(Today) 11 hours ago

Dewji Blog

DC Hapi aagiza Polisi kumuweka ndani Afisa Uthamini kwa kosa la kumzimia simu

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameagiza Jeshi la Polisi kumuweka ndani siku mbili, Afisa Uthamini wa wilaya hiyo, Einhard Chidaga kwa kosa la kutotekeleza majukumu yake pamoja na kudharau wananchi kitendo kinachodaiwa kusababisha uwepo wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake .

Hapi ametoa maagizo hayo leo katika mkutano wake na wananchi wa Kata ya Wazo uliofanyika kwenye viwanja vya Mkanada.

Baada ya wananchi wengi kulalamika kutolipwa fidia zao na manispaa licha ya uthamini wa...

 

(Yesterday)

Channelten

Jeshi la polisi nchini Afrika Kusini limefanikiwa kudhibiti machafuko yaliyoibuka ya kuwavamia wahamiaji

Jeshi la polisi nchini Afrika Kusini limefanikiwa kudhibiti machafuko yaliyoibuka ya kuwavamia wahamiaji waliopo nchini humo mjini Pretoria katika eneo la Marastabad, linalokaliwa na wengi wahamiaji raia wa Somalia.

Maafisa wa polisi waliingilia kati vurugu hizo na kuwatimua kwa kutumia ndege aina ya helikopta ambapo walitumia risasi za mipira, maji ya kuwasha na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao kuzuia makundi ya wahamiaji yaliyojitokeza yaliyojihami na fimbo, mawe na...

 

(Yesterday)

Habarileo

Polisi waongeza nguvu Kibiti

KUFUATIA tukio la watu wasiofahamika kuwaua watu watatu kwa kuwapiga risasi akiwemo ofisa upelelezi wa wilaya (OC-CID) Kibiti mkoani Pwani, Mrakibu wa Polisi, Peter Kubezya, jeshi la Polisi limeongeza nguvu kwa kuzidisha doria za usiku na mchaka kuwasaka wahusika.

 

(Yesterday)

Mwananchi

Polisi yawagomea makomandoo Simba, Yanga

Jeshi la Polisi limewakomoa makomandoo wa Simba na Yanga baada ya kuwalaza nje ya Uwanja wa Taifa kwa siku mbili mfululizo kabla ya pambano la timu hiyo la leo jioni.

 

(Yesterday)

Malunde

STEVE NYERERE AKAMATWA NA POLISI

Utata umeibuka juu ya kukamatwa kwa msanii wa filamu nchini Steven Mengele a.k.a Steve Nyerere, mara baada ya kuwepo kwa taarifa hizo ambazo zimetolewa ufafanuzi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro.
Akizungumza jana na wanahabari, Kamishna Sirro alisema yeye hajamuita Steve Nyerere lakini huenda akawa ameitwa na maafisa wake wa upelelezi kwa ajili ya mahojiano, jambo ambalo ni sahihi.
Sirro alisema kuna kikosi maalum alichokipa kazi hiyo na endapo msanii...

 

(Yesterday)

Malunde

WATANO WAKAMATWA NA POLISI KWA KUUA KWA MAPANGA NA MASHOKA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA


POLISI mkoani Rukwa inawashikilia watu watano wakituhumiwa kuwaua kikatili watu watatu wa familia moja ambao ni wakazi wa kijiji cha Mfinga kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga kwa kwa kucharangwa na mapanga na mashoka kwa kile kilichoelezwa kuwa ni imani za kishirikina.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando, aliwataja marehemu hao kuwa ni Joachim Kayanda (60), mkewe Evelina Mwanakatwe (47) na mtoto wao wa kiume aitwaye Emanuel Kayanda (27) .
Kwa mujibu wa...

 

2 days ago

Channelten

Abiria wa mabasi walipongeza jeshi la polisi kwa zoezi la madawa ya kulevya

BAADHI ya abiria wanaotumia usafiri wa barabara kuu ya Dar-es-Salaam ñ Mwanza hadi nje ya nchi wameunga mkono mbinu inayotumiwa na jeshi la polisi Mkoa wa Singida la kutumia mbwa wenye mafunzo maalumu ili kuwasaka watuhumiwa wa kusafirisha,kuuza pamoja na watumiaji wa madawa ya kulevya.

WAKIZUNGUMZA na KITUO HIKI abiria hao wameelezea kufurahishwa kwao na zoezi hilo linalofanyika katika Mkoa wa Singida kwa kuwatumia mbwa waliopatiwa mafunzo maalumu ya kubaini madawa ya kulevya kuwa tofauti...

 

3 days ago

Malunde

MBOWE KUTOENDELEA KUKAMATWA WALA KUWEKWA KIZUIZINI NA POLISI HADI MACHI 2

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameongea na waandishi wa habari jana jioni baada ya kutoka Mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa w Dar Paul Makonda na Kamshna Sirro.

Lissu amesema Amri ya kuzuia Freeman Mbowe asikamatwe na wala kuwekwa kizuizini na Polisi inaendelea isipokuwa wanaweza kumuita kwa Mahojiano ambapo pia Mahakama itatoa maamuzi Tarehe 2, March 2017

 

3 days ago

BBCSwahili

Polisi nchini Malaysia wagundua kilichomuua Kim Jong Nam

Polisi nchini Malaysia wamesema kuwa wamefichua kemikali iliyotumika kumuuwa nduguye wa kambo, kiongozi wa Korea Kaskazini, na kuitaja kuwa VX dawa ya neva

 

3 days ago

Zanzibar 24

Taifa ya Jang’ombe wapata pigo, kumkosa captain wao “ninja” katika mchezo wa Polisi

Timu ya Taifa ya Jang’ombe jana imepata pigo kwa Beki wao kisiki wa kati ambae pia ndie Nahodha wao Abdallah Haji “Ninja” baada ya kuoneshwa kadi ya njano na Muamuzi Rashid Farahan “Webb” katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar ambapo Taifa walishinda 2-1 dhidi ya Mafunzo.

 

Kadi hiyo imemfanya Ninja kukosa mchezo unaofuata ambapo Taifa watacheza na Polisi siku ya Jumamosi tarehe 4/3/2017  baada ya kuoneshwa kadi za njano tatu mfululizo katika michezo ya Taifa dhidi ya KVZ, Kilimani City...

 

3 days ago

Habarileo

Walioua Polisi Pwani wahusishwa na ugaidi

WAKATI watu watatu akiwemo Ofisa Upelelezi wa Wilaya (OC CID) wa Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, Mrakibu wa Polisi, Peter Kubezya, wakiuawa kwa risasi usiku wa kuamkia jana, serikali imesema itawasaka na kuwatia nguvuni wote waliohusika na mauaji hayo yanayohusishwa na matukio yenye mwelekeo wa kigaidi.

 

3 days ago

Zanzibar 24

Mkea wa Bilionea Marehemu Msuya ashikiliwa tena na jeshi la polisi kwa kesi ya mauaji

Jeshi la Polisi limewakamata mke wa bilionea marehemu Msuya, Miriam Mrita na mwenzake R. Muyela muda mfupi baada ya Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwaachia huru.

Mjane huyo aliwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji ya wifi yake (Mdogo wa mume wake), marehemu Anathe Msuya aliyechinjwa kinyama Mei 25, 2016 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni.

 

The post Mkea wa Bilionea Marehemu Msuya ashikiliwa tena na jeshi la polisi kwa kesi ya mauaji appeared first on Zanzibar24.

 

3 days ago

Bongo5

Polisi amuua mwenzake kwa kumpiga risasi na yeye ajiua baada ya mechi

Polisi huko nchini Kenya, amemuua mwenzake kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo na yeye amejiua baada kutazama mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kati ya Manchester City na Monaco.

Kabla ya polisi huyo, Konstebo Constable Patrick Kihagi kujiua kwa kujipiga risasi kichwani, alimjeruhi polisi mwingine kwa kumpiga risasi begani.

Polisi aliyekufa ametajwa kwa jina la Konstebo James Makokha, na kabla ya kifo alikuwa akifanya kazi Jogoo House. Inadaiwa kuwa Makokha alipigwa risasi wakati...

 

3 days ago

Habarileo

Polisi yajifua netiboli A. Mashariki

TIMU ya netiboli ya Polisi Morogoro imeanza mazoezi na kutamba kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika Nairobi, Kenya kuanzia Aprili 23 hadi 30 mwaka huu.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani