1 day ago

Michuzi

MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA KWENYE DVD PEMBA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limemkamata mwanamke mwengine akiwa na jumla ya kete 969 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya DVD.
Mwanamke huyo ambaye amekamatwa na wenziwe wawili wanaume katika maeneo ya PBZ Chake Chake anakuwa wa pili kukamatwa ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya Septemba 9 mwezi huu kukamatwa mwengine akiwa na jumla ya kete 3621.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Madungu Chake Cheke Kamanda wa Polisi Mkoa...

 

1 day ago

Zanzibar 24

Ratiba ligi kuu ya soka Zanzibar kituo cha pemba 2017

The post Ratiba ligi kuu ya soka Zanzibar kituo cha pemba 2017 appeared first on Zanzibar24.

 

2 days ago

Zanzibar 24

Watatu wabambwa na madawa yakulevya ndani ya DVD Pemba

Katika kuendeleza msako mkali wa madawa ya kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limewashikilia watuhumiwa watatu wakiwa na kete 969 za madawa ya kulevya yakiwa kwenye DVD.

Watuhumiwa hao ni Ali Nyoro Tilima (32), Asha Mohamed Yussuf (30) wote wakaazi wa Wawi Chake Chake na Salum Said Kombo (23) mkaazi wa Konde Wilaya ya Miceweni Pemba.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Sheikhan Mohamed Sheikhan alisema kuwa, tukio hilo lilitokea jana saa 11:00 jioni katika...

 

3 days ago

Zanzibar 24

Habari Picha: Waziri wa Afya akifungua Kituo cha Mkono kwa mkono Pemba

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, (kulia) akikata utepe kuashiria kukifungua Kituo cha Mkono kwa mkono, kilichopo hospitali ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, akiwa na Mratibu Mkuu wa masuala ya ulinzi na uhifadhi wa mtoto, kutoka shirika la Save Children Zanzibar Ramadhan Mohamed Rashid.

 

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo, akitembea kuelekea kwenye mazungumzo na wananchi, wanafunzi na madaktari wa Hospitali ya Micheweni, mara baada ya kukifungua Kituo...

 

4 days ago

Zanzibar 24

Vikoba vyanawirisha ndoa Vitongoji Chakechake Pemba

WANAWAKE wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, wamesema kujiunga kwao kwenye vikundi vya kuweka na kukopa, ‘hisa’ ni hatua muhimu kwao kuwasaidia waume zao huduma za kila siku, hasa kwa vile hutokezea siku wanakosa.

Walisema wanaume hawana mkataba na Muumba, kwamba kila siku watakuwa wanakamilisha hudua za ndani ya nyumba, hivyo kuingia kwao kwenye vikundi hivyo vya kuweka hisa, pamoja na mambo mengine, lakini pia ni kuwasaidia wenza wao huduma za lazima.

Wakizungumza...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Viongozi wafurahia mafunzo Pemba

Viongozi wa dini, Viongozi wa Serikali za mitaa na wanajamii, Kisiwani Pemba, wamesema mafunzo ya haki za binadamu, waliopewa na kituo cha huduma za sheria tawi la Pemba, yamewapa uwelewa wa mambo mbali mbali ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kujua wajibu wao, ndani ya jamii.

Wakizungumza kwenye mkutano wa tathimini uliofanyika kituo cha huduma za sheria mjini chakechake,wamesema kabla ya kupewa mafunzo hayo, hawakuwa na uwelewa huo kwa jamii wanayoizunguruka.

Wamesema, kwa sasa wameshawaambia...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Wito wa usaili kwa wizara mbalimbali Pemba

Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia wale wote walioomba nafasi za kazi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Wizara ya Afya, Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana na Wizara ya Fedha na Mipango kwa nafasi za Pemba wanatakiwa kufika kwenye usaili kwa mujibu wa taasisi aliyoomba kwa utaratibu ufuatao:-

MCHANGANUO WA USAILI – PEMBA

1. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI – PEMBA – Skuli ya Fidel – Castro Pemba saa 2:00 asubuhi

16/09/2017 •...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Wataalamu wamaliza maradhi ya kichocho Pemba

Timu ya watalamu wa afya kutoka nchi nane barani afrika wakishiriana na  madaktari bingwa kutoka   china kwa msaada wa shirika la afya ulimwenguni( WHO) wapo kisiwani Pemba kwaajili ya kupanga mikakati ya kumtokomeza kabisa konokono anaesababisha maradhi ya kichocho ilikumaliza ugonjwa huo visiwani zanzibar.

Wakizungumza katika mkutano wa siku nne unao fanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Pemba Misali Wesha nje kidogo ya mji wa Chake chake Mwakilishi wa Shirika la afya ulimwenguni WHO  Dr...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Chen, daktari wa kichina atamani kubakia kisiwani Pemba milele.

“Jina langu ni Chen Er Dong, nimezaliwa mwaka 1975 kijiji cha Nan Jing nchini China”.

Chen Er Dong, ameanza kwa kusema kuwa maisha ya China nayo sio mepesi sana kama wasiokuwa wachina wanavyofikiria, bali ni kupambana kama ilivyosehemu nyengine duniani.

“Kila kitu ni mapambano, na kila eneo ulilozaliwa lina mapambano yake ya kimaisha kwa mujibu wa mahitaji ya anaepambana na maisha, hata China unabidi upambane ili upate maisha”,anasema.

Ukurasa huu wa makala, ulimuuliza dk Chen, iwapo taaluma...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Jeshi la Polisi laendelea kufanya msako Pemba

Jeshi la Polisi mkoa Kusini Pemba inavishikilia vyombo 65  vya moto yakiwemo magari 11 ya daladala za abiria kwa makosa tofauti  kufuatia msako mkali ulio tangazwa mkaoni hapo wa siku 5 za uvunaji wa zao la karafuu.

Akizungumza huko kwenye kituo cha polisi madungu chake chake kamanda wa polisi mkoa kusini pemba kamishina msadizi mwandamizi wa jeshi la polisi mohamed shekhani mohamed amesema  vyombo hivyo wamevikamata wakati wa msako maalum vikiwemo vyombo ambavyo havina bima Road Lecens Plet...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

ZLSC yahamasisha usomaji wa Katiba Konde, Wete Pemba

SHEHA wa shehia ya Konde wilaya ya Wete Pemba Abdalla Omar, akifungua mkutano wa wazi wa uhamasishwaji usomaji wa Katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba na kufanyika skuli ya msingi Konde, (Picha na Haji Nassor, Pemba)WANANCHI wa rika tofauti wa shehia ya Konde wilaya ya Wete kisiwani Pemba, wakifuatilia mkutano wa wazi wa uhamasishwaji usomaji wa Katiba, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika skuli ya...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Wanne watiwa mikononi na KMKM kwa magendo kisiwani Pemba

Raia wanne wa Kenya wamekamatwa na kikosi Maalumu cha KMKM Kamandi ya Pemba wakiwa na magunia ishirini  (20) ya nazi ambazo walikuwa wakiingiza nchini bila ya kufuata taratibu za kulipa kodi .

Akizungumza Oifisini Kwake Wete , Kaimu Kamanda wa KMKM Kamandi ya Pemba , Luteni Kamanda Hassan Hossein Ali amesema wakenya hao wametiwa mikononi na KMKM katika bandari ya Kichungwani Ungi Shehia ya Msuka Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema Mzigo huo  ulikuwa ndani ya chombo...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

CUF yangundua njama inayosukwa kuvunja ngome ya chama hicho kisiwani Pemba

Uongozi wa chama cha wananchi CUF kisiwani pemba umewataka wafuasi wa chama hicho kukaa mbali  na mpango ulio gundulika wa kuleta mamluki ndani ya matawi ya chama hicho  kisiwani pemba kwa lengo la kuivuruga ngome ya cuf  kisiwani hapo.

Akizungumza na wandishi wa habari huko afisi ya wilaya chake chake katibu wa CUF  wilaya chake chake Salehe Nassor Juma amesema mamluki hao wanaletwa  kwalengo wananchi wachokozeke ilikuwapa nafasi mazombi ambao watakuja pamoja kuwapa sababu ya  kuwapiga watu...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani