(Today) 3 hours ago

Michuzi

WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA UJENZI NYUMBA ZA POLISI ARUSHA


Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba jana Mchana ametembelea jijini Arusha na kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za Polisi zinazoendelea kujengwa baada ya ajali ya moto iliyotokea mwishoni mwa mwezi Septemba ambayo ilisababisha familia za askari 13 kuunguliwa vitu mbalimbali na kukosa makazi.
Mh. Mwigulu alitumia fursa hiyo kwa kuishukuru kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ambayo inaoongozwa na Mkuu wa mkoa Mh. Mrisho Gambo lakini pia...

 

(Yesterday)

Michuzi

MBUNGE KABATI ATOA SH.MILIONI MOJA KWA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE MKOANI IRINGA (TPF)

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) akiwa sambamba na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi.  Kabati aliliomba jeshi la polisi mkoani Iringa kuhakikisha wanapeleka dawati la jinsia katika shule za msingi na sekondari ili kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi kwa kuwa watakuwa wazi kuzungumza...

 

(Yesterday)

Zanzibar 24

Sheikh Ponda afunguka sababu ya nyumba yake kupekuliwa na Polisi

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye alishikiliwa na polisi kwa takribani siku mbili ametoa sababu ya kupekuliwa nyumbani kwake Ubungo Kibangu na polisi hao, kuwa ni kutafutwa kwa nyaraka za uchochezi.

”Kuhusu upekuzi uliofanyika nyumbani kwangu Ubungo – Kibangu, polisi walidai wanatafuta kama kuna nyaraka zozote za uchochezi, lakini hawakuzikuta”. Amesema Sheikh Ponda

Sheikh Ponda alishikiliwa na polisi kutokana na kuzungumza na waandishi wa...

 

(Yesterday)

Michuzi

JUKWAA LA HAKI JINAI LATEMBELEA MAGEREZA NA VITUO VYA POLISI IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA

Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome inatembelea Magereza katika mikoa ya Iringa, Njombe  na Ruvuma ili kujionea changamoto zinazowakabili  wafungwa na mahabusu nchini katika kupata haki zao wakiwa vizuizini au magerezani na kuangalia namna ya kuzitatua. Akizungumza katika siku ya kwanza ya ziara hiyo mjini Iringa, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Mchome amesema utekelezaji wa mradi huo pia...

 

2 days ago

RFI

Amnesty International yasema Polisi nchini Kenya wamewauwa wafuasi wa upinzani 33

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International limetoa ripoti inayoeleza kuwa Polisi nchini Kenya waliwauwa wafuasi wa upinzani 33 kwa kuwapiga risasi.

 

2 days ago

RFI

Polisi ya Kenya yashtumiwa kuwaua kwa makusudi waandamanaji

Mashirika mawili ya Haki za Binadamu yameiomba serikali ya Kenya kuchunguza na kuwachukulia hatua za kisheria maafisa wa polisi wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya watu wengi wakati wa maandamano yaliyoitishwa na upinzani wiki iliyopita kutaka kufanyike mageuzi katika Tume ya Uchaguzi IEBC.

 

2 days ago

BBCSwahili

Kenya yatakiwa kuwachukulia hatua polisi waliohosika na mauaji

Mashirika mawili ya Haki za Binadamu yameitaka serikali ya Kenya kuchunguza na kuwaadhibu maafisa wa polisi wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya watu wengi

 

4 days ago

Malunde

SHEIKH PONDA AACHIWA POLISI KWA DHAMANA

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Pondà ameachiwa leo Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.
Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: "Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi."
Awali, Kamanda wa Kanda...

 

4 days ago

Malunde

JESHI LA POLISI SASA KUKOMAA NA MAADMIN WA MAGROUP YA WHATSAPP

Naibu mkuu wa kitengo cha makosa ya mtandaoni, Joshua Mwangasa amewataka viongozi wa makundi ya whatsApp kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika katika makundi yao kwani kwa kiasi kikubwa makundi hayo yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.

Ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa kutapunguza na kudhibiti makosa mengi yanayofanywa mtandaoni na kutasaidia polisi kuchukua hatua dhidi ya muhusika aliyefanya uhalifu huo.

Lengo kubwa likiwi ni kukabiliana na ongezeko...

 

5 days ago

RFI

Polisi yasambaratisha maandamano ya upinzani nchini Kenya

Polisi ya Kenya imefaulu kuzima maandamanno ya muungano wa upinzani nchini Kenya NASA kaika mji mikubwa mitatu nchini humo.

 

5 days ago

VOASwahili

Polisi yatangaza kuviwajibisha vikundi vya Whats App Tanzania

Viongozi wa makundi ya What's App nchini Tanzania wanatakiwa kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika kwenye makundi yao.

 

5 days ago

Zanzibar 24

Polisi: WhatsApp Group Admin Kueni makini na Group zenu

Jeshi la Polisi limewatahadharisha viongozi wa makundi ya WhatsApp kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika kwenye makundi yao.

Hii ni kutokana na kukithiri kwa makosa ya kimtandao huku makundi ya WhatsApp yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.

Viongozi wa makundi hayo hawatakiwi kuvumilia makosa hayo hivyo wanatakiwa watoe taarifa kwa Jeshi la Polisi. . “Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata...

 

5 days ago

BBCSwahili

Polisi wazuia maandamano ya upinzani miji mikubwa Kenya

Polisi nchini Kenya wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa muungano wa upinzani National Super Alliance waliokuwa wakiandamana katika miji mikubwa mitatu nchini humo.

 

5 days ago

BBCSwahili

Sheikh Ponda ajisalimisha katika kituo cha polisi Tanzania

Katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu nchini Tanzania Sheikh Issa Ponda amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Central

 

5 days ago

Michuzi

KITUO CHA POLISI MOROMBO KUPUNGUZA MSONGAMANO “CENTRAL” ARUSHA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akiongoza askari kuhamisha udongo "Kifusi" toka kwenye msingi wa ujenzi wa nyumba za Polisi na kupeleka kwenye mtaro.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Ujenzi wa kituo kidogo cha Polisi cha Morombo kilichopo kata ya Murieti halmashauri ya Jiji la Arusha  huenda ukawa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambalo linakuwa kwa kasi kibiashara na ongezeko la  idadi ya watu.
 Uwepo wa kituo hicho utawezesha kusogeza...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani