2 months ago

Zanzibar 24

Rais wa FIFA: Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania Mbwana Samatta anacheza Genk

Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta anaipeperusha vilivyo bendera ya Tanzania, hiyo ni baada ya Rais wa FIFA Gianni Infantino kumtaja wakati akipiga stori mbili tatu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

“Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania Mbwana Samatta anacheza Genk, hii ni nchi ya mpira licha ya changamoto za shirikisho siku za nyuma lakini kwa sasa mpo kwenye mstari kutokana na uongozi mpya kwa kushirikiana na CAF pamoja na...

 

2 months ago

Zanzibar 24

Zitto Kabwe amtembelea Mbwana Samatta nchini Ubelgiji

Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe jana Februari 12, 2018 alikwenda kumtembelea  Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta nyumbani kwake huko Genk nchini Ubelgiji.

“Nilipata nafasi kumsalimu @samatta77 jana jioni nyumbani kwake Genk. Nimefurahi kuwa anaendelea vizuri na anapambana kuhakikisha anaendelea kukuza nchi yake na yeye mwenyewe. Ana mawazo mazuri Sana ya kuendeleza soka la Tanzania. Mungu atamsaidia Samata wetu...

 

5 months ago

Michuzi

SAMATTA NJE WIKI SITA, AUMIA GOTI SASA KUWAKOSA BENIN NOV 12

NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ anayekipiga na KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta atakuwa nje ya uwanja kwa majuma sita akiuguza majera ya goti aliyopata katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa sare tasa dhidi ya Lokeren.
Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada kuumia dakika ya 40 nafasi yake ikachukuliwa na Nikos Karelis aliyerejea hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa muda mrefu pia kutokana na majeraha.
Ripoti ya daktari iliyotokana na majibu ya vipimo...

 

6 months ago

BBCSwahili

Samatta, Olunga na Onyango kuwania taji la mchezaji bora Afrika

Denis Onyango wa Uganda, Mbwana Samata wa Tanzania na Micheal Olunga wa Kenya wameteuliwa kuwania taji la mchezaji bora barani Afrika 2017

 

9 months ago

Mwanaspoti

Samatta amva Rooney leo

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji  leo Jumamosi atakuwa katika vita ya kibabe na staa wa Everton, Wayne Rooney.

 

9 months ago

Zanzibar 24

Samatta sasa achukua ubalozi wa maalbino Tanzania

Sasa Streika wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amekuwa Balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) nchini Tanzania kwa  kusema yupo tayari kuwalinda na kuwatetea.

Samatta amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuwepo tatizo kubwa nchini Tanzania la kuuawa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani ya kishirikina.

“Nimefurahi kuwa balozi wa watu wenye ualbino Tanzania, nipo tayari kuwalinda na kushawishi watu wengine waendelee kuwalinda pia. Mimi ninawathamini...

 

10 months ago

Mwanaspoti

Samatta kuwafuta machozi Watanzania kwa kuivaa Everton

 Mshambuliaji Mbwana Samatta atabeba jukumu lingine la kuiwakilisha Tanzania wakati atakapoingoza KRC Genk kuivaa Everton mwezi ujao.

 

10 months ago

Mwanaspoti

Everton kumfuata Samatta

KAMA mshambuliaji, Mbwana Samatta, ataweza kuchanga karata zake vyema dhidi ya  timu ya Everton mwezi ujao, inaweza kuwa ufunguo wa ndoto zake za kucheza Ligi Kuu England iwapo atafanikiwa kuishawishi ipasavyo.

 

10 months ago

Mwanaspoti

Samatta: Nikiondoka Genk nakwenda England, Hispania au Italia

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta  amesema  amepokea ofa mbalimbali za kucheza soka la kulipwa katika klabu za Ligi Kuu za England, Hispania, Ujerumani na Italia.

 

10 months ago

TheCitizen

Samatta signs deal with DTB Tanzania

The national soccer team, Taifa Stars, captain Mbwana Samatta has signed a six-month endorsement contract with Diamond Trust Bank Tanzania Limited.

 

10 months ago

Mwanaspoti

Samatta kuwanoa vijana nchini, asaini mkataba

Nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubeligiji, Mbwana Samatta ameingia mkataba maalumu na Benki ya DTB na pia ataendesha kliniki ya soka kwa mamia ya vijana zoezi lililofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar es Salaam.

 

10 months ago

Mwanaspoti

Samatta awaita Mbeya City mezani, huku akiwaweka njia panda Prisons

Mbeya City inamuwinda mshambuliaji wa Prisons, Mohamed Samatta katika kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao.

 

10 months ago

Michuzi

Samatta apongeza udhamini wa SBL kwa Taifa StarsMchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Sammata ameihakikishia kampuni ya Bia ya Serengeti ambayo ni wadhamini wa timu ya taifa Taifa Stars kwamba wachezaji wa timu hiyo watajituma ili kuhakikisha kuwa wanashinda mechi zote walizopangiwa kwenye ratiba.

Samatta ambaye ni nahodha wa timu hiyo ya taifa alitoa hakikisho hilo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuhudhuriwa na Meneja Masoko wa SBL,...

 

10 months ago

MillardAyo

VIDEO: Samatta kaeleza sababu za kuonesha hasira game ya Taifa Stars vs Lesotho

Jumamosi ya June 10 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza game yake ya kwanza ya Kundi L ya kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019 nchini Cameroon dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi. Katika game hiyo Taifa Stars walilazimishwa sare ya kufungana 1-1, goli la Taifa Stars […]

The post VIDEO: Samatta kaeleza sababu za kuonesha hasira game ya Taifa Stars vs Lesotho appeared first on millardayo.com.

 

10 months ago

MillardAyo

VIDEO: Walichozungumza Samatta na Ulimwengu kabla ya game ya Lesotho

Kesho Jumamosi ya June 10 2017 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itaanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019 nchini Cameroon dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi. Taifa Stars ipo Kundi L lenye timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho  katika […]

The post VIDEO: Walichozungumza Samatta na Ulimwengu kabla ya game ya Lesotho appeared first on millardayo.com.

 


Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani