(Yesterday)

Michuzi

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI WA VITUO VYA UMEME KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akifurahia jambo na wahandisi na mafundi wa TANESCO alipotembela  mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kigamboni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2017. Naibu Waziri, Mhe. Subira Mgalu(katikati), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANSECO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (anayeshughulikia usafirishaji umeme), Mhandisi Kahitwa Bishaija, (kushoto), wakiwasili kwenye...

 

(Yesterday)

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha kawaida cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2017. PICHA NA IKULU

 

2 days ago

Michuzi

Afisa elimu mkoa wa Dar es salaam ahaidi kuzitatua kero zinazowakabili wamiliki wa shule binafsi

Na Michael Utouh
AFISA Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lissu ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule Binafsiinafsi wa mkoa huo ikiwemo ya tozo kubwa za biashara zinazotozwa shule hizo .
Pia amewaomba wamiliki wa shule hizo kipindi cha likizo wajitolee kuwafundisha masomo ya sayansi wanafunzi wanaotoka shule za serikali kwa kuwa wana walimu wengi wa masomo hayo.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua Mkutano Maalumu uliowakutanisha wadau mbalimbali na...

 

3 days ago

Michuzi

INTRODUCING BAHATI BEAUTY SHOP @ CHANG'OMBE DAR ES SALAAM

Jipendezeshe! Mpendezeshe umpendae!Kwa furaha kubwa twawatangazia kufunguliwa duka letu la Vipodozi!BAHATI BEAUTY ni duka lako jipya la vipodozi vya uhakika, ORIGINAL kutoka Ulaya!Fika ujipatie lotions, creams, nail varnish, mafuta ya mwili na nywele, lipsticks na wanja. Bila kusahau Perfumes Za majina makubwa, handbags, anti perspirants na deodorants za aina mbali mbali na vikorombwezo kedekede. Bei nafuu kwa ubora harusi.Tuko Chang'ombe Mtaa wa Mganda, jijini Dar.Ukifika Tameco ni Mtaa wa...

 

3 days ago

Michuzi

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Yakabidhi Hundi ya Milioni Hamsini Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda Kuchangia Ujenzi wa Vyumba Vya Walimu wa Shule za Jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonga kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo...

 

4 days ago

Michuzi

Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman yawasili Dar es salaam kutokea Zanzibar

Meli ya kifahari ya Mfalme wa Oman Mhe. Qaboos bin Said ‘Fulk Al Salamah’ iliyofika Zanzibar Oktoba 12, 2017, imeng’oa nanga leo mchana kuelekea Dar es Salaam kuendelea na safari yake ya kusambaza ujumbe wa ‘Amani na upendo’ duniani. Taarifa kutoka ubalozi mdogo wa Oman zimeeleza kuwa, meli hiyo itakaa Dar es Salaam kwa siku nne kabla kuelekea Mombasa Kenya kwa madhumuni hayo hayo. Akizungumza baada ya kuagana na ujumbe wa meli hiyo bandarini Zanzibar, Balozi Mdogo wa Oman Dk. Al Habsi,...

 

6 days ago

Channelten

Kumbukumbu ya Kifo cha Mwalimu, Kivukoni wafanya usafi katikati ya jiji la Dar es Salaam

Nyerere

Wananchi wa kata ya KIVUKONI leo wameungana na wananchi wenzao wa TANZANIA katika maadhimisho ya siku ya baba wa taifa kwa kufanya usafi katika maeneo ya katikati ya mji ambako ndipo ilipo kata hiyo na kutoa mwito kwa wananchi wenzao kuwa usafi ni muhimu.

Akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi hilo maeneo ya PAMBA ROAD, afisa tarafa wa tarafa ya KARIAKOO, KRISTINA KALEKEZI, amesema baba wa taifa alipenda usafi na katika hotuba zake kadhaa alisistiza jambo hilo ili kuepuka magonjwa...

 

7 days ago

Michuzi

PRINCE AGHA KHAN AZINDUA STEMPU ZA POSTA ZENYE KUMBUKUMBU ZA TAASISI YAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia Ismailia, Prince Agha Khan (kulia), akiangalia picha za stempu zenye kumbukumbu ya Taasisi yake wakati alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, kabla ya kuzizindua jijini Dar es Salaam jana. Walioshika bango lenye picha za stempu hizo kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi na kushoto ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo. Anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Mkoa,...

 

1 week ago

CCM Blog

SHAKA AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIET YA BARAZA KUU UVCCM TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiongoza kikao cha Secretariet ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwa  maandalizi ya vikao vya kikanuni vya Umoja wa Vijana wa CCM vitakavyofanyika Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine vitajadili waombaji wa nafasi mbali mbali za uongozi kwa nafasi za Mkoa na Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa CCM kabla kuwasilisha katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi kwa uteuzi wa mwisho.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )

 

1 week ago

Malunde

MASENETA WA MAREKANI WAKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU DAR ES SALAAM

Rais John Magufuli wa Tanzania, amefanya mazungumzo na ujumbe wa maseneta wa Baraza la Seneti la Marekani.

Taarifa ya Ikulu ya jana Jumatano imesema maseneta hao ni wajumbe wa kamati ya mazingira inayoshughulikia hifadhi ya taifa, wanyamapori na misitu ya Marekani.

Maseneta hao wamekuwepo nchini Tanzania kwa siku tatu lengo likiwa ni kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk Inmi Patterson.

Taarifa ya Ikulu...

 

1 week ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS SAMIA AKUTANA NA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, IRELAND NA MOROCCO KWA NYAKATI TOFAUTI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Paul Sherlock, Ikulu jijini Dar Es Salaam.Balozi alizungumzia masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha wanawake katika nafasi za kisiasa, Masuala ya Mimba za utotoni  na namna ya kukabiliana na vifo wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliiomba nchi ya Ireland kuendelea kusaidia Tanzania katika kutoa elimu...

 

1 week ago

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KIONGOZI WA JUMUIYA YA ISMAILI DUNIANI H.H. PRICE KARIM Al-HUSSAYNI AGA KHAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta  jambo na kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia H.H.Prince Karim al-Hussayni Aga Khan alipotembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika...

 

1 week ago

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MASENETA WA BARAZA LA MAREKANI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Seneta James Inhofe pamoja na Maseneta wa Baraza la Marekani  walipotembelea na kufanya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 11, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamiss Kigwangala, Naibu Waziri wa Mambo ya nje Suzane Kolimba pamoja  Maseneta wa Baraza...

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani