, kwani hawezi kupambana naye.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi kufanana naye na kila mtu ana muda wake, kama ambavyo Spika wa bunge aliyepita mama Anna Makinda...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Mapambano yaendelea dhidi ya Zitto Kabwe na Spika Ndugai

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Mh. Zitto Kabwe ameendelea na Spika wa Bunge Job Ndugai na kusema kuwa ameibuka na sakata lake yeye ili kutaka kufunika nguvu ya wananchi kuhoji juu ya kupigwa risasi  tundu Lissu.

Zitto Kabwe amesema hayo leo mara tu baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai leo bungeni kusema anauwezo wa kumzuia Mbunge huyo asizungumze bungeni hadi mwisho wa bunge hilo kwani Zitto hawezi kupambana naye.

“Nimegundua Spika Ndugai ameibua mashtaka yangu...

 

2 weeks ago

Malunde

ZITTO KABWE AMCHANA SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kuwa anamsikitikia sana kama haoni jinsi  heshima ya Bunge inavyoshuka.
Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge Zitto Kabwe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo...

 

2 weeks ago

MwanaHALISI

Ndugai kama Magufuli, hataki kuguswa

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ameagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, kuhakikisha inamsaka mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) na kumfikisha katika kamati hiyo kesho, anaandika Dany Tibason.  Mbali na Spika kumtaka mbunge huyo kufikishwa katika kamati hiyo pia mbunge mwingine ambaye ametakiwa kufika katika Kamati ya  ya Kudumu ya Bunge ...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Zitto Kabwe afunguka mazito kuhusu spika Job Ndugai

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kupitia mtandao wa kijamii kuwa anamsikitikia sana Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kama haoni jinsi heshima ya Bunge inavyoshuka.

kauli hiyo ameitoa leo mara baada ya Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano tanzania  Job Ndugai kuagiza wabunge Zitto Kabwe na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani